MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

Kama binadamu anaweza kufikia kupewa heshima ya kuwa “taasisi”(institution) katika jambo fulani basi Bi.Kidude anaweza kuwa mmojawapo. Ukiiweka mezani historia ya muziki wa taarabu na tamaduni za unyago visiwani Zanzibar ni wazi kwamba katika meza hiyo pembeni yake ni lazima aketi Bi.Kidude. Uzoefu na uelewa alionao katika idara hiyo hauna mpinzani. Inaaminika kwamba ndiye mwanamke,mwimbaji mkongwe kupita wote Afrika Mashariki na Kati.

Picha hii ni kwa hisani ya Marcel Mutsaers aliyompiga Bi.Kidude wakati wa Tamasha lijulikanalo kama Festival Mundial kule Tilburg-Uholanzi mwezi June mwaka 2006.

Umri wake halisi haujulikani. Kinachojulikana ni kwamba ana umri zaidi ya miaka 90 na hivi sasa sio ajabu akawa ameshafikisha umri wa miaka 100! Amekuwa muimbaji tangu miaka ya 1920 akiwa ni mfuasi wa Sitti Bin Saad mmojawapo wa waimbaji wa mwanzo kabisa wa taarabu visiwani Zanzibar.

Hivi leo anatambulika na kuheshimika kama malikia wa taarabu na mambo ya unyago asiye na mpinzani. Alizaliwa katika kijiji cha Mfagimaringo katika familia ya watoto saba. Jina alilopewa na wazazi wake alipozaliwa ni Fatuma Binti Baraka kabla jina maarufu la Bi.Kidude halijashika baadaye alipoanza kuwa maarufu katika uimbaji.Wazazi wake walikuwa ni wafanyabiashara ya kuuza nazi enzi hizo za Zanzibar iliyokuwa chini ya utawala wa wakoloni.

Katika mahojiano mbalimbali aliyofanya na vyombo tofauti tofauti vya habari ulimwenguni Bi.Kidude anasema alianza kuimba akiwa na umri mdogo wa miaka 10. Anasema uimbaji alijifunza kutoka kwa Sitti binti Saad tena kwa kujificha nje ya nyumba na kumsikiliza Sitti binti Saad akiwaimbia wageni ambao mara nyingi walikuwa wakipelekwa pale na yeye Bi.Kidude.

Akiwa na umri wa miaka 13 tu hakuwa na jinsi bali kukimbilia Tanzania bara(Tanganyika enzi hizo) ili kuepuka kuozeshwa kwa nguvu. Akiwa Tanzania bara alizunguka kila kona ya nchi akiwa muimbaji katika makundi mbalimbali ya muziki wa taarabu likiwemo lile maarufu la Egyptian Musical Taarab. Baadaye alihamia nchini Misri kwa kifupi kabla hajarejea kisiwani Zanzibar mahali ambapo anaishi mpaka hivi leo.

Mbali na uimbaji Bi.Kidude pia ni mfanyabiashara.Anauza “wanja” na “hina” ambazo anazitengeneza mwenyewe. Pia ni mtaalamu wa dawa za mitishamba lakini zaidi ya yote yeye ni Mwalimu wa “unyago” ambapo anacho chuo chake mwenyewe huku akijivunia rekodi kwamba katika wanafunzi wake wote hakuna ambaye ameshawahi kupewa talaka na mumewe. Pengine hii ndio sababu mwaka 2004 ulipozuka umbea kwamba Bi.Kidude amefariki dunia wakati alipokuwa katika ziara ndefu ya kimuziki Ulaya na Mashariki ya mbali, kila mtu kisiwani Zanzibar alishikwa na butwaa na majonzi! Kwa bahati nzuri habari za “kifo” chake zilikuwa ni uzushi tu.

Picha kwa niaba ya Issa Michuzi.

