MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

 

Yakitajwa majina ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya ambao, kwa kutumia au kupitia muziki, wamekuwa ni “mabalozi” wazuri wa Tanzania katika nchi mbalimbali duniani, basi jina la Nice Lucas Mkenda au maarufu kama Mr.Nice ni vigumu au itakuwa sio uungwana likikosekana.

Tangu alipoibuka katika anga za muziki mwanzoni mwa miaka hii ya karne mpya, wengi wamecheza nyimbo zake, wakubwa kwa wadogo. Kwa wakubwa nyingi ya nyimbo zake zimekuwa zikiwakumbusha enzi zileeee… wakati kwa wadogo amekuwa akiwapa ladha ya wakati huo katika mirindimo ya kisasa. Nyimbo kama Kidali Po, Kikulacho na ule wa Fagilia ambao kwa muda fulani uligeuka kuwa kama wimbo wa taifa ni baadhi tu ya nyimbo zilizomfanya Mr.Nice asikike kila kona.

Katika siku za hivi karibuni, yamekuwepo maneno mengi sana juu ya msanii huyu. Yuko wapi? Mbona haonekani? Ni kweli kachacha na kufilisika kimuziki? Hivi nini kimemtokea? Ilimradi kila mmoja amekuwa na maswali yake na majibu yake mwenyewe hata kama sio timilifu.

Hivi karibuni kabla hajaungana na wasanii wenzake katika tour ya FIESTA, BongoCelebrity tulipata muda wa kufanya naye mahojiano yafuatayo ambapo alijibu maswali mengi yakiwemo hayo hapo juu ambayo wapenzi wa muziki wamekuwa na hamu ya kupata majibu yake. Anatarajia kutoa albamu yake mpya hivi karibuni. Kazi kwenu

BC: Unaweza kutueleza kwa ufupi historia ya maisha yako. Ulizaliwa wapi, ukasomea wapi na vitu kama hivyo?

MR.NICE: Mimi nimezaliwa Rombo katika mkoa wa Kilimanjaro tarehe 8/8/1978. Shule ya msingi nilisomea Ilala Boma jijini Dar-es-salaam kabla sijaelekea tena Moshi kusoma katika seminari ya Maua.

BC: Umekuwepo katika muziki unaojulikana kama muziki wa kizazi kipya kwa muda mrefu sasa. Ulianza vipi mambo ya muziki?

MR.NICE: Muziki ulikuwepo kwenye damu yangu siku nyingi sana. Kwanza nilikuwa mwimbaji mzuri sana wa kwaya makanisani kuanzia zile za watoto mahali kama pale kanisa la Msimbazi. Automatically nikajikuta napenda mambo ya muziki mpaka nilipokuja kuanza rasmi mwaka 2000.

BC: Je ulipokuwa mdogo maisha ya uanamuziki ndiyo maisha uliyokuwa ukiyatarajia mbeleni au?

MR.NICE: Kwa kweli sikufikiria kitu kama hicho. Mwanzoni sikuuchukulia muziki kama ndio itakuwa career yangu. Nilikuwa naimba kama hobby. Lakini baada ya mwaka 2000 ndipo liliponijia wazo kwamba huenda naweza ingawa bado nilikuwa sijiamini sana. Nikajaribu kutoa single yangu ya mwanzo iliyokuwa inaitwa Friday Night. Ile ndio ilinipa mwongozo na msukumo wa kuweza kufanya kazi za muziki maana ilipendwa ghafla bila hata mimi mwenyewe kujua. Kipindi hicho nilikuwa naishi na mama yangu mzazi Zanzibar kwa hiyo nilikuja Dar-es-salaam nikairekodi kasha nikaicha studio nikarudi zangu Zanzibar. Nilirekodi Mawingu Studio kwa rafiki yangu wa siku nyingi sana anaitwa Bony Luv ambaye mmojawapo wa maproducer wa mwanzo kabisa hapa Tanzania. Yeye kumbe ile nyimbo aliijua kwamba ni nzuri.Yeye ndio aliipeleka redioni bila hata kuniambia mimi. Kilichotokea ni kwamba wimbo ukaanza kupendwa bila hata kujua mwimbaji wake ni nani. Kwa hiyo mimi niko Zanzibar bila kujua chochote kinachoendelea ghafla nikaanza kuitwa kwenye interviews mbalimbali na matamasha nk.Huo ndio ukawa mwanzo wa muziki kujiingiza rasmi katika muziki.

 

BC: Unaweza kuielezea vipi style ya muziki wako? Kwanini uliamua kuiita TAKEU?

MR.NICE: Unajua mimi nilitoka tofauti kidogo na wasanii wengine.Kama unavyojua wasanii wengi wa Tanzania wanarap na kufanya style za hip hop. Sasa mimi nikawa naimba sio kwa R& B bali kufuatisha uasili na ndio maana ukitazama nyimbo zangu utakuta kuna mambo ya uasili hususani katika beats ambazo zipo kwenye uasili zaidi na sio commercial kama wanavyofanya wasanii wengi wa hip hop.. Kwa hiyo nikaamua kuuita TAKEU ambapo TA inasimama badala ya Tanzania na KE kwa Kenya na U kwa Uganda. Kwa hiyo ni nimejaribu kukusanya tamaduni za nchi hizi tatu za Afrika Mashariki na kuziweka pamoja. Na utaweza kuona kwamba baada ya hapo wasanii wengi pia wamekuja kuhamasika na kuanza kuimba wakitumia style hiyo. Kwa hiyo naweza kusema mimi ndio mwasisi wa TAKEU style. Kwa sababu mtu anajaribu kuimba na kusema ngoja niimbe kama Mr.Nice na kweli anakuwa. Kwa hiyo imekuwa ni style yenye mafanikio.Unaweza ukasimama mbele ya wadau wa muziki na kusema unaimba style ya TAKEU na ukaeleweka kwamba unaimba style ya Afrika tofauti na styles zingine kama hip hop ambazo kila mtu anajua kwamba ni ya kimarekani. Hiyo imenisaidia sana hata katika kujimarket na ndio maana unaniona imekuwa rahisi kwangu kupata show za nje. Hiyo inatokana na historia yangu, uimbaji wangu na hata uchezaji wangu.

BC: Maneno au tungo unazotumia katika nyimbo zako ni maneno ambayo yamezoeleka miongoni mwa watanzania tangu enzi na enzi. Nyimbo kama Kidali Po, Kikulacho nk. Unaweza kutueleza hatua kwa hatua katika jinsi unavyotunga nyimbo zako? Huwa unaanza na nini kwanza?

