Mwezi wa kwanza wa mwaka 2012 ndio huo tumeshaanza kuuwashia indicator.Upo ukingoni.Wakati tukihesabu siku,kwenye tasnia ya Bongo Fleva,tayari wasanii kadhaa wameshaanza kuachia ngoma zao ambazo itakapofika Desemba mwaka huu,zitakamilisha orodha ya nyimbo zilizotoka mwaka huu.

Leo hapa tunao wimbo kutoka kwa Godzilla,msanii ambaye ana style inafanana kwa karibu na 50….(malizia mwenyewe kama unaafikiana nami).Hapa anakuja na wimbo Milele akiwa amemshirikisha Ally Kiba.Milele ni production nyingine kutoka pale MJ Records chini ya Marco Chali(wenyewe siku hizi wanapenda kumuita Dr.Chali). Usikilize hapo chini

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

 

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

The video was produced by Louise Kamin and shot by the Danish/Tanzanian cinematographer Talib Rasmussen for Caravan Records. The video was shot in a derelict building belonging to the Egyptian embassy along Kenyatta Drive which has now been torn down. It features some of the musicians who perform with Mzungu Kichaa and the legandary Tanzanian boxer Sheni who met with Mohammad Ali during the “rumble in the jungle” fight in Congo in 1974.

The song is about the process of saying goodbye to a loved one and metaphorically could be interpreted as saying goodbye to life. Mzungu Kichaa sings: ‘We have struggled in this world together and now the time has come to say goodbye. It will make me happy if you smile rather than cry. Who knows if we’ll meet in the heavens? We must respect and help each other here on earth, for we might never return again’.

 

Twalumba kabotu / Twalumba kabotu mama… baba

Ndugu zangu, nawashukuru sana / Tumepambana katika ulimwengu / Muda umefika wa kuachana / Tuagane kwa furaha sitaki lawama / Ninakokwenda nayo nikuzuri / Majani yanaota na maji yanakwenda / Nitafurahi ukicheka kuliko kusononeka / Kilatukiachana tutaonana tena

Ninaenda zangu, nina kimbia / Ukiniomba kubaki nita anza kulia

Ndugu na jirani, rafiki na mtu flaani / Muko na mimi moyoni / Mola tu ndyio ana jua / Ndiyo maana tusaidiane / Tuheshimiane / Kuna siku tuta achana, peponi je tutaonana? / Ulimwenguni haturudi tena / Tupendane tukiwa hai

Tunaendelea na session yetu ya Flashback Friday.Leo tunao Next katika wimbo wao Too Close.Hope you enjoy this one and enjoy your Friday!If you gonna drink,please be a passenger and never a driver!

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

One of the things I like doing when I surf the internet is reading the interviews. In most cases,I am an interviewer so when I get a chance to read what other interviewers are asking and what their interviewees are saying, I get over excited. I can, at times,feel my heartbeats going faster. I wanna run,read it faster.Be in the Know! That’s me.

It was,therefore, a great morning for me when I came across an interview featuring Subi a lady who runs www.wavuti.com. I know there are lots of ladies doing a fantastic job of blogging out there. But in my opinion,Subi is a rock. She doesn’t only blogs but also assists a lot of younger bloggers to get where she is or where other bloggers are. She understands what is happening behind the pages full of maneno and photos that a lot of us like to peruse through. I have personally benefited from her “good heart”. When I get stuck with a software issue,I always think of Subi. And she is always there to assist unless she is busy saving lives elsewhere.

Here is the interview she did with Vijana FM(another group of people I admire and appreciate when it comes to dot com stuff and mapinduzi halisi). Well done Subi.

Jina lake unayemuona hapo juu ni Zuwena Mohamed.Ila kwa wengi anajulikana kama Shilole.Sina hakika kama Shilole jina lake la tokea utotoni au ni jina la kisanii.Ni muigizaji wa filamu nchini Tanzania na yes anaimba pia.

BC inajiandaa kuambaa na Shilole katika mahojiano maalum.Je,unalo swali au maswali ambayo ungependa Shilole ayajibu?Kama jibu lako ni NDIO basi usisite kuyatuma maswali yako kwenda bongocelebrity at gmail dot com(anuani pepe imewekwa hivyo ili kupunguza hackers).

ANGALIZO: Maswali yalenge katika kujenga na sio kubomoa

Picha kwa hisani ya Global Publishers.

Mwaka jana mwezi wa nane(August),tuliuliza swali katika post hii hapa.Kichwa cha habari kilikuwa katika lugha ya Kiingereza kwamba Dr.Asha-Rose Migiro:The Next President? Swali lile tuliliuliza kufuatia kilichokuwa kikiendelea katika duru za kisiasa wakati ule. Kulikuwa na tetesi kwamba Dr.Migiro,huenda akajitupa ulingoni kuwania Urais mwaka 2015.Wadau mbalimbali wakawa wakiongelea uwezekano wa Tanzania kupata Rais wa Kwanza Mwanamke na mambo kama hayo.

Kwa bahati nzuri au mbaya,wakati ule Dr.Asha-Rose Migiro bado alikuwa akishikilia cheo chake cha U-naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(United Nations)  na hivyo kufanya tetesi zile ziishie hewani kama vile mvuke wa maji ya moto tu. Mambo yamebadilika kidogo hivi majuzi  ilipojulikana kwamba Dr.Migiro atakiachia cheo cha U-Naibu Katibu Mkuu wa UN kwa sababu muda wake umemalizika.Haijawekwa wazi kwamba kwanini yeye aondoke wakati Katibu Mkuu wake,Ban-Ki Moon bado yupo na kama walikuwa na ajenda basi ni yao wote kuitekeleza.Anyway,hayo ni mambo mengine,tuyaache kwa sasa.

