
Kila anapofanya uzinduzi wa albamu zake huwa inakuwa ni mshikemshike,watu kibao. Uzinduzi wa albamu zake umekuwa ukitia fora sio tu kwa idadi kubwa ya wahudhuriaji bali maandalizi na onyesho lenyewe. Hii ni kutokana na idadi ya wapenzi wa muziki wa kizazi kipya aliojikusanyia. Akiwa peke yake au pamoja na kundi lake jipya la Wanaume Halisi, Nature anakubalika. Heshima aliyonayo kwa wakubwa na wadogo, mapenzi yake katika kushirikiana na wasanii wenzake ni vitu ambavyo vinamfanya azidi kukubalika na kupendwa. Mpaka hivi sasa ameshatoa albamu nne, ya tano anasema iko jikoni.
Hivi karibuni anatarajia kufunga pingu za maisha. Kabla ya kuelekea Shinyanga kwa “wakwe”, tulipata muda wa kufanya naye mahojiano. Kama msanii mwenye jina kubwa miongoni mwa wasanii wa kizazi kipya, alikuwa na mengi ya kutueleza. Pamoja na mengi Nature anaweka wazi ni kwanini katika siku za hivi karibuni miziki yake imekuwa na vionjo vya kwaito kutoka Sauz, anasemaje kuhusu uongozi wa JK? Je ana mpango wa kujiingiza kwenye siasa? Pesa na umaarufu umeathiri vipi maisha yake? Ana mipango gani siku za usoni zaidi ya kuanza kutengeneza familia yake mpya? Haya hapa mahojiano kamili;
BC: Jina lako linajulikana kila kona ya Tanzania, muziki wako unavuma pande zote za nchi na hata nje ya nchi.Pamoja na hayo wapo watu wasiojua ulizaliwa wapi, uliitwa nani ulipozaliwa,ulisomea shule gani nk. Unaweza kutupa hiyo historia kwa ufupi?
JN: Mimi nilizaliwa jijini Dar-es-salaam katika hospitali ya Ocean Road mwaka 1980. Jina langu halisi ni Juma Kassim Ally. Umri wa kuanza masomo ulipowadia nilijiunga na shule ya msingi Kurasini.
BC: Ulipokuwa mdogo ulitaka kuwa mwanamuziki au ulikuwa na ndoto za kuwa nani?
JN: Naweza kusema tangu nilipokuwa mdogo nilikuwa na ndoto ya kuwa mwanamuziki.Hii inatokana na mapenzi yangu katika muziki tangu utotoni.Kwa ujumla mambo ya muziki nimeanzia tangu utotoni,kisha shule ya msingi nk.
BC: Wazazi wengi wa kiafrika, mpaka siku za hivi karibuni tu, mtizamo wao ulikuwa kwamba muziki ni uhuni. Kwa upande wako wazazi wako walisemaje ulipokuwa unaanza mambo ya muziki?
JN: Kwa kweli mimi nashukuru mungu kwamba nilipata ushirikiano tokea kwa wazazi wangu tangia mwanzo. Lakini kama kawaida ya jamii zetu, sio kila mmoja alikubaliana na uamuzi wangu wa kujiingiza kwenye mambo ya muziki. Kwa maana hiyo utakuta kuna nyakati ambazo watu kama majirani kwa mfano wanaweza kuja na kuwaambia wazazi wangu mambo kama kwanini mwanao anafanya muziki, ni uhuni tu nk.Lakini nadhani hayo ni mambo ya kawaida katika tamaduni zetu za kiafrika.
BC: Tangu ulipoanza kufyatua albamu zako umekuwa unatoa albamu mpya kila baada ya mwaka mmoja au miwili; Nini Chanzo(2001), Ugali(2003), Ubinadamu Kazi(2005), na Historia(2006). Kwa kuzingatia mfululizo huo, tutegemee albamu mpya mwaka huu? Kama ndio lini?
JN: Ndio, kabla mwaka huu wa 2008 haujaisha au mapema mwakani natarajia kutoa albamu nyingine. Lakini hivi sasa kama kundi la Wanaume Halisi tunategemea kutoa single inayokwenda kwa jina la La Kuvunda.(halina ubani) ikiwa ni katika kuwasindikiza baadhi ya wasanii wa kundi letu kutoa albamu zao. Hawa ni Inspekta Haroun na Luteni Kalama kama Gangwe Mob,BK na Bob Q ambao ni ndugu na kundi moja na pia Dollo aliyeimba wimbo wa Radhia. Kwa maana hiyo tunatarajia kuwa na uzinduzi wa albamu tatu kwa mpigo kutoka kwa Wanaume Halisi hivi karibuni.
BC: Unaweza kututajia majina ya kundi hilo la Wanaume Halisi?
