MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

 

Ukiiona katuni yake gazetini, huhitaji kutambulishwa au kusaka sana jina la mchoraji hata pale anapokuwa hajaweka sahihi yake. Taswira yenyewe ya katuni itakueleza. Ni katuni ambayo imekuwa sehemu ya maisha ya watanzania kwa miaka mingi sasa. Wengi wetu tunamfahamu kama Masoud Kipanya. Lakini je hilo ni jina lake halisi? Alianza lini shughuli za uchoraji?

BongoCelebrity leo ina furaha kuwaleteeni mahojiano ya kina na Masoud Kipanya, maarufu pia kama KP, mchora katuni maarufu, mtangazaji wa CLOUDS FM na pia mbunifu mahiri wa mitindo (fashion designer). Katika mahojiano haya, pamoja na kuweka bayana maswali mawili yaliyoulizwa hapo juu, KP anaongelea zaidi maisha yake kama mchora katuni zikiwemo kasheshe alizowahi kukumbana nazo, mtizamo wake kuhusu jamii au nchi zinazoendelea kama yetu ya Tanzania, anatoa ushauri kwa wanaotaka kuwa wachoraji kama yeye na zaidi ya yote anao ujumbe maalumu kwa Watanzania kuhusu viwalo vya KP vitakavyokuwa sokoni hivi karibuni.Yafuatayo ni mahojiano yenyewe;

BC: Awali ya yote, hebu tueleze Kipanya ni jina lako halisi au ni jina la katuni wako? Na kama ni jina lako halisi kwanini uliamua kulitumia kwa ajili ya katuni wako maarufu kama KIPANYA?

KP: Jina langu halisi ni Ali Masoud, jina la Kipanya ni matokeo ya katuni ya Kipanya niliyoibuni karibu miaka 13 iliyopita.

BC: Kwa ufupi unaweza kutuambia ulianza lini na kivipi kuchora katuni au vikaragosi kama ambavyo wengine wanaziita?

KP: Mapenzi ya kuchora yalianza nilipokuwa darasa la pili, na nilianza kwa kuiga tu katuni za ndani na za nje kama ilivyo kawaida kwa yoyote anayeanza kufanya kitu, ila professionally nilianza rasmi mwaka 1988, huo ndio mwaka ambao katuni yangu ya kwanza ilitoka katika gazeti la Heko.

BC: Je unatoka katika familia ya wasanii au wachoraji? Unao ndugu zako ambao nao ni wachoraji?

KP: Hapana, bahati mbaya katika familia yetu hakukuwa na mchoraji kabla yangu, isipokuwa baada ya mimi kuna mdogo wangu ambaye tayari ameshaanza kuja juu katika fani ya katuni, ila baba na mama yangu ni watu ambao ingawa si wachoraji, lakini mfumo wa maisha yao inatosha kabisa kusema nao pia ni wasanii.

BC: Hivi sasa wewe unastahili kabisa kuitwa “professional cartoonist”. Unadhani lini hasa ulifikia kiwango hicho?

 

KP: Nadhani pale nilipoanza kuaminika na katuni zangu kuingia magazetini, naweza kusema mwanzoni mwa miaka ya tisini.

BC:Nini raha hasa ya kuwa mchora katuni?

KP:Raha ya kuwa mchora katuni, ama kuwa mchoraji kwa ujumla ni kwamba unaweza kufanya kile ambacho mpiga mpicha hawezi kufanya, yani unaweza kufanya mbingu ikawa ardhi na ardhi ikawa mbingu, unaweza kumfanya Bush ama Kikwete waonekane wana miguu kama spoku za baiskeli nk.

BC:Ni vikwazo gani unavyokumbana navyo kama mchora katuni? Na je huwa unavivuka namna gani?

KP:Kikwazo kikubwa kwangu ni censorship. Kwa wasioelewa, censorship ni ile hali ambayo unachora katuni halafu kabla haijachapishwa inapitiwa na kama itaonekana ina madhara kwa mtu ama jamii Fulani, basi itarekebishwa ama isichapishwe kabisa. Hayo yamenitokea mara nyingi tu katika maisha yangu nikiwa katika magazeti mbalimbali. Mara nyingi censorship hutokea pale inapoonekana unachora katuni zinazosumbua mioyo ya walengwa hususan wanasiasa wasiopenda kukosolewa.

BC: Katika maisha yako kama mchora katuni ni lazima umeshakumbana na mengi. Je kuna tukio lolote ambalo hutokaa ulisahau kamwe? Ilikuwaje?

