MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

Sio lazima uwe mtu wa makamo ili kuwa mwanasiasa. Ukweli katika hilo unaweza kuuthibitisha kwa kutizama jinsi ambavyo baadhi ya vijana wanakuwa wamejikita katika siasa. Miongoni mwa vijana hao wanasiasa nchini Tanzania ni John Mnyika(pichani) ambaye ni Mkurugenzi wa Vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA).John Mnyika alizaliwa tarehe 21 August mwaka 1980 jijini Dar-es-salaam.Kwa habari zaidi kumhusu John Mnyika,bonyeza hapa.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

40 Responses to “KIJANA MWANASIASA,JOHN MNYIKA”

  1. Comment by mnaku on May 6th, 2008 4:10 am

    Ni moja ya vijana washupavu na wapigania haki ambao Tanzania imejaaliwa kuwa nao.Vision yake kisiasa ni kuhakikisha kuwa watanzania wanapata uhuru wa kweli na maendeleo yanayoonekana kiuhalisia,siyo yale yanayohubiriwa majukwaani kwa takwimu na waliopo madarakani sasa. Najivunia kuwa na John Mnyika na watanzaia wakiamka na kuujua ukweli,watawaunga mkono vijana kama yeye na hapo ndipo uhuru wa kweli utakapopatikana,na huo ukipatikana maendeleo ya kweli yataonekana kwa watanzania wote,wawe wa vijijini,manzese, na sehemu kama hizo ambazo kiuhalisia kwa sasa, these places are so marginalised

  2. Comment by Amina on May 6th, 2008 9:21 am

    hilo shati kapewa na bosi wake mbowe…ila ni handsome ameoa?

  3. Comment by Chris on May 6th, 2008 11:15 am

    Mshikaji namkubali, ni kichwa! Alituongoza Dar mtihani wa kumaliza la saba nakumbuka… Binafsi kwa ninavyomjua, angefaa zaidi kama angeji-involve kwenye kazi za utendaji zaidi kuliko siasa! Anyway kila mtu ana-aspirations zake…

  4. Comment by Bablii on May 6th, 2008 11:35 am

    Mhh! wabongo twapenda kujisifia kwa sifa nzuri, lakini ni wepesi wa kuficha mule tulimoteleza!

    Bwana Manyika kajitahidi kutuonesha matokeo yake ya form four, tena kwa ufafanuzi wa hali ya juu, katumia lugha zote 2 kiingereza na kiswahili, ilimradi watu waelewe ” amefaulu kwa daraja la kwanza nukta saba, yaani division one points seven, akiwa na alama A tisa …” Tena hiyo A imekuwa bold.

    Lakini chakusikitisha nikiwa na hamu yakutaka kujuwa na matokeo yake ya form six, hakuthubutu kuyataja, zaidi yakuambiwa baada ya kumaliza form six alijiunga na chuo cha diplomasia cha jijini Dar es salaam katika kozi ya itifaki na mahusiano ya jamii, kisha akajiunga na masomo ya jioni pale udsm.

    Jamani tukiamuwa kujisifia mafanikio, basi pia tuoneshe na madhaifu tuliyopitia, ni sehemu ya mafundisho kwa wengine!

  5. Comment by zachariah on May 6th, 2008 12:47 pm

    hamna ki2 hapa wakuu

  6. Comment by Gervas on May 6th, 2008 1:44 pm

    Kweli Bablii nakuunga mguu.

  7. Comment by tish on May 6th, 2008 3:17 pm

    ua so handsome young man hope ua single 4me kila la kheri na kazi njema

  8. Comment by Tanzanian Female on May 6th, 2008 6:49 pm

    Bablii,
    We upo dunia ipi? Mtu hutakiwi ku-emphasize kwenye mabaya rather mazuri. But then again, maybe you’ve never even had a CV. Otherwise you are hating on the young man because you are bitter probably much older and havent accomplished anything. Wabongo hii tabia mbaya muache.

  9. Comment by Lizzy on May 7th, 2008 3:53 am

    Kijana anaonekana ni mwenye Akili nzuri tu kitu ulichoniangusha u have wested ur time kutoendelea vizuri na shule kutokana na majibu yako ya mtihani nadhani ulikuwa na nafasi ya juu sana kielimu sio kuishia au kupoteza muda kwasasa .watu kama hawa ni rahisi sana kuwa ma academic doctors na hivi bado umri unakuruhusu please consider this .juzi nilikuwa nasoma habari za msichana mmoja marekani at the age of 18 amekuwa professor na ndio mwenye umri mdogo kuliko prof yeyote hapa duniani kwasasa lakini issue yake yeye tofauti walimrusha sana madarasa alianza kusoma akiwa na 8 month .vipaji pia tunavyo bongo

    Lizzy

  10. Comment by Lizzy on May 7th, 2008 3:55 am

    I mean kusoma vitabu na maandishi na umri wa miezi 8 sio kuattend shule please dont court me wrong

  11. Comment by Bablii on May 7th, 2008 4:06 am

    Tanzania female,

    I never argue with a woman…!

