MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

Leo ni siku ya kumbukumbu ya kitaifa ya tangu kufariki kwa Sheikh Abeid Amani Karume miaka 36 iliyopita.Raisi huyo wa kwanza wa Zanzibar aliuawa kwa kupigwa risasi huko visiwani Zanzibar.

Ni uongozi wa Hayati Sheikh Amani Abeid Karume na Hayati Julius Kambarage Nyerere ambao ulitupa Tanzania tunayoijua hivi leo ukiwa ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar tangu mwaka 1964.

Kumbukumbu ya mwaka huu ya Sheikh Abeid Amani Karume inakuja huku bado kukiwa na “mpasuko” wa kisiasa huko visiwani hususani kuhusiana na suala zima la muafaka ambalo mpaka kufikia hivi sasa bado hayajapatikana maafikiano ya kueleweka.Ni imani yetu kwamba muafaka utakuja kufikiwa na amani itazidi kutawala.

Ili kujua au kujikumbusha vizuri historia ya Sheikh Abeid Amani Karume bonyeza hapa na hapa bila kusahau kutembelea mtandao wa zanzinet.org ambao umesheheni mambo mbalimbali kuhusu visiwa vya Zanzibar ikiwemo pia historia kamili ya visiwa hivyo. R.I.P Sheikh Abeid Amani Karume.

Katika picha hii ya zamani anaonekana Mjane wa Sheikh Abeid Amani Karume,Fatma Karume(kulia), akiwa na Mama Sophia Kawawa(marehemu) katika moja ya mikutano enzi hizo.Picha kwa hisani ya Issa Michuzi.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

34 Responses to “TUNAPOMKUMBUKA SHEIKH ABEID A.KARUME”

  1. Comment by Gervas on April 7th, 2008 4:33 am

    Huwa najiuliza kila mara hivi nani alimuua karume? na kwa misingi gani aliuawa? je hiyo misingi iliyopelekea kuuawa Karume ni kweli haina uhusiano wowote na mpasuko wa siasa uliopo sasa zanzibar? je kabla ya vyama vya siasa kuanza Tanzania, ni kweli hapakuwa na mgawanyiko wa wazanzibari? walikuwa wamoja kweli? sababu nahisi huu mpasuko wa sasa hausababishwi na matokeo ya changuzi zilizopita pekee yake, kuna chanzo haswa. Kuna anayefahamu lolote juu ya haya niliyouliza hapa? naomba msaada wana-blog.. maana leo ni siku ya Kudadavua mambo kadhaa, its Karume day.

  2. Comment by Anonymous on April 7th, 2008 11:15 am

    Soma siasa za Zanzibar utajua yote hayo tafuta makala za zaamni za Rai iliyokuwa ya Generali Ulimwengu kila kitu kiko wazi. Kuna vitu vinaitwa AfroShiraz na Hizbu party. Hizbu ilikuwa ya Wapemba na Afro Shirazi ya Waunguja na wengine waliotaka kujikomboa chini ya usultani. Hizbu hawatambui mapinduzi yaliyomtoa Sultan kwa sababu majority wana asili ya uarabu. Na Afro Shiraz ndio waliofanya mapinduzi ya kumng’oa Sultan na kuweka utawala uliopo madarakani, hii Afro Shiraz party iliyounda serikali ya Mapinduzi ZNZ ndio iliyoungana na Tanganyika na baadae chama hicho kiliungana na TANU mwaka 1977 na kukazaliwa CCM.

    Hayo mambo ya siasa za visa Zanzibar yanaanzia tangu wakati wa kutawaliwa na Sultani ambako si unajua tena mambo ya matabaka ya rangi, na ubaguzi wa rangi na thamani ya bwana na mtwana. Sasa kulivyotokea mapinduzi ndio uhasama ukazidi kuendelea kati ya wanzazibari weusi na washirazi na wazanzibar wenye asili ya alikotoka Sultan.

    Angelikuwepo huyo bingwa huyo ungesikia cha Muafaka wala cha nini na hata hii CCM sijui kama ingekuwepo nafikiri kila nchi ingebaki na chama chake cha siasa.

    Samahani siwezi kuingia zaidi ndani ya hii ishu ni sensitive ndio inayoleta siasa za kubaguana ya huyu muunguja na huyu mpemba na ubaguzi wao unaenda mpaka kwenye nafasi za kazi za masomo na kadhalika, iko deep sana sio kama watu wanavyofikiri. Na ukizingatia sasa hivi hao waunguja ni wengi sana kuliko wapemba (wapemba wengi walikimbia ZnZ hata kabla ya awamu ya 3 na wamejikita sehemu mbali mbali duniani) ni rahisi sana kwa CCM kushinda kura ya maoni, inawezekana kutokana na historia ya siasa zao wanachama wa CCM walioko Unguja wakasema hatutaki serikali ya mseto. Hivyo CUF wataloose chance ya kuwa sehemu ya serikali ya ZNZ ili kuondoa huo ubaguzi uliopo miongoni mwao. Na walivyo na ushabiki na ushindani sijui itakuwaje hiyo siku ya kura ya maoni kama vile chungwa na ndizi Kenya!

  3. Comment by Gervas on April 7th, 2008 12:49 pm

    Duh, anony.. hapo juu, nakushukuru saana, maana maelezo yako japo ni machache lakini yame-hit point kwa mtu muelewa. najua sio mimi tu, watu wengi hawajui hasa chimbuko la soo ya Zanzibar. Kumbe sio issue ya kukurupukia tu na kutoa judgment ya mpasuko wa zanziabar. Asante kwa niaba ya wengi.

