Yapo mambo ya kijamii ambayo sisi sote tunatakiwa kuungana katika kuyapiga vita na kuyatokomeza kabisa.Mojawapo ya mambo hayo ni mauaji ya ma-albino au zeruzeru ambayo yamekuwa yakiendelea nchini Tanzania.Hali hii,ambayo sio tu inalitia aibu taifa letu ,ni ukosewaji mkubwa wa haki za binadamu.Kisa kikubwa inasemekana ni imani za kishirikina na kutafuta “utajiri” wa haraka.Hivi kwanini?Utajiri wa kumtoa roho mwenzako ni utajiri gani huo?Hebu itazame video hii hapo chini ujionee mwenyewe.
BC inaungana na kila mpenda haki katika kupinga hali hii.Shukrani msomaji na blogger mwenzetu Pius Mikongoti kwa video hii.
Feedback / Comments
19 Responses to “MAUAJI YA ALBINOS:KWANINI?”
Leave a Reply


Nilikuwa napitia jarida moja la washington post (online)
ambalo kwa upande moja liliniudhunisha pale mwandishi
alipokuwa anamuhoji mwanamziki Salif Keita kutoka
nchini Mali! ambaye ni zeru zeru(albino)
mwandishi alianza swali kwa kuhuliza Je? unajisikiaje
kuwa Zeru zeru? wakati nchini Tanzania kuna tabia ya
kuhuliwa watu kama nyinyi? aliendele kuandika kwa
kusema kuwa mwalimu moja kando ya ziwa Victoria nchini
Tanzania kamuhuwa mwanae kwa kuwa ni zeru zeru?!
Lakini nchi kama Mali inajivunia mtu kama wewe!
kwa kweli chanzo cha kichwa cha habari kama hiki
kiliniudhunisha sana!
Tabia za baadhi ya watu wanaofanya mauhaji kama hayo
inaonekana ndio desturi na utamaduni wa watanzania
wote
´KWELI INASIKIKITISHA SANA KWANI HAO NAO NI WATU NDUGU JAMAA NA MARAFIKI ZETU JAMANI MAANA AIBU HATA KUSEMA UNATOKA TANZANIA PICHA YA MUULIZAJI MPJA KWA MOJA INAPIGA UFISADI NA UUWAJI WA ALBINO.ZAMBI YAKE KALI SANA
HURUMA JAMANI UTAJILI GANI HUO HURUMA HURUMA
.Yataisha tu ni ukosefu wa elimu ndio unaosababisha ila siku hizi
karibu kila mtanzania anapata elimu ya msingi.
Inasikitisha sana jamani, Albino ni binadamu kama binadamu wengine kabisa kwani hakuna aliyependa kuzaliwa vile.
Watafutao utajiri kwa njia hizo za kuua Maalbino kwa kweli namuomba Mungu awalaani sana maana leo anauawa zeruzeru na muuaji anaweza baadae akazaa zeruzeru hapo je???atamuua???
Imani potofu na ushirikina ni vitu vibaya sana katika maisha jamani lazima tukubali…maana mtu unaweza jikuta unaua hata wazazi,watoto n.k kwa kutaka tu utajiri!
Mungu awasaidie maalbino wote jamani!
huu ni ukiukaji wa haki za binaadamu,inasikitisha na kutia aibu taifa letu la tanzania hasa kwenye nchi za kigeni,unapoangalia na kusoma vichwa vya habari na mahojiano dhidi ya kuuwawa kwa maalbino nchi tanzania..naona kila mmoja wetu itabidi kuwajibika na kulikemea swala hili wazi wazi bila kuoneana aibu,ni fedhea na ukatili usiostahika katika jamii yetu,serikali lazima ichukue hatua kali kwa yoyote yule aanayehusika au kukamatwa kwa kumua albino..hukumu yake lazima iwe ni kunyongwa,bila ya kujali ni nani au anawadhifa gani.
inasikitisha sana na hiyo yote inatokana na imani za kishirikina,sijui tutasemanje mbele za huyu Mungu aliyeziumba mbingu na nchi,kweli sijui.
mti mkavu #1 sio kuhua ni kuua halafu sio kuudhunisha ni kuhuzunisha,samahani usijisikie vibaya kwa kukurekebisha.