  12. Comment by mazagazaga on May 7th, 2008 6:09 am

    Keep it up Boy!I know the going may be rough but so what?Umejitumbukiza katika siasa mapema sana kwa hiyo jifunze kisha kamilisha ndoto zako.Nilikuwepo pale DSM maeneo ya Ubungo wakati ule ukigombea ubunge katika jimbo lile.Nilifanya ushushushu wangu nikagundua yule Mze wa chama si unakijua(?), ulimshinda kwa mbali katika kura lakini WIZI WA KURA mdogo wangu ulikuangusha!Watu wa jimbo lako walikukubali.Usikate tamaa.Iko siku utaibuka kidedea.Tunalaumu kwa wenzetu tu lakini hapa kwetu mijitu haina hata haya macho makavu mtu anajisifu kashinda uchaguzi,kumbe kwa kura za wizi!Watanzania safari hii lazima MKOMAE NAO.Kila mtu avune alichopanda!Combat naliona mshikaji wangu!Lina promote Sera au siyo?

  13. Comment by Edwin Ndaki on May 7th, 2008 7:37 am

    Mnyika binafsi bila kujali itikadi za chama naamini ni mfano mzuri na unatuwakilisha vema vijana.

    Najua kama wasingekufanyi “mauza uza ” kama ya kenya au zimbabwe leo hii ungekuwa mh wa jimbo la UBUNGO.

    Tutafika tu.

  14. Comment by ma'reen on May 7th, 2008 10:10 am

    Bablii,
    Watch your mouth you excuse of a man! You never argue with a woman HUGH!? Uko dunia gani, unafanya kazi gani, umesoma wapi na umekulia katika mazingira ngani? Ninachomaanisha ni kwamba ungebahatika kumaliza japo primary school, kufanya kazi na watu wa jinsia tofauti zaidi ya hiyo unayofanya ya kuuza madafu, kukulia katika jamii ya watu waliopanuka mawazo, ungeona upeo na mawazo ya manawake na usingekuwa bado una mawazo finyu kama ya sisimizi! Inasikitisha kwamba katika dunia ya sasa hivi bado kuna watu wawazao kama wewe. Nilikua na hasira ila zimesha, nakuonea huruma sana, wewe na kila kiumbe wa kike aliye na uhusiano wowote na wewe, maana u mzigo mkubwa kwa jamii inayokuzunguuka. YOU ARE A LIVING SHAME TO ALL MEN!

  15. Comment by Gervas on May 7th, 2008 11:31 am

    Kijana anaonekana anapenda sifa, na kuna watu wanamdanganya nyuma yake. Alipaswa ashauliwe akazanie shule kwa umri huu alionao, kwani shule aliyonayo saizi mbado ndogo kwa mwanasiasa wa karne ya 21. Tanzania na dunia inabadilika, watu wanaelimika kama mwanasiasa unatakiwa umwage sera ambazo utakubalika sio kama siasa za zamani za kupayuka na kushangiliwa tu. Unamuona Zito kabwe amefocus mbele, hapo alipo hagombei ubunge next term, anataka akapasue kitabu zaidi. Hivo Bwana Mdogo Mnyika anakipaji cha kuongea basi akikoleze na kitabu na asipende visifa vya watu saizi.

  16. Comment by DUNDA GALDEN on May 7th, 2008 12:46 pm

    Ndugu wabongo wenzangu kama mtu anaouwezo au kipaji tujaribu kumpa sapoti ya kuendelea mbele si kumvunja nguvu au ndio tushabweteka na imanai zetu zile za kale wivu chuki fitna na majungu
    huu ni ushauri tuu tujaribu kubadilika ndugu zangu mimi si mfaham huyu jamaa lakin akiwa ana uwezo wa kimaendeleo kwa nini tusimsapoti?
    chafosa

  17. Comment by Tanzanian Female on May 7th, 2008 8:42 pm

    Bablii,
    You dont argue with women because we are not worthy arguing with or because you respect us? Whatever your reason, I take back what some of the things I said but I was REALLY pissed by your response.

    Huyo kijana anadeserve a chance otherwise tutabaki kuwakandamiza wanasiasa vijana kisha tunaishia kulalamika kwamba tulionao hawafai.