  4. Comment by Mswahilina on April 7th, 2008 1:49 pm

    Hayati Sheikh Abeid Aman Karume, Mwenyezi Mungu akulaze pema peponi. Amen.

    Hayati Mama Sophia Kawawa, Mwenyezi Mungu akulaze pema peponi. Amen.

    Mlikuwa majemedari wetu Watanzania kwa nyakati zenu.

  5. Comment by mkereketwa on April 7th, 2008 1:49 pm

    Nakubaliana na maelezo yako hapo juu, na ukitaka kuona kasheshe ya watu hawa inabidi utembelee Zanzibar ujionee. Nilifanikiwa kuwa zanzibar kati ya mwaka 1992 – 1995 wakati machafuko ya siasa ya vyama vingi imeanza na niliyoyashuhudia sintosahau hadi leo. Jazba yao ni ya hali ya juu na kama ulivyosema imeanza siku nyingi vizazi hadi vizazi na watu wameendeleza historia na kuweka vinyongi moyoni mwao. it’s all about history. Mambo yatabadilika tu iwapo wakakubali kujiita na kujitambua kama WAZANZIBARI AU WATANZANIA THAN MNGAZIJA OR MPEMPA OR…. Hali hii inaendelea hadi nje ya nchi kwani sisi wote ni watanzania lakini bado utaona kuna mgawanyiko mkubwa baina yetu. Wabara hatujali kama mtu ni mmatumbi, mgogo, mchanganyiko wa mgogo na mzungu au mhindi. Kama kuna jambo limetokea kama msiba au ugonjwa la mtanzania yeyote linanigusa na kama kushiriki kwa hali na mali. THIS IS THE PROBLEM!

  6. Comment by Kasusula on April 7th, 2008 2:48 pm

    Shukrani sana wadau wote wawili hapo juu , aliye uluza swali na aliye jibu swali, swali ni safi na muhimu sana na jibu linalidhisha mno, ni wengi tulikuwa hajui huo ukweli na ukungu kidogo sasa umetutoka.
    shukrani

  7. Comment by Kasusula on April 7th, 2008 2:49 pm

    Shukrani sana wadau wote wawili hapo juu , aliye uliza swali na aliye jibu swali, swali ni safi na muhimu sana na jibu linalidhisha mno, ni wengi tulikuwa hatujui huo ukweli na ukungu kidogo sasa umetutoka.
    shukrani

  8. Comment by Kyoma on April 7th, 2008 3:16 pm

    Wazee maojua historia ya mzee Abeid Amani Karume, nimefuatilia hiyo website iliyotolewa hapo juu….baada ya bonyeza hapa na hapa…http://www.bookrags.com/biography/abeid-amani-karume-sheikh/ . Hivi maelezo yaliyoandikwa kuhusu asili ya mzee Karume na jinsi alivyo uawa ni sahihi?

  9. Comment by Bablii on April 7th, 2008 4:12 pm

    Tunakumbuka kifo cha Karume, ni vizuri pia tukakumbuka sababu za kifo chake!

    Mimi simwana historia, lakini kwa sababu nimejitahidi kuifuatilia historia ya zanzibar kabla na baada ya mapinduzi, kwa kusoma vitabu mbali mbali vya historia, vikiwemo vile vinavyoeleza kwa kuegemea watawala (CCM), vile vinavyoogemea wapinzani(CUF) vile vilivyotungwa na waandishi huru na zaidi nimehadithiwa na shuhuda aliekuwepo wakati wa vipindi vyote hivyo (Bibi yangu Mungu amlaze amrehemu ahera aliko), nathubutu kujiita gwiji la historia ya zanzibar tu!

    Ukitaka kupata sababu za kifo cha karume, vizuri ukasoma kitabu kiitwacho “UKWELI NI HUU” Kitabu hichi bahati mzuri kimetungwa na mmoja wa mawaziri wa SMZ, kabla hajaaamuwa kuisaliti jamii yake na kukubali kupewa uwaziri (Hivi sasa anaomba kitabu hichi kisisomwe tena! lakini ndo hivyo tena Jani likisha anguka halirudi tena mtini…). Pia waweza kusoma kitabu kiitwacho “KIVULI KINAISHI” ingawa kitabu hichi kimeandikwa kisanii sana, lakini kiufupi anazungumzia hali ya zanzibar baada ya mapinduzi ya 1964

    Kwa hakika kifo cha Karume ni matunda ya mbegu aloipanda baada ya mapinduzi. Madhila, mateso, dhiki, mashaka,jitimai la roho, maonevu, dhulma, manyanyaso, mauwaji na kila aina ya kisicho stahili kufanyiwa kiumbe kilicho hai, basi ndicho walichofanyiwa wale waliohisiwa kutoyakubali mapinduzi ya mwaka 1964, mapinduzi yaliyo mpinduwa “Mpemba” Mohd Shamte! Ndio hakuna muarabu aliepinduliwa 1964, ni mapinduzi yakumuondoa mpemba madarakani, ndo maana mpaka kesho hawataki mpemba arudi madarakani (ndo maana hawezi abadani kukubali serkali ya mseto)!

