Feedback / Comments
51 Responses to “RIPOTI YA RICHMOND;KUMEKUCHA!”
Leave a Reply
51
Comments
→ February 6, 2008 → Tags: Breaking News, Bunge, Siasa, Tanzania/Zanzibar →
Feedback / Comments
51 Responses to “RIPOTI YA RICHMOND;KUMEKUCHA!”
Leave a Reply
HAKUNA UBISHI WANATAKIWA KUWAJIBIKA,WOTE WAOLITAJWA ,HASA UKICHUKULIA TANZANIA NI NCHI AMBAYO INAMIKATABA MINGI YA AJABU AJABU HAINA MASLAHI KWA TAIFA INASAINIWA IPO KIMASHAKA MASHAKA UNASHANGAA NCHI IPO IPO TU YAANI KAMA WATU HAWAKWENDA SHULE,NCHI KAMA HAINA WASOMI NI AIBU NCHI KAMA HAINA MWENYEWE,HONGERA KAMATI WABUNGE TUNATAKA KUSIKIA UTAIFA SIYO UCCM SASA
mmmmmmmmmmmmmmmmmhhhhhh kazi kwelikweli
Hapa inaonyesha ni jinsi gani Tanzania tunadidimiza maendeleo ya wananchi hasa walala hoi. Kwani binafsi nadhani kwamba kama ubadhirifu huu utatokomezwa katika nchi yetu basi itafikia wakati tutafika malengo ya viongozi wetu kwamba ” Maisha bora kwa kila mtanzania” lakini mpaka sasa bado tunaendeleza “Bora maisha kwa kila Mtanzania”
Bila shaka hapa anaeumia ni Mwananchi tena mlala hoi na si mwinginewe.
Kwa kweli taarifa inasikitisha na inatisha! Hata mtoto wa miaka saba anaweza kubaini mapungufu! Ajabu TAKUKURU wakasema ni safi! Lakini haishangazi kwa TAKUKURU kusema hivyo kwani wao wanyonge wao ni watendaji wa vijiji na kata, mahakimu wa mahakama za mwanzo, manesi,! KWA KWELI TAKUKURU wanastahili pongezi kwa umakini wao! Kama kweli wameshindwa kuona hayo mapungufu ! tusiwalaumu bali tuwape hongera kwa kushiriki kikamilifu kutukaanga watanzania kwa mafuta yetu wenyewe!
Welldone Dr. Mwakyembe.
It is a big blow to the Government, PCCB and the office of Chief Justice. Very few MPs can have such a courage to submit such a wonderful report.
I tnink the time for change has come whether ‘they’ like it or not. We need more of Mwakyembes within the ruling party.
Mh. Dr. H. Mwakyembe na Wajumbe wote wa Kamati teule,
Naomba nichukue nafasi hii ya kipekee kuwapongeza na kuwashukuru kwa kutoa ripoti ya uwazi na ya kufichuo uozo wa mkataba wa Richmond kwa moyo wa uzalendo na wa ushujaa. Ripoti hii itarudisha imani ya Watanzania juu ya mienendo yao. Ninayo imani kabisa wapo viongozi waadilifu na wale wachache ndio wanaoharibu sifa ya wenzao kwa mienendo yao.
Ripoti imejieleza na imefafanua vizuri na kujibu maswali yote niliyokuwa najiuliza moyoni. Imenisikitisha sana kugundua kuwa serikali ilweza kuingia mkataba wa mabilioni fedha na kampuni ya mfukoni au “mission town”!.
Wito wangu: Kila mtuhumiwa awajibishwe kwa nafasi yake na zoezi liendelee katika maeneo yote yenye mapungufu hasa katika mikataba.
PONGEZI NYINGI KWA KAMATI KWA KUWA WAZALENDO NA WALE WOTE WALIOSIMAMIA KIDETE SUALA HILI KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE. BINAFSI MMENIONGEZEA MATUMAINI YA KUWA SIKU MOJA MTANZANIA WA KAWAIDA ANAWEZA KUYAFAIDI MATUNDA YA NCHI YAKE.
