MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

Jina Kamili: Mrisho Mpoto.

Jina la Utani/Lakabu: Mjomba.

Mahali na Tarehe ya kuzaliwa: Songea, tarehe 27-10-1978.

Shule nilizosomea: Shule ya Msingi-Ilala Boma.Sekondari-MESAC

Jiji/Mji nilipendalo: Warsaw,Poland.

Chakula Nikipendacho:Wali na Maharage.

Wimbo Niupendao: Salamu Mjomba.

Filamu ambayo sitokaa niisahau: South Central.

Michezo/Mchezo niipendayo: Kuogelea.

Wasanii niwapendao: Wote wanaotumia fikra katika kuishi na zaidi Poets wote.

Siku niliyokuwa na furaha zaidi maishani mwangu: Nilipopata VISA ya kwenda Marekani wakati sikujua kuongea kiingereza.

Siku iliyokuwa ya huzuni maishani mwangu: Nilipopata mafanikio makubwa katika maisha yangu ya sanaa.Nilipofanya onyesho langu watu wakajaa mpaka wengine wakakosa nafasi ya kukaa na tiketi zote zikawa zimeisha. Kumbe ilikuwa ni ndoto tu.Hiyo siku naikumbuka sana maishani mwangu.

Msemo uniongozao(Life Motto): “Huwezi kwenda kwa jirani kama hukutokea kwako”.Ngugi

Huyo ni Mrisho Mpoto,mshairi mahiri,kijana wa kitanzania.Ukipata nafasi ya kumsikiliza akighani mashairi yake, utakubali kwamba “Mjomba” ni gwiji katika sanaa.Tulimuomba Mrisho atupe japo kipande kidogo cha ushairi wake,alitupa kitu kifuatacho

KILA LUGHA INA ROHO, NYINGINE KAMA WAJUA

BALI KIREMBA NA JOHO,UVISHWA MTU MZAWA

NA HILI KAMA HOHOHO, UWASHA NA KUPUMUA

NIMECHOSHWA NA UROHO,SASA NATAKA PUMUA

 

KATIKA MAAMKIZI,MEPESI SANA NA MEMA

LUGHA ZOTE HAZIWEZI, NYINGINE KUDAI KIMA

NA HII KAMA HAZIZI, YANIPASA KUSEAMA

SHIKAMOO MZAZI, AMA MTU WA HESHIMA.

Mrisho Mpoto pia ni mwanablogu.Unaweza kuisoma blog yake kwa kubonyeza hapa.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

40 Responses to “USHAIRI WA MRISHO MPOTO.”

  1. Comment by Mchunguzi on November 26th, 2007 5:14 am

    Li mwili lote hilo kumbe mtoto wa juzijuzi hapa tu!?!
    Watoto wasiku hizi bwana (ma-broilers) wanakua kama kuku wa kizungu!

  2. Comment by Kaka Poli on November 26th, 2007 5:59 am

    Mjomba!!!!!

  3. Comment by Dinah on November 26th, 2007 6:06 am

    Inaonyesha sanaa anaiweza, ingekuwa bomba kama mngetuwekea Audio. Alafu 1978? Mbona anaonekana alikuwepo toka vita vya Idd Amin (mzee) sio baada :-)

    Keep it Up Mjomba.

  4. Comment by Edwin Ndaki on November 26th, 2007 8:12 am

    aaaaaaaaaaaah….jamani hizo comments….mmmh..jamani mnataka waje na besi satifiketi?…sina mbavu..lol..

    Baab kubwa Mrisho Mpoto namkubali sana.

    Lakini naomba BC na MPOTO au yeyote anayejua ili atusaidie.

