MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

Miongoni mwa sauti za wanamuziki/waimbaji nchini Tanzania ambazo huwa hazihitaji kutumia msuli sana kuzitambua ni ile ya Muumini Mwinjuma. Na kwa wale mnaozikumbuka enzi za nyimbo kama “Tunda” mtaelewa zaidi ninaongelea nini.

Burudani yetu ya leo inatoka kwake huyo huyo Muumin Mwinjuma. Wimbo unaitwa Kilio Cha Yatima.Ni utunzi wake Muumin na umeimbwa enzi akiwa na kundi zima la Double M Sound maarufu kama Wana Mshikemshike.

Wimbo huu ulikuwa ni kati ya nyimbo za Muumini za mwanzoni kabisa baada ya kujitoa kwenye bendi ya Tamtam.Wimbo huu aliuimba maalum baada ya kugombana na mwajiri wake wa kwanza pale Muumini alipokwenda kumuuguza na hatimaye msiba wa baba yake mzazi Mzee Muumin Mbughuza (RIP).

Kwa sasa Muumini ameunda kundi lake jipya linalojulikana kama Bwagamoyo Sound na kwa sasa wako kambini wakijiandaa na uzinduzi wa kundi lao ambalo anasema litakuwa moto wa kuotea mbali.Pata Burudani na Ramadhani njema.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Habari na burudani ya leo imeletwa kwenu na Pius Mikongoti anayeblog kupitia Spoti na Starehe.Bonyeza hapa umtembelee.

**Shukrani kwenu wote mlionitumia salamu za pole na kunitakia afya njema.Nipo fiti sasa.Zawadi yenu hii hapa.Wimbo unaitwa Kuteleza sio Kuanguka kutoka kwake Lady Issa.Unamkumbuka?

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

36 Responses to “KILIO CHA YATIMA-MUUMINI MWINJUA NA DOUBLE M SOUND”

  1. Comment by Majita on September 12th, 2008 12:29 am

    ndugu wakuru mimi nawafwagilia kiafande afande.Yaani mmeniunganishia ujumbe mbili zinazofanana hadi nikabaki natoa majino na majicho kwa furaha.Duuu

    Muumini anaimba “…Shida ni Utelezi wa Maisha….” Lady Issa yeye anakwambia ‘….Maisha ni mlima,kuna kupanda na kushuka,BALI KUTELEZA SI KUANGUKA..”
    Haya Kaazi kwenu wanazuoni.Nani kamjibu mwingine,na wanafanana vipi katika ujumbe,na nia ya hawa wanafasihi ilikuwa nini.BC nimewakubali kabisa.Mkubwa Piusi hongera sana.mimi umenigusa coz nimefikilia mbali sana.

    Muumini nakupa big up kwa kuamua kutunga wimbo huo kwa kumkumbuka baba yako.Tuliofiwa na baba zetu tunajua sana ulikuwa katika hali gani wakati unatunga wimbo huo,hope ndo maana umesimama sana.

    ILA Muumini Bwana ulinisikitisha sana kumuacha yule mke wako wa Pale Chumbageni-Msikitini pembeni mwa hilo duka la Shakaza hapo mkono wa kulia kama unaelekea Nguva Bar/opposite na min depot ya breweries/Misitu au kwa minchi.Nakumbuka sana siku ile ya arusi yako nilovyopiga ubwabwa na ndizi yangu niliyokuja nayo mfukoni niliyonunua barabara ya 13.Yaani wewewe muumini wewewewe!!! Edo Ndaki kaka upoooo???? Nafikiri wewe siku hiyo ulimtoroka Kimathi pale mjengoni kama siyo kumkimbia Mwakasaka wa Galinos kuwahi ubwabwa kwa sababu nilisikia ulikuwa unasoma tution kwake.hahahahahaha.

    Ka wimbo ka Lady matona kananikumbusha ile miaka ya 80 mwishoni kalivyokuwa kameshika moto.eeh ile pyeeee siku hizi arusi zoote Bongo lazima wakapige kawimbo aka.Bwaaaaa.Maty upooo,binti-mzuri,Rahma,mkubwa Nalitolela,RebbyGod,Mkuu mswahilina,chris,mama mkwe mama wa kichaga,blackmannem,na wewe Kahindi wewe na wengine wote wapenzi wa BC haya sasa uwanja wa muziki huo.Kwani nimesema ukipanda ngazi utakatalia huko huko???Hata kama UNAPANDA NGAZI UKATIE OKO KWENYE TUNDU LA BATI,utashuka tuuuu(mhh tumetoka mbali??Zumbukuku).Duu kaaazi kwelikweli.
    Majita