- TUUCHUKIE NA KUUKATAA UFISADI
- TUSIMAMIE HAKI SIKU ZOTE HATA KAMA NI KWA VITISHO
Mambo kama haya yanatufanya tumkumbuke Baba wa Taifa. wapi maadili ya viongozi, wapi transparency? Riport Hii ni sawa na kuponyokwa tauro kiunoni ukweni pia sawa na kioo cha kujitizama tunakoenda. Sasa hii ni Richmond pekee, vipi mikataba mingine? sijui 2020 Tanzania itakuwaje!! Kwa nchi zilizopevuka katika maadili ya uongozi kama Wingereza, hii ilikuwa haihitaji mjadala wa hao wahusika kuwaachia wengine waongoze. Hata hivyo wanawajibika chini ya Ministerial Responsibility, watoke tu wasione aibu. Tatizo letu waTanzaia (African) Ushikaji na undugunization ukiuchanganya la politics ndo haya tunayoyaona. I wish mwalimu could be here! Maana hatuna sasa mtu kama kiranja au Guardian wa kumwogopa na kuweza kusema NO!
Ama kweli mambo sasa Tanzania siyo tena Transparency bali Nakedness!. Mambo yote hadharani na huu ni mwanzo tu.
For once Tanzanians now know what they want. Nothing but the truth. Let us wait and see the results. Hope it will be a lesson for our leaders both in public and private sectors to learn to be accountable or otherwise be kicked out. And at the end of the day parliamentarians should not be appointed to be Ministers; instead they should stay in their constituencies and provide political leadership those who elected them to resolve their problems.
Katika hali ya kawaida kwa viongozi wote waliotajwa na report ya Kamati teule ya bunge wanatakiwa kujiuzulu. Kuendelea na madaraka itakuwa ni sawa na ugaidi kwa inchi na wananchi wake. Wao si viongozi pekee katika nchi hi,i wawape watu wengine nafasi wawatendee haki wananchi wa Tanzania. Nawapongeza wabunge wetu kuamka katika usingizi mzito waliokuwa nao miaka ya nyuma ya kupitisha mambo mbali mbali ya serikali bila hata kujua kilichomo ndani, kwa ushabiki tu wa kisiasa. Ni wakati muafaka sasa kuweka maslahi ya nchi mbele na ubinafsi wa mtu na familia yake kapuni. Inawezekana kila mtanzania akaishi maisha mazuri kama kila kiongozi atatimiza wajibu wake na sio mazoea ya kuitwa mheshimiwa. Tunamwomba mheshimiwa Lowasa achukue uamuzi wa busara kwa kuonyesha mfano kwa kujiuzulu. Kuna maisha pia pasipo kuwa kiongozi au waziri.
Nimesikiliza habari chanel 10 kupitia jumptv wanamwonyesha Luwasha,Msabaha na karamagi wakati ripoti inasomwa wala hawana wasiwasi,yaani nimeingiwa na mtimanyong0 kiasi cha kutamani kujichukulia hatua mikononi kama vile wanavowafanya vibaka bahati mbaya niko mbali,nina matumaini kama hawatatoka ndani ya baraza la mawaziri na kwamba 2010 tusiwaone tena kama Prof.Mbilinyi vinginevo tutatafuta sababu yoyote kuhakikisha ccm wanatoka madarakani.Watanzania tumechoka kuibia wakati tunatazama tu.
Hongera kwa ripoti iliyo wazi na kweli.Kwa maana wananchi wamechoshwa na viongozi ambao wanaonekana kuwa na busara kwa sababu ya nywele nyeupe zilizopo kichwani kumbe ni pambo la jeneza ndani kuna maiti ya ufisadi.
Mwenyezi Mungu, Mungu wa Rehema; mlinde Mh. Dr. Harrison Mwakyembe (Mbunge wa Kyela) pamoja na Wanakamati wenzake, dhidi ya yule muovu shetani na ma-ajenti wake ambao watataka kuwamaliza au “kuwamwagia tindikali”. Amen.
