MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

WAZIRI wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika(pichani) amepiga marufuku wananchi kuweka wimbo wa taifa katika simu zao za mkononi.

Mkuchika alisema kufanya hivyo ni kuudhalilisha wimbo wa taifa pamoja na nchi kwa ujumla kwani inapaswa kuheshimiwa mahali popote .

”Unakuta mtu ameweka wimbo wa taifa kwenye simu yake ya mkononi halafu anapopigiwa ama yuko kwenye ulevi au mahali kwingine ambako wimbo huo hauhitajiki, hakika tunaokosesha heshima kama wimbo unaowakilisha utaifa wetu,” alisema.Kwa habari zaidi bonyeza hapa.Nini maoni yako?Unakubaliana na Waziri?

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

35 Responses to “MARUFUKU KUTUMIA WIMBO WA TAIFA KAMA “RINGTONE””

  1. Comment by Mimi on August 5th, 2008 12:21 pm

    How about viongozi wa serikali/mawaziri kwenye madangulo na mabaa wakivizia mabaa medi na watoto wadogo…hilo hawalioni kama linadhalilisha taifa…!!! What’s wrong having a national anthem as ringtone…that shows patriotism!I just don’t understand these clowns!

  2. Comment by Mtanzania on August 5th, 2008 12:47 pm

    MKUCHIKA hapa sikubaliani nawe huwa ni ubabe na udikiteta, wala huna mamlaka yoyote yale ya kupiga marufuku wimbo wa taifa, no maana watu wengi hawaujuwi kwa tabia zenu hizo za kikoloni, wimbo wa taifa ni wa kila mtu si serikali tu na mtu anaweza kuimba mahala popote pale anapotaka kuuimba, ebu achane fikara za kizamani, hii hoja ulitakiwa kuipeleka bungeni na bunge lijadili na kupeleka kwa wananchi fo referendum, wanaichi wenye waamue juu ya wimbo wao si wewe, wewe ni nani kupiga marufuku wimbo wetu. NAOMBA SWALA HILI LIFIKISHWE MBELE ZETU KUPITIA BUNGE NASI NDO TUTOLEE MAAMUZI SI MKUCHI PEKEE YAKE, WATU KAMA HAWA WAKIWA RAIS BASI TUTAKIONA CHA MOTO, TENA NAHISI NDIO NDOTO ZA ZA BAADAYE KUGOMBEA URAIS. HATUWATAKI WA-DIKTETA

  3. Comment by Malenga on August 5th, 2008 1:19 pm

    Huyo waziri hana akili hata kidogo,wimbo huo ni wa kujivunia uwapo katika hali au mahali popote,aidha kwenye raha shida,matatizo au ulevi.Mafisadi hawaaogopi kuwafisadi wanainchi wanaowaongoza ambapo huapishwa kwa heshima ya wimbo huohuo, itakuwa wimbo huo kusikika katika simu ndio tija? Mwangalie alivyovimbiana hajui hata utamaduni ni nini na bado anaitwa waziri wa utama…duni…hakika akili yake ndio duni…..Aibu

  4. Comment by Frateline on August 5th, 2008 1:57 pm

    Hi Guys kutoka Helsinki

    Kwa hili ninapenda kumuunga mkono waziri, kumbuka ndugu yangu Says tofautisha masirahi ya Taifa(national interests) na personal interests(masirahi binafsi)- Kiongozi kuwa mwizi au malaya au fuska, this has nothing to do with national interests, at the end of the day, he will not get votes, LAKINI mtu kudhalilisha wimbo wa Taifa, ni kudhalilisha utaifa wetu, kwa mfano Bongo ni tofauti na huku Ulaya, ukiwa baa au sehemu za starehe watu wanapokea simu za milio tofauti tofauti kama vile bongo flava, inakuwa kama mashindano mtu anapigiwa simu anachelewa kupokea kila mtu anasikia huo wimbo, mimi tangia nasoma ninajua nikisikia wimbo wa Taifa lazima kuna jambo la kitaifa(national interests) either Rais anahutubia au ni jambo la kitaifa kama vile mashindano ya kimataifa, hivyo sio vizuri wimbo wa taifa uwe kama bongo flava eti kisa ni uzalendo, huo sio patriotism bali ni kinyume chake. Pia nimekumbuka watoto wa shule za secondary DSM ni fashion kuwa na simu za mkononi na wanachezea milio kwenye dala dala, sasa hii kwa wimbo wa Taifa ni Dharau, Hongera waziri kwa uamuzi mzuri, LAZIMA WIMBO WA TAIFA UPATE HESHIMA YAKE TOFAUTI NA BONGO FLAVA:

