
Yawezekana umeshapata ujumbe uliosambazwa na Issa Michuzi mwenyewe au ule ambao Da’Chemi wa Swahili Times blog ameusambaza ikiwa ni tahadhari kuhusu e-mail ya kitapeli ambayo ilisambaa jana na bado inaendelea kusambaa hivi sasa ikidai Issa Michuzi amekwama hotelini huko nchini Nigeria na hivyo anaomba msaada wa kifedha.
Tungeweza kuipuuzia tu e-mail kama hiyo.Tatizo ni kwamba sio tu ni ya kitapeli,bali hivi sasa imemfanya Issa Michuzi ashindwe hata ku-update blog yake maarufu. Kimsingi e-mail ya issamichuzi at gmail ambayo ndio aliyokuwa akiitumia kuingia ndani ya blog yake haipo mikononi mwake tena! Ndio maana kama mnavyoweza kuona ukiitembelea blog yake tangu jana hajaweza kuweka picha mpya,jambo ambalo sio kawaida yake kabisa.
BongoCelebrity imewasiliana na Michuzi na kufanya naye mahojiano yafuatayo. Yasome na kisha mkumbushe na mwenzio kuhusu kwamba aipuuzie tu e-mail kama hiyo. Hapa Michuzi anaelezea nini kilitokea,lini ataweza tena kuendelea ku-update blog yake(archives zote bado zipo na zinapatikana online),vipi unaweza kuepuka yasikukute yaliyomkuta na anapatikana kwa njia gani hivi sasa? Majibu haya hapa chini;
BC:Nini hasa kimetokea? Ilikuwaje?
MICHUZI: Jana mnamo saa tatu na robo usiku nilifungua mtandao nyumbani na kupost picha kama nane hivi, ikiwa ni pamoja na za Rais mstaafu wa Marekani Bill Clinton na kumalizia na ya mafuvu ya wahanga wa mauaji ya kimbari kule Rwanda ambayo kuna mdau alinitumia. Kisha kama kawaida nikaingia kwenye issamichuzi at gmail.com ili kupitia maoni kama kawaida kwani issamichuzi.blogspot.com nimeitegesha kwamba maoni hayaendi moja kwa moja bali yanapita kwanza kwenye email yangu ndipo kama naona yanafaa nayaruhusu na kama hayafai nayazuia. Basi bwana, kwenye saa tano kasorobo hivi, ukaingia ujumbe ukidai unatoka kwa ‘Gmail Team’ unaofanya censor kutokana na malalamiko kwamba gmail siku hizi bomu kwa kuwa watu wamekuwa wengi, hivyo ujumbe ukanieleza jaza details zako ndani ya siku saba kama hutaki account yako kufutwa toka gmail.
Siku ya kufa nyani miti yote huteleza. Na mimi ujumbe kama huo sio mara ya kwanza lakini wa safari hii, kama ningekuwa naamini juju-nangai ningesema jamaa wamepulizia maana nikajikuta najaza jina langu, umri na hata password na kusend. Huo ndio ukawa mwisho wa issamichuzi at gmail.com kwani nusu saa baadaye nikawa siwezi kuingia kwenye gmail tena.
BC:Uligundua vipi na saa ngapi kwamba e-mail yako imekuwa hacked?
MICHUZI: Niligundua niko hacked kwenye saa sita kasoro kumi wakati Da’Chemi aliponipigia kutoka Marekani na kuniuliza nimeenda lini Nigeria naye alipoondoka aliniacha Dar? Nikajua nimeshaumia baada ya kunieleza kwamba kuna mtu kaiba email yangu ya Gmail na anasambaza ujumbe wa kuomba msaada wa pesa kila mahali. Tukaingia kazini mimi na Chemi kuanza kuarifu watu wote tulioweza kuwafikia. Yeye kupitia blog yake ya Swahili Times nami kwa simu ya mkono na email yangu ya yahoo. Kwa kweli imenisaidia sana la sivyo saa hizi tungekuwa tunaongea mengine kwani wengi wangeamini ni mimi na kutaka kutuma pesa. Tena jamaa walivyokuwa hawana haya ati wamendikia hata mimi mwenyewe kupitia anuani yangu ya yahoo kuomba msaada wa pesa. Hahahaaaa!