MR.NICE: Kwa kifupi naweza kusema mimi nina bahati ya kupendwa sana na watoto wadogo.Halafu nina bahati ya kupendwa pia na watu wazima wenye heshima zao. Sasa hapo kuna mambo mawili, ni lazima nijitahidi kukidhi haja za makundi hayo mawili ya watu kwa wakati mmoja. Kwa hiyo ninapokaa kutunga mashairi yangu nahakikisha kwamba kama baba, mama na mtoto wamekaa sebuleni wanaweza wakasikiliza au wakaangalia. Kwa sababu ukianza kuweka yale maneno mazito mzazi hawezi kukubali mtoto wake akasilikiza au mtoto hawezi kuyasikiliza mbele ya wazazi wake au akaangalia mbele ya wazazi . Kwa maneno mengine unakuwa umewatenga watu katika makundi fulani fulani.Lakini mimi nakuwa nipo kote kote. Ukichukulia nyimbo kama kidali po kwa mfano..wewe uliimba mimi niliimba, babu zetu waliimba, baba mama na hata watoto zetu wanaozaliwa sasa hivi bado wanauimba huo. Kwa maana hiyo hata usipoupenda wewe mwanao anaweza akakushawishi ukaupenda.Ukisikiliza utakumbuka jambo fulani au enzi fulani. Ninachojaribu ni kuepuka kurekodi wimbo ambao watu watashindwa kuangalia au kusikiliza mbele za watu kwa sababu ya kuona aibu jambo ambalo linamfanya mtu asiwe na jinsi bali kuzima TV au redio.

Pia nyimbo hizi zinanisaidia kujenga urafiki wa kudumu na watoto kuanzia wakiwa wadogo.Kwa maana hiyo jina langu litaendelea kuwepo vichwani kwao kwa miaka mingi sana ijayo. Pia kwa sababu napiga miziki ya kuburudisha zaidi inakuwa inanipa heshima kwani ndio maana napata mialiko mingi. Wanaonialika wanakuwa wanajua kwamba tukimleta Mr.Nice hapa tutapata show nzuri na ya heshima isiyo ya kihuni. Huwezi kumfukuza mtoto kwa sababu wimbo wa Mr.Nice umeanza kupigwa.

 

Mr.Nice akiburudika na watoto.

BC: Kuna wakati ulikuwa ndio msanii anayelipwa au ghali zaidi (kwa kila tamasha) kuliko msanii yeyote Afrika Mashariki. Ni kitu au vitu gani ulivyovifanya au kununua kutokana na kipato “kinene” kama msanii?

MR.NICE: Mpaka hivi sasa bado nabakia kuwa msanii anayelipwa zaidi. Hakuna msanii anayenifikia kwa kulipwa kwa show moja moja kama mimi.Ukweli ndio huo.Hivi sasa nafanya show kwa dola 7000 kwa show za nje ya nchi. Kwa Tanzania ni dola 1500. Promoters wa muziki nchini wanafahamu hilo na ndio maana unakuta show zangu zinakuwa chache lakini ninapofanya show moja ninakuwa na uhakika wa kudunda kwa muda fulani bila kukimbilia show nyingine. Hii yote inatokana na uhakika wanaokuwa nao promoters kwamba ukimleta Mr.Nice atafanya show nzuri,watu watafurahi na hela yake itarudi.

Kitu ambacho nimewahi kukifanya kwa kutumia hela yangu ambacho nilijivunia na nitaendelea kujivunia mpaka kufa ni kwamba nilikuwa msanii wa kwanza duniani kwenda kutoa msaada kwenye kambi ya wakimbizi kule Ngara ambapo niliweza kutoa Tshs milioni nane (Tshs 8m.) kutoka mfukoni kwangu kitu ambacho hakijafanywa na msanii yeyote duniani. Sikutuma mtu bali nilienda mimi mwenyewe kwa wakimbizi wale ambao sasa hivi nadhani ndio wanaanza kurudi rudi makwao. Sasa milioni nane kwangu mimi, kama mtanzania ni nyingi sana. Ni zaidi ya milioni 100 au hata 200 kwa mastaa wa Ulaya na Marekani. Pia niliwafanyia wakimbizi pale show ya bure ambapo wote walifurahi sana,walilia sana. Kwa hiyo naweza kusema hicho ndio kitu cha maana sana nilichokifanya. Vingine hivi ni vya kawaida tu. Huenda hata bila muziki ningeweza tu kuja kuvifanya ..magari na nyumba kwa mfano havipewi nafasi sana nafsini mwangu. Nimejaribu tu kukumbuka kile ambacho nilikifanya kwa hela ambayo nimepewa na mashabiki wangu kwamba nilikifanyia nini. Pamoja na hayo nimekuwa nikisaidia sana watoto yatima. Na sio Tanzania tu bali pia Kenya, Uganda, Comoro misaada mingi tu kwa kadri ya uwezo wangu. Ndicho kitu najivunia na ndivyo vya ufahari kwangu.

BC: Nini kinakusukuma kwenda kusaidia watu kama wakimbizi, watoto yatima nk?

MR.NICE: Unajua kuna kitu kimoja ambacho mimi nafikiria..kila mtu ana roho yake, kila mtu ana sehemu yake ambapo anakuwa na kitu kinachomgusa sana. Mimi nimelelewa na mama yangu. Kwa bahati mbaya baadaye mama akafariki (RIP) kwa hiyo nikabaki peke yangu. Katika hali tuliyokuwa tunaishi na mama yangu ambaye alikuwa ananipenda sana.Tulitokea katika maisha ya shida mpaka baadaye yakaja maisha ya raha. Sasa ninapoona watoto yatima huwa najaribu kupiga picha,hivi vipi kuhusu yule mtoto ambaye amezaliwa hana kabisa baba wala mama wa kumuona halafu ni mtoto mdogo. Fikra hiyo ndio ilinisukuma na kwenda kutembelea kituo cha watoto wadogo kilichopo Dodoma ambao wanaishi na virusi vya ukimwi na ni watoto yatima. Nakumbuka nilitoa msaada wa magodoro na vyakula. Huo ndio ukawa mwanzo wangu wa kujitoa kusaidia jamii kila ninapoweza. Ukijaribu kuuliza utakuta kwa Tanzania nimechangia sana katika kutoa msukumo kwa wasanii kugeuka na kuwa wasaidizi wa jamii. Watoto kama wale pale Dodoma,hawana msaada na wanahitaji sana msaada wetu.

BC: Mpaka siku za hivi karibuni ulipoanza kuonekana tena kupitia vyombo mbalimbali vya habari, watu wengi sana wamekuwa wakijiuliza kwamba ulikuwa wapi nk.Maneno ambayo yamekuwa yakisemwa zaidi ni kwamba umechacha na kufilisika kisanii na ndio maana umekuwa ukijificha. Unaweza kutueleza nini kuhusiana na hilo?

MR.NICE: Labda nikuambie kitu kimoja kuhusu suala hili kwamba sijui nimechacha, sijui nimeishiwa kimuziki. Hii yote ni kwa sababu kila mtu ana mdomo wake na hakuna anayeulipia kuongea. Ukweli ni kwamba mimi sijatetereka kwa chochote, nipo na sio kweli kwamba sionekani. Unajua kuna stepu mtu inafikia ni lazima ubadilishe style ya maisha. Kama binadamu nina malengo na mipango yangu. Ninachoweza labda kuwaeleza wapenzi wangu wote ni kwamba wasiwe na wasiwasi na mimi.