Hapa ndugu Watanzania, tusubiri uamuzi wa Mheshimiwa Rais wetu Jakaya Mrisho Kikwete. Uozo wote umeanikwa, na hata TAKUKURU tuliokuwa wengi tunaifagilia, kumbe ni ya “RICH-MONDULI”? du siamini niliyoyasoma kwenye taarifa hii.
Mungu Ibariki Tanzania na watu wake. Amen
Hongera sana Dr. Mwakyembe na wanakamati kwa ripoti nzuri na pia kwa kutokutafuna maneno wala kuficha majina ya wahusika.
Hivi mliotajwa kuhusika na uozo huo wa Richmond mnasubiri nini madarakani? Hivi ni lini mtakuwa responsible & accountable kwa matendo yenu.?! Juu ya hilo Richmond ilijitangaza kwa uongo kuwa inafanya shughuli mbalimbali hapa Tanzania, hivi kweli maatapeli wameshafikia hatua ya kutumia jina la nchi yetu kwa manufaa yao!? Mhh kweli Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu.!
John Nolan (kama jina sijalikosea) aliposema Tz ukiwa na $5 kama mtaji ndani ya miaka 5 unakuwa bilionea hakukosea maana unatajirika kwa kula deal na viongozi wakuu serikalini.
Hii ya Richmond ni mwanzo tuu, hakuna lenye mwanzo lisilokuwa na mwisho, Chama Cha Mafisadi dawa yenu inachemka jikoni. Kura ya wananchi/mlalahoi iliyowaweka madarakani ndio hiyo hiyo itakayowatoa 2010.
Just wait and you will see.
Ila sitashangaa kuona wahusika hawachukuliwi hatua yeyote zaidi ya JK kuunda tume nyingine ya kuwachunguza!
Mungu ibariki Tanzania.
YA BALALI NA BOT NDO YASHAPITA !! SASA YA LOWASSA NA RICHMOND NAYO YATAPITA TUTASAHAU KWA VILE KICHAKA ANAKUJA NDO TUTAZUBALIA HUKO AKIONDOKA ZITTO NAE ATAKUJA NA RIPOTI YAKE BASI TUTAHAMIA HUKO HAKO NDO KAMCHEZO KETU,HATUONI CHA KUWAJIBISHWA WALA NINI.
USHAURI WANGU ONDOA LOWASA WEKA MWAKYEMBE KUWA PM,NA DR SLAA KUWA WAZIRI HARAKA.
wabongo wenzangu tusishangilie ripoti tu,ila naomba tusubiri kushangilia maamuzi yatakayochukuliwa na wahusika wa mkataba huo,na pia rais ambae aliunda hiyo kamati,ila mpk hapo alipofikia dr.mwakyembe ni pazuri,na hongera kwa kuthubutu.
huyo anayesema kichwa cha wendawazimu, sasa naona huu ni mwaka wa kufichua mafisaid wote, na huyo karamagi ni namba moja, mwambieni atoe hiyo mitaji ya madini anayosign na kuwapa wananchi maskini, hafai huyo atolewe mara moja.
Mheshimiwa Mwakembe na wajumbe wengine wa kamati ninawapongeza sana kwa kazi nzuri na kwa uwazi mkubwa kwenye hii kashfa ya Richmond. Infact mmeonyesha mfano mzuri kumbe bado kuna watz safi ambao ambao wanaangushwa na mafisadi wachache pia.
Hapa hakuna la kuunyaunya Lowasa,Karamagi,Msabaha,Mwaipungu na hao wengine CHONDE CHONDE TUNAOMBA MJIUZURU MAPEMA KABLA HATUJAJA KUWATOA OFISINI JAMANI HII NCHI NI YETU WOTE SI YENU PEKE YENU MMETUTIA AIBU SANA KAMA NCHI.