JN: Kwa ujumla kundi la Wanaume Halisi ni kama familia moja kubwa, kwa hiyo tuko wengi sana.Ila naweza kusema lead man ni Inspekta Haroun, mimi mwenyewe, Luteni Kalama, Dollo, Richie One, Bob Q, BK, D Chief,A Man, Kakaman, Maripo,Mzimu na Eddo.
BC: Umeshatoa zaidi ya albamu nne mpaka hivi sasa. Je kuna wimbo wowote katika albamu zako zote hizo ambao unapenda zaidi kuuperform? Kwanini? Kati ya hizo albamu zote ipo ambayo ni “kipenzi” chako zaidi?

JN: Nianze kwa kujibu swali la kipengele cha pili. Albamu ambayo ilikuwa ni kipenzi changu zaidi ni albamu yangu ya kwanza iliyokwenda kwa jina la “Nini Chanzo”. Niliipenda zaidi kwa sababu ilikuwa katika mahadhi ya hip hop zaidi ambako ndiko asili yangu.
Kwa upande wa kipengele cha kwanza cha swali; ni vigumu kusema kama nina wimbo mmoja maalumu ambao ninapenda zaidi kuuperform.Hii ni kwasababu nazingatia zaidi nyimbo ambazo mashabiki wangu wanazifeel zaidi.Kwa mfano kwa uzoefu wangu nyimbo kama “Mugambo” na “Hili Game” zimekuwa zikipokelewa zaidi na mashabiki hususani nikiziperform live.Ila kwa ujumla napenda kuperform nyimbo zangu zote.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
BC: Baada ya albamu nne kibindoni, ukiangalia nyuma unadhani ni wimbo gani uliokuwa mgumu zaidi kuuandika na kwanini?
JN: Nyimbo niliyoiona ngumu na ambayo ilinisumbua sana akili kuiandika ni “Nini Chanzo”. Katika nyimbo hii nilikuwa nazungumzia vitu vinavyosababisha migongano, ukosefu wa maelewano,vita nk katika jamii au kwa maneno mengine nini chanzo.Kwa hiyo ili kupata uelewa zaidi wa nilichokuwa nataka kuandika ilinibidi niwaulize watu na pia kujadili nao kuhusu ‘nini chanzo’.
BC: Maonyesho ya uzinduzi wa albamu zako umekuwa ukitia fora kila mara kwa idadi ya wahudhuriaji. Hii inaonyesha kwamba sio tu unapendwa bali unao mashabiki wengi kupita kiasi. Je imeshawahi kutokea mshabiki wako akakupa zawadi yoyote binafsi? Kama ndio ilikuwaje na ilikuwa ni zawadi gani?
JN: Kwa kumbukumbu zangu ni watu wengi sana wameshanipa zawadi (ahsanteni) na hivyo sio rahisi kumtaja mtu mmoja mmoja. Hii ni kwa sababu nimezunguka nchi nzima na nimefanikiwa kujipatia mashabiki kila kona.Lakini zawadi ambayo naikumbuka sana ni zawadi ya saa niliyopewa na Chameleon. Bila hata kunifahamu vizuri, Chameleon aliniletea zawadi hiyo kutokana na jinsi alivyokuwa anaufeel muziki wangu ambao alikuwa anausikia na pia kuwasikia watu mbalimbali wakiusikiliza hata alipokuwa kwenye matamasha yake huko Marekani na kwingineko.
BC: Baada ya kufanya kazi na P-Funk aka Majani (produza na mmiliki wa Bongo Records) kwa muda mrefu namna hii, unamuongelea vipi P-Funk?
JN: P-Funk is a good boy. Mshikaji kwanza ana upendo na watu na anaelewa nini maana ya maisha na jinsi ya kuishi na watu. Pili anafanya kazi nzuri inayoaminika halafu yuko serious na kazi. Anajitahidi kuupangilia muda wake binafsi vizuri na pia muda wa studio. Nadhani kwa kuzingatia utendaji wake wa kazi ndio maana kazi zake zinakubalika.Kwa ujumla ni mtu mzuri.
BC: Baada ya kuvunjika kwa kundi la Wanaume, hivi sasa unatamba na kundi lako jipya la Wanaume Halisi. Kabla ya hapo uliwahi pia kuwa solo artist. Unaweza kutuambia nini tofauti na ugumu wa kuwa solo artist ukilinganisha na kuwa kwenye kundi?
JN: Kila kitu kina faida na hasara zake.Tofauti ya kuwa solo artist na kuwa kwenye kundi ni kwamba ukiwa kwenye kundi utajua mengi zaidi. Kwa maana hiyo utaweza kutunga vitu vingi zaidi na wakati huo huo kujifunza mengi zaidi. Hii inatokana na ukweli kwamba binadamu tuko tofauti kwa hiyo mnapojumuika,mkiwa wengi, kuna mengi yanazungumzwa yakiwemo mafanikio na matatizo.Inakuwa sio lazima utembee ukayasikilize bali unaweza kuyapata yanayoendelea huko mitaani hata ukiwa nyumbani kwako. Huo ni upande wa faida.