Kama utakumbuka Michael Jackson alipotoa Thriller, alikaa ni miaka saba au nane bila kufanya albamu yeyote. Kwa sababu gani? Kwa sababu albamu alizokuwa tayari ameshatoa zilikuwa zinauza. Sasa sio kwamba nataka kujifananisha na Michael Jackson kiusanii au kimapato. Ninachojaribu kusema ni kwamba mimi kwenye muziki nimekaa zaidi kibiashara, sijakaa ili kuimba tu kwa sababu naweza kuimba. Ninapokaa na wadau wangu wakaniambia kwamba bado albamu au singles nilizotoa zinafanya vizuri sokoni, na bado zinaniletea income ya kutosha haina haja ya kufanya chochote sasa hivi, pumzika ili zizidi kuuzika zaidi mpaka zitakaposhuka ndio utoe nyingine ninakuwa sina budi kuwasikiliza. Nadhani hata kwenye masoko ya kimataifa ndivyo wanavyofanya. Ingekuwa watu wanatoa tu albamu kwa sababu wanajua kuimba basi watu kama kina R.Kelly wangekuwa wanatoa albamu kila ijumaa. Nadhani badala ya kuniponda watu wangeweza kunisifu kwa kuwa msanii ambaye anaweza kukaa muda mrefu bila kutoa albamu na bado aendelee kuwepo kwenye game.

Kitu kingine ambacho ningependa kukiweka sawa hapa ili wapenzi wangu waelewe ni kwamba wengi wanaoongea maneno kama hayo ni maadui zangu ambao wengi wao walikuwa marafiki zangu. Mimi nilikuwa nina tabia kwamba naweza nikakaa baa na kundi la watu hata ishirini nikiwanywesha bia, nyama choma nk. Zile enzi zikafika mwisho, nimekua. Sasa wale marafiki zangu ambao wakawa hawamwoni tena Mr.Nice akiwanunulia bia wanakasirika. Wengi wao walizoea kulala na kuamka, kumpigia Mr.Nice simu na kupanga leo tutakwenda wapi kutumia nk. Hao hao ndio baadaye walipoona mirija imekatika ndio wameanza kuvumisha maneno ya ajabu ajabu.

Huwezi kupima uwezo wa fedha wa mtu kwa kutumia vigezo kama vile siku hizi haonekani bar au kwenye clubs. Yaani unakuwa unaupima uwezo wangu kwa kupitia starehe? Je kuna mtu anaijua akiba iliyopo kwenye account yangu inasoma shs ngapi? Siwezi nikaishiwa halafu nikawa namiliki gari la milioni 18! Kumbuka kwa Tanzania hizo ni hela nyingi sana Jeff tofauti mahali kama huko Canada au Marekani na Ulaya. Siwezi nikawa nimeishiwa nikajenga, siwezi nikawa nimeishiwa nikaendelea kununua viwanja. Kwa hiyo bwana hayo ni maneno tu ya wabaya wangu ambao wameamua kwa sababu wanazozijua wao kuniharibia jina langu. Mimi ni mchaga bwana kwa hiyo najua fika jinsi ya kuiendesha pesa. Sijawahi kwenda kwa muda kumuomba pesa wala kumlilia shida hata siku moja. Hivi sasa mimi naelekeza zaidi nguvu zangu katika kuwasaidia watu wanaohitaji msaada wangu. Hivi majuzi tu nimetoka Kilimanjaro kutembelea vituo vya watoto yatima. Kumbuka hiyo sitegemei mfadhili yeyote. Ninakwenda kwa gharama zangu mwenyewe.

Mwisho badala ya watu na vyombo vingine vya habari kuangalia mambo yasiyo na msingi ningewashauri waangalie upande wa mazuri ambayo nimeshayawahi kuifanyia nchi yangu. Kumbuka kwamba mimi ndiye msanii ambaye nimetembelea zaidi ya nchi 28 duniani kote huko nikiitangaza Tanzania katika show zangu. Mambo kama hayo nadhani ndiyo yanastahili kupewa kipaumbele.You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

 

BC: Umejifunza nini baada ya mambo yote hayo?

MR.NICE: Hivi majuzi nimetoa wimbo mpya ambao nimeupa jina la Maumivu. Katika wimbo huu nimezungumzia marafiki ambao wamenitenga baada ya kuona kwamba hawapati tena walichokuwa wanakipata bila kukitolea jasho. Kwa kujifunza nimejifunza kuachana na marafiki wabaya na pia kutokujibu mambo mbalimbali yanayoandikwa magazetini na kusikika kwenye vyombo vingine vya habari ambayo mara nyingi ni maneno kutoka kwa wabaya wangu. Nilifikia uamuzi huo baada ya kugundua kwamba wa wanaosema hayo maneno ni watu wachache sana kati ya mamilioni ya watu nchini Tanzania. Wengi wao wanasema maneno mengi kutokana na wivu tu.

 

BC: Ni kwa kiasi gani inakuwia vigumu kwako kuamini tena watu baada ya mambo kama hayo unayosema yamekutokea kupitia kwa marafiki zako?

MR.NICE: Ni kweli matukio yote haya yamenifanya niwe mgumu sana katika kuwaamini baadhi ya marafiki zangu. Roho yangu inakuwa kama imetandwa na ukungu fulani hususani kwa marafiki zangu.Wapenzi wangu sina matatizo nao na ninawashukuru sana kwa support ambayo wanaendelea kunipa kwa kununua miziki yangu nk. Najaribu sana kuwa makini zaidi ili kuweza kutambua marafiki wa ukweli na wa uongo. Maneno ambayo yamekuwa yakisemwa juu yangu sio kwamba hayajanifikia, yamenifikia na kusema ukweli yamekuwa yakinisikitisha sana kwa muda mrefu haswa baada ya kugundua kwamba wanaovumisha maneno kama hayo ni watu ambao nilikuwa nadhani ni marafiki zangu wa kweli. Ushahidi ninao. Kwa kweli I hate marafiki wa aina hiyo. Kwa hiyo siku hizi ukinikuta na mtu ujue ni rafiki ambaye ni rafiki wa kweli. Bahati nzuri ni kwamba rafiki wa uongo hata ukimuangalia usoni tu hivi unaweza kujua.

BC: Katika baadhi ya mahojiano uliyowahi kufanya siku za nyuma ulikaririwa ukisema ulichagua jina Mr.Nice kwa sababu ulitaka jina ambalo litakuelezea vizuri wewe kama msanii na pia kama binadamu. Je kuna tofauti yeyote kati ya Lucas Mkenda na Mr.Nice?

MR.NICE: Mimi jina langu kamili kabisa naitwa Nice. Kwa maana hiyo jina Nice sio kwamba ni jina nililojiita kwa sababu za kimuziki tu. Mimi naitwa Nice Lucas Mkenda. Lucas ni jina la baba yangu na Mkenda ni jina la ukoo. Hilo ndilo jina lililopo kwenye vyeti na vitambulisho vyangu rasmi. Kwa hiyo labda nichukue nafasi hii kuwaambia wapenzi wangu kwamba jina langu kamili ni kama hilo hapo juu na sio kwamba ni jina tu la kisanii.

Kwa hiyo hakuna tofauti yoyote kati ya mimi kama msanii na mimi kama binadamu tu wa kawaida. Always Nice!

BC: Ni wanamuziki gani ambao kazi zao au maisha yao yanakuvutia?

MR.NICE: Wanamuziki ambao nawapenda na kupenda pia kazi zao ni kama Chameleon wa Uganda, mkongwe Mr.II, Lady Jay Dee. Nazipenda pia style zao za maisha. Hawa wote hawapendi kukwaruzana na mtu. Kimataifa nawapenda sana R.Kelly na Michael Jackson.

BC: Katika matamasha (concerts) nyingi ambazo umeshafanya duniani ni lipi ambalo unalikumbuka zaidi? Kwanini?

