MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

 

Ni vigumu, nasema ni vigumu.Haiwezekani.Huwezi kuizungumzia fani ya uandishi wa fasihi (literature) nchini Tanzania na usimzungumzie Shafi Adam Shafi(pichani) na bado ukaeleweka unazungumzia nini. Huyu si tu mwandishi, bali hazina ya historia ya nchi yetu, mila na tamaduni zetu, uandishi wa riwaya uliobobea. Ingawa kitabu chake cha KULI ndicho ambacho wengi wanakitambua zaidi( ni mojawapo ya vitabu vinavyofundishiwa mashuleni kwenye somo la Kiswahili), Shafi anavyo vitabu vingine kama vile Kasri ya Mwinyi Fuad (ambacho kimetafsiriwa kwa Kifaransa, Kijerumani na Kirusi); Vuta n’kuvute (ambacho kilimpatia tuzo ya mwandishi bora nchini Tanzania mwaka 1998) na Haini ambacho ni cha hivi karibuni zaidi. Vitabu vyote vya Shafi ni riwaya.

Hivi majuzi alikutana na mwandishi mwingine mahiri, Freddy Macha, huko Milton Keynes nchini Uingereza. Waliketi kitako kwa zaidi ya masaa manne.Waliteta,wakazoza,wakapeana historia,wakapashana habari.Wakachambua umuhimu wa waandishi na wasanii. Lakini kabla hatujakuambia pa kwenda ili usome alichoandika Freddy Macha kuhusu “mkutano” wao, hii hapa historia fupi ya gwiji huyu wa fasihi.

Adam Shafi alizaliwa mjini Zanzibar mwaka 1940. Baada ya elimu yake ya shule ya msingi alijiunga na Chuo cha Ualimu cha Seyyid Khalifa (sasa Chuo cha Ualimu cha Nkrumah) mwaka 1957 hadi mwaka 1960. Alipata Diploma juu katika fani ya Siasa ya Uchumi katika Chuo cha Fritz Heckert, katika iliyokuwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Ujerumani mwaka 1963. Alipata mafunzo ya uandishi wa habari mjini Prague, nchini Czechoslovakia (sasa Jamhuri ya Czech) mwaka 1964 hadi mwaka 1965, nchini Sweden mwaka 1982 na nchini Marekani mwaka 1983.

Adam Shafi alikuwa mwenyekiti wa Umoja wa Waandishi wa Vitabu Tanzania (UWAVITA) kuanzia 1998 hadi 2002. Alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa Baraza la maendeleo ya Vitabu Tanzania (BAMVITA) mwaka 2002.

Haya twende sasa.Bonyeza hapa ili usome alichokiandika Freddy Macha kuhusiana na mkutano wake na Shafi Adam Shafi. Mahojiano yetu na Freddy Macha mwenyewe yatawajieni hivi karibuni.Hutaki kuyakosa mahojiano hayo!

Picha kwa hisani ya Freddy Macha.

Historia ya Shafi kwa msaada wa Longhorn Publishers.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

15 Responses to “UKIKUTANA NA SHAFI ADAM SHAFI…”

  1. Comment by Sesemi on December 19th, 2007 6:28 am

    Naam,huyu ni bongocelebrity haswa.Nimefurahi kuona ametua kwenye site yenu ingawa ni kupitia kwa Macha.Safi sana.Mungu ambariki aendelee kuandika.

  2. Comment by bongocelebrity on December 19th, 2007 1:08 pm

    test comment in french, salut jeff j’espère que ça va bien à toronto, a+

  3. Comment by Hailin on December 19th, 2007 3:17 pm

    this is a wonderful blog!

  4. Comment by Zange on December 19th, 2007 3:33 pm

    Duh,kweli BC inatisha.Mpaka mchina kawakubali?!!Hongereni sana.