  5. Comment by Frateline on August 5th, 2008 2:10 pm

    Na hii kwa ndugu yangu Says,
    Viongozi wa serikali yeyote dunia wakiwa hawana maadili wanalazimishwa kuwajibika na kujihudhuru maana ni wao wanaoharibu sifa zao binafsi za kuwa kiongozi, kwa mfano hata Clintoni alipofanya ufuska ktk Ikulu ya marekani aliandamwa yeye, Mzee wa ANC Bondeni Zuma baada ya kubaka ameandamwa yeye sio taifa, vivyo hivyo bongo viongozi kwenda na machangu doa sio ajabu kwani viongozi wetu sio malaika hawatoki mbinguni, lakini wanaharibu sifa zao za kuwa viongozi, Kwa wimbo wa Taifa ni utambulisho rasmi wa Taifa( symbol of sovereign state), na ndiyo maana mkuu wa nchi anapokuwa ktk nchi nyingine kikazi anapigiwa wimbo wa Taifa lake kwa heshima ya watu wake, Hivyo waziri hajakoea kabisa kulinda heshima ya wimbo wa Taifa.

  6. Comment by Bablee on August 5th, 2008 2:12 pm

    Frateline;

    Bahati mbaya katika kiswahili hakuna neno “MASIRAHI” nimejaribu kuangalia kamusi nimeona neno “MASLAHI” jee ndilo ulilokusudia?

  7. Comment by Mama wa Kichagga on August 5th, 2008 2:20 pm

    Mimi sina hoja ya nguvu hapa leo ila nina swali.

    Je, umuhimu wa bendera ya taifa na wimbo wa taifa uko tofauti? Kwani siku hizi tuna hata vitambaa vya kufuta mafua vyenye rangi ya bendera, magauni, kanga vikombo nk!

    Ktk kutumia rangi na hata bendera ya taifa tunadai ni utaifa Je mwimbo wetu nao sio utaifa?

    Vinginevyo namuunga mkono Mtanzania hapo juu kuwa tusijichukulie sheria mikononi bali tujitahidi kuwa na majority votes pale suala linapokuwa na mtizamo wa kitaifa ili kujenga na kukuza demokrasia ktk ngwe hii ya utandawazi.

    HIZI SIO ZAMA ZA KUMTISHIA MTU MZIMA SHAU!

  8. Comment by injinia on August 5th, 2008 3:07 pm

    Waziri mpumbavu amekosa cha kuongea. Period

  9. Comment by Mimi on August 5th, 2008 4:28 pm

    My point is kama una kiongozi anayekimbizana na wanafunzi au malaya unategemeaje huyo mtu kukemea hivyo vitu since we all know kuwa ni moja ya vitu vinavyoandamiza society yetu. Tusisahau kuwa kiongozi anatakiwa kuwa mfano bora kwa wananchi…please think outside the box b4 you make your judgement…! I know hatuwezi kuwa na ma-saint kama viongozi but at least watu wenye kufikiria kabla ya kuongea au kutenda…just a thought

  10. Comment by pilipili on August 5th, 2008 6:20 pm

    Ama kweli Mkuchika umekosa sera! suala hilo ni sawa na lile la bendera, eti bendera ya taifa ilikuwa inafungwa na minyororo watu wasiipate kisa wataidhalilisha, sasa yako wapi? mbona mmebana mpaka mkaachia. Fikra hizo finyu ni dalili za kukosa mwelekeo wa kuwafanya wananchi wajivunie vitu vyao, ebu Mkuchika tueleze nini kibaya hapo? dictate issues not minor things like N.E! hiyo minaiona imesinyaa haina mvuto na haina mantic vitu vidogovidodo visivyo na impact yoyote kwa taifa. Kudadeki Mkuchika umeisha hivyo kisiasa?