    Baada ya mapinduzi, kuna waliochukuliwa majumbani mwao, usiku wakila chakula na familia zao, eti wanaenda kuhojiwa lakini mpaka hii leo hawajarudi tena majumbani mwao (1964 mpaka 2008)…! Kuna waliolishwa chumvi pishi nzima (pishi ni sawa na kilo 2.5) nje ya markiti (soko) la wete na kupigwa
    viboko eti wao ni hizbu! Loh kuna ambao dada zao walinyanyaswa , mama zao wakauwawa akiwemo huyo Mahmud (alielipiza kisasi kwa kumuuwa karume). Waswahili wanasema “mwenda tenzi na omo hurejea ngamani” Kwa hiyo pamoja na kuwafanyia unyama familia yake akajikuta anamlea huyu mahmud (ni mfano wa Firauni na Mussa), akampandisha vyeo jeshini, kumbe ndo anamrahisishia kazi ya kumrudi! Basi
    ilipofika nyakati za alasir tarehe 7/4/1972, Mahmud akalipiza kisasi (ndio kwa mujibu wa dini yake Alkisasu l-haki) “Auwae kwa upanga huwawa kwa upanga”

    Lakini bado matunda ya 1964 tunayavuna, maana serkali ya zanzibar imekuwa ni ya wa unguja na wapemba ndio watawaliwa,siasa za chuki, majungu, fitna dharau ilimradi, tafrani. Wapemba wamekuwa kama wageni kwenye kisiwa chao!
    Ah ambae hajenda Pemba aende akaone, asije sema mie muongo nabawatuka atiiiiii.

    Ngoja ni sign off…wasije wakanipoteza

  10. Comment by Matty on April 8th, 2008 4:17 am

    Asante sana Gervas kwa kuuliza Swali la maana na jibu tumepatiwa linalordhisha, maana hata mimi nilikuwa sijui kitu kuhusu kuuawa kwa Karume.
    Asante wachangiaji Anonimous hapo juu na Bablii.

  11. Comment by Ms Bennett on April 8th, 2008 4:31 am

    inaonekana wewe bablii ulitaka waarabu waendelee kukaa kwenye ardhi isiyo ya kwao mapka leo.bravo sheikh abeih karume na mwalimu Nyerere kuwatimua masultani na usultani wao,hawa watu wanakasumba sana wameacha ubaguzi mpk leo kwa hao wanajiita waarabu watanzania

  12. Comment by Ms Bennett on April 8th, 2008 4:31 am

    inaonekana wewe bablii ulitaka waarabu waendelee kukaa kwenye ardhi isiyo ya kwao mpaka leo.bravo sheikh abeid karume na mwalimu Nyerere kuwatimua masultani na usultani wao,hawa watu wanakasumba sana wameacha ubaguzi mpk leo kwa hao wanajiita waarabu watanzania

  13. Comment by Gervas on April 8th, 2008 5:01 am

    Babii, Kuna kitu kinaitwa “biasness” katika uandishi wa vitabu ambapo mwandishi anakuwa either negatively or positively influenced na habari ambayo anataka kuiandikia kitabu hicho, mwandishi anatakiwa kuwa neutral. Sasa hapa msomaji unatakiwa kuwa makini kidogo, japo vitabu ulivovitaja sijavisoma. Mimi nafikiri hii dhambi ya kubaghuana haitaisha maana inaonekana inapandikizwa kizazi hadi kizazi. Kwa mtindo huu hata hao mnawaita wapemba wakiingia madarakani sio siri kazi ya kwanza itakuwa kulipiza kisasi. Nasikia kuna wengine walikimbilia wingereza wanajiita wakimbizi, wakachana passport zao Jk alivoenda Wingereza wakaanza kumuomba tena wapatiwe pass mpya na hali waliukana Utanzania. Mbona kuna Wapemba wengi tu wanamafankio makubwa ya biashara bara? maana Sheria ya nchi haimkatazi mtanzania yeyote kuishi popote ndani ya nchi. Mbona hata Bara kuna mikoa mingi tu haina maendeleo kabisa, wilaya hazina umeme!, Pemba ni sawa tu na mikoa mingine kama Kigoma, Rukwa n,k. Mimi nafikiri swala la zanzibar litaisha/pungua kama wananchi wake kwanza wapunguze jaziba, waondoe “dhambi ya ubaguzi” huku swala la mpasuko likishughulikiwa.

  14. Comment by Chris on April 8th, 2008 5:38 am

    Simply forum its a medium for open discussion or voicing of ideas. This discussion has added sthg that I didnt know.

    Thanx for Gervas, any and Bablii… Babli ntapataje hivyo vitabu UKWELI NI HUU and KIVULI KINAISHI…

    Cheers guys.. Long Live BC

  15. Comment by Amina on April 8th, 2008 8:22 am

    mmh mi nasoma tu hata sielewi kitu hapo ,ila nimeshukuru jana ilikua holiday sikwenda kazini

  16. Comment by Amina on April 8th, 2008 10:28 am

    Wajina una mambo!! kama hukuelewa ungewauliza Kina Gervas na Bablii kinachokutatiza ni nini; kwa hiyo umeridhika na kutokuelewa kwako??!! basi hukuwa na haja ya kuandika kitu…