    Kwa ufahamu wangu huo wimbo wa SALAMU MJOMBA najua ulitungwa na Irene Sanga ambaye kwenye wimbo huo ameimba sehemu ya KORASI ila alimshirikisha Mpoto na yule bwana mwingine ambaye kwenye SHUTINGI anaoneka naye akiimba KORASI…

    Ila zaidi ya yote Mpoto kweli kafunika kisawa sawa.Pia namkumbuka vema huyu bwana kipindi cha msiba wa baba wa taifa mwl Nyerere(AKA… means Apumzike Kwa Amani)ubunifu uo. aligani vema sana kwenye lile dude..NENDA MWALIMU..

    KILA LA KHERI MPOTO..Kumbe na wewe ni wa kunyumba..sehemu gani…bomba mbili,Seedfarm ulishakunywa MUYAKAYA…

  5. Comment by herieth on November 26th, 2007 8:51 am

    Mjomba unakamua babake nikupigia saluti

    Keep it up!!

  6. Comment by gasto on November 26th, 2007 10:58 am

    Ha Ha Ha Kweli ukubwa wa pua si wingi wa makamasi.

  7. Comment by mchapakazi on November 27th, 2007 9:28 am

    DUUUUh! Poteleambali umri wake! Jamaa kazi yake mzuka kinoma, tunamkubali sana mimi na WACHAPAKAZI FAMILY kutoka pale kimara-temboni maskani. Tunamtakia kila la kheri na kazi yake na endelee na speed hiyo hiyo ya kuifumbua macho jamii. Gud work, all da best.

  8. Comment by Alhaj meddie on November 28th, 2007 1:16 am

    eeeeh bwana mjomba unatisha…..nakufagilia kinoma, unajua nini umefunika,amini mungu umewaacha watu wazima kibaooo…
    kaza buti eeehh baba

    Jivvummuzisheee kwa amani mwanawaneee!!!

  9. Comment by amina on November 30th, 2007 2:10 am

    UPO JUU KAMA MUASHOKI

  10. Comment by hans on June 17th, 2008 1:03 pm

    nakukubali sana mrisho, keep it up

  11. Comment by faraj maleta on September 13th, 2008 6:17 am

    mjomba mi nakukubali sana maana mashairi yako si mchezo
    mbona utoi wimbo mwingine?

  12. Comment by Mary Mkwaya Malamo on October 22nd, 2008 2:22 am

    mjombaaaaaaaaaaaa! unanifurahisha weweeeeeeeee!

  13. Comment by Georges Mchayano Ngoyani on November 2nd, 2008 2:49 am

    Huyu bwana mdogo ana kipaji,ninamkubali.Viongozi nao wasikie maneno ya watunzi.Kwa kweli yale mashairi ya wimbo wa mjomba ni ya hali ya juu sana.

    Namwombea aendelee kupaa kama huyo bwana aliyesema kama muashoki.

  14. Comment by Salvatory Kimboka on January 11th, 2009 3:32 am

    Kwa kweli kijana Mrisho Mpoto ni tunu ya watanzania wote hasa baada ya kuwapoteza watunzi wetu wa zamani kama akina TX Moshi William. Wimbo wake wa Mjomba na sasa Nauli ni nyimbo ambazo zimebeba maudhui yanayoonyesha hali halisi ya jamii ya Tanzania ya leo huku zikiacha hamasa na hisia ya jamii kuhusu Tanzania ya kesho…Hongera Mrisho nitakutafuta

  15. Comment by joswam B benjamin on March 10th, 2009 12:25 pm

    hi,
    napenda kutoa shukurani kwawote walio andaa program hii mimi kama mwana- technology hii napendakuwajulisha kuwa mmenibamba kinoma. big up MJOMBA Mjombarisho mpoto make kijana huyu wa makamu ana stahili poongezi mimi ni mmoja ninaye penda nyimbo zaukweli kama HIP HOP Na mashairi kama yamweshimiwamrisho mpoto na napendaanavyo jitofautishana wana muziki wengine kwa kujitambulisha kama mwana mashairi, kweli kaka wakati ni wako tupe raha watanzania na sisi tunakuunga mkono kwa kununua kazi zako big up. BY Joswam buberwa benjamin student of university of dar es salaam computing center city brunch (manzione04@hotmail.com)