  11. Comment by wabusara on August 5th, 2008 6:51 pm

    vijana wakivaa nguo zenye bendera ya taifa ya UK au US wanalalmikiwa eti ni kuiga tamaduni. Mtu akiimba wimbo wa taifa wa US au UK wala hakamatwi.Akiimba wa TZ marufuku.!!!!!!!!!!!!!
    Vijana msiweke ringtone za wimbo wa taifa ili mkuchika na wenzake wafurahi.
    Wekeni ringtone za madona,doggy snoopy,mariaha carey,Profesa Jay, mwana Fa, AY, Lady jide n.k.
    Hawa akina mkuchika wakifa tutaimba wimbo wetu wa taifa.
    Ukibishana na mjinga watu wanaweza kutojua tofauti.
    Hawa ndio watu wa JK bwana!!! wakiambiwa EPA,richmond,kiwira humsikii hata mmoja, wakisikia ringtone za simu kila mmoja ataongea.
    Huyu Mkuchika ni mtu wa gwaride,kama alipita shule sijui.

    Jamani msiendelee na mjadala maana mnapigana na ukuta.

  12. Comment by Masudi on August 5th, 2008 7:55 pm

    Mkuchika una akili FUPI kama maisha ya FUNZA, period

  13. Comment by nzehe on August 5th, 2008 8:46 pm

    mkuchika tembea na ubadilike na wakati.huu ni wimbo wa taifa popote utakapouimba unaonyesha pride ya utanzania wako.ktk ringtone ndio inanoga zaidi.message delivered

  14. Comment by george on August 6th, 2008 3:48 am

    hapo ndugu waziri ninaona amechemsha,vitu vya kipuuzi ndivyo wanavyovipigia kelele,sasa mtu kutumia wimbo wa taifa kuna dhambi gani?

  15. Comment by wetu on August 6th, 2008 4:35 am

    mimi sioni kosa kuweka ringtone ya wimbo wa taifa kwenye simu .wewe waziri mzima hujui la kuongea au umeamka na hangover?usisahau kitambaa cha kufutia jasho cha mwano ni bendera ya taifa..sasa hujui hilo pia ni kosa?kama ni marufuku basi hata jezi zetu za wacheza mpira wa miguu ni bendera ya taifa kama.nyimbo yetu ya taifa kwa hiyo ipigwe mafuruku pia
    stop talking like a small kid..sisi wengine tuna akili timamu.

  16. Comment by Ras Mo Fire on August 6th, 2008 5:30 am

    Jamani! Hivi kweli kuweka ringtone ya wimbo wa taifa kunadhalisha nchi kuliko kiongozi kuiba mabilioni ya shilingi za wananchi? Au viongozi kutia mikata mibovu ya kuhujumu mali za nchi na wanachi?

    Issue ni ringtone tu, basi ukomeshe vitambaa, khanga, jezi, kofia na vyote vinavyfanana na rangi ya bendera ya bongo, maana vinadhalilisha pia bendera. Pumbavu!

    Kweli Duniani uombe bahati, inashangaza mtu kama huyu kupewa wadhifa muhimu kwenye serikali. Tunategemea tz itapiga hatua kimaendeleo karibuni kwa kiongozi kama huyu? sidhani.

    Baada ya koboresha michezo, kazi za wasanii wa kibpngo kutangazwa nje y nchi, na mambo mengine muhimu ya kuboresha kwenye wizara yako. Unakuja na hoja ya ringtone, ambayo si burning issue kwa watz. Wakumbushe wakubwa wako huko mh. Rais na Waziri mkuu, tunataka kuona mafisadi wanafikishwa mahakamani na pesa za kodi za wananchi zinarudishwa, sio kufumbia macho mambo muhimu na kufuatilia yasiyostahili kufuatiliwa. Get to real work mr. Mkuchika

  17. Comment by Mr.KT on August 6th, 2008 8:34 am

    These are the kind of leaders we have here in TZ!!Ni nani anashangaa kwanini TZ haiendelei na mali zake zinaliwa na wageni na wajanja wachache, huku mwananchi akiendelea kuwa hohehahe?? We have many leaders of this type in our govt, and that’s explain many many things!!