KP: Matukio yako mengi, kwa uchache tu, nakumbuka siku niliyomchora mtu mnene akiwa amemshika kamba iliyomfunga mbwa ambaye ameandikwa ‘polisi’, maana ya katuni hii ukiangalia kwa haraka haraka ni kwamba jeshi la polisi haliko kwa manufaa ya umma bali kwa manufaa ya watu wachache hasa viongozi wa chama tawala.Hiki kilikuwa ni kile kipindi ambacho wapinzani walikuwa wakibughudhiwa na polisi kila walipotaka kufanya mikutano yao ya hadhara. La pili ni wakati ule mbunge mmoja aliyejulikana kwa jina la Tuntemeke Sanga alipokuwa anaumwa, nilichora katuni inayomuonyesha mheshimiwa Sanga akiwa amelazwa huku akiwa ametundikiwa damu, halafu pembeni yuko serikali akiwa amegeukia upande mwingine huku akivuta sigara kana kwamba hajali, bahati mbaya siku iliyofuata Mzee Sanga akafariki, naikumbuka siku hiyo vizuri, aliyekuwa katibu wa bunge wa wakati huo, Mzee Mlawa, alivamia ofisi za gazeti la majira, bahati nzuri, wakati anaingia mimi nikawa natoka, na pengine kutokana na umbo langu, hakuweza kudhani kwamba pengine huyu ndio masoud kipanya. Kilichoendelea kati yake na mhariri wangu kwa kweli sikukifahamu.

BC: Unaye mchora katuni yeyote ambaye alichangia uamuzi wako wa kuwa mchora katuni?


KP:
Kwa kweli kama msanii, naweza kusema wasanii wengi niliokuwa nikitazama kazi zao wakati ule walini-inspire niweze kupiga hatua.


BC: Maendeleo ya tekinolojia duniani yanabadilisha kila kitu kadri siku zinavyokwenda. Tofauti na hapo zamani ambapo wachoraji mlitumia zaidi kalamu na karatasi siku hizi mnatumia kompyuta nk.Wewe unatumia vifaa gani katika kufanikisha kazi zako?


KP:
Pamoja na kukua kwa teknolojia, bado kuchora kwa kutumia mkono, kalamu na karatasi ndio mtindo unaoendelea kutumika, kompyuta inatumika tu katika kuboresha kazi ya msanii.

BC: Mara nyingi wachora katuni wanakuwa na hadhira (audience) ya aina mbili, wanaochukia na wanaocheka wanapoiona na kuisoma katuni. Unaupenda zaidi upande upi?

KP: Kwangu pande zote ni muhimu na ninazipenda. Kwanini? Wote wananifanya niamini kuwa kazi inafanyika, ukichukia maana yake kazi inafanyika, ukifurahi pia maana yake kazi inafanyika.

BC: Nini maoni yako kuhusu tuhuma kwamba wachora katuni wengi, hususani wanaochora katuni za kisiasa (wewe unachora pia japo sio kila mara) huwa wanaegemea zaidi upande wa mabaya (negatives) zaidi ya mazuri(positives)?

KP: Bahati mbaya sana tunaishi katika mazingira ambayo mustakabali wa maisha yetu unategemea sana maamuzi ya wanasiasa tofauti na nchi kama Japan ambayo mwanasiasa ni mtunzi na msimamizi wa sera tu na mfanyabiashara na mkulima ndio wanaoweza kubashiri mustakabali wa nchi kutokana na trend ya kilimo na biashara kwa ujumla. Kwa nchi kama Tanzania, bahati mbaya, wengi wa hawa wanaopewa dhamana ya kuamua hatma ya maisha yetu wanachokifanya kwa kweli ni madudu tu, na ndio maana wakati wote tunalazimika kuwa negative kwao si kwa chuki bali kuwekana sawa ili na sisi tuweze kuishi kama wanavyoishi wenzetu katika maeneo mengine ya dunia. Sitaki kupoteza muda na nafasi ya safu hii kuanza kuorodhesha dhambi za baadhi ya watendaji wetu, kila mtanzania anafahamu.

BC: Mara kadhaa katuni zimesababisha sokomoko za aina yake kutokana na wengine kuhisi wamekashifiwa kutokana na mchoro wa katuni. Unawezaje kuhakikisha kwamba katuni zako hazisababishi sokomoko au mitafaruku ndani ya jamii?