MR.NICE: Zipo nyingi sana lakini concert ambayo sitoisahau ni ile niliyofanya visiwani Comoro. Hiyo ilikuwa na wahudhuriaji kama 27,000 jambo ambalo lilikuwa ni rekodi mpya kwangu.

BC: Kwa mtazamo au maoni yako, mitandao ya internet inasaidia au kuumiza fani ya muziki? Kwa njia gani?

MR.NICE: Internet inasaidia sana ukuaji wa muziki. Kwa mfano hivi majuzi nimepata mwaliko wa kwenda kufanya show nchini Madagascar. Nitakwenda huko kwenye mwezi wa kumi na moja. Sasa walionialika wameniambia kwamba wameujua muziki wangu kupitia kwenye internet. Kabla ya hapo nilikuwa siwajui na wala wao hawanijui. Kwa hiyo kwa mtindo huo msanii anaweza hata kuuza muziki wake katika sehemu ambazo hakutarajia kabisa kuuza. Lipo pia suala zima la watu kupata wazo la kwenda kununua kwa mfano kazi zangu baada ya kuona baadhi ya miziki yangu kwenye internet. Masuala kama ya wizi wa kazi za wasanii kupitia kwenye mitandao ni mambo ambayo ni magumu sana kupambana nayo kwa hiyo inabidi tuutumie zaidi mtandao kwa faida.

BC: Nini kinafanya wimbo au albamu iwe nzuri?

MR.NICE: Labda nirudie kule mwanzo kabisa tulipoanzia. Kinachofanya wimbo au albamu kuwa nzuri ni mpangilio mzima wa wimbo wenyewe au albamu nzima. Kama msanii, unaweza ukaongelea masuala mengi sana kama vile ukimwi, njaa, matatizo nk. Lakini kumbuka kwamba kuna mtu ambaye ukimtajia shida anakuwa hakuelewi kabisa.Kuna watu ambao hawajawahi kuona shida duniani. Believe or not. Kwa hiyo mtu kama huyo ukimuimbia wimbo kuhusu shida na mambo kama hayo anaweza kukuambia zima muziki huo. Kwa upande mwingine kuna mtu ambaye hajawahi kuona raha duniani. Huyu anakuwa hajui hata kesho itafikaje. Mtu kama huyu ukimuimbia kuhusu raha na mambo kama hayo anaweza hata akakupiga manati. Kwa hiyo cha msingi ni kuangalia jinsi ambavyo unaweza kutengeneza wimbo au albamu ambayo itakubalika kwa pande zote mbili.Pia ni muhimu kutengeneza nyimbo ambayo inachezeka na pia yenye vionjo vitamu masikioni kimuziki. Kwa mfano kuna wakati nilifanya show nchini Japan ambapo asilimia ndogo sana ya waliohudhuria walikuwa wanaelewa lugha ya Kiswahili. Lakini kwa sababu muziki ulikuwa unachezeka basi kila mtu alikuwa anafurahia kuwepo pale.

BC: Lini unatarajia kutoa albamu yako mpya?

MR.NICE: Natarajia kutoa albamu mpya baada ya tour ya Fiesta. Nitatumia tour hii kama fursa ya kuitangaza single yangu mpya. Hivi sasa nafanya kazi zangu chini ya PrimeTime Promotions kampuni ambayo ndio kubwa kushinda zote katika masuala ya entertainment nchini Tanzania.Hii ndio kama Def Jam ya Tanzania.

 

Mr.Nice na wanenguaji wake wakiwa jukwaani katika mojawapo ya matamasha ya FIESTA hivi karibuni.

BC: Katika moja ya mahojiano kadhaa uliyowahi kufanya ulisema kwamba dini ni kitu muhimu sana kwako na ndio maana badala ya kuvaa aina zingine za vidani kama cheni nk wewe unavaa rozari. Ni kwa kiasi gani dini ina nafasi katika maisha yako?

MR.NICE: Ni kweli kabisa. Mimi naamini kwamba dini ni msingi mzuri sana katika maisha yangu. Kama kwa mfano nisingekuwa nategemea dini katika kuendesha maisha yangu sidhani kama ningekuwa hapa nilipo hivi sasa. Ndio maana kila siku nawaombea mema wabaya wangu. Kama nisingekuwa naongozwa na dini basi si ajabu ningeshajiingiza katika mambo ya kishirikina kwa minajili ya kulipa kisasi na mambo kama hayo. Badala yake yote nimemuachia mungu na kuzidi kumuomba kwamba awasaidie ili waone kwamba wanachokifanya sio kitendo kizuri. Nampenda sana mwenyezi Mungu na ninaamini kwamba hakuna kinachoshindikana kama unamuamini. Hii ni kwa wakristo, waislamu na dini zingine zote.

BC: Ni kitendo gani cha kufedhehesha (embarrassing) ambacho kiliwahi kukutokea tangu uanze kazi zako za muziki? Ilikuwaje?

MR.NICE: Labda kipindi Dudubaya aliponivamia na kunipiga kwenye steji jambo ambalo halikuwa la kistaarabu kabisa. Zaidi ya hiyo hakuna kingine. Show zangu zote huwa zinafanyika kwa amani na utulivu.

BC: Kabla ya kutoa albamu kwa mfano hii unayotarajia kuitoa hivi karibuni, ni kiasi gani cha pressure unakuwa nacho kuhusu kufanikiwa au kutofanikiwa kwa albamu unayotarajia kuitoa?

MR.NICE: Baada ya kutoa albamu nne zilizopita wasiwasi unakuwa haupo. Hii inatokana na maandalizi ambayo yanakuwa yamefanyika kabla ya kutoka kwa albamu yenyewe. Kwa hiyo vitu kama promosheni ya albamu vinasaidia sana katika kuondoa wasiwasi wowote unaoweza kuwepo kabla albamu haijaingia sokoni. Labda pressure ninayokuwa nayo hivi sasa ni kujaribu kufikiri nini cha ziada nifanye ili washabiki wangu watakaokuja kuniona majukwaani wafurahi kama walivyokuwa wakifurahi siku za nyuma.

BC: Baada ya matukio yote yaliyokutokea kama ulivyotueleza hapo juu, je unaamini kwenye “kusamehe”? Kama ndio ni katika mazingira gani unaamini katika msamaha?

MR.NICE: Mimi kwa kweli naamini kwenye msamaha. Ndio maana sijawa muoga wa kuwataja wazi kwamba waliokuwa marafiki zangu wa karibu kabisa ndio wanaozunguka sehemu mbalimbali wakieneza maneno ambayo sio ya kweli juu yangu. Ndio maana sijalenga mtu mwingine yeyote. Sijasema wapenzi wangu wala nani bali marafiki zangu mwenyewe. Ndio maana kwa msingi huo mimi nimewasamehe ingawa sitaki tena uhusiano nao. Waniache nifanye shughuli zangu. Hiyo itanisaidia mimi kuendelea kufanya shughuli zangu za kusaidia jamii na kuitangaza nchi yetu kimataifa. Naamini mashabiki zangu bado wananipenda na kuhitaji burudani zaidi kutoka kwangu.

BC:Umeoa au una mtoto?