  16. Comment by simple mudy on March 13th, 2009 5:25 am

    mjomba unaweza.nikipata nauli ntakuja kukusalimia. mi ni shabiki wako

  17. Comment by Emmanuel Mwahaja on March 22nd, 2009 11:55 pm

    Mrisho hongera saana.Katika wasanii wachache ambao wana uzalendo na nchi yao basi wewe ni namba moja.Sisi Watanzania tupo pamoja na wewe,tunakuombea MWENYEZI MUNGU akujalie rehema uweze kuendelea kutupatia vitu vikali(nyimbo) katika siku za usoni.

  18. Comment by joswam B Benjamini on March 25th, 2009 3:03 am

    kaka nilikua nikipita pande kadhaa ktk jiji letu nikifanya re-search kuhusu mkali wa mashahili yanayo wafikia watanzania kwa haraka ni huyu mrisho mpoto aka mjomba ila niweke wazi kuwa ujumbe wako unafika kutokana na tungo zako kuwagusa watanzania wengi hasa wa maisha ya kawaida na wapenda maendeleo, make unauwezo wa kumfanya mwananchi kipofu kuweza kuona maovu yanayofanywa na viongozi wachache wanao jisahau kuwa sasa watanzania wapo macho sana dhidi ya mali zao. mjomba nakutakia safari njema mjomba,mungu atakusaidia ongera kwa hapo ulipo fikia na nakuomba uongeze bidii. am out

  19. Comment by Omary on March 25th, 2009 7:53 am

    Ushairi kazi nzito,si yeyote awezae,
    Wahitaji mwenye mato,na mambo aelewae,
    Apishe watu mapito,wendapo wasijikwae,
    Huyo ndiye aitwae,malenga wa ushairi.

    Ushairi kazi pevu,si yeyote atungae,
    Wahitaji mwekevu,na ungoi ajuae,
    Haupawi mpumbavu,asoelewa mamboe,
    Kazi hino nda mbae,malenga wa ushairi.

    Ushairi ni kipawa,cha mtu aja’liwae,
    Awezae kufumbuwa,mafumbo na kufumbae
    Hapawi asoujuwa,kungaze wala ndiyae,
    Wataka aujuwae,malenga wa ushairi.

    Ushairi mbwa ubongo,na moyo wa atuwae,
    Tena awe na kiwango,cha fasaha ajuwae,
    Na la sawa na la jongo,alijuwe maanae,
    Huyo ndiye aitwae,Malenga wa ushairi.

    Ushairi ni kipambo,cha Lugha kwa ajuae,
    Na kwa kutabiri mambo,ni umbole tangu kae,
    Hunenwa neno kitambo,likajiri baadae,
    Kwa kuzazwa mawazoe,malenga wa ushairi.

    Muradi ni mangi sana,ya ushairi mamboe,
    Una shife zenye jina,kwa mwelewa manae,
    Hata katika kunena,mithali nda manenoe,
    Ilotungwa ni ambae,malenga wa ushairi.

    Tamati ndiyo akheri,na mtunzi niwambie,
    Ndie Kipande Omari,yule yule isimu’e,
    Ambae ni mashuhuri,Bandari mji wa ka’e
    Anenaye ya darajae,Malenga wa ushairi.

  20. Comment by kimaro on March 26th, 2009 6:48 am

    Ile harusi yako ya matembele na vyakula kibao vya asili ulikosha navyo.Mziki wako wa mjomba bomba.Lakini Cover ya miziki yako baadhi badilisha.

  21. Comment by SIMON on April 6th, 2009 2:12 am

    Mjomba, kwakweli mimi natambili ujumbe wako umekuja wakati mwafaka wakati jamii na nchi zimepotea na ambapo tunakuhitaji. Mimi nimekua nikitafuta kanda zako mjini Dar es salaam na kila niendapo hamna.

    Ujumbe huu na upitishwe mbala lote la Africa wajuao kiswahili na kikiwashinda, kitafsiriwe. Hongera hongera!!!

