Filamu za kitanzania zina historia ndefu tofauti na wengi wanavyofikiria. Kama mtakumbuka (kwa waliokuwepo enzi hizo) kuliwahi kuwepo na filamu kama vile Fimbo ya Mnyonge (1974), Harusi ya Mariam(1983) na Yomba Yomba(1983) na nyinginezo ambazo ziliwahi kutamba sana enzi hizo. Baadaye idara ya filamu ikapotea kabla ya kupigwa kikumbo na sanaa ya maigizo(wataalamu wanasema kuna tofauti kubwa kati ya maigizo na filamu). Lakini hivi karibuni enzi za filamu za kitanzania zimerudi,tena kwa kasi. Kama kulivyo na Hollywood(Los Angeles,USA),Nollywood(Lagos,Nigeria) na Bollywood(Mumbai,India), hivi leo inasemekana kuna Bongowood(Dar-es-salaam,Tanzania).

Mmoja kati ya waigizaji wengi wa filamu nchini Tanzania ambao wanasaidia kuzirudisha enzi hizo ni kijana Steven Charles Kanumba. Kwa wafuatiliaji wa filamu za kitanzania, hili jina na sura(pichani) sio geni hata kidogo.Lakini Kanumba ametokea wapi na anaelekea wapi?
Yeye mwenyewe anapasha kwamba alizaliwa mkoani Shinyanga tarehe 8 January mwaka 1984.Alipata elimu yake ya msingi katika Shule ya Msingi Bugoyi huko huko Shinyanga. Baadaye alijiunga na shule ya sekondari Mwadui ambapo alisoma kwa miaka miwili tu kabla ya kuhamia katika shule ya Dar-es-salaam Christian Seminary alipomaliza elimu yake ya awali ya sekondari. Baada ya hapo alijiunga na shule ya sekondari Jitegemee kwa masomo ya kidato cha tano na sita.
Ingawa alianza kuigiza tangu utotoni, safari yake katika fani hii aliianza rasmi mwaka 2002 alipojiunga na kundi maarufu la sanaa za maigizo la Kaole. Hivi karibuni tulifanya naye mahojiano ambapo tulizungumza naye mengi kuhusu kazi yake ya uigizaji na maisha yake kwa ujumla. Tulipomuuliza kuhusu habari iliyokuwa imetawala kwenye baadhi ya vyombo vya habari nchini Tanzania miezi michache iliyopita kuhusiana na uhusiano wake na Miss Tanzania 2006,Wema Sepetu na pia “beef” kati yake na msanii mwenzake aitwaye Frank inayosemekana kusababishwa na wao wawili kumgombea mrembo huyo,hakusita kutupatia majibu yake. Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;
BC : Kanumba karibu ndani ya BongoCelebrity
SK : Ahsanteni sana.

BC : Kwanza kabisa tungependa kujua, kuna tofauti gani kati ya Steve Kanumba muigizaji na Steve Kanumba wa kawaida, huyu tunayeongea naye hivi sasa ?
SK : Steve Kanumba unayeongea naye ni tofauti kabisa na Steve Kanumba muigizaji.Kwanza maisha anayoishi Kanumba ni tofauti kabisa na maisha anayoishi kwenye filamu au michezo mbalimbali ya kuigiza. Kanumba wa kawaida ni kijana mtanashati,anayejipenda,aliye na heshima kwa mkubwa na mdogo na pia anamheshimu na kumuogopa Mungu.Situmii kilevi cha aina yoyote ile.Sivuti bangi wala sigara.
Sasa kwenye filamu unaweza kukuta naigiza yote hayo niliyoyataja hapo juu na mengineyo.Ni uigizaji tu.
BC : Mpaka hivi sasa umeshashiriki katika filamu ngapi ? Unaweza kuzitaja ?
SK : Mpaka hivi sasa nimeshacheza filamu kama 16 hivi. Kati ya hizo 12 zimeshatoka na kuonekana wakati 4 bado hazijatoka ingawa zimeshakamilika na zipo mbioni kutoka.
Kwa majina filamu ambazo nimeshawahi kushiriki ni Neno,Riziki,Ulingo, Johari part I, Johari part II, Sikitiko Langu, Dangerous Desire,Dar 2 Lagos(hii nimecheza na Wanigeria),My Sister part I, My Sister part II,Penina na Cross My Sin. Hizo ni kwa upande wa ambazo zimeshatoka. Kwa upande wa ambazo bado hazijatoka ni A Point of No Return(hii nimecheza na Miss Tanzania 2006,Wema Sepetu), The Director(hii nimecheza na Wanigeria tena), Twins na Signs of Times.

Cover ya mojawapo ya filamu ambazo Kanumba ameshiriki.
BC : Katika zote hizo, ipi ilikuwa ni ngumu zaidi kwako kuigiza ? Kwanini ?
SK : Kila filamu ina ugumu wake katika kuigiza.Lakini ambayo nadhani ilikuwa ngumu zaidi nadhani ni Cross My Sin.Sababu ni kwamba character niliyopewa ilikuwa ni character ambayo sijawahi kuicheza kamwe. Hapa niliigiza kama padri.Sasa kuna ugumu wa kuigiza kama padri ukilinganisha na tuseme kuigiza kama mchungaji. Hii inatokana na jinsi ambavyo mapadri wanavyoishi nk.
Nyingine iliyokuwa ngumu ni The Director.Hii ni kwa sababu filamu hii naweza kusema ni filamu ndani ya filamu(a movie within a movie).Katika filamu hii nashiriki kama muongoza filamu (director) wa filamu inayoitwa Paradise of Love wakati huo huo na mimi napigwa picha na director mwingine ambaye ndio original director wa filamu yenyewe. Hii ilikuwa ngumu sana kuigiza kwani ilihitaji ufundi wa ziada.
BC : Baada ya kuwa umeshashiriki katika filamu nyingi kiasi hicho, unaonaje maendeleo yako kama msanii tangu ulipoanza mpaka hivi sasa. Una mabadiliko gani katika uigizaji wako ? Na je unadhani mchezo au filamu gani ndio haswa unaweza kusema imekufikisha hapo ulipo ?
SK : Mabadiliko yapo,tena makubwa sana.Kwanza utaona kwamba mimi nilipoanza nilianzia kwenye kucheza tamthiliya na hivi sasa nimeacha kucheza tamthiliya na badala yake nacheza filamu peke yake.Kwa maana hiyo nimekaa kibiashara zaidi. Hii ni tofauti na hapo awali ambapo bila malipo yoyote kila mtu alikuwa anaweza kuniona kupitia tamthiliya za kwenye luninga. Hivi sasa ili aone ninachofanya inabidi anunue filamu.
Mabadiliko mengine ni kwamba katika filamu kila mara nacheza kitu kipya kila mara tofauti na kwenye tamthiliya ambapo role inakuwa ile ile kwa muda mrefu sana.Kisanii pia nimeongeza ujuzi,nimeweza kucheza na kwa mfano waigizaji kutoka nchini Nigeria ambao kimsingi ni wazoefu zaidi katika mambo ya uigizaji. Hili limenipa changamoto zaidi katika kuboresha kazi zangu.
Filamu ambayo nadhani ndio ilinitoa zaidi ni filamu ya Johari (zote mbili yaani part I na II).Sababu ni kwamba kwanza filamu yenyewe ilikuwa ni nzuri na ilishirikisha mastaa wengi sana wa filamu nchini Tanzania. Pia promosheni ya filamu yenyewe ilikuwa ni ya nguvu jambo ambalo lilipelekea mashabiki kujitokeza kwa wingi kutaka kuiona na kwa bahati nzuri wakatokea kuipenda pia.