  17. Comment by Anonymous on April 8th, 2008 10:43 am

    Tatizo ndilo hilo kama nilivyosema mwanzo la ubwana na utwana ambalo bado wako wanaoamini kuwa wao ni mabwana ni haki waliyopewa na Mungu kuwa mabwana, sasa haiwezekani watwana wakawatawala mabwana! Ndio maana sikutaka kwenda ndani zaidi ya hayo. Na kigumu ni hili suala la visasi na ushindani na ubishi usio na kichwa wala miguu. Era ile ya usultani ilishapita na Karume aliwalazaimisha watu wenye asili ya kiarabu waolewe na waafrika kwa nguvu na yeye alioa hao wenye asili ya kiarabu (mwangalie mwanawe na mjane wake) ili kuvunja ule uhasama wa matabaka mawili waone kuwa wao ni wamoja. Alitaka kuvunja hilo kwa kuwa na kizazi ambacho ni mchanganyiko wa mabwana na watwana. Huyo Bablii hawezi kukubali hata siku moja hiyo historia iliyoandikwa na weusi. Wengi mmesoma vitabu vya Adam Shafi na aliwahi kutolewa humu BC, lakini rudieni tena kuvisoma, ameandika kwa mtindo wa hadithi lakini ameelezea kwa mapana hali ilivyokuwa visiwani. Huyo sijui nani alifurushwa wakati wa mapinduzi ndio nasikia hapa kutoka kwa Bablii, lakini historia inatwambia Sultani aliyekuwa akitawala alikimbilia Dar wakati wa Mapinduzi na akaondokea Dar kurudi kwao.

    Ni kama vile suala la watusi na wahutu (kimfano tu wa visasi vya kikabila sio kihistoria) Na kama vile tunavyomkandya Mugabe (bila kujua kuwa kulikuwa na makubaliano ya serikali ya UK kuwalipa fidia walowezi na kuwarudisha huko walikotoka ili asilimia 90 ya Weusi wapate ardhi iliyokuwa ikishikiliwa na asilimia 10 ya wazungu (hapa ni mfano tu tunavyoshabikia ya Muafaka bila kutafuta undani wake) .

    Narudia tena mpemba ana mtazamo wake kuhusu mapinduzi (kuondolewa madarakani kwa nguvu bila ridhaa) na muunguja ana mtazamo wake kuhusu mapinduzi (kujikomboa kutoka kwenye utwana na unyanyasaji) na kila mmoja ataandika kulingana na tasfiri na mtazamo alionao kuhusu hilo suala.

    Kosa kubwa lilifanyika baada ya mapinduzi hakukuwa na reconcilliation ambayo ingeleta kusameheana na kuondoa siasa za visasi kuwa huyu alinifanyia hivi wakati wa utwana na huyu alinifanyia hivi wakati wa mapinduzi. Kungekuwa na tume kama ya Askofu Desmond Tutu ya South Africa ambako watu walipata nafasi ya kuyatoa moyoni yaliyowasibu na kupatanishwa na kusameheana.

    Na hata Kenya kama hakutakuwa na hii kitu ya kusameheana na kuendelea mbele badala yake watu wakakazania visasi, basi hata hiyo serikali ya mseto haitafaa kitu. The same applies to Zanzibar, lazima waingie katika hiyo process ama baada ya serikali ya mseto au kabla otherwise ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu. Wanasiasa wanatakiwa watibu majeraha ya zamani ambayo yako ndani ya makovu yasiyotaka kupona.

    Nyie hamshangai hawa wazanzibari asilimia kubwa ni dini moja, lakini hata hilo la kusameheana wao wahalioni kama ni sehemu ya dini, asiwadanganye mtu uislam una mweka kwenye daraja kubwa mwenye kusamehe hata Mtume Muhamad (SAW) alifanyiwa visa alipigwa, na mambo kadhaa lakini alisamehe hakuwawekea watu visasi miaka na miaka.

    Mwenyezi Mungu tunamkosea kila siku na mbali na kuwakosea wenzetu lakini hutusemehe makosa yetu mara tu tunapomuomba msamaha.

    Mwisho kwa sensitivity ya huu mjadala wapo ambao nitakuwa nimewakwaza, hivyo basi naomba wanisamehe kabla sijaomuomba Mwenyezi Mungu anisamehe kwa niliyoyaaandika kwa mkono wangu. Hii ni humility!

  18. Comment by Bablii on April 8th, 2008 12:40 pm

    Chris…
    Hiki kitabu kiitwacho KIVULI KINAISHI mpaka 2000 Kilikuwa kinatumika kwa A’ elevel (watu wa lugha), na hichi UKWELI NI HUU, naskia mandishi amesimamisha uchapishaji wake, lakini ntajitahidi kukutafutia, nikijuwa kinapatkana wapi ntakujulisha

    Anon hapo juu unanichanganya, mara wasema aliepinduliwa ni muarabu, mara wasema wapemba wameondolewa madarakani bila ridhaa…! Ukweli utabaki pale pale Mohd Shamte alikuwa mpemba wa mtambwe -pemba (ambako ndiko anakotoka maalim seif). Usidanganywe, nisawa na uongo unaodanganywa kuhusu Idd Amin eti alikula nyama za watu!

    Kumbuka mtu akitaka kukudhuru huanza kukupa sifa mbaya kwanza, ndo maana hata mwizi hapigwi kwanza mpaka aitiwe mwizi mwizi ndo hufuata kipondo..!

  19. Comment by mie on April 8th, 2008 1:15 pm

    Karume hakuzaliwa Mwera bali alizaliwa Malawi.Huko Mwera hawana nyumba wala nyumba.Aliingia znz akiwa amebebwa mgongoni na mama yake.Ila sio siri amefanya mengi ya maendeleo ambayo toka auwawe hakuna prezo hata mmoja aliefikia hata nusu ya aliyoyafanya.Pamoja na hayo aliuwa wengi ambao walionekana tishio kwake kama kina Hanga kwa kuwafunga mawe ya shigo na kuwatumbukiza baharini.siasa za znz ni ngumu mno.