  18. Comment by Pearl on August 6th, 2008 8:42 am

    Mkuchika sweetheart plz rephrase your statement,i dont understand.

  19. Comment by man 0f peace on August 6th, 2008 12:06 pm

    I think the man has gone crazy, hivi yeye hajui uzalendo ni pamoja na kuupenda wimbon wa taifa!!!!
    Yaani hawa jamaa sijui wana akili gani? mi nadhani kabla ya kuteuliwa kwa m2 yoyote kuwa waziri au kiongozi, basi achunguzwe akili. Maana wengine inawezekana wana matatizo ya kiakili

  20. Comment by hombiz on August 6th, 2008 12:34 pm

    Mimi, mtanzania, malenga, wote kuleni tano toka kwangu. Hivi jina mkuchika lina maana gani!? Lazima maana yake ni mbovu sana kama linavyo-sound.

  21. Comment by monsa on August 6th, 2008 12:51 pm

    Naona sasa mawaziri wameishiwa, anatoka kwenye tv ,magezeti kupiga vita wimbo wa taifa usiwekwe kwenye simu je unatakiwa uwe wapi, maana serikali yenyewe inashindwa kufuatilia mambo muhimu mnafuatilia ring tone,vipi mbona uzungumzii ajira za watu unategemea vipi watu wanaishi maana wewe unamshahara na marupurupu kibao ndio maana unasema hivyo,kama hivyo ni marufuku kwa mawaziri kutumia magari ya serikali kwa shughuli binafsi na mambo mengine yasiyo ya kiserikali.

  22. Comment by BLACKMANNEN on August 6th, 2008 4:56 pm

    Waziri Mkuchika kachemsha sana katika swala la wimbo wa Taifa kuzuia usiimbwe katika simu za Watanzania walioko Tanzania. Hii inaonyesha ni kiasi gani Mawaziri wengine wasivyokuwa na upeo mpana wa mambo ya siasa. Kuzuia wananchi kuutumia wimbo wa Taifa katika simu zao kutasaidia nini katika Taifa la Tanzania? Je, hujafikiria kuwa, serikali inapoteza kiasi gani cha pesa za walipa kodi katika kuyatumia magari ya serikali kuwapeleka na kuwarudisha kutoka mashuleni watoto wa viongozi wa Taifa? Kwanini hilo hujalivalia njuga? Mh. Mkuchika kumbuka watanzania sio wanajeshi kama wewe, wanaopewa amri na kuzifuata hata kama hawzipendi kama majeshini ulikokuzoea wewe wanavyofanya. Wimbo wa Taifa utaendelea kuimbwa katika simu zetu kama kawa, ndani na nje ya Tanzania. Afande Mkuchika, kama umechoka kazi uraiani rudi ulikotoka bado kunakufaa! Huo ni ushauri wangu kwako.

    Blackmannen

  23. Comment by bigsex on August 6th, 2008 7:51 pm

    mie sina mambo mengi kazi yangu ni kuhit the point direct,kwanza kabisa napenda kuanza kwa kumwambia huyu mkuchika inaonekana hajajua njia ambazo zinaweza kuzipotezea heshima taifa la tanzania na hata kupoteza heshima yake kwenye jamii ya kimataifa,kwanza anieleze kuna jambo gani baya kuweka huu wimbo utumike kama ring tone?hapa hakuna ubaya wowote ni kutokana tu na viongozi wetu kama wewe ambao ni vichwa TIKITI MAJI badala ya kufikiria mambo ya msingi kama kupiga vita ufisadi unaoendelea kukua kama alkaida network unakuja kuzusha uzushia ambao hauna kichwa wala miguu wewe fanya mambo yenye maana hapa marekani bendera inatengeneza mpk chupi za wanawake na sidiria sasa sijui kama ingekuwa bongo ingekuwaje?acha uzushi bwana sawa wewe kama umeshindwa kazi tenguka aje mweingine