Afande Said Mwema bado unangoja nini? Taswira na sauti ya halisi ya mvuvi aliyetoa ushahidi kwenye hadhara kuwa anamjua mmoa wa hao wauwaji tayari unavyo bila gharama. Nadhani hata mzungumzaji wa A.Z media yuko tayari kushirikiana nawe ili mtu huyu aisaidie jamii yetu kupambana na hawa wanyama wanaouwa wenzie kwa sababu za kishirikina.
Pili akisha maliza kuisaidia polisi muleteni kwangu najitolea bure kumpa shule mwananana ili asiendelee kuwa na hizo hisia potofu kuwa baada ya kuuwa kweli mwenzake akawa tajiri! Je alifanya utafiti na akawa na sampuli dhibiti (control sample) kujua kuwa kweli kama asingeua asingekuwa tajiri au pia kwamba matokeo ya huo utafiti wake kama si suala la matukio mawili kukukutana kwa bahati (Not a replicable result).
Na je miji au nchi zisiokuwa na Albino kabisa hazina utajiri?
Binasfi nawataka sana watu kama huyu mvuvi niwashulishe maana yeye anajifanya kuwa hausiki na kuwaua Albino wakati wazi wazi anaendeleza ushawishi wenye tasnifu za kishirikina ambao hazina shule wala hekina wala maadili wala utu ambazo zinaweza kuchochea baadhi ya watu kuingia katika mauaji ya kimbari!
Kwakweli huu utajiri wa kuutafuta kwa njia ya kunyofoana roho, sijuwi una maana gani!. Hivi kwa nini watu wanakosa ubinaadamu kiasi hiki!? Watu hawa wameanza toka zamani. Mwanzoni kabisa walianza kuuwa watu wenye vipara.Kisha wakaja kwa watu wenye mwanya, then wakageukia vitoto vichanga, halafu kuchuna ngozi na sasa ma-albino. Huu wendawazimu sijuwi utaisha lini. Pendekezo langu mimi ni kwamba watu wa namna hii wanapokamatwa, wachukuliwe hatua kali sana ili iwe fundisho kwa wengine. Hukumu ya nafuu kabisa kwao ni kifungo cha maisha.
Hii link hapa chini pia inazungumzia mambo hayo ya mauwaji ya albino. It is very sad kwakweli!
http://www.studentpa.info/spip.php?article776
Hi guys, kutoka Helsinki-Finland
Kwa kweli haya mauaji ni ya kinyama sana, Mh. Rais Kikwete usihishie kuteua mbunge acha politics mwambie kamanda mwema kupitia hii YOU TUBE aende amkamate yule mvuvi maana anajulikana tiyari, Jamii pia hasa hasa mikoa ya kanda ya ziwa lazima ishirikishwe na Elimu itolewe, vipi NGOs wako wapi acheni kukimbilia pesa za ukimwi ebu jamani angalieni na haya mauaji TAMWA, HALI ELIMU, KITUO CHA HAKI ZA BINADAMU na wengine mbona mpo kimya wala hata kwenye vyombo vya habari hatuwasikii, tunasikia habari za ufisadi tu, Please wake up, ninauomba uongozi wa Bongo Celebrity ebu waamusheni, sisi wengine tupo mbali ingawa ni wanaharakati.