Lakini Nyerere alimkataza alimwambia Lowasa “hata wewe EDWARD! Rudisha hizo fomu ulizochukua haraka sana kabala sijakuumbua hadhara”.
Tukamuona mnoko. Lakini kale kazee kalikuwa kanaona mbali.
Matokeo yake ndo haya sasa.
JK nae sijui atasemaje maana huyu ni “mshkaji” wake wa pile sasa anabowa.
Wa kwanza alibowa pale NJIA PANDA YA KAWE
Hongera sana kwa Kamati Teule ya Bunge kwa kufanya kazi yenu without fear or favour,am looking forward to the steps to be taken against all the accused.Its high time tuwe na viongozi wanaojali maslahi ya nchi sio wanaojali maslahi yao binafsi na familia zao.
Hongera kwa kamati teuli,
Watanzania tumechoka tunahitaji maamuzi ya haraka.
Mwenyezi Mungu awe nanyi Kamati nzima ya Dr Harrison Mwakyembe. Kwa kweli mmefanya kazi nzuri sana sana ambayo haijawahi kutokea kabisa. Mungu awajalie yote yaliyo mema na awalinde na mabaya yote. Aminaaaaa!!
Umefika wakati Rais kutambua ukweli, na kukumbuka ushauri aliopea alipomteua Waziri Mkuu pia Marehemu Baba wa Taifa.
Kuonyersha kutokua na imani nae(waziri mkuu). Tunapendekeza mali za mafisadi zote zifilisiwe kwa manufaa ya umma ambao umekuwa ukiteseka kutokana na ufisadi wao. angalizo kwa mawaziri watakaoteuliwa kufuata maadili na miiko ya uongozi kama ilivyokuwa wakati wa serikali ya awamu ya kwanza.
Dr.Harrison Watanzania tumekukubali umekomaa kisiasa na kitaaluma .Ripoti yako imeweka kila kitu bayana hakuna kuogopana wala kuoneana huruma.
Watanzania tuige mfano huu wa Dr. Mwakyembe kuwa wakweli.
Mungu akubariki sana .
Mmmmmm! mi chimo kabichaaaaaa kwa kweli.
ndugu zangu, watanzania wenzangu tuzame katika maombi kumuomba Mwenyezi mungu,atuongoze tufike mahali tuwe na viongozi wenye uchungu na huruma kwa nchi yao,pia kuwalinda wachache wanaojitolea kufichua na kukemea maovu na ufisadi,
“EE MWENYEZI MUNGU AWALINDE,UWAONGOZE WATANZANIA WACHACHE WANAOJITOLEA,NA KULIA KWA AJILI YA WATANZANIA WENZAO/ NCHI YAO AMBAO UMEKUWA UWANJA WA MAOVU NA UFISADI”AMEN
Nimeisoma kwa kina taarifa na nimeilewa.
Sasa nahitaji ninye maji japo bilauli moja.Nivute taswira ya maisha yetu sisi wa hali ya chini kisha nimwage MAONI na MAONO.
Nampongeza sana Dr.Mwakyembe kwa ujasiri aliounyesha wakati wa kusoma hiyo riport, ningekuwa karibu ningekupa glass of water maana koo lilikauka kwa ujasiri.
Sasa tunaanza kuamka, mimi nilikuwa nazani ni maneno ya wakosaji kumbe ni kweli aibuuuuuuu!
Lakini tayari PM LOWASA ashatangaza kujiuzuru safi sana na waliotajwa pia wajiuzuru haraka ili nafasi zao zishikwe na wenye uwezo kiutendaji.
Jk, pls pls waadabishe haraka hao watu na umpe UPM MAGUFULI AU MWAKYEMBE WE NEED CHANGES!!!!!