BC : Umaarufu huwa unaambatana na mambo mengi sana, mengine mazuri na mengine mabaya. Kwa upande wako unajisikiaje kuwa muigizaji maarufu nchini Tanzania mpaka hivi sasa na je familia yako inakabiliana vipi na umaarufu wako ?
SK : Mimi binafsi najisikia faraja kuwa muigizaji.Uigizaji ilikuwa ni ndoto yangu ya muda mrefu.Pia nashukuru kwamba uigizaji ndio umenisaidia kuwa hapa nilipo hivi leo.Uigizaji huo huo umeweza kunijengea sifa na heshima mbele ya makundi mbalimbali ya watu wakiwemo viongozi wa kiserikali,mataifa mbalimbali na jamii kwa ujumla.
Kuhusu jinsi ambavyo familia yangu inakabiliana na umaarufu wangu ni kwamba kwanza kabisa nashukuru kwamba familia yangu inanielewa na inaelewa kwamba nikiingia ndani ya nyumba naingia kama mtoto na mwanafamilia na sio staa au muigizaji.Katika raha na shida tunashirikiana kama wanafamilia.Lakini pia nashukuru kwamba familia yangu akiwemo mama yangu mzazi anaelewa kwamba kutokana na kazi zangu kuna wakati nakuwa busy sana kiasi kwamba naweza hata kushindwa hata kuhudhuria baadhi ya shughuli za kifamilia nk.Familia yangu inaelewa kwamba kikitokea kitu kama hicho kinakuwa sio kwa makusudi.Nawashukuru sana kwa hilo.

BC : Katika ulimwengu wa uigizaji imeshawahi kutokea mara nyingi sana watu waliogiza katika sinema moja kama wapenzi wakatokea kupendana kikweli katika maisha ya kawaida. Je wewe imeshawahi kukutokea hiyo ? Kama hapana unawezaje kuzuia hisia zako hususani kama unaigiza na msichana ambaye unavutiwa naye kimapenzi ?
SK : Mimi binafsi haijawahi kunitokea. Nadhani inakuwa ngumu kitu kama hicho kutokea kwa sababu kwanza anayeigiza pale anakuwa si mimi bali Kanumba muigizaji ambaye anakuwa amepewa jina lingine na kila ninachokifanya pale ikiwemo ninachokiongea kinakuwa kimeandikwa katika script ambayo kama muigizaji sina budi kuifuatilia.Kwa maana hiyo ninachokifanya pale kinakuwa sio hulka yangu wala hisia zangu binafsi bali script inavyonielekeza na pia maelekezo kutoka kwa waongozaji(directors). Hayo ndio maoni yangu.Lakini mbali na hapo kama ikitokea watu wakapendana hiyo inakuwa ni makubaliano yao wenyewe ambayo sio lazima yaanzie kwenye kurekodi filamu.Kama unavyojua love does not ask why.
BC :Je imeshawahi kutokea ukacheza character ambayo kwa namna moja au nyingine unaona ilifanana sana na ulivyo wewe mwenyewe kama Steve Kanumba ? Ni ipi na ilikuwa ni katika filamu gani ?
SK : Ndio nadhani ishawahi kutokea katika mchezo mmoja wa kuigiza ambapo niliigiza kama mtoto kipofu ninayenyanyaswa na kuteswa na mama yangu wa kambo. Hiyo nadhani iliakisi kwa kiasi fulani maisha yangu binafsi kwani kitu mithili ya hicho kishawahi kunitokea hapo zamani.
BC : Katika uigizaji wa filamu mara nyingi inabidi upakwe make-up kwa sababu ya taa na mambo kama hayo. Kama kijana wa kiume wa ki-Tanzania make-up sio utamaduni wetu. Ilikuwaje kwako mara ya kwanza ulipopakwa make-up na je kitendo hicho kilikuathiri kwa namna yeyote ile hususani siku hizo za mwanzo ?
SK : Unajua fani ya uigizaji unapoiingilia ni kama vile mtu anayeingia shuleni.Kuna sheria na taratibu zake.Unaambiwa hapa utavaa suruali ya khaki na shati jeupe.Sasa wewe unaweza ukawa hujazoea kuvaa vitu kama hivyo lakini ili upate ulichokifuata (elimu) huna budi kufuata masharti ya shule.Hali ilikuwa ni hivyo hivyo kwangu nilipoingia kwenye masuala ya uigizaji filamu.Ilinibidi nifuate sheria na taratibu za uigizaji ili picha ziwe na ubora unaotakiwa na mambo kama hayo.Kisaikolojia haikuniathiri sana kwa sababu nilijua nilichokuwa nikikifuata.Kimwili ndio, kwa sababu mwanzoni nilikuwa sijui vizuri make-up zipi zinaendana na ngozi yangu na zipi haziendani kitendo ambacho wakati mwingine kilinisababishia vipele usoni.
BC : Suala la ubora(quality) wa filamu za Tanzania zikilinganishwa na filamu za kutoka Hollywood (USA), Nollywood (Nigeria) na hata Bollywood (India) bado linalalamikiwa na wapenda sinema wengi. Kwa maoni yako, unadhani wenzetu mpaka leo,hususani wanigeria kwa mfano, wanatushinda nini ? Nini kifanyike ili tuongeze ubora wa filamu zetu hususani kwenye mambo kama sauti na upigaji picha kwa ujumla ?
SK : Kwanza kabisa ni vifaa wenzetu wanavyotumia.Vifaa vyao kidogo viko advanced ukilinganisha na vyetu.Lakini naomba nieleweke kwamba hapa sisemi kwamba movie industry nzima ya Tanzania haina vifaa vyenye ubora,la.Hapa nchini pia tuna makampuni yenye vifaa vizuri mno na wanatengeneza movies zenye viwango vizuri tu wakati mwingine kuliko hata hizo nchi ulizozitaja.
Wakati huo huo hata katika hizo sehemu zingine ulizozitaja na hususani Nigeria (hawa ndio tunaonekana kushindana nao zaidi) sio kila movie yao ni yenye viwango.Kuna movie nyingine za Kinigeria ukianza tu kuitazama unakuwa huna hata hamu ya kuendelea kuitazama.Hali ni hiyo hiyo hata Hollywood au India.Kuna movies ambazo hazina viwango kabisa.Kwa hiyo tatizo la ubora halipo Tanzania tu au Nigeria tu bali ni kila sehemu. Kwa hiyo, kwa sababu movie industry ya Tanzania ndio kwanza inaanza kukua inakuwa rahisi sisi kufananishwa na wenzetu hao uliowataja na wakati mwingine hata kukatishwa tamaa kwamba hatuwezi kuwafikia wenzetu.
Mimi naamini kwamba tunakua kisanii, kivifaa na production kwa ujumla.Mabadiliko yanaonekana na ninafikiri baada ya miaka michache tutakuwa tumesonga mbele sana.Kwa hiyo mimi napinga mtazamo kwamba filamu zote kutoka Nigeria zina viwango.Zipo nzuri na zipo mbovu.Hali itakuwa hivyo hivyo hata hapa kwetu,sio kwamba baadaye kila filamu itakayokuwa inatengenezwa itakuwa yenye viwango bora.Kuna nyingine zitakuwa hivyo na zingine zitabakia kuwa za kawaida au mbovu kabisa.
BC : Unadhani ni kwanini basi Wanigeria wameweza sana kujitangaza kimataifa kuliko sisi ?
SK : Cha kwanza ni support wanayoipata wenzetu kutoka katika serikali yao.Mimi nimeenda kule Lagos, Nigeria na kujionea mwenyewe.Serikali ya wenzetu nadhani imeona kabisa jinsi movie industry inavyoweza kutumika kuitangaza nchi,kutoa ajira kwa vijana na watu wazima kwa ujumla.
