Ni ijumaa tena.Wakati mwingine wa kupata midundo.Leo tunatoka ndani ya jiji mpaka mji kasoro bahari.Pale tunamkuta marehemu Mbaraka Mwinshehe(pichani) akiuambia umma kwamba sasa amehamia Mtaa wa Saba,kutoka kule alikokuwa akiishi ambapo mapaka yalikuwa hayaishi kulia lia.Anasema ile nyumba aliyokuwa anaishi sio nyumba,ilikuwa na mikosi…Wimbo huu ni kutoka katika mkusanyiko wa nyimbo zake ulioitwa Ukumbusho Vol.2.
Hivi ni kweli kwamba mahali unapoishi panachangia sana kufeli kwako au kufanikiwa kwako?Wewe unasemaje?Sikiliza ujumbe,pata mdundo,sikiliza nyuzi bin nyuzi ya gitaa la Mbaraka.Ijumaa Njema!
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Feedback / Comments
10 Responses to “MTAA WA SABA-MBARAKA MWINSHEHE.”
Leave a Reply


[...] MTAA WA SABA, Throw your mind back! – Today, 08:00 AM MTAA WA SABA-MBARAKA MWINSHEHE. « BONGO CELEBRITY [...]
[...] MTAA WA SABA, Throw your mind back and relax! – Today, 08:08 AM Tume amwa kuhama kutoka mtaa wa PANUA MTAA WA SABA-MBARAKA MWINSHEHE. « BONGO CELEBRITY [...]
Yeah ni kweli kabisa, unaweza ukahamia mahali alafu kila kitu kinakwenda ovyo kutokanana “mikosi” ya mahali hapo (a.k.a nguvu za Giza).
Nakumbuka wakati naishi UK miaka 6 iliyopita,kila nilipokuwa nikihamia napatwa na mauza-uza, Mara nione watu wamenisimamia nikiwa nimelala,sauti za watoto kulia, pesa zinaisha bila kujua umetumia vipi na mbaya zaidi sikufanikiwa kupata Degree yangu ya kwanza, huko ilikuwa North.
Nikahama makazi (nchi jirani) na kila kitu kikaenda vema kabisa namaua-uza hayakunisumbua tena.
Hivyo haya mambo yapo sana tu.
Mh Dinah acha kutupwaga ngambo na mambo ya nguvu ya kiza wapi na wapi!!!!!!!!!1
Tatizo wabongo wengi mmezoea kudanganywa. Lakini ndio hivyo na mimi mambo ya “mtaa wa saba” walinitokea nikiwa Ulaya.
KAMA MAISHA YANASUMBUA SEHEM, KUHAMA KUNA ZARI ZAKE, HATA MANABII MA8ISHA YALIPOKUWA MAGUMU SEHEM MOJA WALIHAMIA SEHEM NYENGINE, BOB PIA KAIMBA “EXODUS MOVEMENT OF JUH PEOPELE”
We Ally Weweee. Nguvu za giza zipo unajifanya hauelewi basi na wewe ni mchawi au unatumia hizo nguvu ndiyo maana unajifanya kama hauelewi kutuzuga.
kweli dinna nakubaliana na wewe hata mimi yananitokea hayo.
eeee mwaego kuama usawa uhu kama huna,mkwanja, mavumba(hera) inabidi ukubali matokeo yani kuchanjwa chale,kupelekwa saluni,ikiwezekana kama hufai kulala kwenye kitanda utarazwa chini,
I wish I could speak Swahili fluently, I just love the language. Mbaraka makes it much more opulent.