MR.NICE: Mimi nina mtoto mmoja anaitwa Colin. Sijaoa bado kwani naamini ndoa inataka maandalizi zaidi. Wakati muafaka ukifika nitafanya hivyo.

BC: Asante sana Mr.Nice. Tunakutakia kila la kheri katika kazi zako.

MR.NICE: Asanteni sana. Mnafanya kazi nzuri sana.

Picha ya kwanza imenakshiwa ndani ya Chapakazi Productions na zilizobaki kwa hisani ya Michuzi JR wa Jiachie.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

58 Responses to ““SIJATETEREKA KWA CHOCHOTE,NIPO”-MR.NICE”

  1. Comment by miss pauline joseph on September 5th, 2007 3:24 am

    tatizi huyu zilimkuta hela akiwa bado mshamba alijisahau na kufuja pesa,sifa nyingi na madumu wote wake alisahau kuwa mungu ni wa wote.sasa mwache aonje joto ya jiwe.kwani mbona wapo wengi wanasota na maisha asisote kwani ye nani….ila duh mshkaji kumbuka kumwomba mungu maana unasikitisha sana

  2. Comment by kitoto on September 5th, 2007 4:49 am

    Sasa Mr. Nice amekuwa, unajua anachosema ni kweli kabisa, wasanii wengi wa kibongo wanaishi kufurahisha marafiki zao na vyombo vua habari. Mr. Nice umefanya vyema kubadili maisha yako. Kama kila mtu ajinunulie yake. Wenye hasira wameze vidonge kaka.

    Pia amenena vyema sana katika swala zima la kutojibizana na vyombo vile vinavyotumia muda mwingi kuua majina ya watu wengine ili wauze. BC inaleta mabadiliko hapa.

    Mwisho ningependa kumshauri Mr. Nice kutojifagilia sana akifanya mambo ya kimsaada, watu wengine wanaweza kukuzushia kuwa unafanya ili uonekane kuliko kufanyay kwa kusaidia zaidi. Cha msingi anachoweza kufanya ni kwenda na kwenye hizo shughuli zake na vyombo makini kama BC au kina Michuzi na kuwaachia wapige mbiu. Mr. Nice endelea kutenda wema kaka, kisha nenda zako.

    Waache waseme hadi wachoke, wakimaliza unatoa kibao kingine matata ili waseme zaidi.

    Nazidi kukuombea heri. Kama bado uko juu Mungu akuzidishie, kama umetetereka kama maadui zako wanavyosema Mungu akuvushe.

    UHURU!

  3. Comment by Bob Sankofa on September 5th, 2007 6:33 am

    Heko Mr. Nice kwa kuwaacha wabaya wako wamalize kusema na wewe kushika njia na kwenda zako. Walidhani utawaanzishia ligi ili magazeti yauze. Naamini msahuri wako wa sasa ni kiboko sana.

    Heko kwa kukata misaada za kipumbavu (Kunywesha watu 20 kila ukitaka) na kutoa misaada kwa watoto na wenye shida.

    Waache waseme ulikuwa mshamba, lakini ukweli ni kuwa sasa umeerevuka.

    Heko kwa kuamua kuishi maisha ya kukuridhisha wewe na si marafiki na vyombo vya habari. Wanaosema hovyo waache waendelee, midomo ni yao na kodi hawalipii. Naamini unajua unachikifanya.

    Endelea kuponda life kama pia unawekeza.

    heko Nice kwa kuvunja ukimya na kutuambia ulipo na unakokwenda. Wamesema sana, sasa zamu yako.

    Hadi wakati mwingine,

    UHURU!

  4. Comment by Freddyjoe on September 5th, 2007 10:44 am

    Hongera sana Mr.Nice kwa kuwatosa Wapambe- nilikuwa nakuona nao sana pale Club Ambiance, Sinza.

    Wapambe si watu, achana naye huyo miss pauline joseph hapo juu anayekuponda- anaweza kuwa ni mmoja wa waathirika wa ukatwaji wa “huduma” zako ulizokuwa unazitoa zamani.

    Yaani mpaka akina Masanja Mkandamizaji na the comedy crews walitumiwa na wabaya wako “kukumaliza” kuwa wewe sasa ni “kwisha”- shame on them. Wawe makini kwani hata wao waamenza kuboa. Hawana ubunifu tena, their days are numbered.

  5. Comment by babu on September 5th, 2007 11:36 pm

    acha uongo mwanangu maua seminary umesoma lini wakati tulikuwa tunasoma wote lombeta sekondari, acha kujifagilia bila mpango kwa kujifanya ulisoma maua.tatizo la wasanii wengi wa kibongo ni waongo na wanajisahau kwenye interview zao na kudanganya. kuwa mkweli kwenye interview babu

  6. Comment by dj tom in japan on September 6th, 2007 12:31 am

    Tunataka ukweli “lombeta au Maua secondary”?
    tunataka tuone nani ni mkweli, mr Nice au wewe unayepinga!!!!
    tunasubili hapa BC!!!!!

  7. Comment by tom on September 6th, 2007 12:33 am

    mhhhh

  8. Comment by Analyst on September 6th, 2007 12:35 am

    Nadhani tatizo la fedha lipo kwa watanzania wengi sio MR nice tuu, hatujui nini dhamani ya fedha leo and kesho.. hii ipo kwa kina Kikwete, Lowassa and Prof jay, it’s a deases that every Tanzania suffer in one way.

  9. Comment by chediel on September 6th, 2007 1:01 am

    Safi sana kwa kujitokeza kwani tumeambiwa mengi sana kiasi hata watoto wetu huko nyumbani wakawa wanajiuliza ni kweli mara ooh anauza madafu nk. LAKINI hapa umetupa ukweli wa mabmo kaza buti mtu wangu

  10. Comment by Tumaini on September 6th, 2007 1:46 am

    Nampongeza Mr.Nice kwa kukua.Maisha ni sfari na kuna hatua ambazo ukupitia na kuzifaulu basi unabahati.Kugundua makosa na kuyasahisha na kukiri inahitaji ujasiri na kupevuka kwa hali ya juu.Hongera sana Luca Mkenda.Kuhusu misaada ,ache iwe siri yako na ya mwenyezi mungu.
    Its the heart that does the diving not the bank account.It is spiritual so please keep it that way.Utavuna zaidi ukifanya hiyo siri yako na mwenyezi mungu.

    Nakuombea upate ili yatima na wengine walio katika mazingira magumu nao wapate.

    Mtamaduni

  11. Comment by Kimanumanu on September 6th, 2007 3:40 am

    This guy ashalost direction kabisaaa.Nilikuwa nikufuatilia muziki wa Mr.Nice kwa jinsi alivyoweza kupata mapato na akapata sifa kubwa sana kwa ujasiriamali aliokuwa nao katika muziki kwamba angeimba hata madudu ila watu wakakubali kwa ubunifu aliounesha.Nikiwa kwenye taasisi moja ya elimu ya juu kuna mhadhiri mmoja wa mabo ya ujasiriamali aliwahi mtumia Mr.Nice kama mfano wa kuigwa katika ubunifu wa kuingiza mapato hasa pale alipokuwa anatoa zawadi kwa mwanamama aliyeonesha uwezo katika shoo zake lakini kilichompata nashinda hata kuamini.
    Its true kuwa jamaa ana financial crisis kwa sasa regardless ya hayo anayojitetea.
    Guy sit down and think wapi ulianguka utafute mustakabali mwingine

  12. Comment by Loon on September 6th, 2007 9:23 am

    Me naomba kuuliza swali…Quote “nilikuwa msanii wa kwanza duniani kwenda kutoa msaada kwenye kambi ya wakimbizi kule Ngara ambapo niliweza kutoa Tshs milioni nane (Tshs 8m.) kutoka mfukoni kwangu kitu ambacho hakijafanywa na msanii yeyote duniani”.unquote.