BC: Umejifunza nini kutokana na tukio hili? Unawaambia nini wanablog wengine ili wajihadhari na tukio kama hili?
MICHUZI: Nimejifunza mengi sana, lakini kubwa na ambalo limenigusa sana moyoni ni kwamba wadau wananithamini na hakuna aliyesita kuniunga mkono na kuweka wazi kuwa tupo pamoja katika wakati huu mgumu.
La pili nililojifunza ni kwamba mtu usi-panic kwenye aina yoyote ya emergency, keep cool and ponder each and everything in its own perspective otherwise you will compromise your judgement the way your email address has. Usikurupuke.
Tatu na mwisho ni kuhakikisha una plan B katika kila ufanyacho kwenye maisha, hata kama yamekunyookea vipi. Kwa lugha nyingine hata kama blog itakufa leo (na haifi) nina plan B ambayo ni kubwa pengine kuliko blog.
BC: Unawaambia nini wadau wako.Lini site itarudi hewani?
MICHUZI: Asante kwa swali hili kwani wengi wametafsiri kwamba mtandao wa Michuzi ume-kuwa hacked na umekufa ama hauko hewani. Ukweli mtandao haujaguswa na wala hao jamaa hawajaingia huko. Wao wameingia kwenye email yangu ya Gmail na kuiba password kwa nia ya kutapeli watu. Uzuri wabongo sio mazezeta kama hawa jamaa wa ki-Nigeria wanavyodhani. Hivyo kukujibu lini narudi hewani ni kwamba kwa muda mfupi nitaacha ku-posti picha kwani ni hadi google watakaponipa password mpya pamoja ndipo nitaanza tena. Lakini kama unavyoona ukisearch issamichuzi.blogspot.com ama uki-google ‘michuzi’ unaipata blog yako kama kawaida kwani bado iko hewani.
BC: Unawaambia nini wadau,ndugu, jamaa na marafiki ambao walikuwa kwenye e-mail list yako? Wachukue tahadhari gani?
MICHUZI: nawaambia waachane kabisa kabisa na issamichuzi at gmail.com na watumie jina hilo hilo katika yahoo.com
BC: Wanaotaka kuwasiliana nawe hivi sasa watumie njia gani?
MICHUZI: issamichuzi at yahoo.com
Kama bado hujaisoma e-mail yenyewe ya kitapeli unaweza kuisoma pale Swahili Times.
Developing story…
Michuzi hivi sasa anapatikana katika www.isamichuzi.blogspot.com
Tofauti yake na ile blog ya zamani ni “s” iliyopo kwenye issa,badala ya s mbili weka moja.
Feedback / Comments
52 Responses to “TAHADHARI: MICHUZI YUPO DAR SIO NIGERIA!”
Leave a Reply


U can huck us but u can never stop us. Long live issamichuzi.blogspot.com
[...] kuwa yuko Nigeria. Amekwama hotelini. Anakuomba hela. Kisha atakurudishia baadaye. Ni uongo mtupu. Bonyeza hapa usome kisa chenyewe kwenye mahojiano yake na BongoCelebrity. Hongera BongoCelebrity kwa kudaka [...]
Kaka michuzi pole sana. hio kitu ulofanyiwa nashindwa niiteje lakini ingekuwa umefanyiwa ivo kwa simu ningeiita ni social engineering (uhandisi wa jamii!)Pole sana lakini ichukulie kama somo tu, next time kuwa street smart
Kaka Michuzi nimekumbuka hiyo kitu ulofanyiwa inaitwa
“Phishing” watu mnaofanya online banking na online finacial services kuweni macho pia.
Hii ni hatari aisee. Nimeishiwa na maneno yakusema, lakini nampongeza sana kaka Michuzi kwa kuwa na plan B kama alivyosema. Mie iliwahi kunitokea wakati fulani mwaka 2006, kuna jamaa yangu mkenya alinisaidia ndani ya nusu saa nikawa nimerejesha kila kitu kikawa sawa. Pengine ile kamati ya Ufundi ya JUMUWATA itatakiwa kuchukulia hili kama changamoto ya kwanza ya kuifanyia kazi ili kuona namna watatusaidia wanajumuiya tusijetukaathiriwa na hali hii zaidi.