Ingawa kuna hasara za kuwa kwenye kikundi mimi binafsi sijaangalia sana upande huo kwa sababu kama ni hasara zipo au ipo tu.Kikubwa mimi ninachoangalia ni jumuiya na jinsi tunavyoweza kusaidiana kama vijana tunaoishi katika dunia moja,nchi moja kama yetu ya Tanzania. Hii nadhani inatusaidia kujuana zaidi na kusaidia wengi zaidi kwani muziki unasababisha uwe na marafiki wengi toka nchi mbalimbali jambo ambalo ni zuri katika maisha.
BC: Style ya baadhi ya nyimbo zako zimejaa vionjo vya kwaito (aina ya muziki kutoka Afrika Kusini). Nini kilikushawishi kuingiza vionjo kama hivyo? Je huoni kama huko ni kuukuza muziki wa wenzetu zaidi?
JN: Kwanza kabisa mimi ni mfuatiliaji sana wa mambo ya vyama vyama au siasa na kwamba sisi kama waafrika ni kitu kimoja au wamoja.Kwa hiyo kwanza dhana hiyo ya umoja ndio ilinivutia. Pili nilizingatia uhusiano wa muda mrefu ambao nchi yetu ya Tanzania imekuwa nao na Afrika Kusini. Kama utakumbuka msaada ambao Tanzania iliutoa kwa Afrika Kusini wakati wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi na pia jinsi ambavyo Hayati Baba wa Taifa letu,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na raisi mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela walivyokuwa marafiki na mambo kama hayo.
Sasa kwa kuzingatia yote hayo na ukweli kwamba Afrika Kusini ndio pengine nchi ya Afrika inayojulikana zaidi ulimwenguni, nikaona hakuna ubaya kama mimi pia nitatumia baadhi ya vionjo kutoka Afrika Kusini katika muziki wangu.Dhumuni ni kuukuza uafrika zaidi na kuendeleza dhana ya umoja kupitia muziki ili watu wa mabara mengine au mataifa mengine watuheshimu zaidi kwa kutizama umoja wetu na sio kutuona kama manyani tu.

Juma Nature na Wanaume Halisi wakiwa jukwaani!
BC: Katika wimbo wako wa CCM na CUF uliongelea masuala muhimu ya kisiasa na mustakabali wa nchi. Siasa za nchi ni jambo unalolifuatilia kwa karibu?
JN: Ndio siasa ni kitu ninachokifuatilia kwa karibu nikizingatia huko tunakoelekea.Isitoshe hivi sasa sisi tushakuwa watu wazima.Tumeshaanza kuwa na familia zetu. Kwa maana hiyo ni lazima tuangalie tunapoelekea na jinsi gani tutautumia huu utu uzima wetu katika maisha yetu ya kila siku.
Kwa hiyo unakuta nafuatilia mambo ya siasa sio kama mwanasiasa bali kama raia mwema. Kama raia unatakiwa uzijue haki zako na ukitaka kuzijua haki zako ni muhimu ujue na kufuatilia mambo ya siasa.
BC: Je una mpango wa kugombea nafasi yoyote ya kisiasa huko mbeleni?
JN: Aah hapana, kwa kweli mpango huo mimi sina na wala sitaki kabisa uongozi wa kugombea. Uongozi ninaoutaka mimi labda ni ule wa kuchaguliwa tu na wananchi bila ya mimi kugombania.
BC: Unazungumziaje uongozi wa raisi Kikwete? Unadhani anaelekea kuishinda vita ya umasikini, njaa, ujinga na maradhi?
JN: Uongozi wa raisi Kikwete kwa kweli unatia moyo kidogo. Kwa kweli kuna mabadiliko mengi sana yametokea hivi sasa nchini Tanzania. Raisi anajitahidi sana hata kimawazo tu na anajali raia wake kwa kadri anavyoweza. Sema kuna raia wachache ambao hawaangalii kwa mbali na hivyo wanataka matokeo ya mara moja.Kwa kweli raisi tunaye, anapenda watu na hana ubaguzi katika hilo.Anamfikiria kila mtu na anaangalia maslahi ya wananchi wake kwa pamoja.
BC: Umeshashirikiana na wasanii wengi hapa Afrika Mashariki. Je unaye msanii yeyote ambaye hujawahi kushirikiana naye na ambaye ungependa kushirikiana naye siku za mbeleni?