    Is this true?….Mr Nice Ni msanii wa kwanza duniani kutoa msaada wa Million 8 T-Shillings?…au msanii wa kwanza TANZANIA?.

  13. Comment by mtz halisi on September 6th, 2007 9:48 am

    Big up sana Mr. Nice,
    umekua nami siku zote napenda nyimbo zako, huu ni mwaka wangu wa 70 tangu niione dunia lakini nyimbo zako huwa nacheza na wajukuu wangu.
    nasubiri kwa hamu album yako

  14. Comment by Jangala on September 6th, 2007 10:49 am

    Loon,
    Mr.Nice ni msanii wa kwanza duniani kwenda kutoa msaada kwenye kambi ya wakimbizi NGARA.Wasanii wengine wanatoa pia lakini hawakutoa Ngara.Umeelewa sasa?

  15. Comment by Mwali on September 6th, 2007 1:38 pm

    Katika Maisha kila mtu huanguka na kusimama. Mr Nice kuweza kukubali challenges za maisha inaonysha jinsi ulivyo komaa kichwani hali hiyo nayo inatakiwa iendane na ubunifu wa muziki uliokomaa. Albam ya Fagilia ilikuwa bomba mbaya zilizo fuatia kwakweli sio sana. halafu usiimbe nyimbo za kiingereza zina wenyewe.Una nafasi nzuri ya kuukuza muziki wako tunataka vitu vikali kama Fagilia ile kila mtu hawezi kuusahau. nyimbo zako zina maaudhui mazuri sana kwa jamamii. Mwisho kabisa kuhusu maua, besti pale vinaenda vichwa ukiniambia lombeta nitakubali lakini maua tafadhali jaribu tena .

  16. Comment by aliko on September 6th, 2007 7:55 pm

    Nice Msanii nyota wakutegemewa Afrika Mashariki, mkuzaji wa lugha ya kiswahili, muunganishi wa Tza Bara na Visiwani,mtunzaji wa utamaduni wa nchi za Afrika mashariki, ni muimbaji mwenye sauti inayoendana sambasamba funguo ya vyombo vya mziki, mburudishaji makini stejini(live) na kwenye kazi zilizorekodiwa,Asante sana kwa mchango wako katika anga hii ya Sanaa tuko pamoja lini unarelease kazi yako mpya mazee.

  17. Comment by mtamaduni on September 7th, 2007 2:40 am

    Give the guy a chance.Kila binadamu anastahili nafasi maishani,ajaribu,ashindwe,ajifunze,asonge mbele.Kama alivyosema Lady Issa”Kweli maisha ni mulima eeh,Kuna kuopanda na kushuka,ati kuteleza siyo kuanguka eeh…”

  18. Comment by kidumeso on September 7th, 2007 2:53 am

    Mr. Nice ni tu wa kutaka kujionyesha, kuna siku tulikuwa wote pale Billcanas kwenye grocery yake walipokuja wanawake basi aliacha kucheza pool na kuanza kujinadi kwamba watu wanywe bule. huo ni ulimbukeni jaribu kubadilika.

  19. Comment by Salim Simba on September 7th, 2007 1:43 pm

    Pole kaka tatizo umekum,buka shuka Asubuhiiiiiiiiiii!ila jitahidi unaweza ukajikwamua kidogo bt,kama Chammilion ni tajiri ww ungekua na akili ungekua millionea!boya wwe!

  20. Comment by Mary on September 10th, 2007 7:07 am

    Bwana Nice umekwisha wacha kuzuga kuwa mkweli. Your going down. Ila mrudie Mungu na ukumbuke pia ianweza kuwa ni laana kwani ulijivuna mno ulipozipata. Mpanda Ngazi hushuka!

  21. Comment by yesenya on September 11th, 2007 5:15 am

    hongera lakini punguza majidai.

  22. Comment by CASHMONEYHOLLAND on September 19th, 2007 11:03 am

    KWAKO MJOMBA NICE…MIMI MTANZANIA PEKEE ANAYEHISHI ULAYA NA MAREKANI ALIYESHIKA DORLAR NUSU MILLION CASH KATIKA MEZI 3..LAKNI LEO NAPANDA BASKELI KWENDA KAZINI…KUCHOKA KUMO…SEMA SAFARI HII UKIZIKAMATA KUMBUKA MAISHA MBIO ZA VIJITI KUNA KUPOKEZANA KIJITI.KUHUSU MZIKI WAKO..MIMI ZAIDI YA SIKINDE NA MSONDO SIKUJUA KAMA BONGO MNA MZIKI MWINGINE HADI NILIPORUDI BONGO 2004 MITAA YA JOLLYCLUB NIKASIKIA NYIMBO YAKO YA KIKULACHO…NIMEKUKUBALI…MZIKI WAKO UNAMAANA NA SIYO KWA WOTOTO TU..SEMA SHOW YA 7000 UNALIPWA ULAYA GANI AU MAREKANI GANI KANI TULKULETA HOUSTON KWA BUKU 2000…STAY BLESS NICE.

  23. Comment by dj kay(kiango)USA on October 24th, 2007 12:28 pm

    BIG UP 2 U MR NICE.
    litsen bro,mengi yatasemwa but at the end of the day u’ll always be u.Heshima uliyotupa TZ ni mfano mzuri,naomba hao wasema ovyo wamention yao,yana suck.Kaza buti keep doing big things bro,always follow ur dreams.(DJ KAY SAFARI DC CLUB)

  24. Comment by princess on October 25th, 2007 6:37 am

    HEY BABY BOI!NICE TIME WE HAD PAMOJA!HABARI YA BONGO?ME NIKO TU ENJERUMANI BARINDI TU KIASI YAANI!NAKUMISS SANA WANGU WA MOYO!LOOKING 4WARD TO SEE U SONN IN GERMANY!I LOVE U !UR PRINCESS WINNIE

  25. Comment by Emanuely on November 10th, 2007 2:27 am

    mambo vip m2 wangu wanasemaje huko bongo is cool m2 wangu. What is your occupation Am on the line listen 2 u.bongo is just nothing men.Am out

  26. Comment by kay on November 26th, 2007 5:40 am

    Hi mr.Nice kwa sasa siwezi kuamini upande wowote ili kujua yupi mkweli ktk maelezo yenu ila na ww ulizidi kujisahau, siku zote friends hutumia weakness ya mwenzao kuweza kukutumia lakini naamini umejifunza vya kutosha hivyo ukipata nafasi nyingine kama hiyo inabidi uitumie vizuri ili kurekebisha makosa yako yaliyopita na kuprove kwa watu kuwa ile ilikuwa ni uzembe uliotokana na kutokujua kwako.All the best!!!