Hongera Kamati.”Huu ndio utumishi makini na uliotukuka aliotupa Lowasa”Kwa kipindi cha miaka miwili.Huu ndio uchumi unaopaa.Ama kweli Siasa za Tanzania zimejaa Porojo.Ukienda Keko,segerea na kwingineko wamejaa wezi wa simu,kuku,n.k.Mafisadi wa Kimataifa wamekaa wanakunywa Kahawa raha mustarehe sisi huku tunagombana na Tanesco kwa nini wanapandisha Bei za Umeme.Kumbe majibu akina Lowasa wanayo wamekaa kimya.Ama kweli wajinga ndio waliwao.
John Stambuli.
Yani katika siku niliyofurahi maishani mwangu ni leo ,hongera Mr. Lowasa but usione wanakuonea its your responsiblity .
Hayo ndio matokeo ya ufisadi .
Mheshimiwa saini haraka hiyo barua ,Walala hoi tumechoshwa na watu hawa na waliobaki msisubiri kuwajibishwa timueni taratibu .”Mitaji Mnayo”Big up Mwakyembe ripot.
Mmmmmmmmmmmmmmmm sasa uwazi na ukweli ndio huo.Ninapongeza kamati nzima kwa kazi nzuri.Watanzania tuombe wahusika wachukuliwe hatua kali ili iwe fundisho.Hata PM kujiuzulu ni jambo zuri kwani uozo unasikitisha.At least wangeiba then wafanye mambo ya maana hata kujenga shule kusaidia yatima n.k.Mtu mmoja unajilimbikizia hela nyingi hivyo Je unajua ukifa unaacha vyote?Kwanini usisaidie wengine.
Watanzania wenzangu wenye mapenzi mema na nchi yetu tuiombee Tanzania ili mambo haya yasiendelee.
asante sana kwa kuwa muwazi wa kuweza kupata ujasiri mkubwa kama wako nina penda sana wananchi wote tukiwa na msimamo kama wako tutapata maendeleo mungu akusaidie!
Kweli yule msanii alieimba machoni kama watu alikuwa sahihi. Leo tumethibitisha nani (wananchi tusiofuatilia mambo ya kisiasa) aliekuwa anajua kama haya yangefanywa na mtu kama Lowasa, lakini ukweli ndo huo tumepewa. Sasa Tanzania imechangamka, sio kama enzi zileeeee. Tunaomba wabunge wetu wa ccm muendelee kuwa na msimamo kama huu. Kama kitu ni cha ukweli hivi msiwapinge tu wapinzani fichueni mambo ili tuijenge nchi yetu.
Kibo, Kibo!!!! He!!!!!!!!!! Yani ndo ilivyokuwa?????????????????????? Dr. Makyembe Hongera kazi nzuri baba, mh!!! mimi hata siamini!!!!
Watanzania tunataka majasiri kama Kina Mh.Mwakyembe.Mambo ya itikadi za chama tuache.tuangalie utaifa ktk kutetea ukweli.
Kama Rais atakua muungwana naomba afanye kitu cha kuwaridhisha wananchi,na asikubali kudanganywa otherwise ana interest.
Sisi tunakua masikini kwa sababu ya watu wachache wenye ulafi uliokidhiri.
Hii isitufanye tusahau BOT naomba pia ifuatiliwe kwa karibu.
Inasikitisha sana kuona waziri mkuu ndie anayeshiriki kuongeza ufisadi. Lowasa!. Wewe ulikuwa ni waziri mkuu au waziri fisadi wa juu. Mkapa alipokuita ni askari wa miamvuli alikuwa ana maana gani? Au ni miamvuli ya kukinga ufisadi usinyeshewe na mvua ya kupambana na uozo uliopo ndani ya serikali?. Nijuavyo mimi, mtu mpaka afikie kwenye cheo cha waziri mkuu, ni lazima vyombo husika vihakikishe kuwa mhusika yuko clean. Lowassa aliwezaje kupata hicho cheo wakati ni fisadi wa kutupa? Mimi naona serikali ya Bongo imejaa mafisadi wengi sana. Simuamini kiongozi yeyote yule, hata rais. Na sasa nangojea kwa hamu utekelezaji wa ripoti tandawazi.