Mwaka 2005 huko Gateshead, Newcastle nchini Uingereza,Bi.Kidude alipokea tuzo yenye heshima kutoka World Music Expo (WOMEX) kwa mchango wake katika muziki na utamaduni wa Zanzibar. Katika kinyang’anyiro hicho aliwashinda wanamuziki mahiri kama Peter Gabriel, Miriam Makeba na wengineo. Bi.Kidude anasema hawezi kuacha kuimba mpaka siku atakapoiaga dunia kwani akiimba anajihisi kuwa binti wa miaka 14!

Mwaka jana, kampuni ya nchini Uingereza iitwayo ScreenStation kwa kushirikiana na Busara Promotions walitoa documentary iitwayo “As Old As My Tongue-The Myth and Life of Bi.Kidude” inayoelezea historia nzima ya maisha yake. Unaweza kuona dakika kama saba hivi za documentary hiyo hapa chini.Anasema yeye anakunywa na pia anavuta,lakini zaidi ya yote anaweza kuimba bila hata kutumia spika ya mdomo yaani microphone.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video


Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

25 Responses to ““SIWEZI KUACHA KUIMBA”-BI. KIDUDE”

  1. Comment by Mkongwe on August 10th, 2007 5:35 pm

    This is wonderful! Bongo celebrity naona mnajua kazi yenu. Je Bi. Kidude amekwisha andika kijitabu juu ya mambo ya unyago? Anaye msaidizi/wasaidizi watakaoendeleza chuo chake atakapokuwa hayupo? Wengi wetu tungependa kujua siri kubwa ya kutunza ndoa kwani duniani maisha wawili wawili***

  2. Comment by Lizzie on August 11th, 2007 3:13 pm

    Respect bibi kidude tunakupenda

  3. Comment by Kidds on August 13th, 2007 4:08 am

    Big up Kidude, I salute you and you will leave to be remembered for a very very very long time.

  4. Comment by kazuba on August 19th, 2007 1:27 pm

    mambo ya bi kidude

  5. Comment by ChrisK on August 20th, 2007 10:28 pm

    Bi Kidude is legendary!
    long live Bi Kidude! Hata watanzania wa usukumani imebidi tuseme shikamoo bila a kuelewa kila anachosema! Furaha ya wzanzibari kumwelewa inafurahisha peke yake..

  6. Comment by Bob Sankofa on August 24th, 2007 4:10 am

    Niliona performance yake live kwa mara ya kwanza pale Ngurudoto Lodge, Arusha mwaka huu mwezi wa sita. Bibi tunaambiwa ana miaka 95 lakini bado yuko na nguvu kwelikweli. Niliweka picha na habari kidogo ya onesho lile bonyeza http://mwenyemacho.wordpress.com/?s=Bi+Kidude+Noma ucheki balaa alilofanya. Nashukuru Bongo Celebrity kwa kutambua mchango wa bibi yetu hasa katikak ulimwengu wa muziki wa pwani

  7. Comment by Farida on August 24th, 2007 9:03 am

    Bi Kidude unatisha kaza uzi uendelee kuwafunika vijana.Jamani tumuenzi mzee wetu.

  8. Comment by BIG J on September 2nd, 2007 7:07 pm

    SHE IS THE FIRST EVER PERSON TO RAP IN SWAHILI….NO ONE IN THE WORLD CAN QUESTION ABOUT THAT….I’VE READ ABOUT HER ON DAILY MAIL AND THE GUARDIAN HERE IN LONDON….I’LL LOVE TO SEE HER LIVE PERFOMANCE….HOPEFULL NEXT YEAR WHEN I VISIT TZ

  9. Comment by miss pauline joseph on September 5th, 2007 3:51 am

    bibi sasa umechoka,kwanini usipumzike au unakimbia kulima?

  10. Comment by Freddy Macha on November 1st, 2007 10:15 pm

    Aliyesema kuwa sasa Bi yetu Mkubwa Kidude, fahari ya nchi yetu, kachoka; eti apumzike (“akakimbilie kulima”) hajui kuwa wasanii na wachapa kazi kwa jumla huwa hawapumziki? Hata wakishafariki, bado kazi zao huendelea kufurukuta, kugagata, kusereketa, kukarakata, kukata kata na kung’ata ng’ata.