BLOG MPYA IPO ISAMICHUZI.BLOGSPOT.COM NOTO NI ULE ULE MWENDO MDUNDO TU.
jaamaniiii pole sana kaka michuzi, tuko pamoja kaka najua utarudi kwa nguvu mpya na kuendeleza hili libeneke, moto ni ule ule.
Wadau kwa sasa mkuu michuzi anapatikana kupitia
http://www.isamichuzi.blogspot.com kumbuka ni single ‘S’ kwenye
issa na sio tena double ”S”.
[...] TAHADHARI: MICHUZI YUPO DAR SIO NIGERIA! [image] Yawezekana umeshapata ujumbe uliosambazwa na Issa Michuzi mwenyewe au ule […] [...]
Duh!Kaka Michu pole sana kwa yalokukuta but ndo mambo ya wanaijeria hayo ma’ke ni juzi tu umerusha ile walofanyia kazi jina la baba yetu wa taifa leo wamakushika wewe.Keep it up man dats a good lesson to you and to others
Kaka Issa Pole sana, amini tupo pamoja.Hawatuwezi!!!!
kaka jeff kweli nimeamini kuna watu balaa, yaani hata hawafai kiukweli.lakini hakuna mbaya one mistake on goal au sio, pia wanasema kama mlango wa kwanza umefungwa ujue kuna wa pili uko wazi kwa ajili yako wewe mkuu michuzi,so dont give up! Back never 4ward ever.Mkuu michuzi katika maisha hakuna mafanikio yasio na vikwazo.so Keep it up tuko pamoja daima
Mh!Kweli juzi jioni nilifungua blog yako issa(ile ya mwanzo)siukuona kipya.Nikahama.Nikafungua jikomoe.Nakashangaa kuona habari ile.Nilishtuka of course.Hii kitu sio kwamba nilikuwa sijaisikia(ya wizi wa mtandaoni).Nilikuwa nimeshaisikia na kunitokea kabisa!Tofauti kidogo na issa.Ilikuwa hivi.CONGRATULATIONS:YOU ARE EMAIL HAS WON THE UK NATIONAL LOTTERY.Baada ya kuipata mail hiyo.Nini kilifuata?Nilipaniki!Nikajaza fomu niliyoambiwa nijaze amabyo iliyoambatana na barua ile.Nikatuma.Nilipojibiwa nikaambiwa nitume pesa.Wakati nilishindia pesa!Kwa nini?Eti zilikuwa ni kwa ajili ya gharama za kunitumia zawadi yangu ya pesa.Unaona!Halafu sikutakiwa kutumia njia nyingine zaidi ya western union.Kwa vipi.Kwa kutengeneza mwenyewe barua za kubaki kwenye documents za bank kwani ninavyojua mimi hauwezi kutuma pesa nje bila kuwa na supporting document inayokutaka kutuma pesa.Hapo nilishuka!Kumbuka mawasilano yote yalifanyika kwa njia ya mtandao internate,bila hata kupigiana simu.Walitoa namba zao laikini ilikuwa kila nikipiga naambiwa nifanye mawasiliano kwa e-mali!Sikuchelewa kui-bush.Nikaiacha.
Hichi kilikuwa ni kisa ambacho kilinitokea live mwenyewe.So kwa hiyo skendo ya michuzi na kisa changu, ni suluhisho tosha kwa wabongo kuwa macho na matumizi ya mtandaoni.Huu ndio utandawazi.Kuwa makini katika maisha na kwa kila jambo ni muhumu sana kwa kila mtu.Hongera kwa uamuzi uliouchukuwa.
Pale sana kwa yaliyotokea.Tuko pamoja ndugu yangu issa.
Pole sana Issa ila ndo kujifunza maana wakati mwingine ni lazima kitokee kitu kama hiki ndo tunapata mwanga,but all good ni kwamba japo ulitegwa ulikuwa mwepesi kutegua mtego na ni kwa sababu muda wako mwingi unautumia kwenye mitandao otherwise usingegundua mapema.pole sana maana kama watu wangerespond mapema na kuanza kutuma pesa ingekuwa balaa mana matapeli wangefanikiwa.tunakuombea heri ila urudi tena utuletee mambo matamu. GOOD DAY BROTHER!!!!!!!!!