Nitakupa mfano mmoja,hapa nchini hatuna hata tuzo ambazo ni kutoka serikalini.Serikali yetu bado haioni umuhimu wa movie industry. Kupata location(sehemu) ya kufanya shooting bado ni tatizo kubwa sana.Ukitaka kwa mfano kushoot filamu maeneo kwa mfano pale Coco Beach unakatazwa,ukitaka kufanya hivyo hivyo uwanja wa ndege, mahakamani huruhusiwi.Wenzetu wa Nigeria kwa mfano wanapewa mpaka magwanda ya polisi au jeshi kwa mfano ili kuonyesha ile reality.Sisi hapa ni marufuku kabisa.Kibaya zaidi ni kwamba mtu huyo huyo anayekunyima vitendea kazi kama hivyo anakuja anakuambua nyie movie zenu haziwezi kufikia za Hollywood nk.Zitafikia vipi kama uzalendo hakuna ndani ya nchi na wala serikali yenyewe haitoi support ? Serikali ndio baba wetu,haina budi kujitokeza kikamilifu na kutuunga mkono kwa hali na mali kwani isitoshe sisi ndio tunasaidia sana kuitangaza nchi yetu hivi sasa.Kupitia movie mtu anaweza akaona mbuga za wanyama,milima nk na hivyo akashawishika kuja kuitembelea na mambo kama hayo.

Cover ya filamu ya Dar 2 Lagos ambayo Kanumba alicheza kwa kushirikiana na waigizaji wa Nigeria.
BC : Unaongeleaje suala la malipo ya kazi za usanii wa kuigiza filamu nchini Tanzania ? Malipo yanaridhisha ? Vipi kuhusu suala la piracy.Mnakabiliana nalo vipi ?
SK : Naweza kusema japo malipo ni kidogo lakini tunashiba.Movie industry hapa nchini bado ni changa.Kadiri siku zinavyozidi kwenda itazidi kukua na hivyo mapato nayo yataongezeka.
Suala la piracy mpaka hivi sasa bado ni suala la kibinafsi. Mpaka hivi sasa imekuwa kama ni jukumu la mtu mwenyewe kuilinda kazi yake isichukuliwe kwa matumizi yasiyoruhusiwa(piracy). Hapa pia serikali haina budi kuingilia kati katika kutekeleza sheria za haki miliki ilizoziunda. Bila kufanya hivyo ni wazi kwamba kazi za wasanii zitaendelea kuibwa jambo ambalo linaua industry nzima.

BC : Umesema umewahi kwenda na kufanya kazi na wenzetu wa Nigeria. Ulijifunza mambo gani ulipokwenda Nigeria na kufanya kazi nao ?
SK : Nimejifunza mambo mengi sana.Cha kwanza ni kama nilivyosema hapo juu,nimejifunza jinsi serikali ya wenzetu inavyowasaidia wasanii wao kiasi kwamba wamewajengea kabisa eneo moja kubwa kwa ajili ya shughuli zao za kisanii.Nimejifunza kuhusu ushirikiano miongoni mwa wasanii.Nimejifunza zaidi jinsi ya kusimamia malipo ya wasanii.Nimejifunza pia mambo mbalimbali kuhusu kuongoza filamu na jinsi ambavyo wenzetu wanafanya.Kwa mfano wenzetu hivi sasa wanatengeneza movie hata kwa kutumia helikopta !Nimejifunza pia jinsi ya kuwa commited katika kazi. Lakini cha muhimu zaidi nimejifunza mengi zaidi katika fani yangu ya uigizaji filamu.
BC : Katika fani ya uigizaji sinema ni waigizaji gani, kimataifa na nchini Tanzania ambao unapenda zaidi kazi zao ? Kwanini ? Kati ya hao ni wapi ambao ungependa kufanya nao kazi katika siku za mbeleni ?
SK : Kwa kimataifa napenda kazi za Ramsey,Genevive,Desmond Eliot na Mercy Johnson(wote hawa kutoka Nigeria).Nawapenda hawa kwa sababu nawaona kuwa waigizaji makini na pia wakipewa role fulani wanajikita ndani yake kisawasawa.Yaani wanajivika ile role vilivyo na sio kijuu juu.Kwa upande wa Tanzania wapo wengi lakini kwa uchache tu navutiwa zaidi na Ray na Monalisa.Ningependa kufanya kazi na Ramsey na Genevive.Nimeshafanya kazi na baadhi ya hao niliowataja.
BC : Sasa naomba uniruhusu tuongelee kidogo kuhusu habari mbalimbali kuhusu maisha yako binafsi. Kumekuwepo na habari nyingi sana kuhusiana na ugomvi wako na msanii mwenzako Frank kuhusu Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu. Unaweza kutueleza chochote kuhusu suala hilo ? Ukweli uko wapi ?
SK : Kwanza kabisa naomba niseme kwamba sijawahi hata siku kugombana na mtu yeyote kwa sababu ya mwanamke. Kilichotokea ni kwamba Frank nilimuondoa katika filamu yangu ya A Point of No Return kutokana na utovu wa nidhamu.Nikiwa kama muongozaji msaidizi wa filamu hiyo(mimi ni muongozaji msaidizi katika kampuni ya 1st Game Quality) nilimchukua Wema Sepetu ili aigize katika filamu hiyo.Tukawa tumeshaingia naye mkataba na advance ya malipo tumeshampa.
Sasa Frank akawa anamsumbua Wema Sepetu kwa kumtongoza na mambo mengine kama hayo.Matokeo yake ikawa wazi kwamba Wema atashindwa kuendelea kucheza hiyo filamu kutokana na jinsi Frank anavyomghasi.Sasa kwa sababu nilikuwa nimeshaingia naye mkataba nikawa sina jinsi bali kumuondoa Frank ili kazi iendelee.Nikamwambia Frank mimi na wewe tutaendelea kufanya kazi nyingine ila kwa hii hebu tuepushe hii shari kwa sababu huyu msichana ndio kwanza anaanza kazi ya uigizaji.She has to be comfortable.
Nikamuomba Frank arudishe script,akagoma kufanya hivyo na kisha kuanza kunitumia maneno machafu machafu na kwenda kwenye baadhi ya magazeti na mambo kama hayo akisambaza maneno ya uongo.Frank amemjua Wema kupitia kwangu.Mimi ndio nilimtambulisha Frank kwa Wema. Kwa kifupi hicho ndicho kilichotokea.Kimsingi chanzo ni utovu wa nidhamu aliouonyesha Frank na wala si vinginevyo kama ambavyo amekuwa akidai.Nilimualika Frank kwa minajili ya kusaidiana kama vijana lakini naona hizi ndio fadhila.Yote namuachia Mungu,atajua la kufanya.

Steve Kanumba akiwa amepozi na Miss Tanzania 2006,Wema Sepetu
BC : Hivi sasa unapendelea zaidi kuitwa « Kanumba The Great ». Nini chanzo cha jina hili na kwanini umeamua kujiita hivyo ?
SK : Hizi ni nick name tu za kisanii kama ambavyo wasanii wengi wanajiita. « The Great » ni jina ambalo nimelichukua kutokana na watu mbalimbali katika historia waliokuwa wanajiita « The Great ». Isitoshe kwa hivi sasa,kwa jinsi ambavyo mungu amenisaidia kufikia hapa nilipo,I feel Great.
BC : Je umeoa au una mchumba hivi sasa ?
SK : Sijaoa wala sina mchumba wala girlfriend.