  18. Comment by Tanzanian Female on May 7th, 2008 8:43 pm

    I meant to say I take back ’some’ not I take back ‘what some’

  19. Comment by yohana francis on May 8th, 2008 4:35 am

    Watanzania tuache wivu wa kijinga na tumpongeza mtu pale panapotakiwa kufanya hivyo, kijana anajitaidi sana katika siasa na kama walivyosema wengine kama si kamchezo mchafu alichofanyiwa leo hii angekuwa ni mbunge wa ubungo

    Watanzania tukumbuke kuwa kila mtu mungu kamuumba na sifa na akili na kipaji chake, tofauti na mwingine. hivyo mnyika kuingia katika siasa ni matakwa ya akili na kipaji chake. wewe kama huna kaa kimya.
    Kama ni uwezo wa akili na kusoma basi, leo mwalimu Nyerere angekuwa na ma PHD mengi sana, lakini utashi wa kisiasa ulimfanya kuacha kazi yake ya ualimu na kuingia katika siasa na akatupatia uhuru ambao kila mtu leo anaufurahia.

    John kaza buti mwendo mdundo, iko siku utafanikiwa katika malengo yako ya kisiasa.

  20. Comment by Hellen Delhi on May 8th, 2008 11:36 am

    Mnyika kila la kheri na mafanikio mema….mwanzo mgumu!!
    kila mtu anaweza kuwa na la kukushauri ambalo analiona yeye ni jema….si mbaya kila mtu anapaswa kuwa na mtazamo wake,na critics ndio uwachukulie kama changamoto zaidi,wakufanye ujitahidi zaidi…kuwa “prove them wrong”
    naamini kila uliloamua hukukurupuka tu,bali yote yalianza taarabu toka uko Tambaza,na haya yote ni katika kutambua ni nini unapenda zaidi na unakimudu vyema.Go ahead…..hamna kitu chema kama kutambua vipaji vyako na ukavitumia vilivyo,na hicho ndio unafanya.Akili ya darasani na kuendelea na shule ni vitu viwili tunapaswa kutokurupuka kucomment.
    likewise,when Bill Gate left the prestigious Harvard,at that time i believe everyone who knew him must have been thiking he is mad,but what are the fruits of that rare path today??

  21. Comment by binti-mzuri on May 8th, 2008 12:36 pm

    nasikitika kwa watu mnaolumbana hapa,na mnyika mwenzenu anasonga mbele kama Obama….wabongo ndo mana tunarogana…embu acheni wivu wajameni!..LOH..si nawewe jiunge na mrema basi umpe sapoti!?

  22. Comment by Malenga on May 9th, 2008 1:51 pm

    “Anga kaanga,tu chini ya gae…”Mnyonge mnyongeni lakini sifa yake mpeni.Watu husifiwa kwa mazuri sio mabaya…Elimu sio lazima iwe ya ndani ya jengo…Upeo na ufahamu ni mungozo tosha wa ufanisi katika jambo lolote ulitakalo maishani mwako

  23. Comment by Liemy on May 10th, 2008 12:59 pm

    sasa nyie mnaosema sijui angeendelea na shule aliyekuambia hasomi nani? mbona yuko UD, au mnataka ahamie pale chuoni kabisa. acheni upuuzi wa mawazo mgando. hata huku ulaya watu kibao wanasoma vyuo na wanafanya kazi.

    By the way, mnaosema aachane na siasa, nyie mnataka awe nani? mm nadhani kila mtu anazaliwa na interest na dreams zake. Ni wewe tu kutafuta mchongo ili ufanikishe ndoto zako. Sasa nini Shida?

    hata kuna mwanamuziki alisema sio lazima wote tuimbe, wengine tubaki kushangilia.

    Na wengine wanadai oohh mbona sifa kibao kwenye maelezo yake? mimi sijawahi ona mtu akiweka kitu kibaya kwenye CV yake au maelezo, hata kama ni mwizi au fisadi, bado ataandika positive side.

    Unajua watanzania tuna tabia za ajabu, na ndio maana watu umaskini umezidi, Wivu ni kitu kibaya sana. Sifieni inapobidi na kosoeni palipopabaya. na kwa style hii wivu ukiendelee tutaendelea kulana nyama na kunyonyana damu tu ndio mbadala wa maisha watu wanaouona, maana wivu na uchawi hauna tofauti

    John, just go! do it

    After all Kichwa umejaliwa, una aliki kama cheche za Moto.

    Na CV yako ni nzuri.

    All the best

  24. Comment by binti-mzuri on May 13th, 2008 12:33 pm

    nyie mnaosema CV yake nzuri,mmeiona!?

  25. Comment by Radi on May 13th, 2008 2:14 pm

    Hi! Hivi Viwalo vyenu?
    yaani mmekuwa kama vile Tourst Guider!????
    Jaribuni kuwa makini na mavazi

  26. Comment by binti-mzuri on May 13th, 2008 3:21 pm

    hhahaha @ Radi

  27. Comment by mzalendo on May 26th, 2008 8:44 pm

    Mnyika hawezi kuwa OBAMA kwani Obama anaongozwa na shule ya nguvu amesoma Harvard university.

    aliingia siasa baada ya kumaliza digrii ya kwanza na alikuwa rais wa kwanza mweusi wa law department alipokuwa un.