KP: Sio siri, katika kuchora katuni, umakini wa hali ya juu unatakiwa. Na ili uweze kuwa makini basi ni lazima uwe na talent ya hali ya juu hasa katika upande wa uwezo wa kumchora mtu bila ya kumuandika jina lake mgongoni, na pia lazima uwe na analytical thinking ili uweze kuchambua kitu kwa uwezo bila ya kuonekana umemshambulia mtu. Haya ndiyo yanayoweza kukuokoa katika masokomoko na mitafaruku ya kashfa. Kwa miaka mingi nimekuwa nikiwachora viongozi vibaya lakini hakuna hata siku moja niliyompa mtu nafasi ya kunibana kisheria.

BC:Kwa vijana wadogo wanaotaka kuibuka siku moja na kuwa kama wewe au kufikia hapo ulipo unawapa ushauri gani na wanahitaji vifaa gani kuanza kuzijenga ndoto zao?


KP:
Kujua kuchora pekee hakutoshi kukufanya uwe mchoraji katuni mzuri. Lazima uwe mjuzi katika masuala ya general knowledge, ujuzi wa maarifa huzaliwi nao, unatokana na tabia ya kupenda kusoma na kujua kinachoendelea duniani. Kiu ya kutaka kujua zaidi na kutojifanya mjuaji ndio silaha za kukufikisha katika umahiri katika kuchora katuni.

BC: Pamoja na kuwa mchora katuni maarufu, wewe pia ni mbunifu wa nguo na mitindo (fashion designer) na pia mtangazaji wa Clouds FM. Nini au nani alikushawishi kuingia katika fani hizo?


KP:
Yawezekana dhiki na matatizo ndicho kichocheo cha kumfanya binadamu aweze ku-excel katika maisha, nami pia nataka kuamini kwamba matatizo ndio chanzo cha ubunifu katika kukabaliana na mitihani mbalimbali ya kimaisha, yawezekana ndo maana leo hii mimi ni mchoraji, mtangazaji na mbunifu wa mavazi, pamoja na utashi na upenzi katika fani hizo, bado kiu ya kuwa na financial independence ndio ndoto yangu.

BC: Kwa jinsi ulivyo na kazi lukuki ni wazi kwamba una ratiba ngumu ya kila siku. Unaweza kutuambia kwa kifupi ratiba yako katika siku ya kawaida? Yaani unaamka saa ngapi,unalala saa ngapi nk?

KP:Alarm inaniamsha saa 11 alfajiri, naoga, navaa na kuelekea studio. Naanza kipindi saa 12 mpaka 3 asubuhi, baada ya hapo napumzisha akili kwa kama nusu saa kwa kupitia magazeti mbalimbali then naanza kufikiria wazo la katuni, wakati mwingine kama sina wazo hunichukua mpaka nusu saa kudevelop wazo la katuni, by saa 4 asubuhi naanza kuchora editorial cartoon. Huwa natumia mpaka masaa mawili kutegemeana na aina ya katuni, baada ya hapo, saa sita mchana namkabidhi dereva (wa taxi, sio wangu jamani) apaleke katuni ofisi za gazeti la mwananchi kwa ajili ya kesho yake. Baada ya hapo nageukia upande wa illustrations, mara nyingi huwa nina kazi za taasisi mbalimbali za ku-Simplify text into cartoons kwa ajili popular versions za machapisho mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.
By saa 8 mchana huwa nimemaliza, kama kunakuwa na mikutano ofisini naingia, kwa kifupi by saa 10 jioni nakuwa nimemaliza ingawa wakati mwingine humaliza jioni zaidi, baada ya hapo narudi nyumbani kwa ajili ya kubadilisha nguo then naenda mazoezini. Nikitoka mazoezini huwa sitoki tena nyumbani.

BC: Kwa kumalizia, kuna lolote ambalo ungependa kuwaambia wasomaji na watembeleaji wa tovuti hii?


KP:
Ningependa kuwaomba wasomaji na watembeleaji wa tovuti hii wakae tayari kwa nguo zangu ambazo nafanya launching ya nguo za KP kati ya July na August.

Nawategemea sana watanzania walioko nje ya nchi kunisapoti kwa kununua nguo zangu. Kwa kifupi ni kwamba natengenezea nguo hizi Uturuki, India na China. Kwa hiyo jeans, mashati ya kike na kiume, tops, tshirts, skirts na nk zitakuwa zinapatikana. Nakamilisha taratibu za international banking na wanaosafirisha vifurushi ili utapofika muda walio nje waweze kuzipata kwa urahisi, utaratibu wa oda nitawajulisha kupitia tovuti hii.

BC: Asante sana Masoud Kipanya, tunakutakia kila la kheri katika kazi zako.

KP: SHUKRANI.

Ziada: Kwa michoro zaidi ya Kipanya unaweza tembelea tovuti yake kwa kubonyeza hapa.

Picha zote kwa hisani ya Issa Michuzi.

