MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

Ukiachilia mbali blogs au tovuti mbalimbali zinazojitahidi kuhifadhi historia au kumbukumbu za watu wetu mashuhuri mtandaoni,mradi kama Wikipedia ndio pengine unaongoza hivi sasa katika kuhifadhi historia mbalimbali,kuelimishana,kupashana habari nk.Uzuri ni kwamba Wikipedia inaandikwa katika lugha mbalimbali ikiwemo yetu ya Kiswahili. Burudani zaidi inakuja pale ambapo wote,mimi na wewe,tunaweza kuchangia katika kuziandika historia za watu wetu mashuhuri.Hapo hakuna mjuzi zaidi ya mwingine.Kila mtu anajua kitu fulani kwa hivyo anachangia. Kama nitaandika kwamba Tanganyika ilipata uhuru mwaka 1962,nitakuwa nimekosea.Bila kutoana ngeu,unaingia unanirekebisha tunapata ukweli.Huo ni mfano tu,Wikipedia ina maarifa mengi zaidi.

Kwa mfano; Hayati Bibi Titi Mohamed,pichani kushoto akiwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ni mtu mashuhuri na muhimu sana katika historia ya nchi yetu achilia mbali juhudi za ukombozi wa mwanamke.Pamoja na hayo,ukienda kwenye ukurasa wa Wikipedia wa Kiswahili,utakuta kwamba habari za Bibi Titi zimeandikwa kwa kifupi sana. Ni kama vile hakuna anayejua mengi kuhusiana na Bibi Titi,si watu wa enzi zake wala wa enzi hizi.Mbali na uchache wa habari za Bibi Titi kwenye Wikipedia,kwa ujumla mtandaoni habari zake zipo kwa uchache sana.Tunaishi katika nyakati mpya,za habari na mawasiliano ya hali ya juu.Ni muhimu tukazitumia katika kuhifadhi historia pia.Sio za Bibi Titi tu bali wengineo wengi waliowahi kutokea,waliopo na watakaoendelea kutokea nchini mwetu.

“Bibi Titi Mohammed ni mmoja wa wanawake wa kwanza kushika nafasi za ubunge na uwaziri nchini Tanzania na pia ni kati ya wanawake wa kwanza kujiunga na harakati za kugombea uhuru wa Tanganyika.

Mwaka 1969 Bibi Titi Mohammed alikamatwa na mwaka uliofuata alifikishwa mahakamani kwa kosa la kula njama ya kutaka kupindua serikali. Katika kesi hiyo, Bibi Titi alikuwa ni mwanamke pekee katika washtakiwa 7. Baada ya kesi hiyo kusikilizwa alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha. Hata hivyo, mwaka 1972 alisamehewa na rais Julius Nyerere

Ukienda kwenye ule ukurasa wa Wikipedia wa Kiingereza kumhusu Bibi Titi,utagundua kwamba pameandikwa mambo mengi kidogo kumhusu Bibi Titi. Kwanini? Mara nyingi tumekuwa tukiacha historia yetu,ya watu wetu,iandikwe na watu wengine.Wakiandika wanavyotaka wao,kwa kuipotosha, tunalalamika.Ajabu huwa hatuna muda wa kuirekebisha. Zamani tulikuwa na sababu,hatuna tena.

Kupitia kurasa kama Wikipedia,tunaweza rekebisha historia zetu.Kwanini leo usijiandikishe katika Wikipedia na kuanza kuchangia chochote unachokijua kuhusu historia,siasa,jamii zetu? Unaonaje kama tukianza na kupanua zaidi historia ya Bibi Titi Mohamed? Kumbuka unapohifadhi historia huhifadhi kwa ajili yako tu bali vizazi na vizazi vijavyo.Binadamu asiyejua historia yake ni….

Picha kwa msaada wa Issa Michuzi.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

13 Responses to “BIBI TITI,WIKIPEDIA”

  1. Comment by Ombeni on January 15th, 2008 10:04 am

    Ni kweli kabisa mlichosema hapa BC.Lazima tujitahidi kuandika historia zetu sisi wenyewe.Naomba kuwa wa kwanza kuitikia wito.Najiandikisha leo na wikipedia.Thanks a lot.

  2. Comment by Freddy Macha on January 15th, 2008 11:54 am

    Yaani ndugu mhariri wa BC umesema jambo la maana sana hapa juu. Si kuhusu suala la Bibi Titi, pia kuhusu sisi wote kushiriki katika kamusi huria ya Wikipedia.
    Nimekuwa najiuliza miaka mingi kwanini wale wanawake wanaopigania sana ukombozi wa mwanamke hawajaandika lolote kuhusu mwanamke muhimu kama huyu?

  3. Comment by Mama wa Kichagga on January 16th, 2008 1:09 am

    MUNGU AILAZE ROHO YAKO MAHALA PEMA PEPONI MWANAMKE WA SHOKA.

    WEWE NI MFANO WA WANAWAKE WENYE MOYO WA KAZI, NIKISOMA HABARI ZAKO NATAMANI SANA MAISHA ULIYOISHI.