  22. Comment by marsha on May 18th, 2009 7:17 am

    mhhh ungali unang’ara mjomba huku kwetu tunaona mwangaza na pia tunapitia pitia mashairi yako kurekebisha
    JENGA NYUMBA MJOMBA WAPANGAJI NI WENGI,TENGENEZA BARABARA TUSAFIRI PAMOJA KUMFUATA MJOMBA MKUBWA
    U WA KHERI NA SHARI SI KAWAIDA YETU
    KISWAHILI LUGHA YETU KWA PAMOJA TUIENZI

  23. Comment by noel on May 20th, 2009 8:00 pm

    MJOMBA UNATISHA SIYO MWOGA HASA WIMBO WAKO HUU WAKUSAKA NAULI UMEJAA VIBOM,AMA KWELI MWENYE MASKIO HAAMBIWI——.

  24. Comment by lady blandy on June 17th, 2009 8:24 am

    yupo juu mpoto goooooooooooooooooooood

  25. Comment by zito on June 19th, 2009 1:34 pm

    mjomba mimi ni kati ya watu wanaokukubali hapa nchini.we ni mwanamapinduzi,mzalendo,mdumisha mila za kiafrika.sisi wanafunzi wa st john university tunakukubali sana kaza buti.kwel ineamini muamkie mbwa ili uweze pita,ujumbe wako tumeupokea vyema.

  26. Comment by happiness on June 22nd, 2009 4:40 am

    mjomba nakukubali kupita maelezo yaani kwa kweli naomba tu kujua nauli hujapata mjomba ufike kumueleza mjomba ana kwa ana mjomba

  27. Comment by Pam on June 24th, 2009 7:24 am

    mjomba unatisha!!! kuna mwingine mpya unassema asanteni sana kwa kuja nao unafunika kinoma siku ya kwanza sikuuelewa lakini mshkaji mmoja akanifafanulia jamani natamani niusikie kila dk utacheka kumbe anaongelea siku yake ya kufa anawashukuru waliokuja kwenye msiba wake kweli jamaa ni kichwa…. yaani nyumbani kwetu mwombo wake ukipigwa lazima tuitane then ukiisha wote vicheko kwa kwa kwa….HAWA NDO WA KUPEWA TUZO JAMANI WATANZANIA

  28. Comment by shambalangumi on June 30th, 2009 7:43 am

    MNAODAI MRISHO MDOGO KI UMRI TUAMBIENI UMRI WENU NA MLICHOIFANYIA JAMII. KWANI ZITO KABWE ANA UMRI GANI?, LAKINI ANGALIA MCHANGO WAKE KWA TAIFA.

    CHACHA

  29. Comment by Abu Salum (Baba Ally) on July 2nd, 2009 1:45 pm

    MRISHO NI MSANII KWA MAANA YA “REAL ARTIST”. ZAIDI YA YOTE UZALENDO WAKE SIO WA KUTILIWA SHAKA.. 100% MZALENDO HALISI. MCHANGO WAKE KATIKA KUELIMISHA JAMII NA KUWAKUMBUSHA VIONGOZI WAJIBU WAO, NI JAMBO LA KUTUKUKA. LONG LIVE MRISHO!

  30. Comment by hamad said on July 13th, 2009 4:25 am

    mjomba nakukubali sana we ni mkali na huna makuu jinsi unavyoonekana ni tofauti na ulivyo hakika wewe ni kaka wa mama. keep it up

  31. Comment by zubeir thagut on July 13th, 2009 4:40 am

    nakukubali kaka

  32. Comment by Alex GN on August 31st, 2009 3:25 pm

    Ulitukosha sana pale Biafra kwenye kongamano la John Mashaka……!!! Maana usingekuwa wa mwisho kuperform watu wangeingia mitini…!!!

