Kwa wengi siku hizi anajulikana kama Binamu.Lakini alipoingia rasmi kwenye ulimwengu wa muziki aliitwa MwanaFalsafa.Jina lake kamili ni Hamisi Mwinjuma(pichani).Ni mshindi wa tuzo maarufu za Kili.
Tangu aingie kwenye fani ya muziki,sifa moja ambayo amekuwa nayo ni kuwa na mashairi au lyrics kali. Ilikuwa ni lazima uwe na uelewa mzuri wa lugha ya Kiswahili ili upate maana halisi ya nyimbo zake.Uwezo wake wa kwenda sambamba na mapigo (beats) za kimuziki huku akighani ipasavyo mashairi yake ni jambo linguine lililomfanya awe mmoja miongoni mwa wanamuziki wa B Flava wenye mashabiki lukuki..
Hivi karibuni MwanaFA amezindua tovuti yake rasmi.BC tulipata nafasi ya kufanya naye mahojiano kuhusiana na ujio wa tovuti hiyo,muziki wake,mipango yake ya baadaye na mengineyo mengi.Kwanini ameiita tovuti yake binamu13.com? Ana mipango gani katika miaka mitano ijayo? Anasemaje kuhusu ujio wa mwanamuziki 50 Cent nchini Tanzania hivi karibuni?Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;
BC: Kwanza hongera sana kwa kuzindua tovuti yako rasmi hivi karibuni. Pia pongezi nyingi kwa mafanikio ambayo umeyapata tangu uanze kazi za muziki.Mambo yanakwendaje?
MwanaFA:Thanx a lot cuz…Mungu anasaidia sana juhudi zangu zinatoa mwanga wa mafanikio!Nazingatia sana nguvu zake kwenye kila ninachofanya.Najua kila kitu kilishapangwa naye hata kabla sijazaliwa na ninachofanya ni kufumbua mafumbo aliyoniwekea kupata niliyopangiwa kuyapata humu kunako dunia yake.
Mambo kama kawa ndugu yangu…
Labda kabla hatujaenda mbele sana naomba nimpe pongezi na shukrani zangu za dhati my boy Ahmed Babajide kwa kuweza kufanikisha kuwepo kwa tovuti hii.Mungu ataifanya kazi yako yenye thamani siku za karibuni Ahmed.Thanx a lot.
BC: Jambo la kwanza ambalo tumeliona pindi tulipopata habari kuhusu ujio wa tovuti yako rasmi ni kwamba tovuti yako umeiita binamu13.com.Wengi tunafahamu kuhusu jina Binamu lakini hatujui kuhusu namba 13.Unaweza kutuambia namba 13 inamaanisha nini?
MwanaFA: 13 is my birthdate..March 13th!I am a Pieces,like Osama,MethodMan and many others…hahahaha..and I’ve been using the name binamu 13 sehemu kadhaa kwa muda sasa!sikiliza tena intro ya ‘hawajui’ utanifahamu…
BC: Mara nyingi mtu anapoamua kuanzisha tovuti yake anakuwa na malengo fulani maalumu.Kwa msanii kama wewe lengo mojawapo la wazi ni kutumia tovuti yako kujitangaza na kuwasiliana kirahisi na mashabiki wako wenye uwezo wa kutembelea mtandao.Mbali na lengo kama hilo,unategemea kupata nini zaidi kutokana na kuwa na tovuti yako mwenyewe/rasmi?
MwanaFA: Sababu za wazi kabisa baada ya hizo ulizoziorodhesha awali ni kujaribu kuitumia kutafuta njia za kufanya biashara ipanuke.Kwa ulimwengu tulionao watu wengi zaidi wanaweza kukufikia kupitia mitandao kuliko sehemu nyingi nyingine,hasa walio mbali sana na Africa nilipo.Nikijaribu kuwa realistic,hakuna namna msanii wa uzito wangu ataeleweka bila ya kuwa na tovuti.Muda wa mimi kuwa na tovuti yangu rasmi ulishafika.