Saidi Situ ndugu yangu, unadhani wote wanaofanya hayo mambo hawakupita Shule ya Msingi? Watu siku hizi wamekosa utu. Same way jambazi anavyokuua ili apate mali yako; hawa wanaofanya hivi wanajua watapata hela either kwa kuuza parts za Maalbino; au kwa kuzitumia wenyewe katika imani za kishirikina. Kuamini ushirikina sio kukosa elimu ya msingi, ni tatizo la kutaka shortcut ya maisha. Mbona “wasomi” wanatumia juju kutafuta ushindi katika siasa, vyeo makazini, etc.
Suala la mauaji ya albino kwakweli inasikitisha sana kwani wao ni binadamu km wengine ni mambo ya rangi tu.
Saidi situ nakubaliana nawe kwa kiasi fulani kuwa ukosefu wa elimu unachangia hali hii kwani naamini upeo wa watu wengi wanaojishughulisha na laana hii ni mbumbumbu. Lakini hata hvyo, namuunga mkono Nalitolela, p.s. pia. Kwa watu wengine swala la ushirikina imekuwa ni kama utamaduni. Kuna watu ambao wamesoma na wana P.H.D za mauala mbali mbali lakini wanaamini ushirikina kwa kiasi kikubwa mno. Misikitini wanakwenda, kanisani wanakwenda, jamatini wanakwenda, “wherever religions they believe in”, still they believe in witchcraft! It is a shame!. Bwana Saidi Situ, usije kushangaa itakapobainika kuwa mmoja wa wauwaji wa albino ni kigogo anayewania ngazi fulani ya uongozi serikalini. Vile vile sitashangaa nikisikia mbumbumbu fulani kauwa albino ili apate utajiri wa haraka.
Cha msingi ni kuimarisha vita dhidi ya imani hii potofu, ili hawa binaadamu wenzitu waweze kuishi kwa amani na tusaidiane pamoja ktk kulisukuma hili gurudumu la maisha mbele.
Huyo jamaa aliyetoa ushaidi hapo (mvuvi) anatakiwa abanwe ili amtaje huyo rafiki yake aliyeuwa huyo binti na asifungwe wala nini bali ahukumiwa kifo moja kwa moja, nyoka wa zamani hawa.
Jamani hii ni habari ya kusikitisha sana. How on earth can this happen in Tanzania. Rais Kikwete has to do something right now!!! – people do not kill a fellow human being because of their colors’ appearance, it is barbaric to do that…these people need to be brought to justice. I am getting really sick to my stomach right now. ……oh my goodness, i am so saddened by this…….Haya mambo ya witch craft should be banned in Tanzania.
mmmh nalitolela tunakuzimia…umesema pointi.mi nishasikia haaadi viongozi wa juu serikalini ambao wanaenda kwa karumanzira..
This is a terrible thing. I can only pray that these people be brought to justice who are doing this to the albinos.
It’s a strange thing to even think that an albino brings luck and money if you kill one, or bring some albino hair with you when you are fishing or whatever……! A sick thing to think that is!
What about blondes then? They have even more shiny hair! Så you have to take some scandinavians 2!
Djiiiiz….. Open you eyes up.
You create you own happines, not by taking other lifes.
What goes around, comes around! REMEMBER that!!!
And by the way… We live in 2008 now!
It’s not the stoneage!
Pole sana! What this tells me is the dire need for better international eduacation everywhere. Only with education will they cease to believe in things like witchcraft. I hope in the future there can be opportunities for them to see other views that will give them hope and replace their need to obtain it in ways that don’t exploite or harm any livinig thing.
Yaskitisha sana kuona watu wetu Afrika wako nyuma. Ila nalaumu sana serilkali zetu za kubali watuwetu wae na huu unyuma wakati huu.Haya maboyauchawi yange kua mambo tunasikia kwenye hadithi tuna simuliwa na bibi zetu.
Viungozi amkeni tuaelimushe watu wakwetu. Wawo ndio watuokoa tuki wasomesha haya mambo ya wachawi kumaliza zeru zeru kwa sababu ya umaskini hayange kuoko.
Jamani SERIKALI okoa watu wetu wa Afrika na tena waduniani.