  20. Comment by Albert on April 8th, 2008 3:26 pm

    KWA WOTE WATOWA MAONI MNAKUMBUKA KULIKUWA KUNA MTU MMOJA KATIKA KESI YA UHAINI AKIITWA ME X NA MPAKA LEO HAKUWEZA KUTAJWA JINA LAKE LAKINI ALIKUWA ANAFAHAMIKA SANA NA IPO SIKU AMBAYO MMUNGU AMEIWEKA ATATAMBULIWA NA ULIMWENGU KUWA ALIKUWA NDIO MR X

  21. Comment by Amina on April 9th, 2008 4:43 am

    we unayeeita amin usinizingue mi nimeandika ninachojua sasa unaniambia nilikua sina haja ya kuandika kivipi?kwani wewe nani?

  22. Comment by Mama on April 9th, 2008 6:07 am

    Asante sana wachangiaji hapo juu. Pia asante Albert hapo juu kuhusu case ya uhaini huyu mtu (ME X) hadi leo nimekuwa nikufuatilia ni nani hasa (his true identity), lakini sijawahi pata jibu. Kuna mtu anayejua jamani labda atuambie???

    Hayati Abeid Karume alikuwa ni m-Malawi. Babu wa baba yangu aliwahi kuniambia kuwa Karume alikwenda Zanzibar kipindi kile cha biashara ya utumwa akiwa mtoto mdogo ila ndio hivyo inafichwa kihistoria. Wakati huo wanyasa wengi walikumbwa na hii biasahara haramu kama vile Tanzania bara ilivyoathirika. Ndio maana watoto wake wamesoma Malawi. Hata rais Karume aliyeko madarakani hivi sasa watoto wake pia wamesoma Kamuzu Academmy nchini Malawi. Hadi leo ukienda Unguja kuna baadhi ya familia wanakwambia asili yao ni wanyasa. Babu wa baba alizaliwa unyamwezini Tabora na kuchukuliwa utumwani (Unguja) na amefia huko 1989 akiwa na umri wa miaka 93.

  23. Comment by Chris on April 9th, 2008 10:25 am

    Ntashukuru sana Bablii….

  24. Comment by Anon on April 9th, 2008 1:43 pm

    Visiwa vichache sana vina natives, vingi wakazi wake ni wahamiaji kutoka mainland kwenda kwenye hivyo visiwa hasa vikiwa visiwa vidogo, kwa mfano utawakuta wangazija na washirazi mafya (mafia) lakini si wangazija au washirazi tena washakuwa watu wa mafya, na hata visiwa vya Unguja na Pemba watu wa asili mbali mbali walihamia kwa shughuli za uvuvi na biashara hasa ya utumwa. Ndio maana kuna ishu ya ubwana na utwana. Lakini mbele ya Mungu watu wote sawa hakuna huyu aliumbwa kuwa bwana na huyu mtwana, mbora kati ya watu ni yule amchae Mungu!

  25. Comment by Rocky on April 9th, 2008 5:48 pm

    Kwa historia yenye picha nyingi ziendazo na maelezo mafupi yenye kina kuhusu masuala ya kijamii, historia, kisiasa na maendeleo toka 1898 – 2008 (karne 2 yaani miaka 200) tembelea website: http://www.zanzibarhistory.org
    Humo kuna khabari zitakazo jibu kiu chenu cha majibu kuhusu visiwa vya Zanzibar

  26. Comment by Kekue on April 10th, 2008 9:05 am

    Jamani kuna watu wanajua mambo mengi huku!!!! He!! Big up sn, mi sina tofauti na Amina manake nilikuwa sielewi chochote, asanteni sana wajameni.

  27. Comment by junior on April 11th, 2008 11:28 am

    waheshimiwa anony na baslali nashukuru sana kwa michango yenu ambayo kwakweli siyo tu imenitoa ujinga kuhusu siasa za zanzibar bali imeubadilisha mwelekeo wangu wa kuwaona cuf ni washari,waroho wa madaraka nk nk
    Lakini ningeomba mrudi tena na mnifahamishe haya yafuatayo
    1.Kama mapinduzi ya 1964 yalikuwa ni ya kumuondoa Mohamed shamte ambaye ni mpemba na nijuavyo mimi ni kuwa huyu bwana alikuwa waziri mkuu.je muundo wa serikali ya zanzibar kipindi hicho ulikuwaje?je kipindi hicho zanzibar ilikuwa ni monarchy na sultan ndiye alikuwa na kama kiongozi wa nchi na shamte ni mamluki tu?Na shamte kama waziri mkuu,je aliwaletea wadhira,manyanyaso nk nk yoyote watu wa unguja?
    2.Mnaweza kuniambia kwa nini mwalimu Nyerere alimpenda sana Dr.Salim A.Salim na hata kumpa vyeo vikubwa vikubwa wakati akiwa na umri mdogo tu na hata kumtaka awe Rais wa Muungano mara kadhaa ilihali wajumbe wa CCM zanzibar hawataki kabisa Dr.Salim awe rais wa muungano?
    Ntanguliza shukrani zangu