    Mnyika hana shule na huko O LEVEL ALIPATA one kwa vile alikuwa anasoma shule ya kanisa ambako huwa wanapewa mitihani. haiwezekani apate one kali O LEVEL HALAFU FORM SIX apate Four.

    KWENYE siasa anajidanganya anapoteza muda wake tu. hawezi kupata Ubungo eneo lenye chuo kikuu huku yeye ni mbumbu.

    Chadema wanampotezea muda wake kwa vi semina na vi posho wa kijinga.

    aende shule Chadema si chama ni NGO YA WACHAGGA kwa mujibu wa Mswahili wa JF.

    wako wengi walijidanganya na siasa na sasa wanahangaika.
    aende Tumaini UNIVERSITY wanachukua division four anaanza na pre-university baadae anafanya kozi yake ya digrii.
    akimaliza anaenda masters all th way 2 phd.

    inaonekana Chadema ni chama cha wajinga kwani MBOWE NAE KAFELI MASOMO HUKO ulaya.

    Chacha wangwe ni kidato cha nne, Slaa ana digrii ya kwaya kanisani.kwa kundi hilo si rahisi kwa Mnyika kupenda elimu. bora angekuwa CUF angekutana na wasomi au NCCR.

  28. Comment by Asha on July 10th, 2008 12:57 pm

    Dr Slaa ana PHD ya Sheria. Chacha hajaishia form four. Mnyika hajapata Division four form Six. Wewe umemua kudanganya wazi wazi kabisa. Hebu uone aibu. Tembelea http://www.chadema.net utaona maelezo kuhusu hawa viongozi na tembelea website ya bunge utaona maelezo ya wabunge wote na mahali ambapo wamesoma.

    http://ashawazenj.blogspot.com

  29. Comment by Anonymous on July 21st, 2008 3:54 am

    It’s funny how people jump into conclutions bila kujua wanachokiongea. Binafsi nimekua na John toka utotoni na tulikuwa tunashindana katika mitihani, n.k. Kuna mtu kadai alipata 1.7 kwasababu alikuwa seminary na wanaiba pepa; we nani kakuambia seminary wanaiba pepa? They have a strict schedule and are made to work hard that is why they do well. John kwa taarifa yako aliongoza Mbuyuni Pr. all the way mpaka darasa la 7 na akaongoza mkoa mzima wa Dar. Sasa utadai huyu hana akili? Hata alipokuwa Maua he was a class apart kwa uwezo wake darasani. So haikuwa bahati wala wizi wa mtihani.

    Form 6 alipata 2.12; he could have done a whole lot better probably if he was not so involved with other activities, but hey, I bet it’s far much better than most of you lots who are here trashing him. Wengine sijui hata kama mmefika form VI hiyo; na kama mlifika sijui hata kama mlipata hata div III. Isitoshe, nani kawaambia elimu ni kufaulu mitihani tu. Kaombe kazi nchi za nje bila involvement in any extracurriculars tuone kama utapata.

    Nao mnaoponda uamuzi wake wa kujishughulisha na siasa; tatizo mna mawazo ya kibinafsi kama wanasiasa wengi wa Tanzania, mnafikiri unaingia katrika siasa kwa ajili ya manufaa fulani binafsi tu. John is a true patriot at heart and his interest is solely mafaniko ya watanzania wote. For him this is a calling. Kwa taarifa yenu anasoma BBA Mlimani, na hamjui ni kiasi gani amekuwa frustrated by the authorities above na kumtafutia visa vingi hadi kumzuia kufanya paper kwa kisingizio kuwa hakuwa assigned namba ya mtihani.

  30. Comment by Baniani on August 10th, 2008 9:17 pm

    Wewe unaemjua John,

    Amehitimu Chuo Kikuu ?

    Mbona hilo hasemi kwenye tovuti ya CHADEMA ?

    Na hiyo Div 2 ni ya masomo gani ?

  31. Comment by Anonymous on September 8th, 2008 4:33 am

    Baniani, Mnyikahajahitimu chuo kikuu bado lakini anasoma BBA, kwani hujaona kilichandikwa juu hapo ndugu yangu, au? Div 2 yake ni ya EGM, anymore questions?

  32. Comment by Anonymous on September 8th, 2008 4:52 am

    Anayesma Slaa hajasoma kaangalie hapa: http://www.parliament.go.tz/bunge/Mp_Cv3.asp?PTerm=2005-2010&fpkey=254&vusername=GUEST%22)

    Pia Mdee, Zitto, Susan Lyimo, Mhonga na Owenya utasema hawajasoma nao?

  33. Comment by Mary Mkwaya Malamo on October 22nd, 2008 2:24 am

    Mhwaa!