BC : Mwisho ungependa kuwaambia nini washabiki wako ? Unazo project ngapi zinazokuja ? Watarajie nini ndani ya project hizo ?
SK : Kwanza nawapenda sana, kwa sababu wao walinipenda sana tangu mwanzoni na kunipa support tangu mwanzo.Nawasihi waendelee kununua kazi za nyumbani ili kuendeleza fani ya filamu nchini Tanzania. Filamu ambazo hazijatoka kama nilivyozitaja hapo juu ni moto wa kuotea mbali. Wajiandae kupata burudani ya aina yake zikitoka.
BC : Ahsante sana Steve kwa muda wako.Tunakutakia kila la kheri
SK : Ahsanteni na nyie.Mnafanya kazi nzuri sana.
Feedback / Comments
132 Responses to ““SERIKALI ITUUNGE MKONO”-STEVE KANUMBA”
Leave a Reply


Hongera sana bw.Kanumba.
Nakupongeza sana kwa jitihada zako katika tasnia ya filamu.
Ila ushauri wangu.Katika fani hii ya tanzania inabadi watu wakubali kuchagua moja.Mara nyingi ukisikiliza mahojiano au wengie wanataka kuwa waigizaji na wakati huo huo niwaongozaji wa filamu.
Mi nafikiri mtu akiamua kujikita kwa nguvu zote kupata ka elimu ka uzalishaji au uongoaji wa filamu itasaidia zaidi.
Pia changamoto kwa wazaledno wote kwa ujumla.Asilimi kubwa ya watanzania hatupendi kukubali vitu vya kwetu na kuendekeza fikra za kudhani kila kitokacho nje ni bora kuliko zetu.
Ila nawashauri.MNAONAJE hizo ‘tittle’ za filamu zenu mngekuwa mnaziweka katika lugha ya kiswahili maana lugha inayotumika umo ndani ni kiswahili na sio lugha ya malkia?
Maana wenzenu wa Nigeria wanapendelea kutumia english tittle kwa kuwa wanatumia pia lugha ya kiingeereza kwenye filamu zao nyingi ingawa wanazo pia za lugha za kwao?
Pia serikali inabidi kusaidia vijana kama nyie kama kweli wako makini katika kuondoa umaskini.
Kila la kheri Kanumba tupo pamoja.
Kazi nzuri BC.
Hongera Kanumba kwa jitihada zako na Uigizaji wako mzuri ambao unagusa wanajamii (ukigusa jamii kuna mambo 2 hujitokeza chuki na kupendwa kama imetokea basi tambua ujumbe umewafikia).
Kila lililo jema ktk shughuli zako.
BC hii imetulia.
Hi Kanumba, wewe upo juu sana, ila usijali wala kusikiliza maneno ya waswahili bali songa mbele huku ukimtazama mungu wako na utafanikiwa, ukipata mchumba usiogope kuanza nae kwani wewe ni kijana mtanashati unahitaji mpenzi wa kuyaongeza maisha yako kwa furaha na hata kama ni Wema poooa tu!
Nimeona movies chache za Kanumba na nimefurahishwa sana na uigizaji wake. Kwa kweli kijana unajitahidi, kaza buti siku moja utapata nafasi ya kuwa international actor kwani huko ndio pesa nyingi na compatition kubwa.
Big up BC.
Hallo Steve. Tafadhali tuwasiliane, mail yangu ni smiara86@hotmail.com. Kazi yako ni nzuri.
nimeona movie nyingi tuu za kibongo, jamaa wanajitahidi sana ni vijimambo vidogo vidogondio vinawashinda ila muda unavyozidi kwenda watakua poa. pia waache kucheza movie ambayo ukiangalia mwanzo tuuu unajua inaishiaje? nadhani mmenielewa nazungumzia niini!!!
Na we Dina sasa umezidi kimbelembele mpaka unafikia kumkuwadia kijana wa watu, eti hata Wema ni poa tu, kwani kakwambia umtafutie mtu. Tuliza ball mama. Mambo hayaendi hivyo.
Sanaa ya filamu bongo bado sana,kina kanumba inabidi mrudi darasani,Nina uhakika kabisa uwezo wa kuigiza upo ,Nimeshaangalia filamu zenu nyingi,kila moja ina makosa yake ,Jamani filamu haitengenenzwi na watu wanane.cinematografi ndo script writer ndo producer duu!!,Hatuwezi kufika.mwigizaji kama kanumba au ray ana jicostume mwenyewe.Vile vile wadungu movie haitengenezwi mwezi mmoja! Tamaa za pesa na dhiki ndo zinashusha vipaji hivyo.Kaeni tulieni pikeni kitu hata miaka miwili,support tutawapa kutokana na quality ya filamu sio tu kwa saabu ni ya wabongo.serikali inaweza kuwasaidia kwenye copyright muweze kudistributi fresh
Beutness; WHERE did i mention a word wema ON MY COMMENT? U PPL DONT HAVE THINGS TO THING ABOUT BUT DINAH! IT SEEMS MKILALA THE ONLY THING U THINK/DREAM ABOUT IS WHAT DINAH WROTE OR ‘LL COMMENT EVERY OTHER DAY…..whoever ananifuata-fuata must be lonely or her/his life is in ruin….
What do u get by hating ppl especialy DINAH(U DONT EVEN KNOW ME), what have i done to u?
Sijalelewa ktk mazingira ya kiswahili(kutokuwa mstaarabu), sijui na siwezi kupoteza muda kufuata fuata watu au kile wanachoandika/sema as long as hawavunji sheria.
Why dont u comment about the subject/topic which is about bongo’s film & Kanumba.
Dinnah umemaliza???!!1 Kama ndiyo, basi i’m sorry nilioverlook hukuwa wewe bali alikuwa Nerra. Pole!!
Yes Dinnah you are right, We should comment about subject concerned.Pole kwa usumbufu uliupata.Congrats Kanumba you done good job. ALL THE BEST KEEP IT UP.
Lakini hata hivyo Dinnah una kimbelembele sana kila kitu unajua wewe tu. Ndiyo mana kule kwenye mada ya Mwisho Mwampamba ulichambwa ile mbaya, kwa kujifanaya unajua kila kitu kiasi cha kuwapangia watu vile unavyotaka wewe. Punguza!Mwanamke taratibu mamaaa!
It dont need to please any1 incl u beutness.
4 the record; sio kuwa najifanya najua but I do know much about many things (intellectually) than u do, all this is b’cause of my prof. which u don’t know about.
GIve a rest na find something amusing to do.
Kha! wanawake taabu tu.
Pole kumbe we ni mwanaume na si mwanamke, sikujua.
Duuh wabongo bwana katika kitu tunajua ni kubishana….Eti ubora na ubovu upo sehemu zote ni kweli lkn ubovu wa Hollywood i bet my balls ni ubora wa bongo….
Maskini Ramsey ndo idol wa kanumba na mnategemea atakuja kuwa international idol haya tusubiri…The thing i hate bout Bongo ni kuwa kuna maigizo na hakuna Filamu…Kila kitu chao ni fake hakuna REal hata moja…Kuanzia vipaji hadi Scripts fake….Maskini kweli talents are born not taught thou shule muhimu kuweka misingi….
Huyu jamaa ni mbishi zaidi ya kuwa mkweli….Anabaki kudhani uzalendo ni ushabiki wakati maskini Pheew!!! anahitaji kuanza kuona aache kutazama….
Wabongo mlivyo hamjui kutafuta maana mtaanza kunisakama hapa wakati ndugu yenu kaongea upuuzi mtupu….Wanajiita wasanii lkn hawana hata cheti cha wiki moja ya mafunzo/semina/ za uigizaji watakuaje kisanii wakati hawali????