  2. Comment by Dunda Galden on September 12th, 2008 6:28 am

    Home sick again
    Pole sana Nape
    mfungo mwema
    salam wote wadau

  3. Comment by Dunda Galden on September 12th, 2008 6:31 am

    SONGA MBELE MUUMINI KUMBUKA LIFE IS BIG LOAD
    KUNA SAINI ZA KILA AINA UNAPOKUWA NJIANI

  4. Comment by SHUBI on September 12th, 2008 7:29 am

    kweli umenikumbusha mbali na wimbo wa tunda,,,huyu mtu bado yupo mbona asikiki tena! metty umeona ilo tunda?na umekumbuka wapi?

  5. Comment by matty on September 12th, 2008 9:23 am

    heeeeee jamani tunda nitalipataje tunda???tamtam maneno ya tam tam..hee jamani mara hii next wknd aluuu!
    Shubi mbona sasa hujasema wewe ni shubi yupi aiseee…ila nakumbuka mbali sana na hilo bushpank lake Muumin ni soo miaka ile!
    Wknd njema all of you guys!

  6. Comment by Mh Lukamba on September 12th, 2008 9:35 am

    Kipaji bab kubwa,ila PLAN babake!!! ndo huna.

    Wanamuziki wa kibongo inabidi waandaliwe chombo/kitengo kwa ajili ya kuplan maisha yao,Hakuna historia nzuri ya
    mwanamuziki wa kibongo,utasikia kahama bendi,kufungua bendi yake,mara teja,jela,mara kafa !!!

    Hii ndo kitu kikubwa kilichowafanya wazazi wengi kuwanyima watoto wao kuingia kwenye muziki miaka hiyo,ingawa vipaji wanavyo,Suala ni plan ya maisha ya kimuziki ndo poor.

  7. Comment by binti-mzuri on September 12th, 2008 10:54 am

    ai jamani..r.i.p to my dad as well

    weekend njema,board memberz

  8. Comment by sisterTZ on September 12th, 2008 12:06 pm

    Wimbo ni mzuri ila unanisikitisha,….

    Jamani nikisia mwimbo huu nakumbuka nyumbani , Pale kijitonyama.. na pia namshukuru mungu kwa kulelewa na wazazi wangu mpaka ukubwani, maana bahati kama hii watu wengi hawana..

    duh ngoja nimpigie mama yangu simu nimwambie kwamba na mpenda na japo nipo mbali nae namiss sanaaaaaaaaa…

  9. Comment by BLACKMANNEN on September 12th, 2008 1:06 pm

    Jeff,

    Mimi pamoja na wale wote tuliokuwa tunakutakia “Afya Njema” tumefurahi sana kusikia kuwa upo fiti sasa, Mungu ashukuriwe.

    Jeff, upendo wako kwetu na kutujali katika kiwango kikubwa hicho ulichotuonyesha, sisi wote, umetupa moyo wa kuutembelea uwanja wetu huu wa BC, kila dakika ili kuona kilichopo hata kama hatutakuwa na cha kuchangia, lakini kupeana salaamu tu. Tunao akina Binti-Mzuri, Majita, Nalitolela, Matty, Mzanzibar100% na wengine wengi tu, hadi akina “Matapishi” tunao humu pia.

    Jeff, ahsante sana kwa muziki wa “Lady Issa”, wimbo wake “Kuteleza Sio Kuanguka”, una mafundisho mengi. Bila ya kumsahau Pius Mikongoti kwa kutuletea “Kilio Cha Yatima”- Muumini Mwinjuma, wimbo una ujumbe mkubwa.

    It’s Great To Be Black=Blackmannen

  10. Comment by Mswahilina on September 12th, 2008 3:44 pm

    Ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kukuponya Mwenyekiti wetu Jeff.

    Huu wimbo wa Lady Issa unanikumbusha mbali kweli, yaani enzi za ujana wangu.

  11. Comment by matty on September 13th, 2008 5:43 am

    Tunamshukuru Mola kwa kukuponya kaka Jeff!!hakika BC IDUMU MAANA mimi nikikosa kuingia hapa huwa najing’ata mno.

    Majita ndugu yangu nipo tu kama kawa!

    nice wknd all off you guys!