 

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

57 Responses to “KWA KINA NA MASOUD KIPANYA(KP)”

  1. Comment by Naomi on June 22nd, 2007 9:46 am

    kwakweli hii interview ni the best. Sikujua kwamba Kipanya sio jina lake. Nimefurahishwa sana na majibu yake na nimependezwa sana na maoni yake. Masoud unaonekana ni jamaa mwenye msimamo, endelea hivyo hivyo, naamini karibuni utafanikiwa. Bongo celebrity keep it up. We are here waiting for more.

  2. Comment by Luther on June 22nd, 2007 11:43 am

    Safi sana Kipanya.Kazi nzuri.

  3. Comment by king JAMES[SEOUL] on June 22nd, 2007 12:44 pm

    Hii imenifurahisha sana ,keep it up brother MASSOUD..tunafagilia kazi zako sisi tulioko nje hua tunafarijika sana tunapooona waandishi kama nynyi mnafanya kazi nzuri ya kuwakosoa hao wanaokosea..hongera sana bongo celebrity and issa michuzi..

  4. Comment by Matilda on June 22nd, 2007 1:15 pm

    Massoud safi sana kijana unajituma vya utosha mnatakiwa watu kama nyie katika nchi hii ya tz!Napenda sana kazi zako utangazaji uchoraji na udisign safi na mungu akubariki sana.

  5. Comment by Sayed on June 22nd, 2007 2:42 pm

    Masudi anajitahidi kuielimisha jamii kupitia katuni za kipanya.
    Ningependa kumshauri michuzi uwe unatuwekea katuni za kipanya katika blog yako zitokapo tu kwenye magazeti

  6. Comment by grace on June 22nd, 2007 4:41 pm

    uko juu ile mbaya bro, to me the day haijapita bila kufungua website ya kipanya, by the way the interview iko pwaaaaa!!

  7. Comment by muombwa wa Makunduchi on June 22nd, 2007 10:25 pm

    Kwanza nampongeza bwana Masoud kwa kazi yake anayoifanya ya kuelimisha jamii. Kwa kuwa bwana Masoud ni mtu muhimu ni vyema kubadilishana naye mawazo. Nimetofautiana naye kimawazo pale alipoonekana kulinganisha wanasiasa na wafanyabiashara na wakulima. Inaonekana kwa mawazo yake ni bora mustakabali wa maisha yetu utegemee wafanyabiashara na wakulima. Kwa mtizamo wangu nahisi ni sawa na kuwa na nyoka nyumbani. Ni bora wanasiasa mara elfu. Maovu makubwa yaliyotapakaa duniani kuazia Japan hadi Mwanarumango ni kutokana na wafanyabiasha. Hawa ndio waliokamata hatamu ya dunia. Angalia leo kinachofanyika Iraq halafu nenda Palestina ukaone udhalimu. Uvamizi wa Iraq ni kutokana na vishawishi vya wafanyabiashara ambao wanataka kuuza mali na kupora nyengine zilichini ya ardhi. Iraq hivi sasa inaandaa sera ya kubinafsisha mafuta ili wafanyabiashara wafanye vitu vyao; sio kwa faida ya Wairak lakini kwa matumbo yao. Bwana Bush amewekwa na wafanyabishara na hivi sasa analipa fadhila. Chama cha Hamas kimeshinda uchaguzi. Kila mmoja anajua lakini ni Marekani na rafiki zake akiwemo Japan wanaofanya kila hila ili Palestina iongozwe na Chama cha Fatah. Hizi ni nguvu za wafanyabiashara. Karibuni dunia umepitisha maazimio kupiga marufuku uvuvi wa nyangumi lakini Japan amepinga. Hizi ni nguvu za wafanyabiashara wanataka kutunisha matumbo yao. Ni busara sana kwa Watanzania kujikinga na ukimwi. Tusitegemee kupatikana kwa dawa hivi karibuni. Ni wafanyabiashara wakubwa ambao wamemiliki viwanda vya kutengeneza madawa na kwa mtizamo wao ugonjwa wa Ukimwi umewakumba masikini ambao hawana fedha za kununulia dawa. Kwa nini basi wapoteze fedha zao kwenye utafiti wa dawa ambao hauna tija. Hivi vidawa tunavyopewa vya kuongeza nguvu hivi sasa Wafanyabiashara wanataka nchi yoyote ili isitengeneze dawa hizi. Kuna mzozo mkubwa baina ya India na wafanyabiashara hawa kuhusu utengenezaji wa dawa. Kwao wao fedha mbele maisha ya binaadamu baadaye. Kwa kifupi bwana Masoud mustakbali wa nchi pamoja na dunia ni bora mara elfu kuwa chini ya wanasiasa ila nakubaliana nawe kuwa wanasiasa hawa wasiwe ‘bomu’. Mfanyabiashara yoyote duniani ameweka mbele maslahi yake, utu kwake sio biashara ya kufikiria. Pengine bwana Masoud ni mfanyabiashara tofauti. Hebu tungojee siku ya maonyesho ya mavazi yake…..haraka ya nini?
    Ahsante

