MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

 

MWILI wa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Salome Mbatia, aliyefariki dunia mkoani Iringa juzi, unatarajiwa kuzikwa jumamosi hii huko Moshi baada ya kuagwa nyumbani kwake, jijini Dar es Salaam kesho(ijumaa).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Spika wa Bunge, Mheshimiwa Samuel Sitta, nyumbani kwa marehemu Mtaa wa Uganda,Oysterbay jijini Dar-es-salaam leo,mwili wa marehemu utasafirishwa kesho(ijumaa) saa 8:00 mchana kwenda mkoani Kilimanjaro kwa mazishi siku hiyo ya Jumamosi.

Hata hivyo, Sitta alisema hadi kufikia leo mchana, hakuwa na uhakika wa eneo ambako mwili wa marehemu utazikwa na kwamba, suala hilo liko ndani ya maamuzi ya familia.

Lakini akasema huenda mwili huo ukazikwa katika kijiji cha Kirua, Wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani humo ambako mume wa marehemu, Dr.Joseph Mbatia, anatoka kulingana na mila za Kichagga.

Alisema ibada (misa) ya kuuombea mwili wa marehemu, itafanyika nyumbani kwake leo(ijumaa) saa 4:00 asubuhi kabla ya kusafirishwa na inatarajiwa kuhudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwamo wabunge.

Alisema wenyeviti kumi wa kamati za Bunge zinazoongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge), Dk Batilda Buriani, leo walikutana kupanga uwakilishi katika mazishi ya marehemu.

Akizungumzia msiba huo, Sitta alisema kifo cha Waziri Mbatia, kimeacha pengo kubwa bungeni kutokana na kumpoteza Mbunge mwenye vipaji vingi muhimu ambavyo viliwapa matumaini ya kuwa waziri kamili katika siku za baadaye.

 

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

9 Responses to “RATIBA YA MAZISHI YA MH.SALOME MBATIA”

  1. Comment by mesa on October 25th, 2007 3:02 pm

    Jamani hebu tuwe na haki hatakama mtu akifa, sasa mwili wa dereva uko wapi na jina lake? kwani huyo dereva si mtu jamaniiiiii? inauma sana tena sana kwa familia na ndugu wa dereva plz tujulisheni au hiyo ndege hakuruhusiwa? kama ndio hivo basi mungu asi wasamehe woootee wanaowadharau watu wa kima cha chini na tukumbuke dunia tu wapitaji,

  2. Comment by ANNA GABRIEL on October 26th, 2007 1:49 am

    R.I.P SALOME MBATIA

  3. Comment by Farida on October 26th, 2007 8:19 am

    Uko sahihi Mesa sijasikia kitu chochote kuhusu Dereva wa Mheshimiwa, ndugu zangu tukumbuke na hawa wadogo.
    POLENI SANA FAMILIA YA MH. SOLOME MBATIA NA YA DEREVA WA MAREHEMU .MWENYEZI MUNGU AZIWEKE ROHO ZAO MAHALI PEMA PEPONI AMIN.

  4. Comment by A CHAGULA on October 27th, 2007 12:31 am

    POLENI SANA FAMILIA ZA MAREHEMU NA WATANZANIA WENZANGU KWA MSIBA MZITO.MWENYEZI MUNGU NDIYE MPANGAJI NA KAZI YAKE HAINA MAKOSA.MUNGU AZIWEKE ROHO ZA MAREHEMU MAHARI PEMA PEPONI AMEN!

  5. Comment by ANTONY on October 27th, 2007 12:57 am

    SCHEDULE????????????????

  6. Comment by BongoSamurai on October 28th, 2007 4:17 am

    R.I.P Salome Mbatia.
    Ulikuwa mfano wa kuigwa na nilikupenda/admire sana japo sikuwahi kukutana nawe ‘live’ hata siku moja.
    Kwangu ulikuwa kama mama/shangazi na mema yako yote uliyotufunza na kutuachia tutayafuata na kuyatekeleza.
    Kweli wahenga walisema “chema hakidumu” na wazungu walisema “all the good ones die young”
    Rest In Peace Mama wote tuu watu wa njia moja ni vile hatujui saa wala dakika. Uende salama.

  7. Comment by BongoSamurai on October 28th, 2007 4:21 am

    Mesa kama ni msomaji wa magazeti au hata humu ndani ya blog ungekuwa ulishapata habari za maziko ya dereva.Alizikwa Mburahati siku ile ile mwili ulipowasili toka Iringa.
    Nakushauri usiwe mwepesi wa kuhukumu, ni kweli wote tuu wapita njia ktk hii dunia na Mungu ndie hakimu wa haki.

  8. Comment by paulina on January 10th, 2010 2:02 pm

    mungu alitoa na bwana alitwaa jina lake libalikiwe ulikua mfano wa kuigwa mama sifa na busara zifuatwa asnte

  9. Comment by paulina on January 10th, 2010 2:18 pm

    MAMA ULIKUA MFANO WA KUIGWA KWELI SIFA ZAKO NA JITIHDA ZOTE ZITAFUATWA MUNGU ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LITUKUZWE

Leave a Reply