  27. Comment by Lameck LEWI on November 27th, 2007 4:02 am

    Nakupaheko MR NICE !hivi huyu Dudu baya huwa anaimba nini? mwambieni hiyo sio fani yake aende kubeba mizigo hana fani ya muziki aachie wenye fani yamuziki.Aende kubeba mizigo bandarini Kigoma.

  28. Comment by Reg Miserere on November 30th, 2007 9:08 am

    Mi unaniboa kuvaa heleni .

    Ukumbuke na nyimbo ya injili pia maana ulitoka huko!!!…

  29. Comment by Bely Kasambula on December 9th, 2007 6:24 am

    Heko mzee,
    kuna milima na mabonde ktk safari ya mziki na maisha.
    Kaza buti.
    Nataka urudi vile ulikuwa unsumbua mwanzo.

  30. Comment by Mama wa Kichagga on December 20th, 2007 12:37 pm

    Tanzanians we are too much judgemental! Hivi mtu akichacha inakuhusu au kukusaidia nini? Can we mind our own business? Mara mtu kavaa hereni, mara kimini, mara bangili, mara rasta ni bangimen, mara nguo fupi nk ………………. it is too much for nothing! Can we stop judging people negatively and start living and develop our beautiful TZ? Jamani tupeane uhuru na nafasi ya kukua na kuisha kwa amani hapa duniani. TUKUMBUKE MAJUNGU HAYAJENGI WALA HAYANA BARAKA MBELE ZA MWENYE ENZI MUNGU.

    KAKA NICE BIG UP, Ila chagua maneno ya kusema na mengine meza yaani weka kifuani hata kama yamekuumiza! Pia kumbuka “mkono wako wa kulia unapotoa sadaka basi hata mkono wa kushoto usijue”. Maana yake ni kwamba msaada ni siri yako na Muumba wako sio vitu vya kutangaza acha wao waseme sio wewe wasiposema Mungu anajua kaka.

    NAKUKUBALI UNAFANYA VIZURI, WABAYA WACHANA NAO SI UNAJUA TATIZO LA NYONGO IKIZIDI?

  31. Comment by Mama wa Kichagga on December 20th, 2007 12:53 pm

    This is for you Nice:

    1. Concentrate with your career
    2. Enjoy your life to the fullest
    3. Plan your future ahead – houses/plots/cars is not your future these are life’s necessity
    4. Plan an investment in music – recording studio, basic music training school etc
    5. Nabii haheshimiki nyumbani kwake, kama una marafiki nje ya TZ wanakutosha sana wachana na hao watakaokukwaza
    6. Umesema hujaoa, collin katoka wapi? Hapa naona kuna tatizo isipokuwa ukitaka waweza kulirekebisha mara moja. Sio lazima uoe na mafarasi nenda kanisani wewe na wasimamizi wenu ili upate kibali cha baraka maishani mbele za Mungu. Hapa hujanigusa kabisa maana kumbuka wewe ni muhimu ktk jamii hivyo mambo yako lazima yawe yamenyooka! Sina maana ya kukuhukumu ila rekebisha mara moja
    7. Unafanya vizuri sana katika kazi, naamini ukisoma michango yote hapa (chukua yenye mwelekeo + tu) utaweka historia nzuri sana.
    8. Dudubaya kweli alikufanyia kitu mbaya, ila msamehe na kusahau maana hata yeye aliko sidhani kama anafurahia kitendo chake hicho maana ni historia ya aibu kubwa! Naamini angepewa nafasi asingerudia!

    I am always neutral and straight to the point, “NO” means no and “YES” is always yes.

  32. Comment by Mama wa Kichagga on December 20th, 2007 1:09 pm

    Hii ni kwetu sote wanablog na wachangiaji wa mada nina maoni/maombi tofauti:

    1. Blog zinasaidia sana ktk kupashana habari

    2. Tunapochangia huku tukumbuke hizi blog zinasomwa dunia nzima na wa TZ na wasio wa TZ

    3. Mnaonaje tukatumia lugha na ushauri mzuri hapa kwani hii inatunyima maksi sana. Mfano nina rafiki yangu aliwahi kutembelea blog zetu akatoa hoja kuwa waTZ tuna maneno ya kukatisha tamaa zaidi ya kujenga, wivu nk nanukulu “You TZs can you honur your people? I used to hear TZs are nice but I read from you people, and I am starting to hate you, you dont love each other, a lots of non-sense in your blogs. If you dont honor them how can we do it for you?”.

    4. Inabidi kaka mwenye hii blogu atupe somo la lugha nzuri za kuchangia hapa vinginevyo tunaharibu chakula cha watoto hapa!

    5. Tubadili fikra zetu na namna ya mitizamo yetu, sio lazima ukivaa maksi basi kila mtu avae kama wewe. Mtu akivaa mini muache huenda anasikia joto je? Tujifunze kuwa huru kijamii maana naona tuko katika utumwa mkubwa wa mawazo na mwelekeo wetu. Tukumbuke hizi ni zama za utandawazi tukizidi kujichimbia basi mvua na fuko zitaendelea kuwa zetu.

    Ni msaada kwenye tuta hapa,
    Asanteni.

  33. Comment by majaliwa obeid on January 12th, 2008 12:02 pm

    hello mr nice mambo nakuona uko unapolomosha kibao au sio endelea namuziki ok

  34. Comment by mabula julius on January 30th, 2008 9:20 am

    mambo vipi kaka nice nimekuwa mtu wako wa karibu sana kufuatilia kazi zako hivyo naweza kusema nakujua kiundani,mimi tukio la kwanza kusikia nilimsikia salama jabil wa planet bongo kwamba umeishiwa mpaka umeuza gari yako ya kutembelea kuanzia hapo maneno yakawa mengi sana baada ya hapo ukatoa albam ya video ya bahati, nikasema mshikaji bado yuko wima wakati maneno yanaendelea kusemwa ukatoa albam ya bwana shamba.hakika wewe hujaishiwa bali umebadilisha mfumo wa kuishi,big up sana ongeza juhudi kwenye kazi zako bado tunakufill sana.mazuri mengi ya mtu hufichika ila mabaya machache husikika.

  35. Comment by mabula julius on January 31st, 2008 3:12 am

    Ya juzi sio ya jana na yajana sio ya leo umefa nya vizuri sana nice kubadilisha mfumo wako wa kuishi mimi nilijua unavyo zunguka nje lazima utabadilika,pole sana kwa maumivu uliyo kuwa nayo,nyimbo nyingi sana umekuwa ukisema hutoja li unasonga mbele, songa kwelikweli hata wabaya wasiwe na sauti,mimi ni shabiki wako watoka kitambo sana nafill sana nyimbo zako na najua unajua na unaweza,pia naomba utume WEBSITE yako kutumia mail ya hapo juu.

  36. Comment by Mr. Upendo Furaha Amani on February 2nd, 2008 7:02 pm

    Mr. Nice, ni kweli unafanya mambo mazuri na ninakusifu.
    Isipokuwa nina neno na wewe nalo ni: Kwa nini unavaa Hereni??? Ulaya “Mashoga” ndio huwaga wanavaa hereni, wewe tukueleweje?
    Penda haiba yako ndugu Mtanzania, tutasikiliza nyimbo zako na kuhudhuria unapo “pafomu” sehemu yoyote ile hata kama hujavaa hereni. Acha kuiga, utaiga na mengine yasiyoigwa.
    Ninakutakia kila la heri.