  34. Comment by chapombe on November 26th, 2008 9:53 am

    kwani huyu ni mwanamgambo?

  35. Comment by PUZZO on January 30th, 2009 4:05 am

    Kwani tatizo nini? Kwani Lazima awaambie na matokeo ya 4m 6? Muhimu eleweni kasoma hadi chuo! Ingekuwa alifeli six angeendeleaje na chuo? Acheni umbea

  36. Comment by Mjololo Ng,ughuya on May 4th, 2009 7:31 am

    Hongera kijana mwanasiasa mkakamavu wa siasa

  37. Comment by Muhajir on August 1st, 2009 9:06 am

    Wamekuibia kura 2005 wakachukua ubunge,lakini mwakani mwishowao hawa wazee wasiokubali kuachia madaraka.Tunataka tukuone na wewe bungeni umsaidie mkombozi wetu vijana muheshmiwa zitto Kabwe.Mnyika unatisha acha wanaccm wachonge tu mwakani sio mbali.

  38. Comment by Raphael Akaro on August 22nd, 2009 5:51 am

    Ni kweli amekuwa akifaulu vizuri nami nampa hongera nimanfahamu.

    But remember his very early ambition ilikuwa kuwa padri then what had happen latter?.

    Chakujifunza: Alianza vizuri anauwezo mkubwa kifikra na atasaidia wengi. Alijiingiza kwenye harakati hizo mapema kabla ya kujenga zaidi. Ayafanyayo sasa nadhali angeweza kufanya yaliobora zaidi.

    Angeweze kuendelea kielimu ili ajekuwa mwanaharakati msomi mwenye taaluma makini. Lakini wajanja walipomuona walimchukuwa kwa interest zao.

    He has a divine calling within him lakini alipaswa ajijenge kwanza kielimu na kiroho kabla ajaaza kuutomikia wito wake na kusudi alililipewa na Mola.

    Anaonekana anafanya vyema lakini kwa mizani ipi? Inamgarimu sana changamoto ni nyingi sana ili kuleta ukombo wa kweli wa Mtanzania.

    Binafsi Nampenda kwakuwa ana wito wa Mungu lakini je ataweza kulitukia kusudi kwa ukamilifu, usahihi,uwadilifu na na katika nyakati alizoamriwa na mwenyezi Mungu!

    RAI YANGU:tumlinde, tumshauri maana hii nchi ina watu hatari(MAFISADI) waweza kumfuta na asisikike tena, zaidi yayote TUMUOMBEA MUNGU AMUONGOZE NA AWE MWAMINIFU.

  39. Comment by salum on October 12th, 2009 8:53 am

    he huyu ndio nani tena?

  40. Comment by Adam Manoja on December 31st, 2009 4:57 am

    HII MAKALA NIMEISOMA HAPA: http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=11672 , NAONA INA MUHUSU HUYU KAMANDA

    MWISHO wa mwaka ni wakati wa kutafakari tulikotoka, tulipo na tunakotaka kwenda katika mwaka mpya. Ni kipindi muhimu kwa taasisi na hata watu binafsi kufanya tathmini na kujiwekea malengo. Kwa binadamu mmoja mmoja yanaweza kuwa ni malengo ya kiuchumi, kijamii na hata ya kisiasa.

    Maamuzi ya masuala ya kiuchumi na kijamii mara nyingi ni masuala binafsi. Hata hivyo, malengo ya kisiasa hususan yale yanayohusu utumishi wa umma ni muhimu kwa maamuzi yake kufanyika kwa kuzingatia mwelekeo wa kiongozi husika lakini pia kwa kurejea utashi wa wananchi iwe ni faraghani au hadharani.

    Hii ni kwa sababu uongozi wa umma wa kuchaguliwa hufanyika katika medani ya demokrasia ambayo inahusisha utawala wa watu kwa ajili ya watu.

    Katika uchaguzi yapo mambo manne ya muhimu katika kuhakikisha ushindi. Mosi, ni mgombea: haiba, wasifu na uwezo wake kwa ujumla. Pili ni ajenda: ujumbe wenye dira unawagusa wapiga kura na kuamsha kuungwa mkono.

    Tatu ni oganaizesheni: huu ni mtandao mzima wa kuratibu vuguvugu la ushindi, unaweza kuwa wa kijamii, kisiasa ama kitaasisi. Nne, rasilimali: hii ni kwa ajili ya kuwezesha kwa hali na mali kampeni husika, iwe ni fedha, zana, mawazo au nguvu kazi.

    Baadhi ya watu hudhani kwamba rasilimali ni jambo la kwanza kuwezesha ushindi, uzoefu wa kimataifa unadhihirisha kuwa katika kufanikisha kampeni za uchaguzi kipaumbele cha kwanza ni mgombea, cha pili ujumbe, cha tatu ni oganaizesheni.