BC: Kwa kiasi kikubwa tovuti yako imeandikwa katika lugha ya kiingereza kitu ambacho kwa kiasi fulani kinamnyima mshabiki wako asiyefahamu kiingereza nafasi ya kuitembelea na kuifurahia kama sio kusoma yaliyomo.Unaweza kutuambia kidogo kwanini sehemu kubwa umeiweka katika kiingereza?
MwanaFA: Aaamh…kama nilivyosema katika swali lililopita,nalazimika kuwa karibu wa wapenzi wa kazi zangu,HASA WALIO MBALI NA NILIPO.Wengi wanaofahamu Kiswahili tu na sio kiingereza kilichotumika sana kwenye tovuti yangu wapo nilipo…Africa,na hasa Tanzania ambako wana namna nyingine lukuki za kupata habari za maendeleo ya kazi yangu kirahisi.Simaanishi hawatakuwa na nafasi ya kujua kupitia tovuti,no..kadri tunavyoendelea tutakuwa tukijaribu kumfanya kila mmoja ajisikie nyumbani kuipitia…kila mmoja ni binamu yangu!

Binamu a.k.a MwanaFA akiwapa ladha murua mashabiki wake,mashabiki wa muziki wa kizazi kipya hivi karibuni.
BC: Mashairi au lyrics za nyimbo zako, matumizi ya lugha ya Kiswahili ni mambo ambayo yanavutia sana wapenzi wa muziki kiasi kwamba wengine wamewahi kutania kwamba huenda kila unapokwenda huwa huiachi nyuma kamusi ya Kiswahili.Kuna ukweli wowote katika hilo? Je unadhani lugha ya Kiswahili ina nafasi gani kimataifa kupitia muziki?
MwanaFA: Hahahahahaa…sina hata kamusi yenyewe mpwa!Nalichukulia hilo kama compliment anyway!..ukijaribu kuangalia kazi zangu za karibuni nimejaribu sana kurahisisha Kiswahili ninachokitumia ili kuondoa matatizo ya watu kutafuta kamusi ili waelewe nimesema nini…muziki tunaofanya yafaa uwe wa kumpumzisha mtu na sio kumuongezea mzigo wa mawazo..najua unanielewa kama uliwahi kuwa Africa.
Nafasi ya lugha ya Kiswahili sio kubwa kwenye muziki wa kimataifa kwa kweli.Lakini muziki pia unaweza kutumika kukitangaza Kiswahili chenyewe kama utafanywa katika viwango vya kimataifa.Bado tunajaribu kuutoa huu muziki na Kiswahili kwa wakati mmoja.Hakuna namna tutashindana na kina Jay Z kufanya muziki mzuri kwa lugha yao.,so we better stick to ours!

MwanaFA(kulia) akiwa na mshirika wako wa karibu,nyota mwingine wa muziki wa kizazi kipya, Ambwene Yesaya au AY.Kwa pamoja hivi karibuni walitoka na kitu,Habari Ndiyo Hiyo.
BC: Tanzania hivi karibuni imekuwa ikipata bahati ya kutembelewa na wanamuziki mashuhuri kutoka nje na hususani Marekani. Hivi karibuni mwanamuziki 50 Cent na kundi lake la G-Unit walikuwepo nchini Tanzania na wewe ulikuwa mmojawapo miongoni mwa wahudhuriaji.Unadhani ziara kama zile zinawasaidia ninyi wanamuziki wa kizazi kipya kwa namna yoyote ile?Kwa maneno mengine tunaweza kusema kuna mambo yoyote ya msingi ambayo mnajifunza kutoka kwao?
MwanaFA: Yeah,kiaina..Japo kitu haswa tunachoweza faidika nacho toka kwao ni kupata exposure.Nadhani waandaaji wa hayo matamasha wangekuwa wanajaribu kufanya utaratibu wa kutuunganisha nao kufanya kazi za pamoja.Naamini tutatangazika mno kwa mtindo huo!Imagine ujio wa Akon mathalan,angeweza fanya wimbo japo mmoja na msanii wa ‘bongo’,ingekuwa ni hatua ndefu ajabu…sawa 50 is expensive and all,hatuwezi mshawishi hata atupe Lloyd Banks ama Yayo afanye a single verse kwenye wimbo mmoja wa kibongo kweli?lol!Yafaa tuwashawishi watusaidie kujaribu kuuvusha muziki wetu.