Mimi nampa hongera sana mhe rais kwa kuweka “ubraza” pembeni na kumwadabisha swahiba wake.
Ukiendelea na mwendo huo huo labda watanzania tutarudisha imani yetu kwako.
Natoa pongezi kwa kamati teuli kwa ujasili mkubwa na vile vile nimefurahishwa na Mr Lowasa kujiuzulu lakini nataka waziri ajue kuwa hata kama hakuhusika kwa kupata fungu basi anawajibishwa kwa kutuweka hapa tulipo na kudidimiza maendeleo ya kwa kuingilia kazi isiyoyake na uzumbe kwa ujumla. Asiilaumu kamati kwa kumtaja wao wameangalia kwanini alikuwa sana katikati ya huo mradi kama waziri na kuchukua uamuzi mkubwa bila kuwahusisha wataalamu. Mh. usiwechukie wanakamati unawajibishwa kwa uzembe wake wa kulipa taifa hasira na kumuumiza mwananchi maskini. Na kama unausika kwa namna moja au nyingine sheria lazima zichukuliwe zidi yako na uadhibiwe pamoja na kuchukuliwa mali zako zote.
Hongera sana Dr. Mwakyembe na kamati yako, pili hongera watanzania kwa kupata mwamko na kuanza kuona mambo kwa undani wake. Nawashangaa sana wabunge waliowapongeza mafisadi waliosema eti wameonesha nia yao ya kuachia ngazi(ku-resign). Sijui kama wanatambua kuwa ku-resign si swala la hiari, kwa kifupi tumechoka na hatuwataki. Mh.Raisi, kete yako imebaki moja, tulia chagua baraza la mawaziri bila kuzingatia nani alikusaidia wakati unachaguliwa katika chama chako (CCM). Watanzania tulishangazwa sana na jinsi ulivyotengeneza team yako ya mawaziri, kwa sababu uliwajaza marafiki zako ambao ndo hao waliokuja kuchuma jasho la mlala hoi na mlipa kodi masikini mtanzania. Kuna watu wazuri sana ndani ya serikali ila sasa wazuri hamwataki maana watawaumbua! Dr. Kafungua njia, ila pia kuna vichwa vingine vimo humo humo ndani ya bunge ambavyo hasa mi nawesa sema ndo walioleta hii changamoto kufika hapa tulipo fika. MUNGU akupe busara ya kuchagua baraza jipya wachapa kazi na wenye njaa ya maendeleo ya nchi. Last, please please Mr. President, friendship does not govern but rules to its benefits.
Kaka K
naomba kwanza kupongeza tume iliyofanya kazii hii kubwa na nzuri ikiongozwa na Dr. Harrison. pili naomba kuwapongeza wabunge wote waliochangia hoja jana bila kuwapongeza walio jiuzulu.
hivi kwanini tuwapongeze watu kwa kufanya kile ambacho walitakiwa kuwa wamekifanya kabla hata ya tue kuundwa?? kwanini tuwapongeze watu kwa kutimiza wajibu? tafadhali nadhani hapa bado kuna tatizo, hawa watu wafikishwe mbele ya sheria, inachosha na kukatisha tamaa kuendelea kuona hawa mafisadi wakiitafuna nchi, kujiuzulu haitoshi tena naongeza haitoshi!!!!!!
na danganya toto ya balali na BoT isisahaulike.
MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA
Wow!!!! Hongera Dr. Mwakyembe na Kamati teule! Mungu awabariki na kuwafunika dhidi ya mafisadi na waovu.
Hongera Mhe. JK – sasa tunaamini kuwa uliposema “maisha bora kwa watanzania” ulimaanisha lakini ulizidiwa na mafisadi walionyonya fedha yote ya Watanzania.
SASA MALIZIA KAZI KWA KUWAFICHUA MAFISADI WOTE WALIOHUSIKA NA MIKATABA MIBOVU NA KUHAKIKISHA WANARUDISHA FEDHA ZA WATANZANIA.