    Rasilimali huongezeka kwa kadiri ya tija na ufanisi wa vipaumbele vitatu vinavyotangulia kwa nadra mtiririko huu unaweza kubadilika kutokana na upekee wa kimazingira ya kisiasa.

    Tumebakiza siku chache kuingia mwaka 2010, kipindi kingine cha kuelekea uchaguzi mkuu wa udiwani, ubunge na urais nchini. Tayari heka heka zimeshaanza na kauli mbalimbali zimeshaanza kutolewa za kheri na za shari.

    Kwa kweli fikra kuhusu uchaguzi ujao zilishaanza toka 14 Desemba mwaka 2005 kwa wale wanaoamini kuwa mwisho wa uchaguzi mmoja ni mwanzo wa uchaguzi mwingine.

    Binafsi nakumbuka mwaka huo wa 2005 wakati mjadala ukiendelea kuhusu utata wa matokeo ya uchaguzi wa ubunge katika jimbo la Ubungo ambapo mimi nilikuwa mmoja wa wagombea tayari wadadisi wengine wameanza kuulizia masuala ya uchaguzi wa 2010.

    Hali hii ilijitokeza hata katika mkutano wangu na wanahabari Desemba 22, 2005 kwa ajili ya kuwashukuru wapiga kura na kuelezea mafanikio yaliyopatikana, mapungufu yaliyojitokeza na hatua ambazo nilipanga kuzichukua.

    Hata baada ya kutoa msimamo huo, bado mjadala uliendelea katika kipindi cha Januari mpaka Mei 2006; takribani nusu mwaka baada ya uchaguzi mkuu kumalizika.

    Hivyo, baadhi ya masuala hayo niliwajibika kuyajibu kupitia hotuba yangu ya kuwashukuru wananchi na kuelekeza mwelekeo niliyohutubua jimboni Ubungo Mei 28, 2006.

    Ilinibidi niandike pia waraka kwa wananchi wa ubungo na watanzania Juni 4, 2006 wakati huo nikiwa ziarani nchini Marekani waraka ambao ulisambaa kwa umma kupitia vyombo vya habari na njia zingine za mawasiliano ya umma ikiwemo mikutano ya hadhara niliporejea. Waraka huo uliobeba ujumbe ‘kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi’ uliweza kutuliza kwa muda mjadala.

    Katika waraka huo nilielezea masuala mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa azma ya kufungua kesi namba moja ya mwaka 2006 katika Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge katika jimbo la Ubungo.

    Kesi hiyo ambayo nilisimamiwa na Wakili Tundu Lissu ilipigwa danadana za kiufundi kipindi chote na kuishia hewani mwaka 2007 kwa kile kilichoelezwa na wakili wangu kuwa ni kukosekana kwa dhamira ya dhati ya kuisikiliza kesi hiyo.

    Hata hivyo, miaka takriban mitatu iliyopita ya 2006, 2007, 2008 na hata mwaka huu wa nne unaomalizika wa 2009, swali ambalo nimekuwa nikiulizwa ni kugombea ubunge wa jimbo la Ubungo 2010.

    Nimekuwa nikiulizwa swali hili katika mikutano ya hadhara ya kisiasa katika ziara ambazo tumekuwa tukizifanya katika kata zote za jimbo la Ubungo. Katika kipindi chote hicho swali hilo hilo limekuwa likiulizwa hata kwenye shughuli na matukio ya kijamii yawe ni ya kirafiki, kidini, misiba, harusi, michezo, miradi ya jumuiya, ufuatiliaji wa kero za wananchi nk.

    Wakati wote majibu yangu yamekuwa kati ya haya matatu nitajibu wakati muafaka ama umma utajibu ama Mungu akipenda! Najua katika kipindi chote majibu haya yamekuwa yakiwaweka katika mkanyiko waulizaji kwa sababu mbalimbali.

    Wapo wenye mtazamo kwamba majibu kama hayo ni ishara ya kutokuwa na uhakika ama kupima upepo. Wapo wenye imani kwamba kwenye uongozi wa kuchaguliwa sifa mojawapo ya uongozi ni kuutaka uongozi.

    Wapo ambao katika kipindi hicho hicho wamekwenda mbele zaidi kuweka msimamo wao bayana kwamba ni lazima nigombee tamko la wazi la hivi karibuni likiwa ni la mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Makoka na wananchi wa eneo hilo la Novemba 29, 2009. Msimamo huo waliutoa kwenye mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wananchi ambao walinialika kama mgeni rasmi.

    Kilichonisukuma kuandika makala hii ni majadiliano yanayoendelea hivi sasa kwenye mtandao kupitia http://www.facebook.com/john.mnyika kuhusu ‘Ubunge Ubungo 2010: Nigombee Nisigombee?’