    HATA WASIPOKUANDIKA KWA KIREFU SHAURI YAO ILA MIOYONI MWETU UMEANDIKWA KWA KIREFU – PUMZIKA MAMA KAZI ULIFANYA NA ILIONEKANA. ULITUWAKILISHA VEMA SANA INGAWA ULIKUWA PEKE YAKE MWANAMKE WAKATI ULE WA UBEBERU WA MFUMO DUMU – HAKIKA UTAKUWA ULIKOMA UBISHI MAANA SIJUI KAMA WALIKUPA HATA PUNZI UONGEE!

    KAZI NZURI SANA ULIFANYA – TATIZO MAANDIKO NI SIRI YA WALIOSHUHUDIA SISI TULISIKIA TUU REDIONI WAKATI ULE!

  4. Comment by Mchunguzi on January 16th, 2008 5:16 am

    Duh! huo wa BibiTiti ni mkono au paja!?!
    Khaa!

  5. Comment by Mama wa Kichagga on January 17th, 2008 3:52 am

    MKONO

  6. Comment by Dinah on January 17th, 2008 9:24 am

    Bibi Titi alikuwa mwanamke wa kwanza ktk mengi Tanzania sambamba na Kawawa, Nyerere as kwa mwanamke alipaswa kukumbukwa zaidi ya jina lake kuwa jina la barabara hapo ktkati ya jiji…….Jamii na Taifa kwa ujumla inaonyesha kusahau kiaina. Wanawake wanaharakati embu mkumbukeni Bibi yetu huyu ei?

    Samahani nimetoka nje yakinachozungumzia…..

    *Nikirudi kwenye mada husika, ni kweli kabisa mimi nitakwenda kuandika au kuongezea historia ya Sitta (spika wa Bunge), Hayati Maswanya na Hayati Korimba.

  7. Comment by Upendo Furaha on January 17th, 2008 1:22 pm

    Ukiona vinaelea, ujue vimeundwa.
    Ndugu wadau wenzangu wa B.C. Tujue kuwa ukiona Nchi yetu ilipofika sasa, kuna watu ambao walijitoa Mhanga kwa ajili ya maendeleo yake.
    Hivyo tumshukuru Mungu kwa kutunyanyulia watu hao (Nyerere na Bibi Titi) ambao ndio Waanzilishi wa Taifa letu.
    Mungu Ibariki Tanzania. Mungu Ibariki Afrika, Mungu wabariki Walimwengu.
    Nawasilisha.

  8. Comment by amina on January 18th, 2008 6:47 am

    jamani wakubwa wa nchi lakini wanafaidi..mi namjua bibi titi tulikua tunakaa nae upanga watoto na wajukuu wote wapo mtoni…hiyo historia unaweza ukaiongezea hapo ndugu mwandishi au nimetoka nje ya topic

  9. Comment by ndesanjo on January 19th, 2008 8:46 am

    BC mmesema sawa kabisa. Asante kwa kutumia mfano huu wa Bibi Titi kuonyesha umuhimu wa kujihusisha na mradi kama wa Wikipedia ya Kiswahili ili tuweze kuenzi watu kama hawa kwa kuweka rekodi nzuri ya maisha na kazi zao kwa ajili yetu na vizazi vijavyo.

    Anayependa kushiriki kuandika Wikipedia, anachotakiwa kufanya ni kwenda hapa: http://www.sw.wikipedia.org
    Maelezo ya jinsi ya kushiriki sio magumu kuyaelewa.

    Au pia unaweza kusoma makala hii ya “Wikipediolojia” inayoeleza jinsi ya kuhariri na kuandika makala kwenye Wikipedia:

    http://www.jikomboe.com/?p=1573

  10. Comment by titi on January 22nd, 2008 1:55 pm

    Nawapeni Ongera sana kwa kuanzisha website hii kwani siku zote nilikuwa nasema wanawake wa tanzania siwaelewi wanawezaje kukumbuka siku ya kuanzimisha siku ya wanawake tanzanina bila ya kumkumbuka mwanzilishi mwanzilishi wa chama hicho na mpigania haki za wanawake ktk uongozi wakati huo hakika bibi huyo aliona mbali ingawa hakusoma kama hao waliosoma sasa.Ongereni sana mimi ni mjukuu halisi wa bibi huyo.MUNGU AILAZE PEPONI ROHO YAKE AMINA

  11. Comment by FIDELIS FESTUS on July 30th, 2009 5:30 am

    Nyie niwa ukweli kwa tafiti na nimewasoma nawapa big up sana

  12. Comment by Penye Moshi Pana Moto on November 7th, 2009 12:28 am

    Je nini kilichowakuta bibi titi mohamed na sheikh suleiman takadiri ambao wote ni vigogo wa TANU? wote walitengwa na marafiki na ndugu zao, wakakebehiwa na mwisho wakafa vifo vya upweke kabisa.. Usimpinge baba julius, lake lazima lipite!!!!

  13. Comment by munna on December 5th, 2009 9:26 am

    nasema asanten sana kwa wote wanao mkumbuka bibi yangu kwani bila ya yeye wanawake tusinge weza kufika hapa tulipo fikia. na kazi kubwa sana alioifanya hapa nchin kwetu basi tuendelee kumkumbuka mara kwa mara bibi yetu huyu wa TANU.

Leave a Reply