  8. Comment by Ambrose Nshala on June 23rd, 2007 4:03 am

    Jamaa ana vipaji vingi sana, namkubali sanaaaa. Keep it up Masoud, am sure you can do more!!!!!!!!!

  9. Comment by lulu on June 26th, 2007 9:04 am

    masooud brother,
    umetoka mbali mpaka kufikia hii hatua hivyo kaza mwendo utafika unapotaka kwenda.
    naamini utafanikiwa zaidi ya hii leo.
    na sitochoka kusoma habari zako mpaka nione mwisho wako,tupo pamoja kaka
    big up sana masoud

  10. Comment by michuzi jr on June 26th, 2007 1:49 pm

    sio siri nami bro Kp namzimia sana kwa katuni zake,huwa zinanivutia kupita kiasi, mara nyingi kabla ya kusoma lolote kwenye gazeti la mwanachi, kitu cha kwanza ni kuangalia katuni yake kwa siku hiyo inasemaje then yanafuata mengine. Wakati mwingine nikikutana nae huwa namuuliza maswali kadhaa kwamba anafikiria nini kabla ya kuchora katuni husika.!

    Keep it up bro

  11. Comment by Yasmin Simba on June 28th, 2007 2:52 am

    Nimefurahi kupata undani wake zaidi kwani namzimia Masoud ile mbaya kwa kazi zake, he is really talented keep it up man….sky is the limit!!

  12. Comment by godluck on June 28th, 2007 4:04 am

    kaka kusema ukweli uko juu sana,we kaka ukishikwa na polisi ni bora wakufunge bila ya kupewa fursa ya kujitetea,maana unaweza kweli kujielezea kaka,pamoja na hilo big up na kazi yako ya katuni,utangazaji wako kwenye “power breakfast”!!!!

  13. Comment by maryam on July 3rd, 2007 10:03 am

    nimefurahishwa na kazi yako,i just think its time you expand you are really good at what you are doing keep it up…

  14. Comment by maryam yahya lweno on July 3rd, 2007 10:06 am

    im proud of what u are doing,nyie ndo watu mnaoitwa multi talented.what i think you should do now is enforce in expanding your work to new horizons,we spport you all the way keep it up!!!!

  15. Comment by Masoud Kipanya on July 5th, 2007 5:11 am

    Kwanza asanteni dada na kaka zangu kwa support, kuikubali kazi ya mtu ni support kubwa SANA!!! kwa Muombwa wa makunduchi nakubaliana na mawazo yake, nimetoa mfano wa wafanyabiashara na wakulima wa mazingira ya wenzetu ambao kwao serikali zao zinafanya kazi zake ya kuwa kama REFA wa kutazama fair play kiukamilifu tofauti na kwetu ambapo taasisi kama SUMATRA, EWURA TCRA na nyinginezo ingawa zinatakiwa ziwe kati ya service provider na consumer lakini bado haki ya mlaji iko mashakani. ila all in all ni heri ya kudeal na mfanyabiashara aliye tayari na pesa kuliko kudeal na mwanasiasa ambaye ana njaa na anayedhani njaa yake itaponea akiwa madarakani, huyu ni hatari zaidi!! ni mawazo yangu, sishinikizi tuamini hivyo.

  16. Comment by rwabukamabara on July 9th, 2007 6:20 pm

    kaka interview yako ipo bomba,kaka nitakutafuta tuongee zaidi,big up bro,na mungu akuzidishie nguvu na upeo zaidi wa kufikiri.

  17. Comment by toxeeq on July 13th, 2007 4:57 am

    masoud,like i said napenda kazi yako and i want and i am going to be a run way model so nataku pata pata vipi??coz we belong in the same industry…

  18. Comment by mamii on July 16th, 2007 1:19 am

    Masoud ni kichwa! that’s all I can say kwa sasa hivi! kaka kaza buti, you real insipires peoples’ life especially your “power breakfast show” session. Utangazaji wa Masoud sio siri unayeyusha hasira ya foleni ya bongo asubuhi maana ukiwa unasikiliza power breakfast unasahau machungu ya foleni asubuhi! Big Up brother!