  24. Comment by anon on August 6th, 2008 9:32 pm

    hii nchi ndo maana nimeikimbia kwa upuuzi huu huu nashukuru mungu, viongozi wake vichwa maji vitu vingi wanavyoongea hawawezi kuvi-defend hata siku moja sijui alikuwa matingas au alitaka kuonyesha ubabe tu
    mi nimekata tamaa na hii nchi mlongo mzima karibia bado vilevile hakuna la maana lililobaki nilikuwa nasubiria dual citizenship ije ila haina maana ni upuuzi tu kesho asubuhi natuma fomu nibadilishe kabisa uraia
    pumba tupu

  25. Comment by kekue on August 7th, 2008 10:18 am

    Ss mkuchika inabidi kila kona uweke doria ili mtu ikisikika tu kaweka wimbo huo akamatwe, cjui utaweka kwenye kila daladala cjui bar anyway ndo ulivyoamua, sawa baba tufanyeje,

  26. Comment by binti-mzuri on August 7th, 2008 11:42 am

    hahaha Bablii kakangu kwa kupendaga visa,nimecheka posti namba 6 walahi!

    huyu waziri hakuwa na hoja,akaamua kubwabwaja..embu aongelee mambo mazito yanayoikabili wizara yake…asituzeveze saaizi…MI NTAUTUMIA

  27. Comment by Mimi on August 7th, 2008 4:03 pm

    wewe muhishimiwa umedata kuna mambo ya maana kupigia kelele na sio itikadi za kijamaa mi hata mkipiga huo mwimbo wenu mi sitasimama wima ni lipi la kujivunia na ufisadi na ufishenzi huu !

  28. Comment by neema on August 7th, 2008 8:50 pm

    oyah bwana mkubwa acha ushamba wewe tuliza ball wacha tujigode na wimbo wetu wa taifa…….

  29. Comment by Matty on August 8th, 2008 5:26 am

    Mr.politician tu huyu nae sijaona jipya hapa!

  30. Comment by pat on August 9th, 2008 4:58 am

    jamani waungwana wenzangu mie naungana na nyie wote hapo juu mlio mtoa maoni ni mazuri wenye hasira wameandika kwa hasira wenye kupooza wamepooza japo kidogo. maana mmemchambua kwa kwenda mbele.

    Swali langu ni jee? hizi comments zenu amezisoma au anazisomaga? maana kwa mtu mwenye ubongo wake kamili kama anazisoma, angeongea lakini kimya nyi mnazidi kumwashia moto tu huyo mzee ni wa kizamani km mchangiaji mmoja alisema zamani kwenye mlingoti wa bendera na minyororo ju.

    ni maoni tu waungwana.

  31. Comment by shafii on August 9th, 2008 9:22 am

    Huyu jamaa mshamba kweli…
    wenzetu wanajivunia kuweka nyimbo zao za taifa kwenye hata simu zinazotengenezwa katika viwanda vyao leo huyu jamaa anazuia kuweka wimbo kama ringtone.

    Huyu anazeeka vibaya au alikuwa anatafuta atoke vipi gazetini.

  32. Comment by KIPANGA on August 10th, 2008 5:38 pm

    KWELI AFRIKA ; VIONGOZI MACHIZI WAKO WENGI
    MUGABE TUNAMUONEA!

  33. Comment by maspidi on August 11th, 2008 6:07 am

    Kwanza hiyo instrumental yenyewe ya wimbo wa taifa ni ileile ya wimbo wa taifa la afrika ya kusini,je?Ilitungwa hata kabla Mandela hajafungwa jela na makaburu.Ni copy and paste tupu!Cha kujivunia hapo ni kipi?Asituyeyushe Mkuchika bora akapachike kwingine hapa kapotea njia au vipi?Kupenda sifa tu kwa jasho la wengine!Ring tone ya instrumental ina ubaya gani?Copyright ya hiyo instrumental anayo kwanza?

  34. Comment by MPIGANAJI on August 11th, 2008 11:05 am

    WIMBO WA TAIFA SAWA KABISA.JE? NINI HASA MAANA YA BENDERA YA TAIFA?

    MBONA INAKANYAGWA BUNGENI?

  35. Comment by Amina on September 24th, 2008 7:55 am

    mshamba nini huyu

Leave a Reply