  12. Comment by kindo on September 13th, 2008 6:20 am

    Pole sana Jeff, mimi nilikuwa gizani sikujua yaliyokufika!! Nyimbo zote ni nzuri sana…wikiendi njema wadau

  13. Comment by Mama wa Kichagga on September 13th, 2008 1:18 pm

    Majita mkwe uko wapi siku hizi? Au uliwaruhusu mbu wakakung’ata?

    Wadau wote wa BC nawatakia mapumziko mazuri ya mwisho wa wiki na msisahau kuwaombea na kuwasaidia mayatima woote hasa wale waliopata janga hili wakiwa ndio kwanza hawauelewi ulimwengu huu!

    Usiombe kuishi maisha ya uyatima au single parent (tena huyo single awe Mmama) halafu uishi tz na tena uishi klm! Hakika utaionja kadhia ya dunia hii!

    Nyimbo za Mwinjuma ni nzuri sana na zinampangilio mzuri mno wa sauti ambazo huchoki kuzisikiliza ila huu siupendi kabisa mimi kwani kila nikiusikia unaniharibia mood yangu na naishia kulia kwani unanikumbusha sana nilikotoka! Ila yote ni kheri tuu na yeye Mungu ndiye ajuaye mipango yake kwetu sisi wanadamu na pia namshukuru sana huyu huyu Mungu kwa kuniinua na kuniweka mahala pa juu palipoinuka na kunipa nguvu ya kusonga mbele.

  14. Comment by Chris on September 13th, 2008 3:36 pm

    Jeff tatizo lako kila weekend unanipa wakati mgumu sana na majirani zangu! Lakini nafurahi ni kama washazoea na wanahisi ikifika ijumaa nahudhuria coffee shops!

    Kwa wote mliopoteza your lovely daddies! Stay strong and focused always! R.I.P kwa madingi wote wa wanabongocelebrity wote waliotangulia mbele ya haki na wengineo!

    Majita umenena nilipokua napataka! Nami nilikua na duku duku hilo la ujumbe wa hizi nyimbo na Jeff BC kuziweka nikajiuliza nani kamjibu mwenzake!

    Nikimkumbuka Mwinjuma na wote aliowataja humo kwenye wimbo na bado wanatesa na yeye ndo “maisha yashamtenda” japo ana hiyo band! Najisemea kweli maisha ni kitendawili! Nazidi kujiuliza hivi maisha na urafiki yanajengwa kwa misingi ipi?

    Tuko pamoja wote! Matty, Majita, Eddo, Bro. Mswahilina, Dunda, Wa-Kichaga mama, Kekuu (husikiki), na wengineo wote… weekend ndo hii! Enjoy!

  15. Comment by mwandiga on September 14th, 2008 2:07 am

    Mhh mhh hii ni public view blog,sasa mambo ya kuanza kueleza habari za vijiweni,uani au majumbani ni off point.
    Tengenezeni web msalimiane.
    mna bore! eti knje jana ulinunua bia, rugarabama umepata scholarship, mwakipesile mtoto anatembea, msuya mvua zinanyesha huko, sasa yote haya yanahusiana nini na mwinjuma.
    Acheni hizo,mna bore tena stiff.
    BC msipoteze uelekeo kwa kuendekeza wa boaji

  16. Comment by Mswahilina on September 14th, 2008 8:22 am

    Mama wa Kichagga, hebu tuhabarishe huko klm kuna tatizo gani kwa single parents hasa akina mama?

  17. Comment by Mswahilina on September 14th, 2008 8:25 am

    Du, Mama wa Kichagga, pole kwa matatizo yaliyokupataga wakati huo. Ninachomshukuru Mungu pia ni kuwa umemkimbilia yeye naye akawa ndiye ngao/mwamba wako wa maisha. Mungu azidi kukubariki na kukuneemesha siku zote za maisha yako. Amen.

  18. Comment by hombiz on September 14th, 2008 1:52 pm

    Life is fever fair! Dawa ni kukomaa nayo tu. Macho mita 100. Full kusonga mbele 100%

  19. Comment by Chris on September 14th, 2008 5:20 pm

    Mwandiga kwanza elezea public ni nini na what it takes something (km BC) to be public? Baada ya hapo naamini hutatoa tena msg kama hiyo! Usijianike namna hiyo!

    Pamoja!

  20. Comment by Pearl on September 15th, 2008 2:45 am

    mwandiga what is really happening to u!!!!???? u are over reacting.

  21. Comment by Matty on September 15th, 2008 5:23 am

    To you Mwandiga,
    u sounds arrogant to us, u ar new comer in this site…u better pass through and leave pipo alone.
    pls refrain from verbal words!
    HABARI NDO HIYO!