  37. Comment by Neno on February 2nd, 2008 8:38 pm

    Mr upendo Furaha Amani. Ni ulaya gani hiyo unayozungumzia???

  38. Comment by Mr. Upendo Furaha Amani on February 3rd, 2008 4:11 am

    Europe.

  39. Comment by jomaeli on March 5th, 2008 6:53 am

    hihhihi..we mama wa kichaga unataka kusema nini/kama mtu anakua mwongo asiambiwe?

  40. Comment by mariam on March 6th, 2008 3:01 pm

    hallo my name is mariamu
    nina taka kuku salimiya.
    ukipenta email yangu uniyandi kiye byeee

  41. Comment by zaina seif on May 10th, 2008 7:20 pm

    Upendo, kwahiyo hata wewe nishoga sio? kwa sababu hata wewe unava hereni pia! aca izo mpe kijana haki yake hereni sio uhanithi . naulaya gani hiyo unao ongeleya wewe? mombasa au! Big up Mr nice kazi bomba unayo ifanya wanao chonga achananao.

  42. Comment by Mr. Upendo Furaha Amani on May 12th, 2008 2:48 pm

    Hivi wewe Zaina Seif unaamini kwa Mungu Muumba wa Mbingu na Nchi kweli?

    Lakini hata Jina lako linaonekana kuwa wewe Unaamini kwa mungu wako SHETANI.

  43. Comment by zaina seif on May 13th, 2008 2:45 pm

    Upendo, hivi wewe ni dini gani? huamini kuwa kuna dini na dunia? na ndio maana M/mungu aliwatakasa mitume ili wasifanye maovu! kikubwa nikuomba mwisho mwema tu mungu hakuandika kweye kitabu cake kuwa hereni ni uhanithi! nadhani wewe ndio mwenye hiyo dini ya ushyetwani. aca izo muunge kono tz mwenzio ndio maana hatuendelei , yeye siwakwanza va hereni na wala hatokuwa wamwisho. so mpe haki yake unajita upendo huna upendo wala nini we nimajungutu, ujuwi cocote kuhusu upendo! wewe mbona unava hereni lkn!!!!!!!!!!! huwa tunaliya na mola kumbe binadam ndio wanaba. Big up mr nice nakufagilia

  44. Comment by annie on June 26th, 2008 1:19 pm

    hivi we emmanuel hapo juu,hata kuspell jina yako ni shida n u still write ur comments in english sijui cha wapi,nenda kwanza english course ndo uje kutuandikia,si kama wengine hatujui na si kama ukiandika in english ni mbaya kinachotakiwa kujiuliza ni,r u fluent in speaking it?can u write following all the rules required?acha kujiabisha.
    na si wabongo tuache kuchanganya matumizi ya l na r mana comments nyingi watu wamechanganya badala ya hereni mtu anasema heleni,raha mtu anasema laha jamani tunaribu kiswahili na ni aibu pale tukijaribu kujivunia lugha yetu,kabla ya kumsema mr nice tujirekebishe wenyewe kwanza.

  45. Comment by Mr. Upendo Furaha Amani on July 18th, 2008 4:51 pm

    Ndugu unayejiita ‘Zaina Seif’; kabla ya kutoa maoni yako, na kunitukana ungesoma kwanza post yangu #36 vizuri.

  46. Comment by zaina seif on July 29th, 2008 5:50 pm

    Unamaanisha nini ningeisoma vizuri! huh? umesema kuva hereni ni ushoga! kwa hiyo mr nice anafanya mambo ya kishoga! si ndio? ukasema inamana hiyo ulaya, mimi kama mshabiki wa mr nice iliniuma kwa sababu siyo kweli kwamba mwanamume kuva hereni ni ushoga, nipambo kama pambo lingine! mbona wamasai wanava! huh? mimi sijakutukana, ila wewe ndie ulie niambia hata jina langu linaonekana naamini muumba wakishetani!! naomba uliambie jina langu linakasoro gani, na kwa nini liwe la kishetani?! Ushetani unakuja vipi katika jina langu Zaina Seif nieleze labda kweli ni lakishetani mimi sijijuwi!! labda kweli dini yangu ni yakishetani kwa sababu ukisoma jina langu unaijuwa dini yangu moja kwa moja! so upendo nambie ushetani wa jina langu please. mimi pia naishi ulaya kwahiyo siamini maneno yako.

  47. Comment by maasai boy on July 31st, 2008 10:00 am

    zaina na upendo hamjiheshimu!!!!!!!!!!upumbavu wenu mnauweka hadharani!!!!!!!!!!!!!!that s stupid!!!!!!!!!!!!!!

  48. Comment by zaina seif on August 5th, 2008 2:40 pm

    Oh realy!!!!!!!!!!!!!
    pole we!!!! hahaha, utajiju! ilimradi ujumbe umemfikia muhusika yatosha! uite utakavyo, stupid, sijiheshimu, kikubwa nimesema yaliyo moyoni mwangu! kama kimekuuma saga chupa umeze! au sio?

  49. Comment by Mr. Upendo Furaha Amani on August 5th, 2008 6:02 pm

    Zaina Seif = Yezebeli

  50. Comment by zaina seif on August 14th, 2008 12:51 pm

    Zaina Seif=Yezebeli manayake nini ?!!!!!!!!!
    ha ha ha, upendo pole wee. hahaa unafurahisha sana.
    Yezebeli kama ni tusi unajuwa linarudi kwa nani?

  51. Comment by audace on August 25th, 2008 10:48 am

    i do like how Mr nice sayes
    i be happy 4that

  52. Comment by chapombe on November 26th, 2008 10:13 am

    huyu mr nzuri kwanza mi alikuwa ananikera kuwaibia nyimbo zao watoto wetu chekechea na kuziimba yeye.sijui watoto wetu wangeimba nini tena

  53. Comment by sabiti sefu on February 21st, 2009 3:22 pm

    nina shida za nyimbo za mr nice, muni tumie ata kwa email ya ngu mimi ni mwana inchi ya kongo DRC ni kosasa kinshasa nilikuwa mbele KALEMIE sa sa nini KINSHASA ku nanyimbo tu ya luga ya ngine sa maani munitumie

  54. Comment by HEZZY OMARE MICMASTA on February 25th, 2009 11:51 am

    vipi mwana wa kwetu bwana toka hapa kenya tunakutakia mazuri kila siku usife moyo bratha you can do it once again lakini labda uachane na mambo yaliyo kuangusha instead ya kusingizia maadui tu japo na kwaba chuki binafsi ipo.all tha best.mie ni radio presenter si ulete hiyo ngoma yako mpya Nairobi kwa mafans tuku promote nangoja kusikia.

  55. Comment by big Denny on February 28th, 2009 10:58 am

    vingi vitapotea lakini kipaji chako kitasimama,dont give up keep doing ya things,there is a thin line between rich and poor,bg denny

  56. Comment by NASSORO BELLEKO on October 9th, 2009 8:03 am

    KAKA UMECHOKA.

  57. Comment by JOHN SONGAY on March 6th, 2010 11:30 am

    big up mr nice, tunasumbiri hiyo mpya tunasubiri hiyo albam mpya

  58. Comment by zabibu suzana on March 11th, 2010 3:25 pm

    jambo mr nice

Leave a Reply