  28. Comment by zanzibar on February 20th, 2009 2:53 pm

    NYINYI WATANGANYIKA HAMUJUWI SIASA ZA ZANZIBAR ,TUWAACHIENI WENYEWE PLS

  29. Comment by mohd on March 28th, 2009 4:32 am

    MSAADA KWA ANE FAHAMU
    NINAVO FAHAMU MIMI KILA MZANZIBARI ANA KWAO
    KAMA MIMI NAISHI MJINI UNGUJA ILA KWETU NI MAKUNDUCHI ALIPOTOKA BABA ANGU NA KUNA KIAMBO CHAO (KIJIJI CHAO)NA FUMBA ALIPOTOKEA MAMA ANGU NA KUNA KIMBO CHAO JE!
    KARUME WAZEE WAKE WAMETOKEA WAPI NA VIAMBO VYAO VIKO WAPI? BABA AKE KATOKEA WAPI? NA KIAMBO CHAO KIKO WAPI? NA MAMA AKE KATOKEA WAPI NA KIAMBO CHAKE KIKO WAPI?

  30. Comment by Mwanamke wa Shoka (UK) on March 29th, 2009 6:05 pm

    wow…!!…miye historia niliiacha nikiwa form two…ati nikajikita kwenye mchepuo wa sayansi…kule warsaw….ila hapa BC nimepata a full course of history….

    thank you ever so much you all wadaus here.

    It has been an eye opener….a jaw-moving history session…

    truly, reconciliation seems to be a way forward….kama kweli TUNAMCHA MUNGU….

  31. Comment by castico on April 16th, 2009 4:20 pm

    Nyie mnaejitia kujuwa historia za Zanzibar toka lini? ikiwa utumwa basi ni nyie watu wa bara ndio mkiuzana wenyewe kwa wenyewe na kukamatana!! Na sisi wakaazi wa Unguja ndio tukikununuweni na kukuuzeni nje ya Zanzibar!! hebu niambieni nani aliopo Zanzibar mwenyewe asili ya utumwa na kununuliwa? hakuna !! Na ikiwa waarabu ndio waliokuwa wakinunuwa hao watumwa, hivyo kweli soko yake wangeiweka ndani ya makanisa? umesikia wapi warabu kuwa wamasihi khasa africa? wacheni kasumba zenu hizo, Zanzibar ina wenyewe !!