Sometimes metaphor muhimu ili kuweka Jamii mguu sawa….Najaribu kuwasaidia ndugu zangu wanaotaka kuwa successful unahitaji kuwa Real,Real and Real ndo uanze kushindana otherwise Itabaki ni mchezo ya kuigiza iliyopewa jina la Filamu….Adios
Tanzania dream. nakubaliana na wewe katika sentensi chache, kwamba bado Tanzania watu wanafanya maigizo, lakini tunaomba ukumbuke pia kuwa ndio kwanza hawa watu wanaanza, atleast kanumba amesema anamzimia Ramsy kama Muafrika mwenzake, je unataka aseme Denzel Washington? Kwanini tusifie continent za watu wengine wakati tunayo continent yetu? Hata hao Hollywood walianza hivyo hivyo.
Duuh sasa hivi kweli mwalimu wako akiwa kipofu si atakupotosha?
Ramsey na Denzel nani Bora? hustahili hata kufananisha…Kinatochuponza ni kuona kila cha mzungu kibaya hata katika ambavyo tunahitaji kuiga mradi tu tujifanye wabishi kama ndio hivyo uigizaji umeanzia huko huko na umekomaa huko huko kwa wazungu why not tusiwaige???
Ramsey will never be gud since anaiga Bollywood,Bollywood ni Hollywood wannabes kwahiyo unaetetea kitu chochote fanya tathmini kwanza ni nini unachotetea….Uigizaji ulianza mwaka late 70’s au early 80’s una nerves gani za kusema umechelewa bongo???
Haki ya Mungu ndo maana bongo inabaki haikuwi kwenye kitu chochote…..
Mmmmh asante sana Dinna kwa kunisaidia kumchemsha huyu anayejiita Beutness, hivi imekuuma kumfugalia Wema kwa Kanumba! yaani yote niliyoandika haukuona umeona hiyo comment tu! ama kweli we ni Mmbongo na mswahili au unaishi manzese nini? Na kama wewe ni interllectual kweli mbona haujaelewa nilimaanisha nini kwa sentesi yangu, naomba uwe unatulia uelewe ndiyo utoe maoni yako, hapa tuko kuendeleza vipaji na kuchangia maendeleo yao sio malumbano yasiyo na faida, na unavyoonekana sio mwelewa mpaka ume overlook kwa Dinna mmmmhh! Pole! Kanumba keep it up and God Bless you!
sijachemshwa popote, nyie ndo mnaochemka.Poleni na maumivu naona mmeumia sana.
Dinnah the great.
Achana na hao watoto wakikuwa ……….
Kwakweli wewe beutness amechemsha!!!!!!!!!!!! Kubali yaishe. Aliyeanza topic amesema hata akiwa na Wema kwake poa, sasa wewe ukaibuika ooooooh unamkuwadia!! Isitoshe hakuwa Dinah. Eh jamani hapa kama ni kimbelembele unacho wewe. Pole we.
Naona na wengine mmeongezeka, poleni sana kwa maumivu mliyoyapata. Can I call a doctor for u?!! May be u need a first aid.
Hongera kanumba,ur amazing thats why beutness wants something good for you not WEMA please, u deserve more than that!!!!!
Thanks Yassie for concluding this issue, kwani beautness alitaka kutuitia doctor na tumeshukuru doctor umetokea na kumtibu pia yeye. All in all Kanumba songa mbele na target zako za kazi na maisha kwa jumla na mungu atakusaidia.
poleni tena.
Asante sana tumeshapoa beutness. Kazi njema
nawe pia.
thanx evry bdy 4 de comments….Mungu awabariki.
Kanumba kazi yako inakubalika lakini ningeshauri kupitia script kwa makini kabla ya kuanza production,napia ningependa kuuliza wadau wanachukuliaje suala la kuchanganya lugha katika film
I don’t know the guy, but he sound like a great actor. My opinion is toward editor of this journal, when you interview celebrity like this first tend to get the life background, so we can benefit where they are coming from. Don’t prepare the question, ask him as interview proceed. You did a good job, just work hard to be the best.
Eddt sijui una maanisha nini ukisema life background kwani page ya kwanza kabisa ya journal Kanumba ameelezewa historia yake kwamba amezaliwa wapi, Elimu yake mpaka maisha yake leo hii au mimi sijakuelewa au wewe haujasoma vizuri labda utueleweshe!?
big up bwana kanumba kwa burudani unayotoa.lakini ninakushauri sana katika filam za kibongo kutoutia unaijeria kwa mfano jinsi mnavyo vaa majoho ya vitenge na majumba mnayoact(eg;dengerous desire) sisemi muekti vichochoroni kwenye uchafu kama wafanyavyo kina bambo,kingwendu na wachekeshaji wengine ila nyumba za standard safi na siyo mabangalow kama mtumiayo kwa sababu reality life standard ya bongo tunaijua wote.pili katika filam zako nyingi ukristo umetawala kupita kiasi sasa hili nalo ungeliangalia kwa sababu bongo si nchi ya wakristo peke yake(eg;johari).mengine ni kua nakufagilia sana kwani unajitahidi au ningependa kusema umeleta mabadiliko makubwa sana katika filam za kibongo kwani filamu na vichekesho vingi vilikua ni aibu tupu kwa sisi wabongo tunaoishi nje ya nchi yetu kwa mfano unaangalia michezo yote ya kina kingwendu wamevaa nguo chafuchafu,wanalala katika mabanda na vyoo vya wazi wakati si kweli kua kila mchekeshaji ili achekeshe basi avae uchafu.samahani si kua nadharau mazingira lakini ni kweli jamani inabidi tubadilike.huo ni mtazamo tu
mungu akuzidishie kipaji ulichonacho, na maarifa zaidi,god bless u
We Dinnah na wenzako apa sio mahali pa kujibizana,kama mnajuana uko uko,Kanumba unafanya kazi nzuri sana huwa unanifurahisha sana unapokuwa una cheza filam yoyote ile,na nahisi kama ungekuwepo kwenye Filam ya Fake Pastor ungeifanya ingekuwa nzuri zaidi,Navutiwa na kazi yako.Fanya kazi kwa bidii madem wenyewe watakuja.reen_minja@yahoo.com
Poa Steve, K.
Kazi nzuri baba……
kaza msuli
lilian i guess ur more after uafrika.HEY sis its not about Ramsey being our fellow african…NOT AT ALL.The issue here is:Does Ramsey realy deserve 2 be a proper model 4 Kanumba?
The ishu is not kwamba kwa sababu Ramsey ni mwafrika mwenzake basi Kanumba amfuate kama real model wake..NO,Lazima 2angalie quality bwana.I guess TZdream is somehow right..Think it over again.
hey mambo kijana kaza buti sisi tunakuunga mkono
i am the nigerian Director who directed penina,my sin ,the director.i just want to say KANUMBA is such a wonderfull Actor and i also want to say a big kudos to MR.GABRIEL MTITU for his effort to bridge the AFRICAN FILM INDUSTRY THANK TO THE PEOPLE OF TANZANIA FOR YOUR HOSPIYTALITY ,KEEP UPM THE GOOD WORK
hi,i like everything about you kanumba,keep it up
kwa kweli nakupa hongera sana kwa kazi nzuri kanumba mungu akubariki ktk maisha yako yotee!!! keep well and GOD BLESS YOU FOREVER!!!!
mnajitahidi sana ktk maigizo yenu nawatakia mafanikio mema.na mungu atawazidishia.
amen
says
vicky
ongera si haba ulipofikia lakin umeanza kujisahau alfu nimesha wai kuona kuwa katika filam zako nguo moja unafanya nao filam zaidi ya mbili hii inaonekana kwua kwa siku unafanya filamu mbili au 3 kwa mda mmoja yani saa5 asubui apa saa9 kule na 11 jioni sehemu nyingine hali inayokupelekea kurudia nguo hio hio movies zaidi ya 2 kwa hivyo badilika dan tumia nguo kama hizo ndio zinakufa kutokana na part au s yako unayo tumia
hamna kitu hapa
KEEP IT UP KANUMBA YOU ARE GREAT,I ADMIRE UR WORK
BIG UP BRO!!yaani nazikubali sana kazi zako pia una uwezo mkubwa wa kuvaa uhusika katika kila field ambayo unatakiwa kuact,keep it up bro with more efforts.
sayz SAM a.k.a big SAM frm Tegeta mbweni masaiti
hongera sana kanumba, kazi unayofanya babu kubwa watu wengi wapo kwa ajili ya kukatisha tamaa lakini aliyekianzisha ni mungu na aliyekupa kiapaji ni mungu endelea mbele baba achana na waswahili all in all your gud.