  19. Comment by Alex Kikoti on July 16th, 2007 11:02 am

    Mimi nilianza kukukubali toka wakati ule wa kipindi cha CHUCHU-CHU. Ubunifu ambao wengi hatuna,unejaaliwa na mwenyezi, utumie kaka.

  20. Comment by Zahra on August 9th, 2007 7:47 am

    Keep it up masoud! Mimi napenda kusema kwamba mama yangu ni mpenzi sana wa kipindi cha power breakfast na hakuna cku anapenda akose kipindi chenu, Cku ukiwa haupo studio anakosa raha, anapenda team yenu ikikamilika sometime akiwa anawasikiliza anacheka peke yake kwa porojo zenu na jokes zinavutia, Hongereni sana.

  21. Comment by elisante on August 13th, 2007 10:25 am

    you know masoud is realy cool, i give him my respect on how he draw those cartoons b cause they are real nice.congra man
    REMEMBRE ALWAYS THE FIRST IS THE BEST NOT THAA REST ELISANTE CONFESS.
    it;s excellent 2b on net
    http://www.elisante.tk

  22. Comment by anny mwiya on August 15th, 2007 12:17 pm

    hello my bro nakupa big up sana tuu kwakweli unatisha ktk anga za utangazaji kaza buti…. were 2gether…thanx man……

  23. Comment by anny mwiya on August 15th, 2007 12:20 pm

    hi mr masoud nakupa hongera sana na mungu atkuzudishia inshallah keep well alwaysss……. chao

  24. Comment by anny mwiya on August 15th, 2007 12:22 pm

    i am with alwaysss…. your really smart….. kaza buti bwana au sio bwana……ha ha huh wenye wivu wajinyonge…..tataaa

  25. Comment by ukende on September 3rd, 2007 3:45 pm

    Hii masod..u knw wat,yo rily talented keep it up..u knw and you can do it 4rely, to be honest with you you alwys inspire me especilly on the power breakfast session and other good stuffs that you doin.yan u don knw how hard i have played to search 4u atlist u culd hear 4rm me,i rely wish to share with uu concerning you desinigs…yan nataman nitokee hata kwenye la advertsements za nguo zako ambazo zitatoka.you can count on
    me and i wll be grateful if you will think abt my proposal. wape hii yo family..GOD bless you always

  26. Comment by ukende on September 3rd, 2007 3:51 pm

    Hii masod..u knw wat,yo rily talented keep it up..u knw and you can do it 4rely, to be honest with you you alwys inspire me especilly on the power breakfast session and other good stuffs that you doin.yan u don knw how hard i have played to search 4u atlist u culd hear 4rm me,i rely wish to share with uu concerning you desinings…yan nataman nitokee hata kwenye tangazo la advertsements za nguo zako ambazo zitatoka.u knw im gud in markerting and you cn count on my support,

  27. Comment by Pope Pius on September 25th, 2007 12:02 am

    Kaka Mathudi!!
    Ni mara chache sana katika Bulogu Post ikasifiwa mwanzo mpaka mwisho, hii ni ishara tosha kwamba unakubalika kwa unachokifanya ila haimaanishi kwamba ubweteke na michango ya wadau, binafsi nakufahamu kwani tulifanya kazi pamoja Majira na kazi zetu ziliingiliana kwa namna moja au yingine hivyo sina ubishi na kazi zako na utendaji wako, ur the best but take this posts as challenge for the better of tomorrow kaka!!
    Big Up KP!!

    Wabillah TAwfiq

  28. Comment by Grace Kombe - Arusha on October 10th, 2007 10:51 am

    Good…..Keep it up kijana.

  29. Comment by january on November 6th, 2007 10:46 am

    Bomba sanaaaaaaaa yaani katuni imekwenda shule kinoma, yani hapo UN unge weka mwanangu na tuwatu kidogo wee ingekuwa balaaa, yani wasinge pima kabisaaa

  30. Comment by prisika on November 13th, 2007 2:37 pm

    Masoud nakukubali……kuna siku nilikaa na uncle yangu(who used to work at clouds FM 2003),wewe na Bonda”mkawa mnacheka kwamba wafanyakazi wazima wa Clouds mmekaa kwenye kibanda cha chips mnakula”……kuna moja tena ukasema raha ya kwenda kula sehemu kama African Hotel ni kukutana na mtu anayekujua maana inaonekana kwamba unakulaga sehemu hizo……..u r very funny…….akili yako mkikutana na Bonda yaani uuuuwi…nakufagilia ndugu yangu “kichwa”……yani kijana kichwa, pesa ipo huna majidai……..while stars wengine wa bongo wana jina tuuu wamechoka kipesa maringo hadi vidoleni……hebu wape somo hao!……….kila la kheri!