JN: Kwa hapa Afrika Mashariki, ningependa kushirikiana na vijana fulani hivi wanaitwa Mao Mao wanatoka Dandora Kenya. Sababu ni kwamba hawa ni watu wa kwanza ambao nilianza kujuana kwa upande wa wasanii wenzangu wa Afrika. Nilipoanza muziki mojawapo ya ndoto zangu ilikuwa ni kukutana na wasanii mbalimbali wa Afrika ikiwemo nchi jirani ya Kenya kwa sababu kwa maoni yangu, tuko nao karibu zaidi kiusanii na ndio maana tunashirikiana zaidi katika mambo mengine kama siasa nk.
Pili ningependa kushirikiana na wasanii hawa kwa sababu muziki wanaujua, wapo real na hata ukiwasikiliza nyimbo zao na style zao wanajitahidi sana.Wanaimba muziki ambao ni real kwa kweli.
BC: Mwanamuziki anapoamua kutoa albamu huwa ana matumaini makubwa kwamba itakuwa ni nzuri, itawaburidisha wapenzi wa muziki na mashabiki wake na pia itauza vizuri. Je huwa unakuwa na wasiwasi wowote kwamba itakuwa vipi albamu isipouza na mambo kama hayo?
JN: Ni kweli ninapotoa albamu ndoto matumaini huwa ni kama hayo uliyoyataja. Wasiwasi wa kutokuuza huwa sina kwa sababu mimi sitoi albamu kwa nia ya kutafuta ujiko tu.Kwa maana hiyo kabla sijaamua kutoa albamu huwa nakuwa nimeshajifunza na kuangalia mambo mengi sana kama vile nini nizungumzie ambacho watu wanakipenda na wataendelea kukipenda kwa muda mrefu. Kwa hiyo huwa natunga nyimbo ambazo nina uhakika zitapendwa kwa muda mrefu ili hata siku moja nitakapofariki nyimbo zangu ziendelee kupigwa na kuchezwa.
BC: Pamoja na kwamba jibu la kawaida kutoka kwa wasanii wengi ni kwamba umaarufu na pesa havijawabadilisha, ukweli ni kwamba kwa vyovyote vile vitu hivyo viwili vinambadilisha mtu tukianzia na hata jambo la kawaida tu kama ratiba ya kila siku. Kwa upande wako pesa na umaarufu vimekubadilisha namna gani?
JN: Kusema ukweli, mimi naweza kusema kwamba Nature nimekuwa ni yule yule na niko vile vile. Nature ni yule yule kama alivyokuwa zamani. Labda naweza kusema mabadiliko yako kwa nje zaidi ya ndani.Kwa nje watu wengi wanaweza kusema nimebadilika labda kwa sababu nimenunua gari, nina vijisenti kidogo nk.Lakini mimi kama binadamu naona vitu kama hivyo sio vigezo vya kusema mtu amebadilika kwa sababu kama magari kwa mfano yapo,yalikuwepo na yataendelea kuwepo hivyo ni mambo ya kawaida.

BC: Kilio kikubwa cha wasanii wa Tanzania kimekuwa jinsi “wadosi” wanavyowaminya katika suala zima la malipo ya kazi zao. Pia kumekuwepo na wizi mkubwa wa kazi za wasanii bila hata woga.Unapambana vipi na wezi wa kazi zako kama msanii? Unadhani ni jukumu la nani kulinda kazi za wasanii?
JN: Mimi nafikiri jukumu zima ni la serikali. Huwezi huwezi kufanya kitu bila kupitia serikalini. Vyombo kama vile radio,TV,magazeti na vitu vingine vinavyohusiana na maendeleo ya muziki kwa mfano vyote vinapitishwa na serikali. Kwa maana hiyo nadhani vijana wengi watafanikiwa endapo serikali itatilia mkazo wa nguvu kuhakikisha kazi za wasanii haziibiwi.
Mimi kama mimi kwa kweli sijaweza kuzuia kazi zangu kuibiwa kwa sababu zinauzwa sehemu nyingi sana. Mimi mwenye nimeshawahi kushuhudia na zamani nilivyokuwa na akili za kitoto nimeshafikia hatua ya kumkunja mtu kutokana na mambo haya. Kwa hiyo naamini kama serikali ikiamua kuwasaidia wasanii,kulifungulia macho suala hili itakuwa vizuri zaidi na wasanii tutaweza kufanya kazi nzuri zaidi kwa sababu ya kuongezeka kwa kipato.
BC: Na wadosi je? Kuhusu kudhibiti mapato?
JN: Suala la wadosi kwa kweli mimi sipendi sana kulizungumzia kwa sababu wasanii wote wanaanzia sanaa yao kupitia kwa wadosi. Kama mdosi atakwambia hapendi kazi yako basi kuiuza itakuwa ngumu sana. Hii inatokana na ukweli kwamba wao ndio wenye vitendea kazi vya doubling nk. Kama serikali ingenunua kwa mfano machine kama hizo ingesaidia sana.Ila kwa hivi sasa wadosi hawana competition. Ingekuwa vizuri sana kama washika dau wengine wangejitokeza na kuwekeza ili pawe na competition ili kuboresha zaidi kazi za wasanii na mambo kama hayo.Tunachotaka sisi ni maendeleo na kuitangaza nchi yetu kupitia kazi yetu ya muziki.