Hi kanumba kiukweli me navutiwa sana na moves zako na nimejifunza mengi kupitia filims zako hata hivyo ucfikiri kila mtu atapenda kuona unafanya vizuri sie wabongo ni wachache sana wanaopenda maendeleo ya wenzao hivyo wewe chukulia hayo ni maneno ya wakosaji big up sana brother
wats up Kanumba first of all i appriceate ur acting for sure i real real love your filim and i learn a lot from you by tha way i just want to advice you why do’nt you act with others country eg; American, Asian nk. any way you know when you workhard some people they are jelous but never give up Kaaaaza buti m2222 hiyo ndo life ya kibofongo Says; Mariam wa The Arusha hoteli (department) Hk
Steve.K
Kakangu nakupa big up upo sawa mtu.kazi zako nazikubali unahaki ya kutuzwa kaza buti waswahili kusema kazi yao
Nafurahi kuona vijana wa Tanzania wanavyo chacharika na kupambana na Maisha. Ina tia moyo sana kuona vijana wanajichanganya na dunia (globalization), kwa mfano kucheza movie na wanaijeria ni hatua nzuri. Lazima tuanze na siyo kusubiri serikali. Inasikitisha pale ninapoona watu wanalalamikia serikali kwa kila kitu. Offcourse ni lazima kuanza ndipo support ya serikali itafuata. safi sana.
Mbona watu kama Dinah hawaeleweki? huyu Dinah kazi yake ni kusagia watu, kama una profession kali kiasi hicho humu ndani unafuata nini kama siyo wivu?
Ni wewe ndio Miongoni mwa watu waliomsagia Kanumba kwa mara ya kwanza sasa hivi unakuja hapa kuuza sura?
Naye Jonnie Mashaka ukamsagia vilevile, sasa wewe unachokitaka ni nini? Nadhani unatoa machozi ya wivu, kakoge maji ya baridi jasho la wivu likutoke weye Limbukeni.
Hongera kanumba, hongera Mashaka Tanzania inawasubiri msiwajali hawa wachozu ambao kazi zao ni kuchafua hali ya hewa kwenye ma blogs. Alafu kizungu chako pia kinahitaji msasa
hi my bro? kwa kweli unajitahidi ndungu yangu kaza buti, u never know sikumoja unaweza kuwa kama brud pit or tom cruz, achana nao wasiopenda vya kwao africa, me am from rwanda, nasikuhizi tunaziona huku kwetu rwanda, i swearmnajitahidi, but u knw what naomba plse dont mix languages again, nayenyewe inashusha quality nya movie.
wow.Iam from Kenya and i was very impressed after watch the movie THE POINT OF NO RETURN.Kanumba i should admit you among my best actors.You should be named 8th wonder of modern actor in the world.The way you potrayed your skills mean that you will go so far.Keep up Boy.Stay Firm.Trust God and everything will be okey.Lets nothing stop you.Go on keep in up
Margaret from Kenya.
Hongera saana mr.Kanumba kwakupata awrd hiyo inakustahili
ju wewe ni number 1.Na ningelipenda tuwe tukiwasiliyana kwa njia ya mail ya kwangu ni Queen_Niya89@hotmail.com.kiss
e’ bwana kanumba unatisha ile mbaya nakupa big up mtu wangu endelea na makamuzi hayo hayo speed 180 katika kuandaa filamu bomba sanaaaa.
Yani nina washangaa mnao mfagilia huyo jama
yani katika wakorofi duniani Kanumba yumo mwenye sifa haji sifu husifiwa nawengine. Huwezi kuwa mtulivu ukawa nama farakano nawaigizaji wenzako mfano utasikia
Mara bifu na frenk mara bifu na Ray !je huyo nimtu wanamna gani? Aundo ulimbukeni wamji?
hello bro how you doing i like all the movie you played with johari and i can say that how can i get same god bless you my email is baby_sakina_beautyful@ahoo.co.uk
hello bro how you doing i like all the movie you played with johari and i can say that how can i get same god bless you kanumba my emal is baby_sakina_beautyful@ahoo.co.uk
Asante Steven to get this opp to write this short comment i am writing from South Africa with love of your movies you are doing a great job man .I must say u are the great actor \talented. i must say S.A. support u so very much man .i was watching The lost twins its rocking man .what i love with african movies is that u learn a lot e.g love/ in-laws/hounesty/education . so big up Steve Gloria will support u no matter what. Asante
Hi S.C.K i am wondering if there is going to be part 3 of Opra -Sunday. you are doing a great job man .
kanumba umefanikiwa kuonyesha kipaji kwani unaigiza kiuhalisia sio kama wasanii wengine wa bongo wanaoigiza na unajua kweli hawa wanaigiza kuna kuwa hamna reality mi pia napenda kuwa muigizaji ila sijaanza I LIKE THE WAY YOU PLAY IN ANY SCENE
Hi Steven my main and favourite actor can u do me a big favour i am from South Africa i am sorry i dont understand swahili when i read ur comments. when watching the movie is easy coz i can read words on the screen. i love the fact that most of ur movies are in English thax 4 that keep it up asanteeeeeeeeeeeee.
Hi there my main and favourite actor this is Gloria from South Africa in Johannesburg.thx by using English in most of ur movies in Tanzania.i understand a bit of Swahili there and there but most of the time when i go to ur web its written in Swahili we are very much intr in reading ur profile .the problem we dont understand asante Steven big upsssssssssssssssssss.my email is gsekhethela@yahoo.com
hambali sinzi igiswahiri niko kigali RWANDA
NIPE SIMUZAKO
I LOVE YU SO MUCH
hongera sana kanumba kazi nzuri sana lakini naomba nikushauri watumie waigizaji kuigiza kama nora johari monalisa natasha ray swebe ni mkifanya kazi pamoja inaweza ikatisha sana. halafu script ziandikwe kiswahili tu pia hebu igizeni tabia zetu za kitanzania kiswahili johari uwe unajifunga kanga unapokua nyumbani kama ambavo sisi wabongo tunaishi
Hi Steven i have watched Johari it is interesting indeed and very sad . hoping that everyone would learn the message that u were trying to get across esp the youth of Africa.Asante we are waiting for part 3 .
nakushauri kaka Kanumba achana na wazushi na usonge mbele maana hao ni sawa mfa maji haishi kutapatapa ni wivu unawasumbua tu hamna lolote zaidi chuki binafsi. unafanya kazi nzuri sana hakuna mfano. good job men and god bless bless you for all you doin.
wabongo utawaweza? ni maneno tu ndo mana hawaendi mbele wanarudi nyuma tu kazi yao kugombea mabwana na kuchukua waume za watu. Mh, wamekishindwa choo cha shimo watakiweza cha kuflashi.
na hao wanaobishana wamekiosa kazi uskute wanakutaka ndo mana, kama wamekosa kazi sie kwe2 ha2na houC gal wangekuja tuwaajili tu. so wanakaa kukukomalia tu badala ya kuanza kukushauri mambo ya maana Mh. yatawashinda.