  31. Comment by david benjamin on December 7th, 2007 11:51 am

    I guess Masoud fits more in utangazaji than kwenye fields nyingine.Well,i dont mean kwamba ur not a good cartoonist,NOT AT ALL…Ila mwanangu unasound vizuri ukiwa redioni hasa pale unapotangaza power breakfast ukiwa na machizi wenzako(Fina na Gerald)

    In short u are MULTI-TALENTED ila dont be that much big-headed becauze u still have a long journey 2 go.Try 2 be more critical kwenye katuni unazochora kwani TZ ye2 sasa hivi inahitaji +ve ideas kama za kwenu.Always DARE 4 the IMPOSSIBLES……….

  32. Comment by MC Katelephone on December 11th, 2007 6:10 am

    Ebana mwanagu nakupa hongera sana tena sana
    endelea kuchapa kazi kama kawaida nami naamini kuwa huwa unajipanga vizuri sana katika swalazima la kuugawa muda wako kwa maendeleo zaidi yaani kuna muda wa Utangazaji na pia umetenga muda wa Uchoraji. ebwana Mzuka.

  33. Comment by Mama wa Kichagga on December 20th, 2007 3:08 am

    Jamani jambo woteeeeeee. Mimi nawapahongera kuanzia mtangazaji aliyefanya mahojiano, KP na wachangiaji wote. Mahojiano na comments za namna hii ndizo zinazotakiwa maana zinaelimisha na kujenga kuliko zile za kutupiana lawama, kukosoani na kutukanana, Big up ALL OF YOU!

    Masoud kaka, hongera sana nakufagilia kuanzia tabia hadi utendaji wako wa kazi. Je nyumbani unawajibika kama hivi? You must be having a wonderful family brother. God Bless you in your plans.

  34. Comment by mukrim on March 3rd, 2008 2:40 am

    ya nakupongeza kwa kipaji alichokupa allah lakin pole kwa yale ulioyafanya namini hukuwa unayajua kuitangaza pombe hali ni mtoto wa kislamu laiti ungetumia mda huo kuitangaza dini ingekwua bora mbele ya allah wka hivyo juta kwani kila mtu anapoionja pombe ile basi huandikiwa madhabi kwa kwua ulishiriki kuitangaza kwa hivyo juta kwa hayo allah ni mwingi wa kusamehe kaka ni hayo tu

  35. Comment by bizzybody on March 13th, 2008 11:43 am

    hey masoud,
    honestly i am fond of yu big tym,
    i do listen to powerbreakfast showu rockinnnnnnnnnn,
    more over i love yo designs tho for me are not affordable
    Hey lemmi praise yu bwana u r talented,
    don mind about the comments that arent pleasing manu r a human being and so u have yo downfalls.
    hey stick to this, when the going is tough,the tough gets going……..
    i ove you so muchhhhhhhhhhhhhhhh (annha ila so kivile)
    tres bian….its in french luk for the meaning
    xoxoxoxoxoxoxoxxoooooooooooooo

  36. Comment by kiganja on April 15th, 2008 10:48 am

    Kuacha kwako kuchora vikatuni vya kukebehi uongozi wa Lowassa wakati alipokuwa waziri Mkuu kulihusishwa na wewe kuwekwa katika payrall yake via Roatam agent unajiteteaje?

  37. Comment by Bely Kasambula on August 22nd, 2008 2:10 pm

    Big up Kipanya! Uko juu sana.
    Kupitia katuni zako umeweza kuikomboa jamii kwa kiasi kikubwa mno kutokana na mambo ambayo pengine sio kila mtu angeweza kuyasema moja kwa moja hadharani, tunashukuru sana sababu inasaidia kuwashtua walioko juu ya viti. bila ya kusahau unaelimisha na kuburudisha sana. Mimi ni shabiki wa kazi zako sababu unafanya kile kilicho bora. Huu ni muda wa kuambiana ukweli na ukiwa na fikra za uwazi na ukweli utaishi kwa amani milele bila ya kumuogopa mwenzio ambaye wote mnavuta tu hii pumzi za bure! Hata kama anatembelea hewani yeye ni mtu tu na inafaa aambiwe! Big up bro! Jamii inahitaji watu kama nyinyi ili tufike mahali ambapo tunaweza kuona tumefikia angalau nusu ya maendeleo! Naishia hapa nunda wa block 41.

  38. Comment by gracia on August 26th, 2008 2:44 pm

    Masudi, najiskia Faraja kusimama nakusema nakufahamu sababu najua namfahamu mtu mwenye manufaa..