BC: Ukitizama mbele kiasi,tuseme kama miaka kumi ijayo hivi,unadhani muziki wa kizazi kipya utakuwa wapi? Na wewe mwenyewe nini malengo yako katika miaka hiyo kumi ijayo?
MwanaFA: Well,sina uwezo wa kuona sana mbali hivyo,ila kama kila kitu kitakuwa kwenye reli za juhudi zetu pengine tutakuwa kwenye nafasi ambayo raggatone ipo sasa…tuombe na kuwajibika!
Binafsi najaribu kujijenga vizuri nisishindwe japo kukumbukwa baada ya kuachana na muziki na pia nisitetereshwe na maisha pindi ujana utakapokwisha.Nafahamu sitaweza kufanya ninachokifanya milele hivyo najiandaa.I realy do,na namuomba Mungu sana anisaidie niweze fikia ama kuvuka malengo.
BC: Mwisho ungependa kuwaambia nini mashabiki wako,mashabiki wa muziki wa kizazi kipya?
MwanaFA: They should keep faith in me and I’ll never let them down.
Tembelea tovuti ya MwanaFA kwa kubonyeza hapa.
Feedback / Comments
71 Responses to “NI BINAMU13.COM”
Leave a Reply


Real hard worker young man. Kabla ya kujulikana kwenye dunia ya hip hop kijana alikuwa matata sana, lakini badaa ya kujulikana kwenye ramani ya bongo flava, things has change. MwanFa displine yako ipo juu
Big up
Kutoka kwa black skin fan#1
NAMPENDA SANA HUYU KAKA.. AMESIMAMA KIMISTARI…KILA LA KHERI
Unapotaja wasanii bora, sio bora wasanii wa muziki wa kizazi kipya bila kuweka jina la Mwana Fa utakuwa “unakufuru”.
Ni msanii anaejuwa muzuki unakuwaje, sio kupiga kelele tu!
Ana vitu vyote muhimu katika muziki; Anatunga mashairi yenye maana, yenye vina, lugha fasaha ya kiswahili na vionjo vyake, anajuwa kutofautisha L na R kimatamshi, anajuwa kupangilia beti za wimbo wake, ana style mzuri ya kufikisha ujumbe wake, anasauti ya kisanii, anajuwa “kufloo” na mistari, ana “personality “mzuri.
Zaidi ya yote anauwezo wa kutunga na kuimba nyimbo za aina zote kama vile mapenzi, maadili n.k
La mwisho na muhimu kwa msanii, huyu jamaa ni “very
cooperative”
Wanamuziki wengine wachache waliopo kwenye hadhi yake ni Pof J na na FidQ ( Ila huyu hana personalty)
BABLII I AGREE TOTALLY!!!..MANENO YA WAZI TENA YENYE BUSARA..MMH..WANIPA SHAUKU,NA WEWE NI MWANA-UNDERGROUND MUSICIAN NINI!?..ILA HUYO FID Q NI MTU WA BIFU SANA AISEE,JAPO NAE ANAJUA KURAP,ILA NI MTU WA KUTAKA KUCOMPARE SANA NA MTU WA COMPETITION MFANO MZURI NI NYIMBO ZAKE MWENYEWE AMBAZO ALIMSEMA SOGGY DOGGY NA MFALME SELE
Hata mimi namfagilia sana Binamu. Na naungana na Bablii kuwa wanamuziku wengine kama mwanaFA ni Prof J n.k.Nyimbo zao hazichuji kirahisi.
Binam kazi nzuri zaidi ya sana mchumba nakukata dau ile mbaya.