BC: Jambo moja ambalo Tanzania haijaweza kufikia ni kuwa na muziki ambao ukipigwa tu mtu anaweza kuutambua kama “muziki wa kitanzania au kutoka Tanzania”.Unadhani hilo linatokana na nini? Nini kifanyike?
JN: Naweza kusema kwamba hawa waandaaji wa muziki, Djs nk ndio wanaokosea sana.Kwenye programs zao wanaigana sana. Ingekuwa vizuri sana kama wangeangalia na kudumisha nyimbo za asili yetu kama mdundiko na nyinginezo.Mimi naamini hii ni miziki mizuri tu. Kwa bahati mbaya DJs na waandaaji wa vipindi hawazipigi kabisa aina hizo za muziki na kama wakizipiga zinapewa muda kidogo sana ukilinganisha na zile za nje. Kama nyimbo zenye mahadhi ya kikwetu ingekuwa inapewa muda zaidi radioni na kwenye luninga, kuandaliwa matamasha nk hiyo ingewavuta hata wasanii kuanza kuzitunga nyimbo zenye mahadhi hayo zaidi.Vinginevyo itakuwa vigumu sana kupata muziki ulio kitambulisho chetu kwa sababu nyimbo zinazopigwa zaidi ni kutoka Ulaya na Marekani.Inakuwa kama hatuupi kipaumbele muziki wa kwetu.
BC: Mojawapo ya tatizo kubwa la kijamii linaloikabili Tanzania ya leo ni ukosefu wa ajira kwa vijana. Unadhani nini chanzo na nini kifanyike kubadilisha hali hiyo? Nani wa kulaumiwa katika hili?
JN: Hapo kikubwa ni sisi wananchi wenyewe. Hatuwezi kuwalaumu wazee wetu moja kwa moja. Hatuna umoja, makundi kila siku yanagawanyika. Mimi naamini kama tukishirikiana basi ajira zitapatikana na kitakachopatikana mnagawana.
BC: Zaidi ya muziki huwa unapendelea kufanya nini? Zipi ni hobby zako?
JN: Mimi napenda sana kuelimisha jamii, kukaa na watu na kuelimishana nao.
Na anapenda sana kuchezea computer. Na sasa hivi nina mpango wa kuanzisha studio yangu binafsi ambyo itabeba jina la “Halisi record”
BC: Vipi mipango ya harusi, tunasikia unaoa hivi karibuni?
JN:Mipango inakwenda fresh kabisa. Natarajia kumuoa mpenzi wangu Pili. Send off inatarajiwa kufanyika mkoani Shinyanga tarehe 10 August 2007 na harusi jijini Dar-es-salaam tarehe 18 August 2007.
BC: Kwa kumalizia una ujumbe wowote kwa mashabiki wako na wapenzi wa muziki kwa ujumla?
JN: Ujumbe ninaopenda kuutoa ni kwamba washabiki waaendelee kumuomba Mungu ili awazidishie siku za kuishi. Pia waishi kwa amani na upendo sio maisha ya kuuana na kuchinjana.Hayo mambo nayapinga vita sana. Tuishi kwa upendo,dunia nzima tuwe kitu kimoja mpaka mwisho.
Picha zote kwa niaba ya Ahmad Michuzi
Feedback / Comments
48 Responses to ““UMOJA NDIO SULUHISHO”-JUMA NATURE”
Leave a Reply


Wasanii wa Kitanzania wangekuwa na tabia nusu tu ya jinsi alivyo Juma Nature – kuwa down to earth, calm and collected – muziki wetu ungekuwa mbali. Kwani pamoja na mafanikio ya kuwa mwanamuziki aliye juu kulko pengine mwanamuziki yeyote Bongo, lakini hana maringo, hana skendo na pamoja na kutengana na wenzie hajafanya matatizo dhidi ya kutengana kwao huko. Hongera Juma Nature kwa kuwa kama ulivyo
misupu hapo umeongea point Nature nimekutana nae Ukerewe first time ni mtu fit sana na muda wote anafikiria jinsi ya kujiendeleza.