    Tupo pamoja. napenda kazi zako.

  39. Comment by masika on September 23rd, 2008 4:21 am

    yeah good stuff men i real apreciate whta u are doing men guys shud learn frm u men keep up the good stuff.

  40. Comment by watubwana on October 19th, 2008 11:22 pm

    siri ya mtungi aijuaye ngata.ishi upendavyo na si wapendavyo,usafi si wa mlamgoni,ni hadi uchagoni.hongera kaka,ni mfano wa kuigwa.serikali wapeni uhuru waandishi wa habari wafanye kazi zao.jifunzeni,jirekebisheni mnapokosolewa.

  41. Comment by naomy on January 6th, 2009 12:52 am

    nini maana za uchoraji?elementi za uchoraji hope u will help me.keep it up ma brother upo juu

  42. Comment by Peggy on January 21st, 2009 8:18 am

    …mimi Masoud namkubali kwa kazi zake nzuri na zakuelimisha jamii, be it kwenye cartoon au utanganzaji, man! your listeners are really missing your voice, full of realities…where are u? watu tuna miss… uhondo wa power breatfast, wewe na Fina mango. ucheshi wenu ulikuwa natural. `nakutakia heri na fanaka ktk kazi zako nzuri…kijana.

  43. Comment by FLORA NYELLA on March 11th, 2009 8:36 am

    Keep it up! Brother Masoud, ninafurahishwa sana na kazi yako, of course transparent person kama wewe ni wachache sana hasa katika nchi yetu iliyotawaliwa na mabepari na wanyonyaji wa jasho la mnyonge. waandishi ama wasanii waliowengi wanaogopa sana kusema habari za hawa mafisadi lakini namna yako ya kufikisha ujumbe kwa hawa mafisadi nimekukubali nami nakupongeza sana, mimi ni mwanaharakati wa haki za binadamu na ninaungana nawe brother, Nakutakia afya njema na ufanisi wa kazi hii nzuri.

  44. Comment by trina on April 1st, 2009 6:41 am

    anajitaidi ila ningependa zaidi aongelee familia yake ili 2mpate vizuri

  45. Comment by mohamed on April 19th, 2009 1:07 pm

    Si kazi nyepesi hivo ongeza umakini katika kazi yako na ustie maji ktk tembo

  46. Comment by leah on April 21st, 2009 8:11 am

    masoud nakukubali sana bro keep it up,

  47. Comment by frozia on May 6th, 2009 1:42 am

    hi to all
    hii imetulia sana na mimi binafsi naikubali kazi ya masoud kwasababu yuko katika kiwango cha juu sana kwene uchoraji pia nadhani huyu mshikaji anakipaji chapekee sana katika fani hii kwasababu hajawahi kuchora picha nikashindwa kuipenda

    eebwana eeeh big up kaka
    frozia

  48. Comment by .Speratus Rwezaula. on May 31st, 2009 8:47 pm

    Hongera sana bw.Kipanya elimu unayoitoa kupitia fani yako ni muhimu sana kwa dunia ya leo.MUNGU akubariki ktk kazi yako.

  49. Comment by Mjololo Ng,ughuya on June 4th, 2009 3:31 am

    Hongera kwa kazi nzuri kipanya.mimi ninapenda sana vichekesho vyako.

  50. Comment by fatma on June 20th, 2009 5:28 am

    bib up kwa sanaaaaaaaaaaa

  51. Comment by s.aminieli on July 26th, 2009 5:57 am

    mko sawa kabisa.keep it up!

  52. Comment by masoud on August 6th, 2009 4:10 am

    upo juu kijana….vp maisha plus yako au?pa1 kaka

  53. Comment by SABEBE HOT POT FAMILY WABISHI WA MJINI on August 14th, 2009 5:23 pm

    safi sana kaka,haya ni matunda na malipo toka kwa mungu,manyanyaso uliyo pata ukiwa mdogo,manyanyaso dalili ya neema masood,msamehe na wasamehe,kazi njema

  54. Comment by yussufu laiza on September 14th, 2009 1:36 am

    Kipanya atueleze siri ya maisha plus.

    Tunataka kuiga kwani vizuri huigwa

  55. Comment by Mateso on November 6th, 2009 5:36 am

    masudi hongera keep up

  56. Comment by fred mwanichisye on November 18th, 2009 10:44 am

    big up masood mi nakukubali ile mbaya mtu wangu jhapo bongo kipaji ndio dili

  57. Comment by me on December 12th, 2009 10:41 am

    du kijana u rock men keep on touchn du we mkaliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

Leave a Reply