  33. Comment by kaka ricyeg on October 29th, 2009 12:22 pm

    sASA ANKO UKO ZAIN SAIVI!!GHARAMA BADO KUBWA TUNGEKUFUATA IYO YA MAFISADI ANKO!!!!

  34. Comment by Mshabiki wa Mpoto on November 11th, 2009 11:55 am

    AMA KWELI MJOMBA WE NI MKALI KAMA WEMBE WA GILLET UNAKWANGUA HADI CHUNSI BILA DAMU KUTOKA M2 WANGU. MJOMBA MI NATOA USHAURI KWAMBA UWE NA WEBSITE YAKO AMBAYO ITAKUWA NA UFAFANUZI WA MASHAIRI YAKO KATIKA LUGHA RAHISI AMBAYO ITAELEWEKA KWA URAHSI KWA WA2 WOTE, KWANI SI WOTE WANAELEWA MASHAIRI YAKO YANAMAANISHA NINI!SI UNAJUA WOTE SI WAPENZI WA MASHAIRI NA ELIMU YETU NDO HIVO TENA KWA WATOTO WA WAKULIMA AMBAO NDIO MASHABIKI WAKO WAKUBWA. “MJOMBA SALUTI”

  35. Comment by Eliud on November 12th, 2009 2:37 pm

    Hongera sana kwa mashahili yenye mvuto sana hapa nayapata nikiwa Australia ila naamini nyumbani ni nyumbani. Big up kwa kuelemisha jamii hasa vijana

  36. Comment by Ray Ephraim Ndewingiya Njau on November 19th, 2009 5:38 am

    HUU NI UTHIBITISHO KUWA LUGHA YA KISWAHILI IKIWEZESHWA INAWEZA KUTIKISA ANGA LA KIMATAIFA.GHANI ZA MJOMBA NI UTHIBITISHO DHAHIRI WA MANENO YANGU KWA WADAU NA WAPENZI WA LUGHA YA KISWAHILI.KWA MASIKITIKO MAKUBWA WATANZANIA SASA NI MAHIRI KATIKA KISWANGEREZA WAKIDHANI KUWA HUO NDIYO USOMI.USOMI SIYO LUGHA BALI NI UELEDI KATIKA TAALUMA HUSIKA.TAALUMA INAWEZA KUMFIKIA MWANAZUONI KWA LUGHA YOYOTE.

  37. Comment by shabani A shabani on December 7th, 2009 12:55 pm

    kwa kweli Mpoto wewe mmoja kata ya wa2 ninaowakubali. Vinivutiavyo katika zako kazi {I}nyimbo zipo kimaadili ya kitanzania
    {II}Mavazi na maeneo uyatumiayo ayatofautiani na wimbo
    Tofauti na wemzako utakuta wimbo JINA manyanyaso. Video inaonyesha magali na nyumba za kifahari, anaye nyanyaswa kavaa mavazi ya ghalama viatu,cheni nk

  38. Comment by salim on December 19th, 2009 8:03 am

    well done mpoto but i would like
    to meet you.am atUDSM

  39. Comment by Adam Charles on January 30th, 2010 3:04 am

    Bro,upo juu sana na mashairi yako yanaelimisha sana, ila kuna baadhi ya wasanii wanajaribu kukuiga lakini wanashindwa, kama Mpoki na nyimbo yake ya shangazi. Big up mjomba.
    Your’s fun
    Adam from Arusha.

  40. Comment by MOTUKA NYAMWEYA EVANS on February 17th, 2010 8:53 am

    Dah!!!!!!!MJOMBA SALUTI KWAKO INABIDI.KONGOLE KWA KAZI ZAKO ZA HEKIMA NA BUSARATOKA KWANGU NIKIWA KATIKA CHUO KIKUU CHA KISII.YA ZIADA UTAJUZWA LAKINI KWELI MJOMBA UKO JUU.HATA HIVYO SIKU KESHO MASHAIRI YA KWANGU TAYATIA KWENYE WEBSITE.

    Evans matuka Kisii Kenya.

Leave a Reply