Kwa kweli mimi kwa mtazamo wangu nature naona ni mtu mwenye akili sana na halafu sio mbinafsi nilimuona siku moja kwenye MTVBASE hapa uk akielezea maisha yake na mafanikio ya muziki ya livyobadilisha familia yake na yeye kweli nimefurahi sana yaani I will give him support 100% I wish u all the best lil brother
kusema kweli huyu kaka hakuna msanii yoyote hapa bongo wakumfananisha nae yaani yuko tofauti ingawa ana hela lakini ni wa kawaida kwa hali hii ni wasanii wachache sana wapo hivi. uko juu kakaaa
JN, kwa kweli interview yako inatupa moyo, kuwa kuna wasanii kama wewe mnajali wenzenu ambao bado wanaangaika kuwa on top kama ninyi. Ushikamano wako na kupenda kusaidia wenzako ni kitu muhimu sana kwa jamii. Tunakuombea mafanikio mema, na kama ulivyotaka fans zako tuwe na amani, na wewe ndugu yetu endelea hivyo hivyo na moyo wako. Utafika mbali sana. Big UP!!!
Hakuna cha zaidi ambacho hakijasemwa na wenzangu hapo juu, ninachoomba tu kwa nature na wasanii wa kizazi kipya hasa wale waandazi wa nyimbo (producers)wakusanye sampling za midundo na melody za makabila ya hapa Tanzania na afrika kwa ujumla na wazichanganye na samples zao za studio ili kuweza kupata mudundo (beats) fulani za kisasa lkn zikiwa na ladha ya kinyumbani ili kuongeza test katika local music industry kwa ujumla. kama kuna melody ambayo ninaipenda katika nyimbo za juma nature nadhani hakuna zaidi ya “KITU KIPYA”……huuu mwimbo una ladha ya kingoni but still ni mdundo wa kisasa, napenda tuanzie hapo.
hongera sana Nature wewe ni mfano kwa wasanii wa wabongo wanaopenda kila siku majigambo waelimishe tu hivyohivyo ipo siku watayakumbuka maneno yako na wewe utakuwa umefanikiwa saana tu,kila la heri kaka chapa kazi ndio silaha!!
Inapendeza si polepole kuona mtu maarufu kaa Nature apofagilia kupigiana mapande (umoja).Ukweli Nature amekuwa kivutio cha wengi alinimaliza kabisa alipoamua kwenda kugawa vitabu katika shule ya msingi alionyesha wazi kuwa anapenda mabadiliko kwa watu wote. Kaza uzi mzee uondelee kukonga nyoyo za wengi. Mungu ibariki afrika Mungu ibariki Tanzania.
Mi naula ugali http://www.mahusiano.com Nature ni noooma unatisha kamanda.
Kaza buti kamanda wangu. MC # 1 TZ
Fagilia, wawawaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Nakubali kabisa kuwa JN ni msanii halisi na natanguliza hongera nyingi kwa kazi kubwa anayoifanya. Hata hivyo ningeomba basi azidi kutuwakilisha waTanzania kwa dhati kwa kuvaa rangi za bendera yetu, hata kama ni katika sehemu ndogo tu ya vazi lake. Nimeona kofia yake ina rangi hizo lakini imezimwa sana na rangi nyekundu zilizozunguka kila mahali katika mavazi yake.
unakipaji mambo yako nimeyakubali kalini punguza bangi basi haikupendi kabisa!! sura imekukauka utafikiri hauli ukashiba zingatia mlo wanguvu unahitaji marutubisho unawiri kama kipaji chako kinavyonawiri. No hard feeling! One love!!! respect
Ebana kuhusu mshikaji!Me namkubali ile mbayaaa,tena ukiangalia kuhusu kufanya kazi na Inspetor alongside Luten Karama hapo ni funika bovu mtu wangu.All da best
huyu Kijana namkubali kwa kweli ,kwanza anasauti nzuri na ametulia.
lakini nashangaa mbona hatoi album., pia siku hizi matamasha yake sijayasikia tena
Ja nature why so cool?
Big Up BC
nakupa big up sana sir nature,, keep it up kza buti
daa mi sijui niseme nini kwani huyu mtu na mpenda tangu nipo mdogo sana na mpaka sasa,kwanza kabisa namfagilia,mstaarabu,tabia yake haibadiliki,big up man,by WISE BRO’S
nature nature nature!……hii ni msisitizo tuuu kuonyesha kwamba hata sijui nianze kukusifia vipi………ila wangu unatishaaaaaaaaaa!!!…..nilikuwa nasoma habari ya Masoud Kipanya hapa naomba kama stars wengine wabongo wawe kama nyie yaani vyichwa,pesa No Maringo……kina Kyline sijui Rc, East cost(kwa ufupi siwapendi)….pesa mbuzi maringo ya kufa mtu wazimu gani huo aaaaaaah punguzeni!
Nature nakufagilia nakufagilia nakufagilia!
Wanaumeeeeeeeeeeeeeee!