  11. Comment by Mkereketwa on December 17th, 2007 4:14 pm

    I love bi kidude. Yaani inaonekana enzi za ujana wake alikuwa si mchezo huyu.

  12. Comment by extremschmuser on November 5th, 2008 8:35 am

    Thanks for the post,

  13. Comment by venus on March 5th, 2009 2:12 am

    Bi. Kidude keep it up!!!!

  14. Comment by MZANZIBARY on April 28th, 2009 2:36 am

    BIKIDUDE YOU ARE THE BEST. UNAIWAKILISHA ZANZIBAR KISAWA SAWA.UNAFUNDISHA JAMII MILA NA MAADILI. WAPE SHULE HAWA WASANII CHIPUKIZI WAO TARAAB ZAO NA MIPASHO YAO BASI HEBU WAAMBIE NINI HASWA TARAAB. HESHIMA YAKO BI KIDUDE!

  15. Comment by ABUUMACHINE on May 27th, 2009 11:59 am

    KAZA UZI

  16. Comment by sam samy on June 3rd, 2009 3:34 am

    imba dada kwa raha zako.

  17. Comment by vumbikali on July 13th, 2009 2:31 pm

    WEWE BIBI KIDUDE JIHESHIMU MWANAMKE WA KIISLAMU JISITIRI

  18. Comment by Ahmed Salim Ahmed on September 2nd, 2009 6:20 am

    Bibi rudi kwa mungu wako,kila jambo lina mwanzo na mwisho,waachie vijana tena,yako yamekuishia..kadri siku zinavyoenda unajitia aibu.

  19. Comment by Ahmed Salim Ahmed on September 2nd, 2009 6:22 am

    yawezekana ikawa mimi ni kitukuu chako au kilembwe chako,ushauri wangu kwako acha kuimba..ukitaka kunijua zaidi piga 0773101100

  20. Comment by babu peleka on September 10th, 2009 12:45 am

    inatosha tena Bi-kidude Rudi kwa mola wako tena wacha kunywa uzee ndo huo tena tena unajinasib unalewa unavuta!! kaburi linakusubiri

  21. Comment by eddy on October 4th, 2009 4:59 am

    waw,hii ni moja ya mifano bora kwa waafrika kuonyesha kama wanauwezo na wako imara kiafya,na kuimba kama bikidude na umri wake,alio nao na bado yuko jukwaani kuimba nyimbo nzuri,lakini nsio vyema kumuonyesha bibi huyo akijisifia kama yeye anakunywa naanvuta hiyo sio inspiration kwa new vizazi.

  22. Comment by salum on October 12th, 2009 8:43 am

    bi kidude usiache kuimba.ukitubu basi motoni ataingia nani? endelea bi kidude ili uwe wewe ndio moto hukoooooooooooo motoni.

  23. Comment by african prince on October 21st, 2009 11:51 am

    wish to see u…ma Lady..

  24. Comment by Mahmoud Shariff on November 30th, 2009 9:00 am

    Nimefurahi kuona mukimuenzi Bi.Kidude bado akiwa hai. Lakini nawaomba kwa hisani zenu jaribuni kumnasihi arudi kwa mola wake na aanze kutubia bado akiwa mzima mumkumbushe sisi sote ni wapita njia kwa mola tutaregea yahitajika tutubie. shukran

  25. Comment by jh on February 14th, 2010 6:44 pm

    ondoa kipengele cha kunywa na kulewa sijui kwanini editor alikiweka. Kwakweli unyago anaofundisha unasaidia sana kwa wake watarajiwa yaani nina rafiki yangu ambaye mkewe kafundwa na bi kidude saba tatu kila uifika kwake ni furaha tu. na kila nikimkuta anajifusi kuwa kwakweli kapata mke itabidi utaalamu anaoutumia atoe vitabu au aufundishe kwani ndoa za sikuhizi mh

Leave a Reply