  22. Comment by binti-mzuri on September 15th, 2008 1:01 pm

    mwandinga hajawahi shushuliwa .. usitikise kibiriti BC,maana kuna njiti kibao humu ohoo you have been warned.lol

  23. Comment by Gervas on September 16th, 2008 7:39 am

    Mwandiga…..mtindiga nini?

  24. Comment by Dunda Galden on September 16th, 2008 10:25 am

    Binti_mzuri wakati wa kuukaribisha mwezi mtukufu hukunialika
    leo la kumi na ushei umenialika futari bubu,isije ukawa kobe maana michale inanicheza.nikisikiliza
    KILIO CHA YATIMA OHHHOOOOO

  25. Comment by Mswahilina on September 16th, 2008 5:12 pm

    Huyu Mwandiga ni Junia memba wa BC, hivyo msameheni bure.

  26. Comment by samata on September 16th, 2008 11:10 pm

    Ni kweli mwandiga kasema,mimi ni msomaji mzuri wa bc lakini hili la kutueleza mambo ya nyumbani kwenu ni baya.
    Mnasema lakini kawapa sure. Mimi nafwagilia.
    Ila mwandiga acha ghadhabu!

  27. Comment by BLACKMANNEN on September 17th, 2008 2:22 pm

    He he he heeee, Duh!!!! Mwandiga na Samata………!!!!!!
    BC ni umma la Kitanzania linalojaliana, likiongozwa na “UPENDO MKUU” kwa kila mmoja. Kitu hicho mkikijua hamwezi kusema hayo, maneno yenu ya kebehi mnayosema ninyi hapa!

    This Is Black=Blackmannen

  28. Comment by matty on September 18th, 2008 3:01 am

    Samata na wewe unakuja kwa step za woga woga ujumbe wako tumeupata, napenda nikwambie hivi shostito/kaka usimpigie mbuzi gitaa utachoka wewe maana tuko hapa kurelax +refreshing our mind wewe ambaye hufurahii zogo la hapa its better ule kona!

  29. Comment by thms. on September 18th, 2008 7:02 am

    We majita wa kwaza kabisa uko sawasawa wewe, lazima una faili milembe. MUUMINI UNAIMBA VIZURI TATIZO HUNA MWELEKEO WA MAISHA UNAHAMA HAMA SANA ukahama mpaka bendi yako mwenyewe. sasa umeanzisha bwagamoyo sound ukitoa albam moja tu. tutasikia umebadilisha jina au umehama. Tulia sehemu jipange
    kama unakumbuka kipindi cha nchinga sound ulikuwa juu kuliko hata banza na choki tamtam ikakuweka juu zaidi lakini mara tot mara sijui nn, sasa hivi choki yuko mbali sana.
    We ndio uliwaleta nchini wakina sumuni mwezingo na amina na seseme omari ulienda kuwachukua kenya muje kuanzisha tamtam. lkn wenzako kwa sasa wako mbali we kila leo unahama na unaowa na kuacha, we sasa ni mkubwa acha ujinga tulia jipange vizuri,

  30. Comment by halima on September 18th, 2008 10:29 am

    habari kaka jeff nashukuru umepona nilikuwa naomba utuletee huyu model hawa abdulkadir

  31. Comment by binti-mzuri on September 19th, 2008 11:30 am

    haha dunda galden…nimekwambia uje mida flani tufuturu hukutokea we unategemea nini.. anewei,nisiseme sana mwandinga atasema naleta ya nyumbani kwenye public blog.. ila karibu futariii la kunani bidaeeee

  32. Comment by Dunda Galden on September 22nd, 2008 8:48 am

    Achana nae mwache asubili mfungo uwishe atakumbana na wenye ukurasa wao….binti ntakuja

  33. Comment by Amina on September 24th, 2008 6:34 am

    du matty kaandika kingereza

  34. Comment by Amina on September 25th, 2008 2:48 am

    thms umenena

  35. Comment by Matty on September 25th, 2008 8:30 am

    Yes Amina why not?? i feel to use English language BUT sometimes!hujanielewa nini???u better find dictionary shosti hahahahahahaha!

  36. Comment by ntwiga » Archives » musical link: Moji & The Tropicals, Double M Sound on November 18th, 2008 12:39 am

    [...] Jeff of Bongo Celebrity posted a track off this same album a while back that Kilio cha yatima (Cry of the orphan) you can find here [...]

Leave a Reply