Wanaumeeeeeeeeeeeeeeee heeeeee heeeeeeeee heeeee ging ging ging Bomoa stage hahahaaaaaaaaaaaaaa
Juma wee acha tu. Wanangu wanavunja meza na vitanda kila siku kisa wanacheza kama wewe, yaani ni raha tupu. Mbaya zaidi niliitwa shuleni kwao kuhakikisha kuhusu baba yao ni nani maana madaftari yote yana majina yanayoishia na Juma Nature! Ilinibidi nikauke maana sikujua haya. Kucheki vumbani kwao nikakuta albamu na picha za JN kila kona nikaona hapa dawa ni kujiunga nao maana ilikuwa too late kuanza kuzuga.
Siku moja nitakuletea stageni uone mambo yalivyo!
Hongera sana kaka unafaa kuwa kioo cha jamii kutokana na utendaji na usanisi wako ktk kazi
WANAUME EEEEEEEE WANAUME EEEEEEEEEE ASANTE SANA
SORRY, UFANISI
baba unatisha.achana na hao watoto wa mama wa upanga album moja tu full maringo.kaza buti baba unafikra za kimaendeleo zaidiiiiii.
Aminiaaaaaaahh mchizi Nature…….xxxxxx
WATU WAZIMA TUPO. NA TUTAZIDI KUWEPO… NATURE JUS LIKE MIMI KAZI BUTI HAKUNA MARINGO..ILA TOFAUTI YETU NI KWAMBA MM TRUE HIP HOP,,, underground… NATURE LIL BIT BONGO FLAVA TOO MUCH but i lyke this dude… ALIANZA FRESH NA YUKO FRESH.. ILA NATURE GO BACK WHERE IT ALL STARTED….USIFATE HAO WASANII WENGINE TOTO ZA UPANGA.. wanaimba ngojera tu na mashairi yako nonsense..KEEP IT REAL .jn… XL GOTCHA BACK AAI… WANAUME.BABA..kamueni…
We ni mkali ile mbaya! nakubali kazi yako imetulia ile mbaya.
naomba nyimbo za bongo fleva pamoja na za r kely nazipenda sana sina mengi
Mi namkubali nature vibaya mnooo!!!Kwanza anajua kazi yake na anakipaji, mi nakumbuka toka tukiwa shule tunasoma na mjomba Dolo, alikuwa ni balaaa. Pia nakumbuka kwenye uzinduzi wa album ya nini chanzo,pale kilimanjaro pool side mwaka 200,ilikuwa ni noma.Keep it up Nature tupo pamoja katika gemu. Ushauri wangu kwa nature kuwa muziki ni kazi hivyo ajaribu kuvumbua vipaji vya vijana nao wapate kazi, hii itakuwa mchango wake kwa jamii ya watanzania,japo kuwa unajitahidi kupeperusha bendera yetu ya Tanzania kwenye medani ya muziki wa kizazi kipya.
kweli juma nature hafai kusogelea,ni moto wa kuotea mbali kwanza anajua nini muziki,na jinsi anavyouchukulia pia ni jambo lingine linalomfanya kuwa juu siku zote,wasanii wengi wanasema tu”mziki kazi” lakini ukiangalia kiundani huwa wanasema tu sababu wanaojua mziki ni nini wanasema, nafikiri juma sifa na pongezi za ukweli zina mfaa sana kwani hua anafanya kile tunachohitaji hasa sisi wapenzi na wadau wa huu muziki.Ril lyk ur thngs man
kiukweli hakuna bongofleva pasipo TMK,na hakuna TMK ya kweli pasipo wANAUME TMK haijalishi ni halisi AU family na makundi haya bila NATURE hayana uhalisia kwa kifupi mziki wa temeke bila NATURE ni sawa na ubwabwa wa pwani ukose NAZI.HUYU Jamaa ni noma!ndo msanii pekee bongo ambaye unweza ukasikiliza ngoma zake 5 za mahadhi tofauti halaf zote ni heat mfano:HILI GAME{HIPHOP},MUGAMBO{KWAITO},HALI NGUMU{TRADITION YA KIGOGO],MTOTO IDDI{REGGE} nk.further more mchizi ndo mkali wa chorus bongo,east africa,kusini na jangwa la sahara kama sio DUNIA nzima!THEN mbunifu sana wa kucheza,kuimba,misemo vi2 ambavyo vinamake dferenc nawegine.HAYYAH WALI NAZIIIIIIIIIIII,HAPA VUMBI TU!MAKILA KINGA FULENGWA….Dah!mchizi mkali sana ushauri wangu mchizi azidi kukomaa afanyemuzik wa ukweli ambao utamtoa kiduni mi naamini mchizi oneday atakua level za juu sanaaa na tuzo za CHANNEL O,MTV BASE zitarudi tena tena naINSHAALLAH tuzo za GRAMMY pia.BIG UP MKUBWA!