Pole sana KAKA Michuzi; I was suprise na kujiuuliza vipi umeishiwa??? ” kumbe sikujua kuwa ni matatizo; anyway bravo kwa kutupa mtandao mwingine chap chap?? sasa mzee nakubali uko JUU na hao jamaa hawakuwenzi hongera sana kaza buti: HAPO SAWA AU SI SAWA washirikaaa??; SAWAaaaaa!
pole sana my friend kwani mie nilikuwa nashangaa imekuaje jamaa jii… lakini mungu mkubwa.. tupo pamoja thanxxx
Pole kaka Issa,vyovyote itakavyokuwa ujue tuko na wewe tu.lister(Tokyo Japan)
Pole sana bro. tupo pamoja
sasa itakuwaje bwana Michuzi,maana mimi nilishakutumia pesa kidogo nikijua umekwama?!! Hahahaaa, ni utani tu. Pole sana Michuzi. Kisa kama hicho kilishatokea pia kwa Dr Mwambene wa Mbeya. Watu wengi tumejifunza kutokana na visa hivi. TUKO PAMOJA
Yaah life goes on brother! wazulu wanasema vuga maulele pindi uingiapo egoli,yaani fumbua macho kama umelala hapa ni egoli!wabongo tunasema changamka bongo hiyo!yaani hapo km umeshatapeliwaa.sasa michuzi ni hivi hawa jamaa wapo na ukitaka nikusaidie jinsi ya kuwapata ili tuwatokomezee tufanye mawasiliano yaani hawa jamaa wametapakaa dunia nzima ndiyo maana hata kupata visa ya america kwao ni ndoto.kwa hapa dar yaani kila siku nawaona shughuli zao wanazifanyia wapi.nami siwapendi kabisa ila nahofia usalama wangu nikiwachoma,je mtanisaidiaje kwa hilo?ili tuwaondoshe kabisa nchini kwani wataharibu hata vizazi vyetu kwa kuviambukiza utapeli.
Pole sana kaka yetu michuzi kwa yote yaliyokupata. Natumaini sasa hawatajaribu tena kufanya kitendo kama walivyofanya.
Nakupa pole sana tena sana.
Anna V. Mtui
Napenda kukupongeza kaka michuzi kwa kazi yako nzuri ya kutuhunganisha Dunia nzima nipo Lebanon lakini naona matukio ya kila siku Asante sana kwa hilo mungu hatakuzidishia zaidi na zaidi
Kaka michuzi hawo nimatapeli wa kimataifa nazani unawafahamu lakini sisi tunajua michuzi yupo Tanzania nje na hatakae aje
duh pole sana mara nyingi nikifika job tu hua nakucheki sasa leo nimeingia nakuta vitu ambavyo jana na juzi niliviona sikunoti kitu mpaka leo nilipofungua nikakuta yaleyale nikasema mh bro kapatwa na nini, nikaamua kufungua bongo celebrity ndo nakuta haya niliyoyasoma, du pole sana bro i wish u a gud fighting na i hope to see you soon, nakumiss sana kwasababu blog yako ki ukweli imenifanya nijue vitu vingi sana, big up pia kwa bongo celebrity.
Pole sana kaka Michuzi, naona wao wanajisumbua na mimi niko pamoja nawe na mungu atakujalia utarudi tena kwa kishindo.
kaka Michuzi,napenda kukupongeza kwa kutuletea mambo
bomba ya Kibongo na ya Mtoni,ningependeza utuletee na maswala yahusuyo mahusiano na mapenzi,ussusani kwa sisi tulio singo
Pole sana michuzi asante sana kwa ku tu update na mambo yanayoendelea hapa tz and around the world in particular.
poooooooole sana ka michuzi hiyo imetulia lakini inakuongezea umaarufu wanafikiri wanakukomesha kumbe wanajipotezea time.
kaza buti bro blog yako yenyewe iko juu sana. na tunaifeel sana watu wa Dom
BIG UP
Hi Mchuzi!1
Asante sana kwa habari unazotupatia.