Sasa kwa sababu Dr.Migiro anaondoka UN na hivyo kumaanisha kwamba atakuwa na nafasi zaidi ya kuwania Urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, tayari fukuto la maoni ya wananchi limeanza kutanda. Je,agombee mwaka 2015? Je anafaa?Je,Tanzania ipo tayari kwa Rais Mwanamke? Hayo ni baadhi ya maswali yasiyo na majibu ya moja kwa moja ambayo yamekuwa yakisikika iwe ni mtaani,mitandaoni,katika vyombo mbalimbali vya habari hususani Radios nk.Nini maoni yako wewe msomaji wa BC?

Kwa masikitiko makubwa tunawatangazia kifo cha Mzee wetu Robert Jaka wa Forest Hill- Morogoro, kilichotokea katika hospitali ya Regency mchana wa Jumapili ya tarehe 22/01/2012 Dar-es-salaam-Tanzania.

 

Marehemu katika uhai wake alifanya kazi katika vyuo vikuu vya Sokoine na baadae chuo kikuu cha Dar-es-salaam kabla ya kustaafu na kurejea Morogoro. Msiba upo Dar-es-salaam Mtoni-Kijichi (nyumba za maafisa wa Magereza)

 

Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda Morogoro siku ya Jumanne na Mazishi yanatarajiwa kufanyika Morogoro siku ya Jumatano tarehe 25.01.2012.

 

Kwa taarifa zaidi za msiba unaweza kuwasiliana na Kizito Jaka (+255 762 583740) Paschal Kunambi (+255 713 233843) au Exupelius Kunambi (+255 767 201098)

 

Pichani ni Katibu Mkuu wa CHADEMA,Dr.Slaa na mkewe

Anaitwa Noni Zondi.Ni msanii,model na muigizaji mzaliwa wa Afrika Kusini mwenye makazi ya kudumu nchini Uingereza.

Noni Zondi

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video


 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MAHUSIANO MABAYA SANA KATI Y A TFF NA AFRICAN LYON FC

Kwa masikitiko makubwa sana, uongozi wa timu ya African Lyon Fc inapenda kuwaeleza watanzania hususani wapenzi wa mpira wa miguu kuwa, katika jitihada zote za timu yetu ya kukuza na kuedeleza soka hapa nchini, Tumekuwa na mahusiani MABAYA SANA na chama cha mpira wa miguu yaani TFF.

 

Napenda kuweka wazi bila kificho chochote kuwa TFF imekua ikitukandamiza na kutuchafua mbele ya jamii kwa makusudi. Tena ni kana kwamba si mtu mmoja ndani ya TFF bali ni kuwa agenda ya TFF nzima.

 

Kuanzia kwa Rais wa shirikisho kamati ya mtendaji, kamati ndogondogo na pia sekretarieti cha kusikitisha kama si kufurahisha mpaka kwa walinzi wa milangoni siku za mechi.

 

Napenda nitoe baadhi ya mifano michache ambayo tunakutana nayo katika jitihada zao za kutuyumbisha pamoja na vilio vyetu vya kila siku.

 

  1. RATIBA YA LIGI KUU.

Timu zote ambazo zimekua zikienda kucheza mechi kanda ya ziwa zimekuwa zikicheza mechi zote mbili(yaani kucheza na Toto Fc na Kagera sugar). Kitu ambacho African Lyon Fc chini ya uongozi wetu hatujawahi kukutana nacho.

 

Nakama hiyo haitoshi mechi yetu ya mwisho wanatupeleka Manungu Turiani kucheza dhidi ya JKT Ruvu na hali sisi na JKT uwanja wetu ni Chamazi alafu wenyeji wa Turiani (mwenye Uwanja wao) Mtibwa wanapelekwa Morogoro kucheza dhidi ya Moro United.

 

Ni vigezo vipi vilivyowekwa kutupeleka sisi na si Simba wala Yanga. Je hii TFF ni ya Simba na Yanga tu.

 

  1. MBWANA SAMATA

Ndugu watanzania, Tumeandika barua zaidi ya 15 kwa sekretarieti,kamati ya haki ya wachezaji, Raisi Tenga. Lakini hakuna yeyote aliyezungumzia jinsi ambavyo Simba imegushi uhamisho wa Mbwana Samatta kutoka African Lyon Fc. Cha kushangaza ndugu Alex Mgongolwa ambaye pamoja na kupelekewa barua yetu TFF ofisini kwake,kaibuka na timu ya Kimbangulila Fc na African Lyon tumeachwa bila hata kusikilizwa.

 

Napenda kumlaumu kwa nguvu zote ndugu Alex Mgongolwa kwa makusudi yake kabisa tena kwa kukusudia ya kugoma kukaa na sisi na kutisikiliza. Na kwa dharau yake ya kushindwa hata kutujibu japo moja ya barua zetu.

 

 

Na kwa kuonyesha chuki za wazi kwetu ni pale ambapo aligoma kukutana na WAFADHILI wetu aliokuja kutoka Marekani na Uarabuni kutaka kujua maswala haya hususani ya MBWANA SAMATTA. Hawa ni watu waliotumia fedha na mda wao kuja nchini kwetu alafu mtu anagoma.

 

Na si yeye tu aliyegoma hata uongozi wa juu wa TFF uligoma kukutana nao ili hali hawa wote walipata taarifa wiki moja kabla juu ya ujio wa wageni hawa.

read more

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page