NAKUFILL SANA MWANA COZ UNAIWEKA JUU SANA TEMEKE YETU,LEO TEMEKE IMEKUA MAARUFU BONGO KULIKO WILAYA YEYOTE BONGO NA INAWEZEKANA NI MAARUFU ZAIDI HATA DAR ES SALAM! MZUKA SAAANA BIG UP MWANA KAZA NYUZI MKUU TUPO NYUMA YAKO MWANA WATOTO WOTE WA TMK :YOU WILL NEVER WALK ALONE: HAYYYA WALI NAZZZIIIIIIIIIII TENA NAZI NANE MCHELE KILO 1.
AIBU YAOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!
ebwana nature noma japokuwa uko kimya kwasasa nakukubali kwani najua game ndivyo lilivyo kaza buti wangu after that naomba niulize skendo la kubaka kwa nature its true or ?
Sina mengi ila hakuna msanii kama nature,kwa kilakitu.Nyimbo,sauti,porojo mdomoni vyote vyake.
ebana mengi yamezungumzwa lakini ukweli utabaki palepale
kwamba mwana wa tmk halisi yupo juu ile mbaya babuuu…..
napenda tumia fursa hii kusema juma nature anastahili vilivyo kuwa the best artist wa kiume afrika mashariki kwani anakubaliki zaid.big up juma kassim ally kiroboto,a.k.aqbra saluti mwana.i feel da song tatu bira ushind auji kimpopile pampapaaaaaa.
yap yap jamaa namkubali sana,si yeye tu bali nakubali hata kazi zake toka kitambo enzi ziile za kigeto geto lakini siku hizi za karibuni naanza kutomuhelewa na hizi skendo za kujihusisha kimapenzi na mabinti chini ya umri wa miaka 18 daah..namshauri tu akae nao mbali mabinti wadogo hasa watoto wa shule la sivyo watamuharibia mtu mangu..hi to Happy..
Nature huwa unafanya vizuri sana, ila siku hizi sikusikiiiiiiiiiii mchizi wangu. uko wapi? au mamaaa anukbana home hapo,uwe unamchunia bwana siku mojamoja uwe unafanya mambo mkubwa wangu wakazi
poa mzee wa nyumbani
mambo vipi mimi namkubali nature kwani anaimba full facts yani mambo ambayo yanatokea laivu na maisha halisi ya mtanzania
juma naturze katika hip hop kibongo bongo ni sawa na bob marley katika ulimwengu wa ragge
no body compare with him yupo juu ile mbaya.
mbali ya yote anacho hana nobody knows.
katika hilo atazidi kuwa juu mpaka apatikane mwenye tabia kama zake
Juma kasim kiroboto,tunakufagilia ila tunakupa live acha uchawi mkubwa mitishamba sio ishu ona saiz mambo yanavyokubadilikia umekaa kuigaiga nyimbo za kiafrika kusini.SIO ISHU///
Nature we ni mjanja mwana, achana na wanaokuzushia skendal, wanampango wa kukuchafua. *move on man* We ni mtanzania kiukweli huna mashauzi.
kinacho nifurahisha unapenda maendeleo ya vijana wenzako. Mfano halisi ni kuunda makundi yenye akili halafu hukati tamaa hata kama wasioona mbali kama kina chege kukusaliti.
KWELI UBINADAMU KAZI WAMESAHAU ULIKO WATOA wanafiki tu hao.
We ni mwana
BIG UP sana!!!!!!
dah!mimi cjui niseme nini ok!kwa kifupi nature me namkubali kinoma na kwa hapa bongo hakuna kama yeye….big up sir nature
HEHEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE,WALI NAZIM,FANYA DUDE MOJA NA SUMA G NA ISPEKTA,
swahibaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa,wepesi kerere wazito kujizungumzia,yao mfukoni ye2 mdomoni,masikini aishiwi ndoto wajuwa ilo0 kiloboto?
NATURE MM NAKUKUBALI KINYAMA M2 WNG COZ CO B’ TOOZZZ N’ THEN UKO SOCIAL KIGUMU.
NILIKUKUBALI KWNYE SHOW MOJA ULIYOIFANYA A’TWN COZ NAKUKUBALI NILIINGIA NA ULIFUNIKA ILE MBAYA,,
BIG UP SN MTT WA KIUMENI MWENZANGU
a.k.a KIBRAAAAA!!!!!
Noma sana m2 mzima weeee… nikama kimbunga unatisha
UKO JUU NATURE.
NATURE wewe nooooooma!!wanajua ubishi ligi tu!!
kaka we unatisha tena saaaaaana, mambo yao full mzuka, mwemwelemwemwelee nyingi bro upo juuu zaid huna mpizani.
mie kaka kwa kino,ilala nahata nyumbani tmk hawana ubishi heshima kwako kaka.
we mkaaaaaaaaaaaalii!