POLE SANAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
pole kaka. tuliizoea blog. tunai-miss mno
ciao!
Pole kaka Michuzi, naamini utarudi tena kwenye blog ya jamii ambayo kwakweli ilikuwa inatuunganisha na pande zote za dunia. Utapeli wa namna hiyo upo na kwenye ATM mashine huko bongo, umeingia uhuni wa kuweka ndoano ndani ya mashine ambayo inanasa card halafu anajitokeza mtu anayejifanya msamaria anakuambia umpe password akusaidie kutoa. Baadaye anajifanya kashindwa, ukitoka tu anatoa ndoano na card, heee na pasword ndiyo hivyo umempa, anakomba michuzi yote kwa account yako. Unaijeria unatapakaa kila mahali sasa.
pole sana kaka michuzi,,no matter wat yameshindwa mafuso wataweza wao vibajaji,,na bado we stil represent….
POLE SANA MKUBWA,HAO NDIO BINADAMU USIJALI WE KAZA BUTI TU HUENDELEE KUTUPA MANEWS
Pole sana, Michuzi.Tekinolojia inavyokuwainavyobadilika kwa haraka watu wanaitumia kujinufaisha. Tuendelee kuwa na tahadhari, pia kuna ujanja mwingine ambao unaendelea, mtu anakudanganya kwamba anahela nyingi anataka kuzituma kwenye akaunti zako, ukiwapatia taarifa za akaunti yako, wanaanza kukuibia.
Nakupongeza kwa kuchukua hatua ya haraka kuwapigia simu na kutuma e-mail kutoa taarifa kwa jamaa, ndugu na marafiki.
2lia m2 wangu hayo yakaida cunajua wa2 wanataka kukuchafulia jina we endelea ku2pa manews
ISSA WATOTO WANATAFUTA JINA KUPITIA MIGONGO YA WATU BADO UJAWASOMA NA LINGINE NJAA JAMANI DUNIA HII WATU WANA ELA ZAO LAKINI HAWATAKI KUTOA HIVI HIVI NA NDIO MANA ISSA ANAJISHUGHULISHA ACHANA NAO WAMENOA KAKA POLE SANA KWA MKASA ULOKUKUTA KAKA(lilfue)
ACHANA NAO WAPUUZI HAO
Hollow Mr. Mchuzi, i have a plroblem that do face my baby, please i need some sharing of ideas on how to get a solution.
pole san m2 wangu,si unajua watu wapo kwa ajili ya kubomoa na si kujenga.katika hili tukio nakupa pole sana
kwahiyo inatuhusu nini !
wabongo nanyi mnaanza tafuta umaarufu kwa conspiracy… weldone pengine mtafika
See Africa, be in the Serengeti, climb mount Kilimanjaro, visit Tanzania
ndio maisha ya kuishi na wa2 usiopo vumilia huwezi kuishi ndugu tangu vumilia utashinda 2
n a mungu ham2pi mja wake utaendelea kubarikiwa
Mambokama michuzi
kweli unatisha ktk utendaji wako wa klazi nakuombe endelea vizuri na mungua yu pamoja nawe
kaza butiiiiiii
Kaka Michuzi binadamu ndivyo walivyo hawakosi cha kusema sema Inshaallah ili yako yakunyookee. Achana nao.
Issa, Naona Fakhari kukujua Tangia pale Dar YMCA tukiwa vijana sana. Nafurahi sana kusoma makala zako. Keep it up
Pole bro yote majaribu ,ukiona mafanikio mbele ujue na uzito unao.live while forecasting far.
POLE KWA YALIYOKUSIBU BOSS!, BOSS NIMEWEKA KAMBI DODOMA.BARIDI KALI.NAKUOMBEA KILA LA KHERI BOSS!
Don’t give up just keep it up brother!Chaos!
don”give up keep it up brother chaos
jamani inabid yahoo wawe macho kwa vile hata mimi imeshanitokea na kusababisha wazazi wangu kupata mashaka na ndugu. pole sana kaka ila tupe mawasiliano mengini hiyo waachie hao