
Pichani ni kikosi cha kwanza cha Timu ya Soka ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars ambacho jioni hii kimetupwa nje ya Mashindano ya kugombea Kombe la Challenge kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati baada ya kufungwa magoli 2-1 na Timu ya Taifa ya Sudan. Kili Stars imetolewa katika hatua ya robo fainali katika mashindano hayo yanayoendelea katika vituo vya Dar-es-salaam na Arusha.
Majina ya wachezaji hao wa Kilimanjaro Stars ambo wote kwa pamoja ni “celebrities” wakubwa katika michezo (soka) ni kama ifuatavyo. Walio mstari wa mbele toka kushoto, Dani Mrwanda,Amir Mafta,Ali Mustafa ‘Bartez’,Uhuru Suleiman na Nizar Khalfan.
Mstari wa nyuma toka Kulia-Salum Swedi, Shaban Nditi,Michael Chuma,Erasto Nyoni,Meshack Abel na Castory Mumbara.
Safari ya soka la bongo bado inaelekea kuwa ndefu.
Picha kwa hisani ya Issa Michuzi.
Feedback / Comments
3 Responses to “KILI STARS YATUPWA NJE YA CHALLENGE”
Leave a Reply


Samahan Editor hapo hakuna Amir Maftaha,muombe michuzi picha nyingne ndiyo yupo Amir na sio hii.
Asante.
Test comment due to your forum post.
Hii timu ni vilaza wakubwa hakuna anaejua soka hata mmoja, tatizo walizoea kupata sifa za bure enzi hizo tunasikia kwenye radio “”lunyamira na mpira la la la la la la la la la la hatari katika gori pale, mchezaji huyu namfananisha na winga Overmas wa Arsenal”" kumbe hakuna lolote hawa hawafai hizi mechi zote wawe wanacheza walio chini ya miaka 18 ndio tutaona matunda baada ya muda mfupi apart from that “”Bichwa la mwendawazim lililo-laaaaaaaniwa”" litaendelea kunyolewa hata na wakoma