NASIKIA HARUFU YA ANKALA
HIVI NASIKIA ETI HELO NENO LA HABARI NDIO HIYO LILIKUWA LA Q CHILLAH KWA HIYO HAWA WAMEEGEZA ALILI2MIA KWENYE WIMBO WA WANAUME GANI SIJUI ALISHILIKISHWA KABLA YA WIMBO WA DAR MBAKA MORO MWISHO WA WIMBO HUO QCHILLAH ANAMALIZIA NA KUSEMA HABARI NDIO HIYO
ILA BINAMU NA MWENZIO AY MKO JUU SANA NA WIMBO WENU HUO HABARI NDIO HIYO.
MICHANO HIYO MWANANGU.
you rock meeeen, kweli we unaendana na jina lako mwanafalsafa kwa sababu unaitumia lugha(kiswahili)vilivyo, bi up and keep doing!!!!!!!!!
“Lakini Alikufa kwa Ngoma”
Of all the best Kiswahili hip hop songs, the above titled one will always remain #1 on my best list.
Personally, I have known MwanaFA back in all good days when I was busy and serious with Dolph Mobb, a HipHop Crew. Cuz had alot of dreams wit muzic and he was good in putting the rhymes on top of our headz.
To date, he still got that click and remains to be my #1 MC with lyrics, flow, personality, name it all!!
U r the man Cuz!!
kwani nani anamuandikia lyrics mwanafalsafa?ni swali..cause i have heard otherwise
Binamu upo juu sana, hongera mzee! Ushauri wa bure: Tovuti yako ni nzuri lakini naomba ujitahidi kuweka “UPDATES” kila mara, kwani vi-tovuti vingi vya kibongo vinaboa, mambo ni yale yale tu kila siku yaani, “leo ni kama jana”
MCeez wa Bongo wengi mnafanya kazi nzuri lakini bado kilio changu ni kwa Ma-prodyuza, beat hafifu sana, muziki hauchezeki!
Binamu upo juu sana hongera mzeya,All the best kiswahili hip hop songs.
B upo juu ile mbaya mtu mzima thanks kwa kutupa raha mafansi wako ohooooooooo mzukaaaaaaaaaaaaaa h ndio hiyo.
habari ndo iyoooooooooooooooooooooooooooooooooo big up ma brozzzzzzzzzzzzzz
your real gud men,keep it up binam……Habari ndiyo hiyo
no comment
Mwanangu B nimekusoma vizuri tangu ingekuwa vipi,aina noma mtu wangu,kaza kamba kwani wasanii wanaotaka kukushusha wapo wengi.
Niga hiyo imetulia,hasa ktk lile la nangoja ageuke.Yaani kwa jinsi mistari ilivyo mitamu,anaweza ageuke alafu wazungu hawaaaaaaaa.
Mzukaaaaaaa
Hey MwanaFA. Congrats Cousin. You are doing a great job. I always like your tracks. I really like your style. It really shows that you think twice before realising your work. Keep it up.
Have given a listen to bado nipo nipo kwanza. Waoh! it is really a touching number. It is really nice and I think it teaches a lot.
Congrats once again. Keep on keeping up binamu.
ebanaee, nakupa big up sana mtu wangu,nafagilia kazi zako zote mkubwa,kuhusu kuibuka kwenye video mi nahisi bado nipo nipo,sababu sija pata mwaliko toka kwako binafsi,lakini video zingine tuambiane bana au sio
Bado niponipo mwana,
ni balaa mzeya unatisha inajulikana kuwa we kwa mabinti (wanadafada) usahauliwe lakini sio kuoa. we ni mkali kiujumla kula zangu kwako zipo nyingi sana.
hongeara sana binamu,we luv yaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
aah unanitega
Oyamjomba big up sana nakuku bali alafu tume fanana kama ndugu kaza buti mjobma
Ebwana ukoo juuile kinyama nimimi pacha wako mbona amji kulakiti moto hapa legho Ebwana kazeni Buti unakiswahili ambacho akiso meki
Mwaaaaaaaah FA
mmh!
big up ila punguza pozzzzzzzzzz!!!!!!!!