Ni sawa wewe ni handsome skatai na ni zaidi ya handsome I mean handsome zaidi DU! C mchezo. lakini achana na wazushi watakuumiza kichwa tu endelea na kazi yako Baba maana (UNATISHA)
kweli napenda kumfagilia sana wema sepetu huwa anaekti vizuri sana bigup
Kanumba you are a great actor, and very talented.just keep on working harder,and you will achieve more great things. Be blessed!
mimi lulu wa kwa dada Mwanja.
Hi Steven
Please know that SOUTH Africa like you so much .when replying to comments pls reply in English so that your biggest fan Gloria from Johannesburg can understand pls asante Steven keep up the good work.God bless you.Asante asanteeeeeeeeeeeeee.
hi, napenda kumpa hongera steven ,napenda movies zake ,zinanisomesha kiswahili,
keep goin’.I real appreciate ya work ,how can i talk to u.
my number +14019191250,
good job
hi how are you kanumba maybe if you read my comments i will be ahppy good job for what ever you did you are a nice man and actor as weel you say that you dont have girlfriend but issint wema your girlfriend or people are say only for anything my e mail is jamilicious2009@hotmail.com
Hongera sana Kanumba. Huwa naenjoy sana ninapoangalia filamu zako. unajitahidi sana
Mungu akupe maisha marefu uendelee kutoa movie kali zaidi. KAZI YAKO NI NZURI SANA
hi Kanumba….nimefurahi kusikia umesoma Bugoyi Primary school. Nimesoma Mwenege Primary school…a long time ago. Nimekaa sana Shinyanga… Is Sukuma your mother tongue?
Well back to your work: You are doing great. Ila usichanganye LUGHA….oanisha mambo hasa lugha. …kama title ni ya Kiingereza basi the whole thing should follow suit.
been also looking at your portraits…ambazo zinakuwa kama “product cover”…jaribu saana kupunguza make-up….it really shows off….need to do a good blend-in job…
Ni hayo tu….”wabeja baba”.
Kijana umejitahidi sana, na kama ulivyosema una hofu ya Mungu na iwe hivyo, vinginevyo ukijiona wewe ni maarufu utamsahau Mungu, kwani matukio ya hivi karibuni ya wewe na Wema yanakushusha hadhi yako, na jamii kukuona wewe ni muhuni fulani.
Tulia uoe na utulie na mkeo achana na wale wanaojiona ni mastaa kwani unaona wengi wao wanaishia pabaya kwa kumsahau Mungu.
Wish you all the best.
Ua such a wonderful man n wat u did 2 wema z ryt coz she deserve dat. I ril hate wat wema did 2 u bt u also u deserve 2 ‘v wat wema did 2 u coz u btry her n t ril hurts wen som1 cheat on u so u as a ril man try 2 settle dis
hi my lovely fan’s?hope every1 is fine am steve kanumba here. i js say thank u evrybd 4 d wonderful nd nice comment,promise u dat i wl never let u dwn coz i love my fans without u there is no kanumba,thank u 4d support nd GOD bless u all also thank u MR.JEFF MSANGI 4remaindn me 2 ready here am srry am verry verry busy bt i get it.4bussines issue contact me on http://www.kanumba.com…cheers.
YANI MWANA NDO UNAKUJA KUSOMA COMMENTS ZETU LEO????????? TUMETUMA COMMENTS SIKU NYINGI IVO???? ACHA KUWA BIZE KIIVO UWE SIKU MOJAMOJA UNAPITA KWENYE BLOG HII UNACHEK MAMBO. ANYWAY BIG UP SANA KWA KAZI ZAKO HASA ULIZOFANYA NA WEMA. YANI WEMA ANAFAAA SANA HUYU MTOTO KWENYE UIGIZAJI. KWANZA MZURI PILI ANAJUA KUDEKA TATU MPOLE YAAANI SIJUI NISEMEJE WEMA MZURI JAMANI NA ANAFAA KUIGIZA. BIG UP SANA STEV.
Yes man!
You’re real committed to the works. You know what to do and how to do it.
Of course I am not as much hobbing on movies and all that, BUT to that of yours (Kanumba), I dear to use up my presiouse time on them…
Big & kip it up man.
nashukuru sana kwa kuona web site hii leo napendezwa na kazi ambayo ndugu kanumba anafanya hapo TZ mimi naishi marekani ila napendezwa na movie za kanumba im so happy to get your website may God bless you all thanks.tumuunge mkono Kanumba
yes mr mimi napenda kuigiza lakini sina sapoti nanimwanafunzi ktk darajani sec kama vipi naomba sapoti hata kupitia email yangu
nasema asante kwamikanda unayo ceza sasa mimi nina kaa america TX SAN ANTOinoi
nataka nikujurishe kama meme cheza mkanda wewe na mke wako naitaji uniandikie please.
tena hata wa nzungu wanapenda kuona mkanda yako sasa tunaitaji tuone mke wake. okey
If you can do this I can by. god bress you.
hi how are doing my name is juriyetti i’m live ni American i hop u are good acto u did good job i love all u moveise u play i will love .so i want to get u phone number to talk over in phone .my Email is njudihte@yahoo.com if u write to me i will be proud u plz do to me ok thanks have nice day
I found your blog through a google search and have found some great info. Just thought I might post my thanks! So thanks lol.
well done kanumba,kazi yako ina impres,kweli inafanya vizuri sana,lakini nakushauri uangalie mavazi unayovaa kwenye filam,hayapendezi kabisa,yani unaaribu ubora wa filam zako kwa mavazi,jaribu kuchagua nguo zenye qulity,if you go for suit,choose the best one sio zile zenye maua na kumelemeta.
Hongera sana kanumba kwa filamu zako , mimi binafsi nazipenda sana nafuatilia kila unayotoa nnayo, inapendeza unavyotoa part moja ambayo inajitosheleza , na inatupa urahisi kununua, inapendeza sana, Keep it up guy!!!!
kanumba kazi zako bab kubwa .
nakupongeza sana kaka yangu kanumba kwa shuguli unazo zifanya kwani uigizaji wako unaleta msisimko kwa mshabiki.so,keep it up ma brother.
Hi Kanumba
I’m FROM KIGALI.just I’d like to tell you that i like so much your movies.
Hi Steven
You deserve to know that u are still a great actor as ever.I your biggest fan gloria i am really going to support u all the way Steven and Desmond Elliot keep up the good work guys you rock.From your biggest fan in Johannesbug Asante.
my name is findy,l’m 18 years-oldboy.kaka kanumba nakupenda sana.
Upo juu kaka…
Tatizo nini hadi leo hiihuna wife?
Upo juuuuuuuuuuuu, punguza macho juuuuuuuuu chagua kitu kitakachokufaa, kitakachoweza kkuvumilia shisa na raha man.
kama vile……,….., hata mm nipo bwana
Gud work
Mimi ni mkongomani ninahishi nchini Uholanzi, ninakupongeza sana kwa movies zako. Kila siku ni lazima niangalie. na mimi pia ninayo mawazo ya kuanza movies huku Uholanzi. lakini ningekuomba msaada wako mkubwa kwa kunipa mwelekeo kidogo. ninakutegemea sana tena sana.
uko juu kaka big up bt umaarufu ndo umekufanya ujichubue?…cjaipenda hiyo!