    Wachangiaji wote waliotoa maoni yao mpaka sasa wamenitaka nigombee huku wakitoa sababu mbalimbali. Wapo waliotoa hoja ya kutambua uwezo, haja ya kubeba harakati za kizazi kipya kushiriki kwenye uongozi wa taifa letu, kufanya vizuri mwaka 2005 na kuhoji kuhusu mikakati ya kuhakikisha ushindi mwaka 2010.

    Mchangiaji mmoja alirejea mfano wa Barack Obama ambaye alikuwa na mashaka kuhusu kugombea kwake lakini mmoja wa washauri wake wa karibu akamweleza kwamba ‘usipogombea umechagua kushindwa; lakini ukigombea una chaguo la kushinda ama kushindwa’. Walatini wana msemo ‘Sauti ya watu ni sauti ya Mungu’. Si lengo la makala haya kujadili hoja mbalimbali ambazo zimetolewa katika mjadala huo.

    Naandika makala kuwezesha tafakari ya wengine ambao ni sehemu ya wapiga kura ama wananchi kwa ujumla hawana fursa ya kushiriki majadiliano kwenye tovuti.

    Tafakari pana zaidi tunapoelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010; nini kinawasukuma wagombea kujitokeza kugombea: dhamira binafsi ama msukumo wa umma au vyote?

    Mwaka 2005 wakati huo nikiwa na miaka 24 nilipojitokeza kugombea kwa mara ya kwanza nilieleza kwamba ilikuwa ni dhamira yangu binafsi baada ya kuona nina kipawa/kipaji cha uongozi.

    Kusukumwa na dhamira ya ndani inaweza kuwa jambo la kawaida kwa mgombea ambaye utumishi wake bado haujaonekana kikamilifu mbele ya umma.

    Lakini vipi kwa mgombea ambaye anafahamika tayari: nguvu alizonazo, udhaifu alionao, fursa alizonazo na vikwazo vinavyomkabili, naye asukumwe na dhamira binafsi pekee?

    Kwa mgombea ambaye tayari anafahamika ni muhimu pamoja na dhamira yake binafsi pawe pia na msukumo wa umma hii ni kwa sababu nafasi za kuchaguliwa kama ubunge ni za kuwakilisha wananchi.

    Ni muhimu sehemu ya wananchi iwe ni wanachama wa chama, wapiga kura ama baadhi ya watu katika jumuia waone haja hiyo.

    Kuungwa mkono kwa namna hiyo katika dhamira ya kugombea na kuhusisha umma katika kufikia maamuzi nyeti kama hayo yanaweka msingi muhimu wa kuwa mwakilishi wa wananchi husika na hata kuwashirikisha wananchi katika kukabiliana na changamoto za kimaendeleo.

    Kwa upande mwingine, kupanua wigo katika kufikia azma ya kugombea ni njia ya kuunganisha nguvu ya umma hata katika kampeni za uchaguzi. Katika siasa za ushindani ni muhimu harakati za uchaguzi zikaendeshwa katika mfumo wa vuguvugu hususan kwa wagombea wanaopitia vyama mbadala ambavyo havitegemei nguvu ya dola.

    Hivyo, ni muhimu kwa yoyote anayetaka fulani agombee katika eneo fulani, mosi, amtake kugombea kama sehemu ya msukumo wa umma. Pili, ajiunge na harakati za kufanikisha ushindi wake kwa hali na mali.

    Ushindani wa namna hiyo ulijidhihirisha nchini Marekani mwaka 2008 mpaka 2009 kwa wagombea kuungwa mkono na umma; kuanzia wakati wa kura za maoni za ndani ya vyama mpaka kwenye kampeni za uchaguzi mkuu.

    Tunaweza kushiriki kuleta mabadiliko kwa kugombea na kuchaguliwa ama kwa kuchagua viongozi kwa kupiga kura. Ndio maana nachukua fursa hii kuwahimiza Watanzania ambao watakuwa na umri wa miaka 18 na kuendelea mwaka 2010 kutimiza wajibu huu wa kiraia.

    Hivyo, kwa wapiga kura wapya na wote ambao kwa sababu moja au nyingine hawana kadi za mpiga kura wajitokeze kujiandikisha kupitia uboreshaji wa daftari la kudumu unaoendelea ambao kwa upande wa Dar es salaam utafanyika mapema mwaka 2010.

    Izingatiwe kuwa hii ni awamu ya mwisho kabisa ya mchakato huo; kabla ya uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba hivyo kukosa kujiandikisha ni kujikosesha haki ya kikatiba ya kuchagua kiongozi unayemtaka.

    Hata hivyo, izingatiwe kuwa kushiriki kuleta mabadiliko ni zaidi ya matukio ya kugombea ama kupiga kura ni pamoja na kushiriki katika mchakato mzima wa kuleta mabadiliko kwa njia mbalimbali. Mwito wa Mahatma Gandhi kuwa wakala wa mabadiliko unayotoka kuyaona’ unabeba dhana hii.