watu bwana,katika wasanii wa bongo wanao jua umuhimu wa elimu wewe ni mmoja wapo,nashukuru sana kaka kwa kwenda shule itakusaidia sana cz muziki wa bongo unahitaji zaidi ya kipaji,unahitaji elimu na unahitaji mtu uwe unaangalia mbali na sio hapo ulipo.hongera kwa kazi zako nzuri.kua smati siku zote,usijione wewe ndo wewe,jiheshimu,kua msikilizaji kuliko muongeaji,mkumbuke MUUMBA wako siku zote na usikome kumsifu kwa anayokujaalia.thanx bro
Binamu, u been the mastermind in Game since way bak. . .yo stil doin it tight man! Salute u Godfather, the Don himself!
Kip it rockin!
mzee wa falsafa nimekukubali sanaaaaaaa
e bwanaaee siunacheki mipasuo ndo nyimbo nilioikubali ile mbaya kaza msuli kaka achana na wazushi kaka
oya mwana fa,mi nakukubali sana na nayafahamu mambo ya mziki kiasi fulani.usimjibu inspectar haroun,kwa ngoma yake bado upo upo,atajikukuta fala.anatafuta fame kwa kutumia beef.let him be creative.
mwangu hakuna kama wewe DUINIANI hamini hilo mkubwa ila maoni yangu me naona ka vp ungefanya kolabo na m2 mzimz CHID BEENZ me naimanji litakuwa kolabo la mwaka huu.
hongera sana mkaka,kaza buti game ni gumu
wagomba naomba mpokee salam kutoka kwa IGA UFE GROUP LILILOPO MJINI KIGOMA .
ZA KWANZA NI KUTOKA KWA,
1..OMARI HAMISI ALIYOPO ITALIA.
2..MASTER VOICE A.K.A MWALAMI
3..KILULA ISSA
4..MICHAEL MBALE A.K.A CHIEF
5..OMARI DAUDI A.K.A LG
mi nakupa big up sanaaa wangu,unaona mbali kuliko darubini mtuwangu,elimu ndio ngao mwana,najua unalifahamu hilo.nakutakia masomo mema na usikate tamaa,we piga shule,utafanikiwa saana tu,lazima tukuite babu haha.say hi haters,do u see mi nw??waachie vumbi tu kama vipi.watabaki kukuangalia hawawezi kukufikia.good luck man.
waooooooooooooooo! I like this Guy anajua anachofanya Bigg up sana, zuri zaidi umejiendeleza kielimu tht very proud of you. Pambanaaa umewashika mjombaaaa
BIg up sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
big up mtu mzima mimi niko Burundi alafu najiskia kama one day ningefika bongo alafu nikapata bahati japo ya kukutana nawewe japo mi simwanaziki ila mshabiki wa mziki FA upo juuuuuuu zaidi.
Yeah!!!!!!!!M2 mzima umecmama ile mbaya kwenye Track ya NAONGEA na WEWE big up BINAMU
braza yuko juu zaidi ya mvua big sana collabo lako na ay ni la akili. an advise mweke mtu mzimw FID Q nazani itaakua poa zaidi.
hi wazee mambo vipi?????????????????????????
MZEYAAA FA UKO JUU KAMA JANI LA NAZI
Kijana kazi yako ni nzuri sana.Hongera
EBANA MNASOMEKA ILE MBAYA 4SURE HAMNA WAPINZANI HATA MACHIZI WANGU WA IGEGU WANALIJUA HILO AMANI SANAAAAAAAAAA
OYA WA2 WANGU C O CRI HAMNA WAPINZANI !!!!!!!!!!! HUKU KITAAANI KWANGU MNAKUBALIKA C MCHEEEZOOOO MC LEMBE KAZENI BUTI MAJITA .
nampenda sana yuko juu kimziki kaza buti mkubwa
nakufell sana kaka yangu. dont ever look back.be blssed
upo juu kama hawataki kukubali bac wao wanga ila we ndo king wetu hapa Bongo
kaka imekaaa sawa luv much broo!!!!!rspect
name MwanaFA populah known is what gives the man a boost man keep flying He is got the lyrics but mon! AY iz comin afta ya
Hala.