  32. Comment by Zous on May 5th, 2009 9:03 am

    Salamu kwa wote.
    Kabla ya yote napenda kumkosoa Bablii kwamba kitabu cha ‘UKWELI NI HUU” kimetungwa na mzee wetu wa kizanzibari ambaye anaishi nchi za falme za kiarabu anaeitwa Bw.Aman Thani na hakuwahi kuwa kiongozi katika SMZ bali ni mmoja katika vijana wa enzi hizo wenye nafasi za juu katika chama na serikali iliyoongozwa na HIZBU.
    Haya na tuendelee.
    Opinions nyingi zimetolewa hapo ziko nnazo zikubali na nisizo zikubali.Kuhusu kifo cha karume ni kwa sababu ya Uunguja na Upemba hicho nakataa katu! au tofauti hasama ya uarabu na uafrika ndio uliomtoa roho karume pia sio kweli.
    Kwanza ningependa kuanza wakati wa chaguzi za miaka 1961 ambazo ndizo zilizowavuruga Wazanzibari kwa ujumla hadi hii leo naandika hiki kiji comment.Muingereza aliuona mwanya mzuri sana wa kutaka kutawala visiwa vywa Zanzibar kwa kuwabagua Wazanzibari kwa kuchochea Uarabu na Uafrika na kulikua hakuna uhasama wa Upemba na Uunguja kwa wakati ule hilo mtambue vilivo!
    Well..alichokifanya(muingereza) ni kuona wengi wa Waunguja HALISI ni wenye kua na elimu na kujua nasaba zao atleast kwa miaka 120 iliopita ambao ni mchanganyiko ya waarabu wazawa wa Unguja na Waunguja ambao tunawaita au kujiita watu wa mashamba kama vile makunduchi,kizimkazi,tumbatu ..nk na hao wanosema chama cha hizbu ni cha waarabu basi wafuatilie kwa undani sanaa mana mwenyekiti wa chama Al marhum mzee Vuai kitoweo hakua muarabu alikua ni mzanzibari mwenye asili ya shambaa.
    Then kuna Wazanzibari wa kuhamia ambao wameishi zanzibar si zaidi ya miaka 60 kwa kipindi kile cha miaka ya 60.Sasa tizama wengi wa hao wenye kujiita wana mapinduzi na nasaba zao au kama kuna evident report inayosema kwamba mama au baba zao waliishi au kuwazaa wao zanzibar.Nawataja baadhi ya famous revolutionaries.
    1)Kaujore,2)Mfaranyaki,3)Saidi Washoto,na huyo fisadi al-khassah John okelo kama iko evidence inosema kama wazaliwa wa visiwa vya zanzibar na mfano mzuri mbona Okelo baada ya mapinduzi alipoanza kujilimbikizia masifa kama yeye ndio Raisi mbona Karume na watu wake walimtoa katika visiwa vya zanzibar na akina kaujore baada ya kupata uchizi kwa kuua watu bila ya sababu mbona alikimbilia mabara (mrima) kusiko julikana?!
    Then namsema Karume sasa lakini qabla ya hapo mimi binafsi ni mjukuu wa Afro shirazi kwa upande wa mama na Hizbu kwa upande baba ila kwa kipindi hiki sina chama mana zanzibar inakanganya na nitaitoa sababu baadae.Niliwahi kukaa na great grand father wangu sijui nimuite vipi kwa kiswahili na aliwahi kunitamkia binafsi na Mungu shahidi wangu “Abedi ni mdogo wangu anakuja Unguja namuona hivi” na mpaka leo ukiuliza wapi kazaliwa jibu hakuna!!!
    Turudi kwenye point.So wingi wa hawa Wazanzibari wa kuhamia walikua sio wenye kua na uwezo wa kifedha wala elimu kwahiyo waliishia kua makuli na mabaharia kwani kwa wakati ule Zanzibar ilikua bado ni maarufi katika trading in east Africa and every part of the world.Ndio hapa baada ya Wazanzibari halisi kutaka kupewa nchi yao kutoka chini ya mikono ya Muingereza ndipo Mama(Queen) akasema divide them and rule them lakini kwa nguvu za Mungu muweza zika FAIL!Baada ya Hizbu kushinda chaguzi za 1961 ndio Mama akaanza mbinu za chini kwa chini za ku-introduce divide them and crash them,hii haijulikani ila kwa wale waliowahi kufanya kazi za ukachero mana hadi leo zanzibar inasumbuliwa na divide them and crash them ambayo Nyerere ameirithi kutoka kwa Waingereza.Nyerere alikua na Tanganyika tayari baada ya 1961 na hadi leo kuna watu wanojua kwamba makubaliano ya nyerere na waingereza kupeana madaraka it was of Christian religeous agreement na zanzibar ilikua more than 99.3% Islamic state ambayo waingereza hawakuipendelea kwa wakati mwingi so nyerere was a secret weapon of the British.End of 1963 to beginning of 1964 i call this period a critical period for a devine change to Nyerere.Mikutano mingi ilifanyika kipindi hiki baina ya Nyerere na Karume huko ikulu za Tanganyika.Them Abdurahman babu akiwa na na agenda zake za kikoministi akaona aunge mkono mzee nyerere na karume kwani hakumjali karume kwa vile hakuwa msomi na mwenye hikma alimjali sana karume nakuuogopa ujanja wake kwa vile alijua vyema(Babu) kwamba Nyerere nia yake ni kuiteka Zanzibar tu!
    Chama cha Babu (UMMA PARTY)kilikua na vijana wenye hirmu ya miaka 25-35 ambao walipata masomo ya kutosha na familia zao zilikua zenye kujiweza na wengi wao walikua na asili za kiarabu na kingazija(Comorians).Hawa walipewa mafunzo ya kijeshi kwa siri huko Cuba na kuna evidence wakati wa mapinduzi wacuba walishiriki pia na Che Guevara alikuapo zanzibar kwani wakati huo walikua wamepiga kambi congo.So aloyapanga mapinduzi khasa ni Babu na Nyerere na sio karume ila yeye alikua ni front face na ili ku wash brains za waafrika au ati wanyonge ndio mana walewalio kua na mafunzo hasa ya kijeshi na kupigana hawakuitwa wana mapinduzi isipokua mmoja tu Sheikh Ali Mahfoudh na sababu ilikua ni kwamba kwanini asiwe hata mmoja ya wajuzi wa kijeshi kuitwa mwana mapinduzi na inafahamika kwamba Ali Mahfoudh ndie aliekua kamnda wa hao vijana waliopata mafunzo huko Cuba ambao walijiita comrades(na wao yakawafika yalowafika baadae kuwapa nchi unknowledgables)
    Sasa la kujiuliza kwavile tunaishi katika kipindi cha sayansi na teknolojia ni hivi serikali ya Hizbu ilikua haina jeshi mpaka wanyonge wapindue kwa mishale,mapanga na mikuki itaingia akilini kweli?
    Silaha ziliandaliwa kutoka mrima na nyerere pamoja na baadhi ya maaskari na hao makomred na wacuba ndio walokuja kupigana na vikosi vya Hizbu huo ndio ukweli na Marhemu Mohamed Shamte aliomba msaada kutoka kwa waingereza waliokua mombasa vikosi vya maji ili kuja kusaidia walikataa katu katu kama vile Zanzibar haikua chini ya common wealth Mungu atawalipa!
    Mapinduzi yameisha!..asubuhi nchi iko chini ya Afro shirazi sawa.Sasa hapa ndipo chuki na uchafu wa kila aina ukazidi kua mkubwa.Hao walojiita wanyonge ndio wakaanza kuingia majumbani mwa watu kuzini wake na ndugu za watu kuua vichanga kulawiti waume za watu..kama alivosema mmoja wetu hapo juu ZANZIBAR BADO INATOKOTA INASUBIRI SABABU YA KURIPUKA!..Namalizia hapo during the ero of 1960-late 60s.
    Kwenye mwaka 1969 wengi ya wasomi au makomred hawakuwafikiana na mambo alokua akiyafanya karume mana hali ya uchumi ilizidi kuwa ya hini chakula hakipatikani na alikua hataki kupewa ushauri probably may be alijihisi ni mtu wa chini kielimu so alitumia barberic tugh ndio Babu na watu wake wakataka kuandaa mapinduzi mengine mwaka 1972.Babu hakua kama nyerere au karume alikua ni mkoministi with “protocols” nyerere aliiletea Tanganyika uhuru well lakini aliimaliza kwavile hakua na economic knowledge na wala hakutaka ushauri kutoka kwa wachumi pesa zote zimekwenda kusaidia kukomboa nchi jirani leo hao nchi jirani ndio wanatuulia ndugu zetu mfano South Africans shenzi zao.So Babu hakupendelea the ruling system ya Karume mana nyerere ndio aliekua aki control financial support of zanzibar thats why ministry of finance was under Karume himself.Tarehe 7/4/1972 imefika ndio kina Homoud na wenziwe wakavamia ASP head offices lakini Homoud ndiye aliye vuruga mambo mana plan ilikua sio kumuuwa Karume ni kumlazimisha atangaze kwamba nchi iko chini ya mamlaka ya kijeshi na wengi wao ni hao makomred baadhi ni ngugu zetu wa damu.Hamoud had his own agenda hata ingelikua mimi kwa mambo aliofanyiwa ya kuambiwa amuuwe babaake mzazi pasipo kujua ningeingiwa na machungu.Karume kafa kizaa zaa chengine kikazagaa mitaani.Babu akatiwa ndani na nyerere na sio zanzibar jiulize why hapo! na makomred wengi wao wakamalizwa na baadhi yao hata maiti zao hazikuonekana hadi hii leo.Na kabla ya hapo Karume aliwamaliza baadhi ya mawaziri wake wasomi kwa vile walikua hawakubaliani na maamuzi yake.Nitawataja baadhi kwa majina.1)Kassim Hanga(maiti haijaonekana).2)Twala.3)Sheikh Saadallah.4)Dr Othman Sharif hawa wote walikua ni wasomi katika serikali ya Karume.