  5. Comment by NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO on December 20th, 2007 7:50 am

    Nakumbuka na kupenda sana usemi ktk KULI
    ýana mwisho haya’.
    Imekuwa kauli yangu mbiu wakati woowote ninapokumbana na changamoto.

  6. Comment by Mama wa Kichagga on December 23rd, 2007 5:14 pm

    Nyakatakule,

    Umenigusa ndugu yangu! Yaani uko kama mimi kabisaa. Ukiniuzi kidogo basi lazima nikupatie msemo “Yanamwisho”. Na msemo huu umenijenga sana kimaisha kwa kuwa faraja kwangu. Nyaka big up pia kwa michango yako mbalimbali maana inanivutia sana.

    Mzee Shafi asante sana kwa mchango wako katika jamii Mungu aendelee kukubariki na akupe kheri mbinguni.

    Nimefurahi sana kugundua uko hai maana sikuwahi kukusikia zaidi ya kupitia kwenye vitabu vyako.

    Mzee unatisha! Kazi zako ni nzuri sana ila tatizo watanzania hatupendi kusoma! Je unaweza kusaidia katika hili angalau kwa kutoa nasaha zako hapa bloguni itasaidia baadhi.

    BIG UP BABA YANGU MZAZI

  7. Comment by Mama wa Kichagga on December 23rd, 2007 5:19 pm

    Heeeeeeeeee

    Nimesahau kitu,

    Etii Mzee Shafi unampango wowote wa kuweka kazi zako mtandaoni? Hii ni muhimu sana katika technolojia ya sasa na kazi zako zitakuwa endelevu. Kama upo ama utakuwepo huo mpango basi naomba utumuvushie link wadau ili tuendelee kupata nasaha zako

  8. Comment by zanzibar on February 20th, 2009 2:35 pm

    hivyo ndo tulivyo wazanzibar ,na vizazi vipya vitakuwa hivyo hivyo inshaallah ,sio kama nyerere aliyesoma MAKERERE

  9. Comment by mammy on June 22nd, 2009 2:55 am

    mie nakuomba mzee shafi unaweza kutuambia kitabu cha kuli tutakipata wapi changu kimepotea na nakipenda sana thanks

  10. Comment by annobil richard on August 14th, 2009 7:01 am

    ah!! jamani mie nadhani mzee shafi huyu alizaliwa na fasihi nami ingawa mghana najitahidi sana kufuata njia zake katika uandishi. mzee “SAS” kweli wewe ni nyota kabisaaaaaaaaaaaaa!!!!yaani kwa kifupi natamani kuwa ‘SAS’ wa ghana siku mmoja katika uandishi. nimeshaanza kitabu changu kwanza na nikija bongo mwakani kwa hakika ntakujia mzee ili unisaidie kukiboresha kabla ya kuchapishwa.ushabarikiwa baba!!!! I LUV U!! songa mbele na kazi zako hazitasahaulika katu.

  11. Comment by wa morogoro on October 6th, 2009 9:01 am

    Hongera kwa kazi kubwa.

  12. Comment by eddie on October 29th, 2009 2:47 am

    tafadhali tuandikie kidogo maandishi,misemo,ama any stuff ambayo huyu mzee shafi ameandika. kwani wengine hatumjui wala hatujaona kazi yake bado!

  13. Comment by shafi A.J on December 21st, 2009 3:55 am

    Thanx for the article,nimefurah sana kusoma historia ya wajna wangu…yuko juu sana,tena sana..

  14. Comment by Shafi Adam Shafi on January 8th, 2010 8:31 pm

    Baba umependeza sana na pic yako,
    Shukrani zangu za dhati zimwendee bwana Freddy Macha.

  15. Comment by Shaibu Hassan kanyochole. on March 8th, 2010 7:03 am

    Shafi Adam Shafi,usemi wako yanamwisho kutoka kwa Rashidi katika riwaya yako ya KULI,Uwa unanifariji sana na kunipa matumaini pale matumaini yanapopotea.

Leave a Reply