yap am proud of you nigger you got fantastic lyrics.keep it to maintain your flow in music industry.
heheeeeeeeeeeeeeee,uko vizuri,ushuki unapanda,safi kwa kujari kazi.we mkari achana na hawa wanao jiita wakari wakati si wakari,na bado adi nauri watakuja kukuomba,mungu akuzidishie ila ndoa muhimu
BIG UP BINAMU,YAANI SHWARI,I FEEL YOU MAN.JUST GET BUSY!EVERY BODY KNOWS THAT DIAMOND IS VERY WORTHY BUT NORMALY IS BEING SHARPENED UP TO BE MORE ATTRACTIVE AND WEALTH.UKO SO TALENTED NA BADO UNAJIENDELEZA, HAUBWETEKI NA SIFA UNAZOZIPATA. IT IS AWESOME!YOU CAN BE NUMBER ONE,BUT CAN YOU STAY NUMBER ONE? UKO JUU,BIG UP
yaaaah man!!!ni kwel “HAWAJUI”bt watajuwa…..imetulia hiyo!respect!!!!!!!!!!!!!!!!!
big up binamu tuko pamojasana
Nyimbo zako zimebeba ujumbe na zinaburudisha, nadhani hiyo ndiyo tofauti baina yako na wasanii wenzako wa Bongo Fleva.Kaza buti usibweteke.
he bwane mwana FA huko juu.da realy HIP HOP unaiweza coz hip hop ujumbe sio majigambo tu.coz single yako ya utaoa lini man imenibamba ile mbaya coz umenifanya nisiwe na mpango wa kuoa.
Big brothers ********* wewe ni kweli sio bongo fleva … wewe ni mzee wa bongo fleva toka nimeanza kusikia album yako ya kwanza mwanafalsafani … basi mpaka leo bado unazidi kupanda kwenye falsafa yenyewe
( BIG UP BROTHER )
lakini samahani mwenzako nimeshapata mchumba na tayari nimetuma posa … sasa wimbo wako huu 2009 wa kuhusu lini utaoa ?? umeniweka pabaya sijui nifanye nini ?? maana naona kama yatanishinda …
kaza buti bwa mkubwa
HANA MAKUU, KILA MTU NI RAFIKI YAKE
big up sana kaka fa ucchoke kutupa burudani bila kusahau shule m2 wng
AAh!babu mshikaji yupo juu na inabidi wasanii wengine wafate na kufanya mawonders kama jamaa yaan yupo juu kinoma na me nafeel sana slogan anazopenda kutumia kwenye mashairi yake au sio,wewe ni mkali babu
big up man kip it up!
Hallow FA U LOOK SO GOOD AND AM APPLICIATE U AND UR WORK BIG U BRO,DONT LOOSE UR TITTLE CAUSE AT DIS TIME UR IN HIGH POSION,SO GOOD LUCK MA BRO.
YAP BRO CAN U TELL ME WAT IS ZE SECRET OF UR SUCESS CAUSE AS U KNOW 4 DIT TIME ZE GAME IZ SO TAF,ALSO N` UR AMBITION,OKEY BRO I WISHING U ALL DA BEST IN DA GAME AND LIFE
jamaa yuko juu anajua kujieleza
Big up m2 mzima, mpango mzima
respect! mwana FA
MWANA FA WE MKALI KISOOOO C KWA MASHAIRI,SAUTI,KUNATA NA BITI,NA VIONJO VINGINE KIMUZIKI.MI KAMA SHABIKI WAKO NAKUPA BIG UP KAZA BUTI GEMU TAIT KIVILEEEE!MZUXXXXXX!!!
UPO JUU BINAMU NO COMMENT!!!!!!!!!!!!!
NISEMEME NINI BINAMU ILA KUKUPA HONGERA KWA KAZI YAKO MUFTI.UNA MISTARI SANA HASA KWA WIMBO WAKO BADO NIPO NIPO.KONGOLE!!!
upo juu kama kaka mtu akijaribu kukufwata lazima avunjike guu