Jamani mabishasno ya nini?Munachotakiwa ni kupiga saruti kwani Bongo sasa ni moto wa kuotea mbali-Fanya kazi kanumba siku zote dua la kuku halimdhuru mwewe.
wewe kanumba bado ujafika mbali hata kidogo inabidi uwakubali wazungu kwanza ndio uwafuate hao wanaigeria kitu gani watoto wadogo hao
Katika sanaa yeyote inahitaji ubunifu wa hali ya juu sana. Kisanaa ya filamu bado sana ila tunajitahidi kinachohitajika ni ubunifu na kuheshimu kazi ambazo mnafanya. Richard wa BB ni mzuri pia katika filamu inahitaji ushirikiano yakinifu ili mfikie malengo yanayohitajika na siyo kulewa sifa wakati mtoto ndio kwanza anatambaa….! Tupo wengi ambao tuna vipaji vya kutunga na kuongoza filamu kwa mjumla wake ila hatuna support au niseme nafasi ni finyu mno nina script kama sita ambazo zipo full.Mkizihitaji tuwasiliane kupitia B.C, Nawatakia kila la kheri na mafanikio tele.
hongera ngosha
KOKUSHUBIRA du ningefurahi ungenipatia contact yako.Ni muhimu mnooo.
kaka nakukubali pia afu sura yako ka yangu some time watu huniita na kunihoji kuhusu wewe eti labda you are ma bro au lah mimi hucheka sana na sometime hukubali big up bro siangalii movie yoyote ya kibongo ambayo we hujacheza amini hivo kaka wish you lucky
Kanumba anajitaidi lakini nashindwa kuelewa kwanin aliboronga bigbrother.kuna walim wengi wa kingereza ata form six leaver atafute atafundishwa vzuri kuliko kutuaibisha tukaonekana wa tz wote mayayi hayapandi
Kanumba uko juu,kazi zako ni nzuri, songa mbele Mungu akubariki
KAKA KANUMBA WW NI MKALI.I LV DA WEI U AKT,PLIZ WOK HARD U’L MAKE T……………………………………………………….BIG UP MKUBWA……………………
kijan uko juuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu………..
wabongo hawakosi maneno machafu espcl f thy dnt lv u……………….ww wapotezeeeeeeeee………..temana nao.
Hi kanumba
napendelea kutoa shukrani mno for all kind of yo movies i usually watch all of yo movies but i like the famliy tears 1&2 i like both
is that sepetu got a boyfriend or is you his bf?right
and whose the little lady’s name
congrats man……………Wow i miss u i hope to see u in dar in 2010 i wish u the best
hi Kanumba,
i just want to congratulate you for your efforts which hsve made you be the real kanumb athat you are today.
keep it up and ejoy your life.
may God give you many years to live in this earth.
kaka kunumba uko juu nakusihi ujiheshimu acha na wema mchafu kwani anakuchafua tafuta aliyetulia ukimwi ni isu
hao wanakubonda hujui kiingereza wao wanajua uki waleta huku ni ziro mbona mimi niko marekani lakini ninababaisha kuogea kaza buti
safi sana mvuto kanumba yuko juu bwana kwani kingereza kazaliwa nacho kaulize UDSM watu wanaondoka na GPA kali lakini kiengeza kwao sio issue na wanapeta ile mbaya. Big up Kanumba.
Dear Mr Kanumba, I am from Australia but my backroud is Congo {D R C}, and I like to let you know that many African Australians like watching your movies but they still have same confusion and ask many questions a bout, kwanza wana uliza kwa nini mna zohezi la ku change mara kwa mara wa igizaji?kama wa kina Mkono wa Mkunure the fun man in your movie called Jahari, Mwanahidi Suka? na wengine wengi wako wapi?.
By other way I like watching your movie called family tear because that situation happenned in my family when I was young so may GoD bless you.
Pongezi kwako kaka uko juu Mungu aongeze kipaji chako zaidi
kaka upo juu dats y wabongo hawaishi kukusemea mabaya, kiip it up men!!!
Hi Steve: We have seen you from far man you need to make plan by visiting South Africa .I still believe that you and Desmond Elliot can be a good match when acting together you are so talented reveal all your Gods gift to Africa you are going far and far far far God bless you guyys u rock. keep up the good work.
from your biggest fan from Johannesburg, Soweto
Asante sana.
da mtu wangu ndo hivo unakula tu maisha nakushauri fanya kazi usiendekeze ujinga
acha wakupake matope yenye harufu mbaya lakini mungu awasikii ndio kwanza anazidi kukupa vyako vipaji kijana unaaweza tena sana,
KAZA BUTI KAKA WASIKUTISHE WOTE WANAOKUPONDA WANA WIVU NA KAZI ZAKO WW NIMKALI ILAMBAYA NAKUHUSU SWALA LA ENGLISH USIBABAIKE KWANI SS WA TZ TUMEWEKA KISWAHILI MBELE SANA SO NA AMINI SS WA BONGO WOTE TUNA UNGA NA SUPA GLUE AKUNA ANAYEWEZA BIG UP BRO KWA UPANDE WA DEMU UMETOKOTA ACHANA NA WEMA SIFA ZAKE AZIENDANI NA ZAKWAKO TAFUTA DEMU KAMA JOKATE.
kaka upo juu km obama kaza buti m2 wng ni hayu tu
kaka upo juu km obama kaza buti m2 wng ni hayo tu
Uko juu bro kaza buti achana na wazushi watakuharibia kazi. ushauri wangu hata kama umeachana na Wema yale yalikuwa mapenzi na sio kazi, Wema alikuwa anafit sana na wewe kwenye movie so it will be better kama utaendelea nae katika suala zima la kazi. Ni hayo tu kwa leo nakuatakia kazi njema na mafanikio zaidi.
Ndugu yangu kazi zako ni nzuri sana kupita maelezo ila bado ninahitaji mapya na mazuri mengi kutoka kwako mzee.Achana na wanaotaka kukukatisha tamaa
Kanumba is very good,na napenda sana movie zake ,kwakwel anjituma na he knows what he is doing..kip it up boy,God Bless you
Hi Mr STEVE i’m JASON from South Africa i support the decisions you took.If somebody want to enterfire with your life while you stil looking farward to your succes you chase them away.I like your movies and the way you guys acts is perfect and may god give you along lasting life bye and takecare
keep it up bro.
Kaka wewe ni kioo cha jamii ndugu wote ni vijana usilewe sifa leta kazi za ukweliiiiiiiiiiiiiii yaani siooni zaidi ya uzinzi ulionao badilika mtu wangu utafika mbali habari za chaz baba mala wema co inshu. Jimmy new york tchaooooooooooooooo.
Ebwana broo minakukubali sana mtu wangu tena sana kazi zako zapo juuuu tena juu sana broo so naomba ukaze booot mkumbwa bg up
Bonjour Monsieur KANUMBA Steven
Je suis de la nationalité Congolaise (RDC), et je reste dans le Territoire d’Uvira, Province du Sud-Kivu, ville frontalière de Bujumbura (Burundi).
J’estime qu’il est important de féliciter Monsieur KANUMBA Steven de l’œuvre qu’il ne cesse de produire. Néanmoins, la nudité semble être une armée pour ses actrices, car …
Jaribu kurekebisha hayo madogo, ila Congo inakupenda sana.
kanumba kama uliwaipendana na wema hiyo nijambo la kawaida kwa kijana km hajaoa kwa nini usikubali ili kutoa dukuduku kwa mashabiki?uchumba unajika ila ndoa siyo vizuri ingawa wamoja wanachukulia jambo la kawaida
You guys are super we really need to work pamoja