    Swali la kujiuliza, je wewe uko tayari kuwa wakala wa mabadiliko unayotaka kuyaona? Kama Ndio; je umeshawasiliana na chama ambacho unaamini ni chombo cha kuwezesha mabadiliko hayo na kuwaunga mkono viongozi hata ikiwa ni kwa kuwapa ushauri? Ama umeshashirikiana kwa hali na mali au walau kuwasiliana na mgombea mtarajiwa ambaye unaamini anaweza kupeperusha bendera ya kuongoza mabadiliko?

    Kugombea nafasi za kuchaguliwa zinazohusisha kuwakilisha umma hakupaswi kuwa suala la mtu binafsi. Matokeo ya kuwaachia wagombea binafsi ama vyama vyao pekee ni kuwa na viongozi ambao baada ya kuchaguliwa kwao kwa sababu waliingia kwa dhamira zao na wakafanya kampeni ‘kivyaovyao’; hawawajibiki kwa umma.

    Hivyo tunapoelekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ni muhimu kwa wapiga kura na wananchi kwa ujumla kutambua kwamba suala la uongozi wa kuchaguliwa kuwakilisha umma ni wajibu wa pamoja.

    Ni wajibu wa yoyote anayetambua kwamba Mwenyezi Mungu ameijalia nchi yetu na watu wake rasilimali; iwe ni vipaji vyetu, kodi zetu ama maliasili: Hivyo tunawajibika kujenga taifa lenye kutoa fursa ya ustawi wa wananchi. Pamoja Tunaweza!

    Ni wajibu wa pamoja wa watumishi wa umma iwe ni walimu, polisi, wahudumu wa sekta ya afya n.k, ama wafanyakazi binafsi ambao wanataka mabadiliko kutoka katika mishahara midogo na mazingira magumu ya kazi, maslahi duni na kujenga taifa lenye kuthamini utaalamu. Pamoja Tunaweza!

    Ni wajibu wa wazazi, wanafunzi, wazee, wanawake na masikini kwa ujumla wenye kuathirika na kuongezeka kwa gharama za maisha na kuporomoka kwa huduma za kijamii nchini iwe ni elimu, afya, maji, mafao ya wastaafu na waotaka pawepo mifumo thabiti ya usalama na haki katika jamii ili kuepusha migogoro. Pamoja Tunaweza.

    Ni wajibu wa Watanzania wote wenye kukerwa na ufisadi unaolitafuna taifa huku hatua zinazostahili kushindwa kuchukuliwa kutokana na ufisadi kutapakaa katika mfumo mzima wa utawala na kuteteresha hata utawala wa sheria. Tufanye mabadiliko turejeshe uwajibikaji na maadili ya taifa. Pamoja Tunaweza!

    Ni wajibu wa matajiri na wenye fursa wanaoona hatari inayolinyemelea taifa kutokana na kuongezeka kwa pengo kati ya wenye nacho na wasiokuwa nacho, ukosefu wa ajira hususani kwa vijana nk ambayo ni mabomu ya wakati yenye athari vizazi hata vizazi yanayoweza kuepukwa kwa kuweka pembeni ubinafsi na kujali maendeleo ya sekta zinazogusa mustakabali wa waliopembezoni. Pamoja Tunaweza!

    Ni wajibu wa wapenda demokrasia wote wanaotambua kwamba hujuma za kwenye uchaguzi zinaweza kudhibitiwa kwa kuunganisha nguvu ya umma ikiwemo kwa kujenga vuguvugu thabiti la ulinzi wa kura. Pamoja Tunaweza!

    Tukumbuke; mabadiliko ya kweli katika taifa letu hayawezi kuletwa na mafisadi wale wale, wa chama kile kile, chenye uoza ule ule, wakiendeleza yale yale. Kwa falsafa ya Chukua Chako Mapema; Tanzania yenye neema haiwezekani. Tuunganishe nguvu kubadili mfumo wa utawala; mabadiliko yanawezekana.

    Tunahitaji uongozi wenye dira na uadilifu wa kulikomboa taifa; hivyo ni jukumu letu sote kuhakikisha viongozi tunaowahitaji wanashinda. Kwa maneno ya Mwalimu Nyerere jukumu la namna hii linaweza kutekelezwa kama kila mmoja akitimiza wajibu wake; umoja ni nguvu. Kidole kimoja hakivunji chawa; kuelekea uchaguzi mkuu 2010: pamoja tunaweza!

    Mwandishi wa makala hii ni Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CHADEMA anayepatikana kupitia 0754694553, mnyika@chadema.or.tz na http://mnyika.blogspot.com

Leave a Reply