    Sasa nitagusia kipindi hiki cha uhasama wa CCM na CUF Zanzibar.
    Naanza na CCM.
    Ukweli ni kwamba CCM Zanzibar hawajawahi kua na ideological thoughts kwamba wao ni CCM ng’o!..kwani inachuki zake toka mwaka 1972 na wanaamini nyerere was a master mind of Karume’s assassination na wakaitilia mkazo pale nyerere alipounganisha vyama 1977 lakini kila mtu alijiogopea na kuchoshwa kwani Zanzibar toka 60s to 70s damu nyingi mno ilisha mwagika.So CCM Zanzibar itabaki kuwa jina tu lakini inside is and still will be AFRO SHIRAZI just so you know! na hilo CCM bara walijue mana mkorogo wa mafuta ya Pemba ndio litakalozaa kimeta chengine kuliko cha 1984.

    Sasa nakuja kwa CUF.
    Ningependa kuwachambua viongozi wa CUF lakini mikono imechoka na niko kazini nataka kuwahi trein nielekee pangoni kwangu.
    Wengi wa viongozi wa CUF walikua ni mawaziri katika serikali za SMZ ambayo inaongozwa na CCM.Sasa tuje sababu ya Seifu na wenzake kama vile kina Soud Yussuf Mgeni Maulidi Makame,Ali Haji Pandu n.k kukiwacha chama just like that.Ukweli Sefu ndio aliye anza haya mambo ya kuuleta UPEMBA na hii naisema wazi wazi na mimi sio mfuasi wa CCM na sitokua hata siku moja.Kipindi yuko waziri wa elimu alikuwa anawapa wapemba scholarships kisirisiri kwenye miaka ya 80 na kweli Wapemba waliitumia nafasi vilivo na wakasoma lakini sijui kwanini mpaka leo wako ovyo ovyo labda wanaogopana kupigana ndumba.Afisi ya waziri kiongozi wakati Sefu ndie waziri wake ilijaa wapemba na makatibu wake.Idara ya ardhi ilijaa wapemba ndio wakawa wanagawana ardhi huko BUBUBU zanzibar ndio pale washamba nao wakaja juu wakashtukia soo na kufatilia,vikao vya waasisi wa AFRO SHIRAZI wakakaa chini na kutuma vijana wao kama kina Nassor Moyo kumfata Nyerere amtoe sefu kwenye system but it wasn’t easy kwavile nyerere alimuamini mno Sefu kabla ya hapo na SIRI nyingi za nyerere bado ziko mikononi mwake(sefu)ndio mana akashindikana kuwa eliminated kwavile they didnt have any idea who else knew ndio mkamuona Sefu anapeta hadi leo na marupurupu wanamlipa anakulala kuku na wanawe then watoto wa wenzake wanakufa kwenye maandamano na wengine wanakatazwa kwenda mashuleni eti hadi KAFU(CUF)iingie madarakani.
    Kwa kumalizia solution ya kupatikana PEACE Zanzibar jamani aijuae Mola muweza,shughuli nzito jamani.Msiseme serikali tatu au mseto au white paper.Muhimu kwa Wazanzibari sasa hivi ni kutafuta njia ya kujiamulia mamlaka yake ya kiuchumi na siasa za ndani ikiwa ni CUF au CCM ya zanzibar tukae pamoja kisiwa kimedidimaa na huzuniiiiiii.
    Insha Allah kwa uwezo wake Mola atatufikisha.
    Amen!
    Kama nimekosea au kumuumiza mtu kwa maneno yangu naomba kumradhi.
    Zanzibar Forever!

  33. Comment by salum on October 12th, 2009 8:37 am

    mimi nipo upande wa bablii.asate bablii kwa kusema ukweli.wapingao hawajui historia.nahisi bora wakati wa sultan kuliko huu wakati wa luasa,,,,,,,,,,,,haahaaaaaaaa

  34. Comment by medi on January 25th, 2010 1:02 pm

    Mimi nipo Upande wa msema zous..Umenimaliza haswa Mungu akubariki..

Leave a Reply