ASANTE KWA AZMA YAKO YA KUTAKA KUTUONDOLEA LAANA YA MUNGU JUU YA NCHI YETU ILIYOTOKANA NA UFISADI!!
Mungu akubariki na azidi kukupa hekima, maarifa na ufahamu ya kufanya yale unayopaswa kufanya kwa wananchi waliokuchagua kwa imani kubwa.
ALUTA CONTINUA
hombiz naungana nawewe hata mimi simwamini kiongozi yeyote wote lao moja sema hapa ilikua hamna jinsi ndomana wametajana kikwete pia mtu wa madili tu huyu….sijui nikutokana africa tumezaliwa katika hali duni ndomana mtu anashindwa kutumia madaraka yake ipasavyo anaishia kujilimbikizia tu
Hongera Dr. Mwakembe kwa kuwa muwazi.
umeonyesha ujasiri wa hali ya juu sana
big up
Hii ngoma Lowassa hata Hayati Mwl Julius K Nyerere alikwisha ikataa ni corrupt mno na tamaa tele.Yaani we mtu kweli unathubutu kuwaumiza wananchi kwa kiwango ambacho hakielezeki na unawaumiza katika namna ambayo ni endelevu.Ilitosha kuchukua fedha katika ununuzi wa mitambo lakini uliweka mazingira ya kulipwa capacity charge ambayo ni kubwa na itaendelea kulipwa kwa kipindi kirefu.LOWASSA unastaili kufilisiwa ,kuzuiwa kabisa kujihusisha na siasa pia kujihusisha na shughuli zozote za kutumikia jamii kwa sababu wewe si binadamu wa aina ya watanzania.
Inabidi atoke hadharani na awaombe radhi watanzania ili akubalike tene kama ni raia wa tanzania kwa kweli Lowassa ametengwa na jamii hii anahitaji utaratibu wa kurejeshwa kwenye jamii.
[...] Haki, BongoCelebrity and Muhidin Michuzi posted photos of those implicated in the scandal and the actual executive [...]
Kweli Ningekutetea Lowassa lakini hii ni too much! Naomba nikusaidie kidogo kuwa ungepewa nafasi ujitetee maana inaonyesha hapo bungeni mna mabif ya kufa mtu!Wapo watu kibao wanakula hela(kodi) zetu kupita kiasi! Tunataka wote wawajibishwe p`se!
Uwiii…..jamani SYSTEM YOTE MBOVU hadi kwa viongozi wa kijiji sijui tutafanyaje???
TUNAOMBA BASI WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU TUPEWE ASILIMIA MIA MOJA KULIKO PESA YA WALIPA KODI KULIWA NA VIONGOZI WAANDAMIZI WA SERIKARI.
NIMEKUKUBALI MZEE MWAKYEMBE. HIYO NDIYO KAZI TULIYOWATUMA KUTUWAKILISHA IPASAVYO. (NAKUPA BIG UP.) TUKO NYUMA YAKO KUKUUNGA MKONO KWANI KWA MOYO HUO TUTAYAFIKIA MATARAJIO YA WATANZANIA WALIO WENGI.
tumeshaona matunda ya wao kukubali na kujiuzulu lkn kwa nn basi wasingetolewa na ubunge kabisa ili tuwe na watu tulio na imani nao kwan bdo tuna mashaka na serikali yetu, ktk hbr oia inaionyesha rais pia kahusika nae ikiwezwkana pia ajiuzulu hatuna tena imani naeeeeeeeeee hongera mwakilembe, wajitokeze wengine km ww, lkn wanogopa yatawafikia yaliyompata mama kilango malecela. Mungu awadhibu viongozi wetu wawe na huruma na woga kwa wananchi waoooooooooo……………
SORRY ME NLIKUWA NAOMBA KAMA INAWEZEKANA MNITUMIE HIYO RIPOTI YA RICHMOND.NAOMBA KAMA INAWEZEKANA MTUMIE HII EMAIL ADDRESS YANGU